1. Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya Kusini

Mwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). “Kabla ya wakati wa watendaji huduma, mwanadamu hakuelewa chochote kuhusu ukimbizaji wa maisha, ni nini maana ya kumwamini Mungu, au hekima ya kazi ya Mungu, wala hakufahamu kwamba kazi ya Mungu inaweza kumjaribu mwanadamu. Tangu wakati wa watendaji huduma mpaka leo, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ni ya ajabu, haiwezi kueleweka kwa mwanadamu, na akitumia akili yake hawezi kufikiria jinsi Mungu hufanya kazi, na pia huona vile kimo chake ni kidogo na kwamba kiasi kikubwa chake ni cha kutotii. Mungu alipomlaani mwanadamu, ilikuwa ili Atimize athari, na Hakumuua mwanadamu. Ingawa Alimlaani mwanadamu, Alifanya hivyo kupitia maneno, na laana Zake hazikumwangukia mwanadamu kwa kweli, kwani kile ambacho Mungu alilaani kilikuwa kutotii kwa mwanadamu, na kwa hiyo maneno ya laana Zake pia yalikuwa kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kama Mungu atamhukumu mwanadamu au kumlaani, yote mawili humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu: Yote mawili yanafanywa ili kukifanya kamili kile ambacho ni kichafu ndani ya mwanadamu. Kupitia njia hii mwanadamu anasafishwa, na kile ambacho kinakosekana ndani ya mwanadamu kinafanywa kamilifu kupitia maneno na kazi Yake. Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa mkamilifu, na inafaa kwa uhalisi. Kotekote katika enzi zote Mungu hajawahi kufanya kazi kama hii; leo, Yeye hufanya kazi ndani yenu ili muweze kufahamu hekima Yake. Ingawa mmepitia maumivu fulani ndani yenu, mioyo yenu inajisikia thabiti na kwa amani; ni baraka yenu kuweza kufurahia hatua hii ya kazi ya Mungu. Haijalishi kile mnachoweza kupata katika siku za baadaye, yote mnayoona kuhusu kazi ya Mungu ndani yenu leo ni upendo. Kama mwanadamu hapitii hukumu na kuadibu kwa Mungu, matendo yake na ari daima yatakuwa nje, na tabia yake daima itaendelea kutobadilika. Je, hii inahesabika kama kupatwa na Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Maneno haya ya Mungu yananigusa sana. Naweza kuhisi kwamba kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu ni ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Ningependa kushiriki ufahamu fulani kuhusu majaribu ya kwanza niliyoyapitia baada ya kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, ambayo yalikuwa majaribu ya watendaji huduma.

Siku moja mnamo Februari 1991, nilikuwa nikihudhuria mkutano kama kawaida ndugu mmoja alipotuambia kwa furaha, “Roho Mtakatifu ametamka maneno!” Kisha, ndugu wakaanza kusoma: “Sifa zimekuja Sayuni na makazi ya Mungu yameonekana. Jina tukufu takatifu linasifiwa na watu wote, na linaenea. Ah, Mwenyezi Mungu! Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa, na Ameinuka juu ya Mlima Sayuni ulio na uadhimu na mzuri kabisa katika ulimwengu mzima …” “Umetengeneza kundi la washindi, na kutimiza mpango wa usimamizi wa Mungu. Watu wote wataelekea kwa mlima huu. Watu wote watapiga magoti mbele ya kiti cha enzi! Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli na wa pekee na Unastahili utukufu na heshima. Utukufu wote, sifa, na mamlaka yawe kwa kiti cha enzi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 1). Hata ingawa sikuelewa kabisa maneno haya wakati huo, nilipoyasikia, nilihisi kwamba yalikuwa ya kipekee sana, yaligusa sana na hakuna mwanadamu ambaye angeweza kusema maneno kama haya. Nilikuwa na hakika kwamba maneno haya yalikuwa yametoka kwa Mungu na kwamba yalikuwa maneno ya Roho Mtakatifu. Baada ya hapo, sura za maneno ya Roho Mtakatifu zilitumwa kanisani kwetu mfululizo wakati wote, maneno ambayo yalifichua ukweli mwingi kuhusu imani na siri za Biblia, na pia yalituonyesha njia ya kutenda ukweli na kuingia katika uzima. Wakati huo tulifanya mikutano karibu kila siku ili kusoma maneno ya Roho Mtakatifu. Kufanya hivyo kuliruzuku na kusitawisha moyo wangu sana. Kila mtu alijawa na furaha na alihisi kwamba amebarikiwa sana. Sote tulidhani kwamba tulikuwa miongoni mwa waliotangulia kuinuliwa mbele ya Mungu, kwamba tulikuwa washindi ambao Mungu atafanya, kwamba bila shaka tutashiriki katika ufalme wa mbinguni, na tutastahili kupokea ahadi na baraka za Mungu. Sote tulijitumia kwa ajili ya Mungu tukiwa na imani tele. Wengine walikuwa wakinakili maneno ya Roho Mtakatifu kwa nguvu na wengine walikuwa wakiyageuze kuwa nyimbo. Hali zetu pia zilijawa na majaribu wakati huo, kwa kuwa ndugu kadhaa walikamatwa walipokuwa mikutanoni. Sikuhofu wala kuogopa, bali niliendelea kujitumia kwa shauku kwa ajili ya Mungu.

Nilipokuwa tu nimejawa na matumaini ya kubarikiwa na kuingia katika ufalme wa mbinguni, Mungu alitamka maneno mapya na kutuongoza katika majaribu ya watendaji huduma. Siku moja mnamo Oktoba niliarifiwa nihudhurie mkutano wa kanisa lililokuwa umbali wa maili 25 ili niyachukue maneno mapya yaliyotamkwa na Roho Mtakatifu. Nilidhani kwamba hakika kulikuwa na habari nzuri sana, kwa hivyo niliendesha baiskeli yangu kwa furaha hadi mahali mkutano ulipokuwa huku nikiimba tuni fulani mdomo ukiwa umefungwa na nikiwa na nguvu tele. Kwa mshangao wangu, nilipofika niliona ndugu zangu wakiwa na wasiwasi na wote wakiinamisha vichwa vyao. Ndugu mmoja aliniambia, “Roho Mtakatifu ametamka maneno. Mungu anasema kwamba sisi sote ni watendaji huduma.” Dada mmoja alisema huku macho yake yakiwa yamejaa machozi, “Sisi sote ni watendaji huduma. Wachina ni watu wa kuhudumu na hatutapata baraka zozote hata kidogo.” Sikuweza kabisa kuamini kwamba hiyo ilikuwa kweli. Nilikimbia kusoma maneno ya Roho Mtakatifu na nikasoma haya kutoka kwa Mungu: “Nchini China, kando na wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu, wengine wote ni watoto wa joka kubwa jekundu na wanapaswa kutupwa. Nyote mnapaswa kuelewa, hata hivyo Uchina ni taifa ambalo limelaaniwa na Mimi, na watu Wangu wachache hapo ni wale wanaotoa huduma kwa kazi Yangu ya baadaye tu. Kulisema vingine, kando na wazaliwa Wangu wa kwanza, hakuna mtu mwingine—wote wataangamizwa. Usifikiri kwamba Mimi ni wa kuzidi kiasi sana katika matendo Yangu—hii ni amri Yangu ya utawala. Wale wanaopitia laana Zangu ni walengwa wa chuki Yangu, hili ni bila shaka(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 95). Nilishtuka niliposoma haya. Watendaji huduma walikuwa wametajwa mara nyingi katika maneno ya Roho Mtakatifu na nilikuwa nikifikiri neno hilo lilimaanisha wasioamini. Lakini ilibainika kwamba lilituhusu. Maneno hayo yalisema kwamba watu wa China ni watendaji huduma ambao watalaaniwa na Mungu na watakapomaliza huduma yao, watatupwa ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho. Mwili wangu wote ulianza kuwa dhaifu. Sikuwahi kufikiri kwamba nilikuwa mtendaji huduma. Je, kuamini kwa miaka hiyo yote kulikuwa bure? Mbali na kutobarikiwa katika ufalme wa mbinguni, pia nitatupwa ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho! Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimetupwa katika lindi kuu. Nilitaabika sana na malalamiko yakaanza kuibuka. Nilifikiria jinsi nilivyokuwa nimeacha masomo yangu ili kumfuata Bwana, jinsi watu wa ulimwengu walivyonidhihaki, jinsi ambavyo marafiki na familia yangu hawakuweza kuelewa, na kuhusu mateso ya CCP na jinsi nilivyokuwa nimeponea chupuchupu kukamatwa mara kadhaa. Lakini sikuwahi kusita, badala yake, niliendelea kujitumia na kujitolea. Nilikuwa nimeteseka sana, nilidhani kwamba nitaingia katika ufalme wa mbinguni na kufurahia baraka, lakini sasa nilikuwa mtendaji huduma duni. Sikuweza kuelewa hilo. Nilikaa pale kwa muda huku nikishusha pumzi za kukata tamaa. Ndugu wengine walikuwa wakiinamisha vichwa vyao, wengine walilia, wengine walifunika nyuso zao na wakaanza kulia kwa sauti kubwa na ndugu wengine hata waliomboleza kwa sauti kubwa.

Nilipokuwa njiani nikirudi nyumbani baada ya mkutano, nilikuwa na nguvu kidogo ya kuendesha baiskeli yangu. Nilijiuliza nikiwa njiani, “Nawezaje kuwa mtendaji huduma?” Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba nilikosewa na machozi yangu yaliendelea kutiririka. Kule nyumbani, sikuwa na raghba ya kufanya lolote hata kidogo, bali nilitembea huku nikiinamisha kichwa changu na sikutaka kuongea na mtu yeyote. Hata nilihisi kwamba kupumua kulichosha. Sikuweza kabisa kukubali kuwa mtendaji huduma ambaye hatapata baraka zozote mwishowe.

Sura za maneno ya Mungu zilikuwa zikitolewa mfululizo na nilisoma kila sura kwa hamu, nikitamani sana kuwe na chembe ya tumaini katika maneno Yake na kwamba matokeo yangu yaweze kubadilishwa. Lakini mbali na kutoona lolote lililohusu baraka ambazo nilitegemea, pia maneno yote yalikuwa hukumu kali. Kulikuwa na maneno kadhaa ya Mungu ambayo yalisema: “Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo. Hii ni siri ya mpango Wangu wa usimamizi, na kitu ambacho wanadamu hawawezi kuelewa kuhusu mpango Wangu wa usimamizi, lakini pia Nimeliweka jambo hili hadharani kwa kila mtu. Wale ambao si Wangu wako kinyume Changu; wale ambao ni Wangu ni wale wanaolingana nami. Bila shaka hii ni kweli, na hii ndiyo kanuni ya hukumu Yangu kwa Shetani. Kila mtu anapaswa kujua kanuni hii ili aweze kuona haki na uadilifu Wangu—wale wote wanaotoka kwa Shetani watahukumiwa na kuchomwa na kugeuzwa majivu. Hii pia ni ghadhabu Yangu, na mtu anaweza kuona tabia Yangu zaidi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 108). “Baada ya kunifanyia huduma leo, lazima wote waondoke! Msibaki katika nyumba Yangu, msiwe watovu wa nidhamu wala wa kutofanya kazi tu. Wale walio wa Shetani wote ni wana wa ibilisi, na wataangamia milele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 109). Nilipoona Mungu akiwahukumu na kuwalaani watendaji huduma, nilipoteza matumaini yote na nikahisi kwa kweli kwamba nilikuwa nimeanguka moja kwa moja katika shimo lisilokuwa na mwisho. Hata sijui jinsi ya kueleza hisia hiyo ya taabu. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa katika kumbatio la Mungu nikifurahia upendo Wake, lakini sasa nilikuwa nimetupwa nje, nimeshutumiwa na kulaaniwa na Mungu, na kutupwa katika shimo lisilokuwa na mwisho. Nilizama katika kusafishwa katika mateso na nikawa hasi sana. Sikuwa na nguvu ya kuomba, kusikiliza nyimbo au kusoma maneno ya Mungu. Hata nilianza kujutia kila kitu nilichokuwa nimetumia na kutoa hapo awali. Kama ningejua mambo yangeishia kuwa hivyo, ningejiachia nafasi ya kukwepa, lakini sasa niliachwa bila chochote. Kama marafiki na wanafamilia wangu wasioamini wangejua kwamba nitaishia kuwa mtendaji huduma na nitaishia kutopata lolote, je, wasingenidhihaki kila wakati? Ningewezaje kujitokeza mbele ya watu? Ningefanya nini? Nilipofikiria hayo, nilihisi kwamba niliaibika sana. Ninapokumbuka miaka yangu ya kuamini, hata ingawa niliteseka kidogo, nilifurahia neema na baraka nyingi za Mungu. Leo nilikuwa nimeinuliwa na Mungu ili niyasikie maneno Yake mapya na nilikuwa nimejifunza siri nyingi na ukweli mwingi. Sikuweza kumwacha Mungu bila kujali lolote.

Ndugu, ulishindaje mateso kama haya? Wakati mmoja, katika mkutano mmoja, tulisoma maneno haya ya Mungu: “Natamani tu kwamba mtatoa nguvu zenu zote Kwangu kwa mioyo yenu yote na akili zenu zote na kadri ya uwezo wenu. Kama leo au kesho, kama wewe ni mtu ambaye anatoa huduma kwa ajili Yangu au mtu anayepata baraka, nyote mnapaswa kutumia sehemu ya nguvu zote kwa ajili ya ufalme Wangu. Huu ni wajibu ambao watu wote walioumbwa wanapaswa kutekeleza, nao unapaswa kufanywa na kutekelezwa kwa njia hii. Nitavihamasisha vitu vyote vitoe huduma kwa uzuri wa ufalme Wangu ili ufanywe mpya daima, na nyumba Yangu ifanywe kuwa yenye mpangilio mzuri na yenye umoja. Hakuna mtu anayeruhusiwa kunipinga Mimi, na anapaswa kupitia hukumu na kulaaniwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 100). Kiongozi wa kanisa wa wakati huo pia alishiriki ushirika kiasi uliotoka kwa walio juu. “Watu wengi huhisi kuwa ni aibu kuwa mtendaji huduma, lakini hiyo ni makosa kabisa. Kwamba tunaweza kumtumikia Mungu leo ni jambo lililopangwa na Yeye kabla, na zaidi ya hiyo, tulichaguliwa na Mungu ili tufanye hivyo. Kwa kweli, kumtumikia Mungu mwenye mamlaka na uweza ni jambo adhimu kabisa! Sisi ni wanadamu ambao wamepotoshwa sana na Shetani, na mbele za Mungu, sote ni viumbe wadogo sana tu. Ni nani anayefaa kumtumikia Mungu? Kati ya wanadamu wote, sisi ndio tuliochaguliwa na Mungu ili tumtumikie. Tumepata mengi, na kwa kweli huku ni kuinuliwa sana na Mungu. Kauli hii ni nzuri zaidi, na ikiwa huwezi kuielewa, basi una kiburi kupita kiasi. Hebu niwaambie kwa kweli: Mungu ameturuhusu—sisi ambao hatuna ubinadamu kabisa—tumtumikie. Hata hivyo, mnajua Amepitia fedheha kiasi gani? Yeye hukabiliwa kila siku na watu wapotovu kama sisi, lakini ni nani kati yetu aliyewahi kufikiria fedheha kubwa ambayo Mungu amepitia? Sisi humwasi na kumpinga kila wakati, tunamhukumu kwa fikira na mawazo yetu wenyewe, na tumevunja moyo Wake. Je, Mungu amepitia uchungu kiasi gani? Nisikizeni ninaposema kwamba tumejawa na tabia potovu, na tunapomtumikia, sisi hushindwa kufikia matakwa Yake. Baada ya tabia kama hii, hatufai hata kumtolea Mungu huduma. Tunawezaje kufaa kuwa watu Wake?” Nilizinduka niliposikia hayo. Mungu ndiye Muumba na Yeye ndiye mkubwa kabisa. Mimi ni duni na mdogo sana, kwa hivyo kuweza kumtumikia ni ukuzaji na wema ya Mungu. Lakini sikujua utambulisho au hadhi yangu mwenyewe nikiamini kwamba kuwa mtendaji huduma kulikuwa kwa hali ya chini na sikuwa tayari kumfanyia Mungu huduma. Nilikuwa na kiburi sana na sikuwa na mantiki. Ninapokumbuka hayo, ingawa nilikuwa nimefuatilia kwa hamu, nikijitolea na kujitumia, nilifanya hayo yote ili kupata baraka na kufurahia baraka za ufalme wa mbinguni. Nilitiwa hamasa sana niliposoma maneno ya Mungu ya ahadi na baraka kwa mwanadamu, na niliendelea kujitahidi licha ya mateso ya CCP. Lakini nilisoma maneno ya Mungu yaliyosema kwamba tulikuwa watendaji huduma ambao watatupwa katika shimo lisilokuwa na mwisho, nilianza kulalamika na kumlaumu Mungu na hata nikanuia kumsaliti na kumwacha Mungu. Je, nilikuwaje muumini wa kweli? Yale niliyotoa na kutumia yalikuwa yametiwa madoa na nia zangu na uchafu wangu. Nilifanya hivyo kupata baraka, nilikuwa nikijaribu kumdanganya Mungu na kufanya biashara na Mungu. Nilikuwa mbinafsi sana na nilistahili dharau. Nilikuwa nimefurahia neema na baraka nyingi za Mungu, riziki na unyunyiziaji wa maneno Yake, lakini nilitaka kumsaliti mara nilipokosa kuona baraka zangu ndani ya hayo. Sikuwa na dhamiri au mantiki yoyote hata kidogo. Nilijuta na kujilaumu sana nilipofikiria hayo. Nilikuwa mwana wa joka kubwa jekundu. Nilikuwa wa Shetani na sikuwa wa nyumba ya Mungu na hata imani yangu ilitiwa hamasa na kubarikiwa. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, na tabia Yake haivumilii kosa lolote. Kulingana na tabia na mtazamo wangu kwa Mungu, sikustahili hata kuwa mtendaji huduma. Nilipaswa kuhukumiwa na kutupwa kuzimuni na Mungu zamani sana. Mungu hakuwa Akiniadhibu, lakini Alikuwa akiniruhusu niishi kila wakati kusudi nipate nafasi ya kusikia maneno Yake, kukubali riziki Yake ya maisha na kumhudumia Mungu Aliye juu zaidi. Huku kulikuwa kuinuliwa kwa pekee na nilipaswa kumshukuru Mungu. Je, nilikuwa na haki gani ya kulalamika? Nilijua kwamba sikuwa na budi kumhudumia Mungu vizuri!

Mwishoni mwa Novemba, tulipokea maneno zaidi mapya ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo, Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na maafa makubwa; ilhali kila mtu anaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki. Bila shaka Sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu, bali nitawaruhusu tu wapokee neema Yangu. Maana Nimesema kuwa nitawaadhibu watenda dhambi wote, na kwamba wale wanaotekeleza matendo mema watapata starehe yakinifu iliyokirimiwa nami, huu ni ufunuo kwamba Mimi ni Mungu wa haki na uaminifu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 120). Niliona kwamba Mungu hakuwa Ametutelekeza hata kidogo na hakuwa Akituadhibu kwa sababu tulikuwa wana wa joka kubwa jekundu. Bado Mungu alikuwa Akituruhusu tuwe watendaji huduma waaminifu kwa ajili Yake na tumsifu duniani. Jambo hili lilinipa hisia ya ukunjufu na nilichangamka sana. Nilihisi kwa kweli kwamba kuweza kumhudumia Mungu kulikuwa kutukuzwa na Yeye na ilikuwa baraka. Wakati huo, tuliimba wimbo uitwao “Ni Bahati Yetu Nzuri Kumhudumia Mungu” katika kila mkutano. Tunaona jinsi ambavyo tumepotoshwa sana kupitia ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu. Tukiwa tumejawa na azimio na tamaa ya kubarikiwa, tunawezaje kustahili kuishi mbele za Mungu? Hatustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni; kumhudumia Mungu tayari ni kukuzwa na Yeye. Oh! Kwa neema ya Mungu tunatoa huduma na kutoa huduma ni bahati yetu nzuri. Bila kujali iwapo nitapokea baraka au nitapitia taabu, niko tayari kutoa huduma hadi mwisho. Umetoholewa kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Mara tulipofurahia kuwa watendaji huduma na tukawa tayari kumhudumia Mungu, Mwenyezi Mungu alitamka maneno mapya. Hii ilikuwa Februari 20, 1992. Alituinua kuwa watu wa ufalme na Akatamatisha majaribu ya watendaji huduma. “Hali sio kama ilivyokuwa wakati fulani, na kazi Yangu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza. Hilo likiwa hivyo, kutakuwa na njia mpya: Wale wanaolisoma neno Langu na kulikubali kama uzima wao kabisa ndio watu wa ufalme Wangu. Kwa vile wako katika ufalme Wangu, wao ni watu Wangu katika ufalme. Kwa sababu wanaongozwa na maneno Yangu, ingawa wanatajwa kama watu Wangu, jina hili si la chini ya kuitwa ‘wana’ Wangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1). Nilipoona kwamba Mungu alikuwa Amewageuza watendaji huduma kuwa watu Wake wa Enzi ya Ufalme, nilihisi furaha iliyochanganyika na majuto na kujilaumu. Nilijutia kwamba nilikuwa hasi, dhaifu, na sikuwa na matumaini wakati wa majaribu ya watendaji huduma, na hata nilikuwa nimemlalamikia Mungu, nikimwelewa visivyo na kumlaumu. Sikuwa tayari kuwa mtendaji huduma Wake. Sikuwa na moyo wa ibada na utiifu kwa Mungu hata kidogo. Jambo hili liliniacha nikihisi majuto sana na kwamba nilikuwa na deni la Mungu. Nilifurahi kwa sababu sisi kama wana wa joka kubwa jekundu, waasi na wapotovu sana, kwa sababu tu hatukukata tamaa wakati wa majaribu, Mungu alituinua kuwa watu wa ufalme, kuwa washiriki wa nyumba Yake. Niliweza kuhisi upendo mkubwa wa Mungu kwetu, na shukrani na sifa za Mungu zilijaa moyoni mwangu.

Baada ya kupitia majaribu hayo, niliona hekima ya ajabu katika kazi ya Mungu. Yeye huhukumu, huadibu na hata kuwalaani watu kwa maneno Yake na ingawa ni makali na hututia uchungu na kutusikitisha, yote ni ya kututakasa na kutubadilisha. Ingawa nilikuwa nimesafishwa kupitia maneno ya Mungu, nilikuwa nimeona tabia Yake yenye haki. Yeye huchukizwa na nia zetu na uchafu wetu na Yeye huchukizwa na imani iliyotiwa hamasa na baraka. Baada ya tukio hili, mtazamo wangu juu ya imani ulibadilika kidogo. Niliacha kufuatilia kwa dhati baraka na kuingia katika ufalme wa mbinguni, lakini nilihisi kwamba kuwa mtendaji huduma anayemtumikia Muumba ni kuinuliwa na Mungu na ni baraka kwangu. Kunanifanya nijivunie na nihisi kwamba nimeheshimiwa!

Inayofuata: 2. Katikati ya Jaribu la Kifo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

68. Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp