304 Daima Natamani Sana Upendo wa Mungu

1

Ni wakati tu maneno ya hukumu ya Mungu yaliniamsha

ndipo niligundua nilimwamini Mungu na dhana zangu.

Kupuuza maneno Yake na kutoyadhukuru mapenzi Yake

kungeacha majuto moyoni mwangu.

Kushughulikiwa, kupogolewa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara,

kila wakati mimi hulalamika na kubishana moyoni mwangu.

Kujaribiwa na kusafishwa mara kwa mara,

kila wakati nilijaribu kukimbia, ili nijitenge na Mungu.

Nachukia kwamba mimi ni mpotovu sana

na nimeshindwa kuyaridhisha malengo ya bidii ya Mungu.

Ee Mungu! Maneno Yako ya hukumu na ufunuo yameniamsha kutoka ndotoni mwangu.

2

Nimepoteza wakati mwingi;

Nimemwamini Mungu kwa miaka na bado nimeshindwa kuelewa ukweli.

Vyote vya zamani vinaangaza mbele ya macho yangu,

hakuna chochote isipokuwa upinzani na kutotii.

Nilimwamini Mungu lakini sikupitia hukumu na kuadibu Kwake,

na majuto yangu kweli yamechelewa sana.

Si ajabu tabia yangu ya maisha haijabadilika,

na mimi huwa na matokeo duni katika kila wajibu ninaofanya.

Nahisi majuto sana, na nina deni kubwa la Mungu.

Nautamani sana upendo wa Mungu na najichukia zaidi kwa kukosa utu kwangu.

Hukumu ya Mungu inawapa watu uzima;

nitainuka na kutafuta kwa kusudi, kutozurura tena bila malengo.

Nitafuatilia ukweli na kupata uzima;

nitatimiza wajibu wangu vizuri kulipa upendo wa Mungu.

Iliyotangulia: 303 Nampa Mungu Moyo Wangu Mwaminifu

Inayofuata: 305 Mwenyezi Mungu Wetu Mpendwa

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki