151 Kazi ya Mwili na Roho ni Sawa katika Kiini
1 Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.
2 Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa.
3 Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote.
4 Mungu ni Roho na Anaweza kufanya kazi ya wokovu, kama vile Mungu Anavyoweza kuwa mwanadamu. Hata hivyo, Mungu Mwenyewe Anafanya kazi Yake Mwenyewe; Yeye wala hazuii wala kuathiri, wala kufanya kazi inayozipinganisha pande zote mbili, kwa kuwa kiini cha kazi iliyofanywa na Roho na mwili yote ni sawa. Iwe ni Roho au mwili, vyote hufanya kazi kutimiza nia moja na kusimamia kazi sawa. Ingawa Roho na mwili huwa na sifa mbili tofauti, dutu yao ni sawa; zote zina dutu ya Mungu Mwenyewe, na utambulisho wa Mungu Mwenyewe.
Umetoholewa kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili