120 Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho Katika Taifa la Joka Kubwa Jekundu
1 Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake.
2 Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya.
3 Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote” katika Neno Laonekana katika Mwili