899 Nia Ya Mungu ya Kumwokoa Mwanadamu Haitabadilika

1 Ingawa watu wana baadhi ya uelewa wa tabia mbalimbali za Mungu, kipengele cha kile anacho Mungu na alicho na kazi Mungu anafanya, wingi wa uelewa huu hauendi mbali na kusoma maneno kwenye ukurasa, ama kuyaelewa katika kanuni, ama tu kuyafikiria. Yale wanayoyakosa sana watu ni uelewa na mtazamo wa kweli unaotoka kwa uzoefu halisi. Ingawa Mungu hutumia njia mbalimbali kuamsha mioyo ya wanadamu, bado kuna njia ndefu ya kutembea kabla mioyo ya wanadamu iamshwe kikamilifu.

2 Sitaki kumwona yeyote akihisi kana kwamba Mungu amemwacha nje kwa baridi, kwamba Mungu amemwacha ama amempuuza. Ningetaka tu kuona kila mtu katika njia ya kufuatilia ukweli na kutafuta kumwelewa Mungu, akiendelea mbele kwa ujasiri na utashi usiosita, bila wasiwasi, bila kubeba mizigo. Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka aje ama vile ulivyotenda dhambi, usiwache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Nyakati zote, Mungu hushikilia wokovu wa mwanadamu moyoni Mwake; hili halibadiliki kamwe. Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 898 Mungu Anafarijiwa Watu Wanapoyaacha Makosa Yao

Inayofuata: 900 Mungu Amwokoa Mwanadamu kwa Kiwango cha Juu Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp