697 Faida za Kumwamini Mungu wa Vitendo ni Kubwa

1 Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu.

2 Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata.

3 Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa.

Umetoholewa kutoka katika “Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 696 Lazima Ujue Jinsi ya Kupitia Kazi ya Mungu

Inayofuata: 698 Hukumu ya Mungu Hutupa Uzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp