254 Tunakuabudu, Mwenyezi Mungu Mwenye Mwili

1 Mungu amekuwa mwili katika siku za mwisho kuonyesha ukweli, na kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Kama upanga mkali, maneno Yake huichoma mioyo yetu na roho zetu, yakituonyesha ukweli wa upotoshaji mkubwa wa mwanadamu na Shetani. Sisi ni wenye kiburi, majivuno, hila, wadanganyifu, wabinafsi, na wenye tamaa kiasili. Dhamiri, hisia zetu na hadhi yetu zimepotea, hatuna sura yoyote ya mwanadamu. Tunainamisha vichwa ardhini, tukijawa na majuto, na tunakiri na kutubu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu, maneno Yako hutushinda na kututakasa. Kwa kuelewa ukweli, tunaacha tabia zetu za kishetani. Asante kwa upendo Wako! Unatuokoa kutoka katika ushawishi wa Shetani, tunakuabudu!

2 Mungu mwenye mwili amepata aibu kubwa ili kumwokoa mwanadamu. Katika kimya, Amestahimili mateso na ugumu mwingi, dhihaka na kashfa nyingi. Aliyejificha na mpole, Anawanyunyizia, kuwaruzuku na kuwaongoza watu Wake Yeye mwenyewe. Wasiwasi na wahaka mwingi Amepitia kwa ajili ya ukuaji wetu katika maisha. Anavumilia uasi wetu, na Anafanya bidii kutuokoa. Upendo na tabia ya Mungu yenye haki vimekita mizizi mioyoni mwetu. Mwenyezi Mungu, kujificha na upole Wako ni mzuri sana! Maneno Yako yamekuwa maisha yetu, asante kwa upendo Wako! Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunakusifu na kukuabudu!

3 Uweza na hekima ya Mungu vinazidi mbingu na haueleweki kwa wote. Yeye hutumia joka kubwa jekundu kama foili kutumikia ukamilishaji Wake wa watu Wake. Baada ya kupitia shida, mateso, na uchungu, tunaona uso wa kweli wa mfalme pepo. Tunachukia CCP ya kishetani, na tutakuwa waaminifu kwa Mungu hadi kifo na kumshuhudia. Katika enzi hii ya uovu, tuna hakika kuwa Kristo ndiye ukweli, njia na uzima. Tunafuata nyayo za Mwanakondoo na tutashuhudia tabia ya Mungu yenye haki na takatifu milele. Mwenyezi Mungu, kazi Yako ni ya busara, yenye uweza, na ya kushangaza. Umefanyiza kundi la washindi, Umemshinda Shetani na kupata utukufu. Wewe ndiye ukweli, njia na uzima, na tutakusifu milele!

Iliyotangulia: 253 Mungu Amengoja Kwa Muda Mrefu Sana

Inayofuata: 255 Nimeamua Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki