233 Kama ni Kazi ya Roho Mtakatifu, Unapaswa Kuikubali
1 Wayahudi wa wakati huo wote walisoma kutoka Agano la Kale na walijua unabii wa Isaya kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa horini. Mbona basi, na maarifa haya, bado walimtesa Yesu? Hii siyo kwa sababu ya asili yao ya kuasi na kutojua kazi ya Roho Mtakatifu? Wakati huo, Mafarisayo waliamini kwamba kazi ya Yesu ilikuwa tofauti na ile waliyoijua ya mtoto mchanga wa kiume aliyetabiriwa; mwanadamu wa leo anamkataa Mungu kwa sababu kazi ya Mungu mwenye mwili haikubaliani na Biblia. Si kiini cha uasi wao dhidi ya Mungu ni moja na sawa? Unaweza kuwa yule ambaye anakubali tu bila swali kazi yote ya Roho Mtakatifu? Kama ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi ni mkondo sawa, na unastahili kuukubali bila wasiwasi wowote hata kidogo; hufai ya kuchukua na kuchagua kipi cha kukubali.
2 Ukipata ufahamu zaidi kutoka kwa Mungu na kujitahadhari zaidi Kwake, basi hili silo tendo lisilohitajika? Huna haja kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwa Biblia; iwapo ni ya Roho Mtakatifu huna budi kuikubali, kwani unamwamini Mungu kumfuata Mungu, sio kumchunguza. Hupaswi kutafuta ushuhuda zaidi ili Nionyeshe kwamba Mimi ni Mungu wako. Badala yake, unapaswa kupambanua kama Nina faida kwako; hiyo ndiyo muhimu. Hata kama umegundua ushuhuda usiopingika ndani ya Biblia, haiwezi kukuleta kikamilifu mbele Yangu. Wewe ndiye mmoja anayeishi ndani ya mipaka ya Biblia, na sio mbele Yangu; Biblia haiwezi kukusaidia kunijua, wala haiwezi kuimarisha upendo wako Kwangu.
3 Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu. Hasa, haingekuwa tendo la imani ya uwongo kutafuta ndani ya Biblia kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Nini unaweza kupambanua tu kwa kushika Biblia kwa mikono yako? Uwe mkalimani wa Biblia ama mhubiri, nani anaweza kujua mbeleni kazi ya leo?
Umetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili