189 Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

1 Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu.

2 Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 188 Tamanio la Pekee la Mungu Duniani

Inayofuata: 190 Unaijua Kazi ya Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp