52 Chezeni Mkizunguka Kiti cha Enzi

1

Kristo wa siku za mwisho sasa Ameonekana, ufalme wa mbinguni umekuja duniani.

Mungu mwenye mwili Ananena ukweli, akifungua kitabu, hili ndilo Neno linaloonekana katika mwili.


Maneno yote ya Mungu yana mamlaka mengi, yanawashinda watu wote, yakionyesha uadhama Wake.


Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!

2

Tuliisikia sauti ya Mungu na tumeinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi, kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo.

Na tunaweza kufurahia maneno Yake kila siku, kuishi mbele za Mungu ni furaha kweli.


Tumeepuka giza na tumepata uhuru, kwa hivyo tunapocheza zaidi, ndivyo tunavyofurahia zaidi.


Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!

3

Tunakuja mbele za Mungu, tunakuja mbele za Mungu, na kukubali mafunzo ya ufalme.

Kupitia hukumu, usafishaji wa maneno ya Mungu, tabia zetu zinabadilishwa.


Sasa tumepata wokovu wote wa Mungu, na tunafurahia upendo Wake, hii ni neema ya Mungu.


Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!

4

Mbingu na dunia furahini! Furahini!

Mwezi unatabasamu, nyota zinacheza, na ndege wote mitini wanaimba.

Sasa tunaishi maisha mapya kwa shukrani isiyo na mwisho.


Tunatekeleza wajibu wetu wote kwa uaminifu, tukitafuta ukweli na kumshuhudia Mungu.


Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!


Ufalme wa haki umefika, maneno ya Mungu yatawala.

Tumepitia ukandamizaji, dhiki, tunalichukia joka kubwa jekundu kwa mioyo yetu yote.

Tumeamua kumfuata Kristo kwa uthabiti daima.

Maneno ya Mungu yameushinda ulimwengu wote.

Mataifa yanamwabudu, tunaimba sifa Zake.

5

Mungu amefanyiza kikundi cha washindi.

Kazi kubwa ya Mungu imefanikiwa kabisa.

Mapenzi ya Mungu yamefanywa hapa duniani kama mbinguni.

Amemwaibisha kabisa Shetani ibilisi.


Watu wote wa Mungu wanamshuhudia.

Sasa ufalme Wake umetimia kikamilifu duniani.


Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!

Msifu, sifa zote Kwake, wote wanacheza kwa furaha!

Na tunacheza tukizunguka kiti Chake cha enzi!

Wote wanacheza kwa furaha!

Iliyotangulia: 51 Ufalme wa Mungu Umetimizwa

Inayofuata: 53 Yasifu Maisha Mapya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki