586 Poteza Nafasi na Utajuta Milele

1 Kula na kunywa maneno ya Mungu, kufanya maombi, kukubali mzigo wa Mungu, kukubali Anachokuaminia—haya yote ni kwa ajili ya kuwa na njia mbele yako. Kadiri unavyozidi kuwa na mzigo mwingi wa agizo la Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako kufanywa mtimilifu na Mungu. Wengine hawako tayari kushirikiana katika kumtumikia Mungu hata wakati ambapo wameshurutishwa; hao ni watu wavivu ambao hutamani kufurahia faraja. Kadiri unavyotakiwa kushirikiana katika kumhudumia Mungu, ndivyo utakavyopata uzoefu zaidi. Kwa sababu una mizigo zaidi na una uzoefu zaidi, utakuwa na nafasi zaidi ya kufanywa mtimilifu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kumhudumia Mungu kwa uaminifu utazingatia mzigo wa Mungu, na kwa njia hii utakuwa na nafasi nyingi zaidi za kufanywa mtimilifu na Mungu. Kundi kama hili la watu linafanywa kamilifu na Mungu wakati huu. Kadiri Roho Mtakatifu anavyokugusa hisia, ndivyo utakavyotenga muda zaidi wa kuzingatia mzigo wa Mungu, ndivyo utakavyofanywa mtimilifu na Mungu zaidi, ndivyo Mungu atakavyokupata zaidi, na mwishowe, utakuwa mtu anayetumiwa na Mungu.

2 Kwa hivyo mnapaswa kuwa wazingatifu wa mzigo wa Mungu sasa. Hupaswi kusubiri tabia ya Mungu yenye haki ifunuliwe kwa watu wote kabla ya wewe kuwa mzingatifu wa mzigo wa Mungu. Je, si muda utakuwa umeshapita wakati huo? Sasa ni nafasi nzuri ya kufanywa mtimilifu na Mungu. Ukiruhusu nafasi hii ipotee, utajuta katika maisha yako yote, kama vile Musa alivyoshindwa kuingia katika nchi nzuri ya Kanani na alijuta katika maisha yake yote, akifa kwa majuto. Mara tu Mungu ameifichua tabia Yake yenye hakikwa watu wote, utajawa na majuto. Hata kama Mungu hakuadibu, utajiadibu kutokana na majuto yako mwenyewe. Sasa ni fursa nzuri ya kufanywa mtimilifu—huu ni wakati mzuri. Usipotafuta kwa bidii kufanywa mtimilifu na Mungu, mara tu kazi Yake itakapokuwa imekamilika utakuwa umechelewa—utakuwa umekosa fursa hii. Bila kujali jinsi matarajio yako yalivyo makuu, ikiwa Mungu hatendi kazi tena, bila kujali jitihada unazotia, hutaweza kamwe kufanywa mtimilifu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 585 Stahimili Mzigo Zaidi ili Ukamilishwe kwa Urahisi Zaidi na Mungu

Inayofuata: 587 Wamebarikiwa Wale Wanaojitumia Kweli kwa Ajili ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp