33 Sifu Ushindi wa Mwenyezi Mungu

Mwimbie Mwenyezi Mungu wimbo wa sifa.

Acha sauti ya wimbo iruke kutoka kila moyo.

Sifu Mungu kuwa mwili hapa ulimwenguni,

kuonyesha ukweli kumtakasa na kumwokoa mwanadamu.

Tunasikia sauti Yake na kumwona Akionekana.

Kwa mioyo iliyojaa furaha, tunarudi nyumbani kwa Mungu.

Tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunafurahia kazi ya Roho.

Tunaelewa ukweli na mioyo yetu iko huru.

Maneno ya Mungu: ukweli wa pekee, njia ya uzima wa milele.

Tunafurahi kwa ajili ya maisha mapya ana kwa ana na Mungu.

Sayuni inashangilia, kwani ufalme wa Mungu umekuja duniani.

Tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa ushindi Wake,

kwa ushindi Wake, kwa ushindi Wake.

Mwimbie Mwenyezi Mungu wimbo wa sifa.

Acha sauti ya wimbo iimbe upendo wetu Kwake.

Sifu hukumu Yake ya haki kututakasa na kutuokoa.

Kukubali hukumu ya neno Lake, tunakuwa wanadamu wapya.

Tunateseka kwa ajili ya usafishaji na majaribio,

lakini tabia zetu potovu zimebadilika.

Tunatenda ukweli na kuishi katika mwanga.

Tukikombolewa na kuwa huru, tunampenda Mungu kwa uaminifu.

Watu wote wanamtii Mungu, wakimsifu pamoja.

Kwani tunamjua mwenyezi Mungu, tuna mioyo inayomcha Mungu.

Tumemtupa Shetani na kupata wokovu wa Mungu.

Tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa ushindi Wake,

kwa ushindi Wake, kwa ushindi Wake, kwa ushindi Wake.

Mwimbie Mwenyezi Mungu wimbo wa sifa.

Acha sauti ya wimbo iutikise ulimwengu mzima.

Yasifu maneno ya Mungu yanayoonyesha uweza Wake,

yanayomshinda Shetani na kufanyiza kundi la washindi,

yanayoenea katika mataifa na nchi zote.

Ufalme wa Kristo wenye haki unaonekana.

Maneno ya Mungu yanashawishi duniani.

Mataifa yote, watu wote wanamwabudu Mungu pamoja.

Watu wote wa Mungu wanafurahia baraka za mbinguni duniani.

Vitu vyote vinashangilia, kwani kazi kubwa ya Mungu imekamilika.

Utukufu Wake unang'aa sana katika anga nzima.

Hiyo ndiyo maana mbingu na dunia zinaonekana mpya kabisa.

Tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa ushindi Wake, kwa ushindi Wake.

Mwimbie Mwenyezi Mungu wimbo wa sifa.

Vitu vyote vinafurahia pamoja, Mungu amerudi kwa ushindi.

Mwimbie Mwenyezi Mungu wimbo wa sifa.

Vitu vyote vinafurahia pamoja, Mungu amerudi kwa ushindi.

Iliyotangulia: 32 Tunakuabudu, Mwenyezi Mungu Mwenye Mwili

Inayofuata: 34 Chezeni Mkizunguka Kiti cha Enzi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp