III. Maneno Juu ya Kushuhudia Kuonekana Kwa na Kazi ya Mungu

165. Sifa zimekuja Sayuni na makazi ya Mungu yameonekana. Jina tukufu takatifu linasifiwa na watu wote, na linaenea. Ah, Mwenyezi Mungu! Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa, na Ameinuka juu ya Mlima Sayuni ulio na uadhimu na mzuri kabisa katika ulimwengu mzima …

Mwenyezi Mungu! Sisi tunakushangilia; tunacheza ngoma na kuimba. Kweli Wewe ni Mkombozi wetu, Mfalme mkubwa wa ulimwengu! Umetengeneza kundi la washindi, na kutimiza mpango wa usimamizi wa Mungu. Watu wote wataelekea kwa mlima huu. Watu wote watapiga magoti mbele ya kiti cha enzi! Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli na wa pekee na Unastahili utukufu na heshima. Utukufu wote, sifa, na mamlaka yawe kwa kiti cha enzi! Chemchemi ya maisha hutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi, ikinyunyizia na kuwalisha watu wa Mungu. Maisha hubadilika kila siku; nuru mpya na ufunuo hutufuata sisi, daima vikitupatia utambuzi mpya wa Mungu. Kuwa yakini kwa Mungu kupitia uzoefu; maneno Yake daima huonekana, yakionekana kwa wale ambao ni waadilifu. Kwa kweli sisi tumebarikiwa kupita kiasi! Kuwa ana kwa ana na Mungu kila siku, kuwasiliana na Mungu katika kila kitu, na kumpa Mungu mamlaka katika kila kitu. Kwa umakini sisi tunatafakari neno la Mungu, mioyo yetu ni mitulivu katika Mungu, na hivyo sisi tunakuja mbele za Mungu ambapo tunapokea nuru Yake. Katika maisha yetu ya kila siku, matendo, maneno, mawazo, na fikira, tunaishi ndani ya neno la Mungu, na daima tunao utambuzi. Neno la Mungu linapenya; mambo yaliyofichwa ndani kwa ghafula huonekana moja baada ya nyingine. Ushirika na Mungu hauwezi kucheleweshwa; mawazo na fikira huonyeshwa kwa uwazi na Mungu. Kwa kila muda tunaishi mbele ya kiti cha Kristo ambapo sisi hupitia hukumu. Kila eneo la miili yetu linamilikiwa na Shetani. Leo, hekalu la Mungu lazima litakaswe ili Apate ukuu Wake tena. Ili kumilikiwa kabisa na Mungu, ni lazima tupitie vita vya kufa kupona. Ni wakati tu nafsi zetu za zamani zimesulubiwa ndipo maisha ya kufufuliwa ya Kristo yatatawala kwa ukuu.

Sasa Roho Mtakatifu Anafanya shambulio katika kila pembe yetu ili kuzindua vita vya kurudisha! Mradi tuko tayari kujinyima wenyewe na radhi kushirikiana na Mungu, Mungu kwa wakati wowote Ataangaza na kututakasa ndani zetu, na kurudisha upya yale ambayo Shetani amemiliki, ili tuweze kukamilishwa na Mungu haraka iwezekanavyo. Usipoteze muda, na daima uishi ndani ya neno la Mungu. Jengwa pamoja na watakatifu, letwa katika ufalme, na uingie katika utukufu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 1

166. Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!

Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa. Umefungua dirisha la mbinguni na tumeona siri za dunia ya kiroho. Maneno Yako matakatifu yametujaza sisi, na Umetuokoa kutoka kwa ubinadamu potovu uletwao na Shetani. Hii ni kazi Yako kuu na rehema Yako kubwa sana. Sisi ni mashahidi Wako!

Umekuwa mnyenyekevu na kufichika katika kimya kwa muda mrefu. Wewe umepitia ufufuo na mateso ya msalaba; Wewe umejua furaha na huzuni ya maisha ya binadamu pamoja na mateso na dhiki. Wewe umepitia na kuonja maumivu ya dunia ya binadamu, na Wewe umetelekezwa na enzi. Mungu mwenye mwili ni Mungu Mwenyewe. Wewe umetuokoa kutoka kwa lundo la samadi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu na umetushikilia kwa mkono Wako wa kulia; neema Yako imepeanwa huru kwetu sisi. Unafanya juhudi za ukarimu kuingiza maisha Yako ndani yetu; gharama Ulilolipa kwa damu Yako, jasho, na machozi imekuwa katika watakatifu. Sisi ndio matokeo ya[a] juhudi Zako zenye bidii, sisi ndio gharama Unayolipa.

Eh, Mwenyezi Mungu! Ni kwa sababu ya upendo Wako na rehema, haki Yako na uadhama, utakatifu Wako na unyenyekevu kwamba watu wote wanapaswa kutii mbele Yako na kukuabudu Wewe daima dawamu.

Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tumemjua Mungu wa ukweli wa vitendo, tumetembea ndani ya maneno Yake, tumetambua shughuli zetu na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kila kitu tunachoweza kutumia kila rasilmali yetu kwa ajili ya kanisa. Tunapaswa kuchukua kila muda kuwa kimya mbele Yako na kutilia maanani kazi ya Roho Mtakatifu ili mapenzi Yako yasizuiwe ndani yetu. Miongoni mwa watakatifu kuna upendano, na nguvu za wengine zitafidia dosari za wengine. Tembea katika roho kila muda na upate nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu; fahamu ukweli na uuweke katika vitendo mara moja; kuwa sawa na nuru mpya na kufuata nyayo za Mungu.

Shirikiana kwa utendaji na Mungu; kumruhusu Yeye Achukue uongozi ni kutembea pamoja naye. Mawazo yetu yote wenyewe, fikira na maoni, mitego yetu yote ya kimwili, hutokomea kama moshi. Tunamruhusu Mungu Atawale katika roho zetu, kutembea naye na kupata uwezo unaozidi sana wa mwanadamu, kushinda ulimwengu, na roho zetu huruka kwa uhuru na kufikia ufunguliwaji; haya ni matokeo ya Mwenyezi Mungu kuwa Mfalme. Tunawezaje kukosa kucheza ngoma na kuimba sifa, kutoa sifa zetu, na kutoa nyimbo mpya?

Kweli kuna njia nyingi za kumsifu Mungu: kuliita jina Lake, kukaribia karibu na Yeye, kumfikiria Yeye, kuomba kwa kusoma, na kuwa na ushirika, kuzingatia, kutafakari, na sala, na pia kuna nyimbo za sifa. Katika aina hizi za sifa kuna raha, na kuna kupakwa mafuta; kuna nguvu katika sifa na pia kuna mzigo. Kuna imani katika sifa, na kuna utambuzi mpya.

Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake. Kanisa la Filadelfia limechukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu na linajidhihirisha katika utukufu wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 2

167. Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Sayuni na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai ndani yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa. Hukumu ya aina hiyo itakuwa papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Moto ya ghadhabu ya Mungu itachoma makosa yao ya kuchukiza na janga litawafikia wakati wowote; wao hawatajua njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao, na watajiletea maangamizi.

Wana wa ushindi wapendwa wa Mungu kwa hakika watakaa katika Uyahudi, kamwe wasiiache. Umati utasikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa uangalifu matendo Yake, na sauti zao za sifa Kwake kamwe hazitakoma. Mungu mmoja wa kweli Ameonekana! Tutakuwa na uhakika juu Yake katika roho na kumfuata kwa karibu na kukazana kusonga mbele bila kusita. Mwisho wa dunia unajitokeza mbele yetu; maisha sahihi ya kanisa pamoja na watu, shughuli, na mambo ambayo yanatuzunguka sasa hata yanayafanya mafunzo yetu yawe makali zaidi. Acha tufanye hima kuchukua tena mioyo yetu ambayo inapenda dunia sana! Acha tufanye hima kuchukua tena maono yetu yaliyozibwa! Hatutasonga mbele zaidi tusije tukazidi mipaka na tutashikilia ndimi zetu ili tuweze kuishi kwa kufuata neno la Mungu, na tena hatutazozana juu ya faida zetu wenyewe na hasara. Acha upendo wako wa dunia ya kawaida na utajiri! Ah, jiwekeni huru kutoka kwake—upendo wenu wa kuning’nia kwa waume zenu na mabinti na wana wenu! Acha maoni yako na upendeleo! Amka, kwa sababu muda ni mfupi! Iruhusu roho yako iangalie juu, angalia juu na umruhusu Mungu Achukue uongozi. Usijiruhusu kuwa kama mke wa Lutu. Kutelekezwa ni jambo la kusikitisha sana! Ni la kusikitisha kweli! Amka!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 3

168. Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka kwenye mikondo yao, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.

Leo hii ni kwa sababu ya uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kabla kwamba Ametuokoa kutoka kukamatwa na Shetani. Yeye kweli ni Mkombozi wetu. Maisha ya kufufuliwa ya Kristo milele yametugusa ndani yetu, hivi sisi tumejaliwa kuhusiana na maisha ya Mungu, tunaweza kuwa naye ana kwa ana, kumla Yeye, kumnywa Yeye, na kumfurahia Yeye. Huku ni kujitolea kwa Mungu kwa bidi na kusio na ubinafsi.

Majira yanakuja na ku kuenda, yakipitia upepo na jalidi, yakikumbana na taabu, mateso na majonzi mengi sana ya maisha, kukataliwa na kukashifiwa duniani, serikali kusingizia mashtaka, hakuna upungufu wa imani ya Mungu wala kusudi. Kwa ukamilifu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, ili usimamizi wa Mungu na mpango utimizwe, Yeye huweka maisha Yake Mwenyewe kando. Kwa ajili ya watu Wake wote, huwa Hapuri juhudi yoyote, kwa uangalifu Akilisha na kunyunyizia. Haidhuru kiasi cha ujinga, tu wagumu kiasi kipi, tunahitaji tu kutii mbele Yake, na maisha ya kufufuka kwa Kristo yatabadilisha asili yetu ya zamani…. Kwa wana hawa wazaliwa wa kwanza, Yeye hufanya kazi bila kuchoka, huachilia chakula na usingizi. Ni mchana na usiku ngapi, ni kupitia joto ngapi kali, na baridi ya kuganda, Yeye hutazama kwa moyo mmoja katika Sayuni.

Ulimwengu, nyumba, kazi vimeachiliwa kabisa, bila kusita, bila raha za kidunia kumgusa…. Maneno kutoka kinywa Chake yanatupiga kwa ndani, yakifunua mambo yaliofichwa kwenye kina cha mioyo yetu. Ni vipi haturidhishwi? Kila sentensi inayotoka katika kinywa Chake inatendeka wakati wowote kwetu. Kila kitendo chetu, hadharani na faraghani, hakuna ambacho Yeye hakijui, hakuna Asichokijua. Kwa kweli vyote vitafichuliwa mbele Yake, licha ya mipango yetu wenyewe na matayarisho.

Tukiwa tumeketi mbele Yake, roho zetu hufurahia, kustareheshwa na tulivu, daima kuhisi tupu ndani, kwa kweli kuwiwa kwa Mungu. Hili ni jambo la ajabu lisilofikirika na lisiloweza kufanikishwa. Roho Mtakatifu anathibitisha vya kutosha kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli! Asiyepingika! Sisi, kundi hili la watu, kwa kweli tumebarikiwa! Kama si kwa neema ya Mungu na rehema, lazima tuangamie milele na kumfuata Shetani. Ni Mungu Mwenyezi pekee Anayeweza kutuokoa!

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Ni Wewe ambaye Umefungua macho yetu ya kiroho, kwamba tumeweza kuona siri za dunia ya kiroho. Taswira za ufalme hazina na mwisho. Kuweni waangalifu na wenye kusubiri. Siku haiwezi kuwa mbali sana.

Mioto ya vita huzunguka, moshi wa bunduki huelekea, hali ya hewa huwa vuguvugu, tabia ya nchi hubadilika, tauni litaenea, na watu lazima wafariki, na tumaini ndogo la kuishi.

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Wewe ni mnara wetu imara. Wewe ni kimbilio letu. Sisi tunakusanyika chini ya mabawa Yako, na janga haliwezi kutufikia. Huu ni utunzaji Wako mtakatifu.

Sisi sote tunainua sauti zetu, kuimba sifa, sifa ambazo zinavuma kote Sayuni! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo ameandaa hatima hio tukufu kwa ajili yetu. Kuwa mwangalifu—mwangalifu! Wakati hauwezi kuwa mbali sana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 5

169. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

Lugha za mataifa mbalimbali ni tofauti na kila nyingine lakini kuna Roho mmoja tu. Huyu Roho huunganisha makanisa kote ulimwenguni na ni mmoja na Mungu, bila tofauti hata kidogo, na hili ni jambo ambalo halina shaka kabisa. Roho Mtakatifu sasa anawapaazia sauti na sauti Yake yawaamsha. Hii ni sauti ya huruma ya Mungu. Wanaliita kwa sauti jina takatifu la Mwenyezi Mungu! Wao pia wanatoa sifa na kuimba. Hakuwezi kuwa na mkengeuko wowote katika kazi ya Roho Mtakatifu, na watu hawa hufanya linalowezekana ili kuendelea kwenye njia sahihi, huwa hawajitoi na maajabu yake hulundikana juu ya maajabu. Ni kitu ambacho watu huona ugumu kufikiria na kisichowezekana kukikisia.

Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme wa maisha katika ulimwengu! Yeye huketi juu ya kiti kitukufu cha enzi na huihukumu dunia, huwatawala wote, huyaongoza mataifa yote; watu wote hupiga magoti Kwake, humwomba, huja karibu naye na kuwasiliana na Yeye. Bila kujali muda gani mmemwamini Mungu, jinsi hadhi yenu ilivyo ya juu au jinsi ukubwa wenu wa vyeo ulivyo, kama nyinyi humpinga Mungu katika mioyo yenu basi ni lazima mhukumiwe na lazima msujudu mbele Yake, mkitoa sauti chungu ya kusihi kwenu; huku kweli ni kuvuna matunda ya matendo yenu wenyewe. Sauti hii ya kupiga mayowe ni sauti ya kuteswa katika ziwa la moto na kiberiti, na ni kilio cha kuadibiwa na fimbo ya chuma ya Mungu; hii ndiyo hukumu mbele ya kiti cha Kristo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 8

170. Mwenyezi Mungu! Mwili Wake mtukufu waonekana wazi wazi, mwili mtakatifu wa kiroho watokea na Yeye ndiye Mungu Mwenyewe kamili! Dunia na mwili vyote vimegeuzwa na mabadiliko Yake juu ya mlima ambaye ni nafsi ya Mungu. Amevaa taji la dhahabu kichwani, mavazi Yake ni meupe kabisa, kifuani ana ukanda wa dhahabu na vitu vyote katika dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Macho Yake ni kama mwale wa moto, na upanga mkali wenye makali kuwili uko ndani ya kinywa Chake na Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume. Njia ya kwenda kwa ufalme ni ng’avu bila kikomo na utukufu Wake watokea na kuangaza; milima huwa na furaha na maji hucheka, jua, mwezi na nyota zote zazunguka kwa mpango wao wa taratibu, ukimkaribisha Mungu wa kweli na wa kipekee, ambaye kurudi kwake kwa ushindi kunaashiria ukamilisho wa miaka elfu sita ya mpango Wake wa usimamizi. Zote zaruka na kucheza kwa furaha! Shangilia! Mwenyezi Mungu amekaa juu ya kiti Chake kitukufu cha enzi! Imbeni! Bendera ya ushindi ya Mwenyezi inainuliwa juu ya mlima mwadhimu, mtukufu wa Sayuni! Mataifa yote yanashangilia, watu wote wa mataifa wanaimba, Mlima Sayuni unacheka kwa furaha, utukufu wa Mungu umetokea! Hata katika ndoto Sijawahi kufikiri kwamba Ningeuona uso wa Mungu lakini leo Nimeuona. Uso kwa uso na Yeye kila siku, nauweka wazi moyo wangu Kwake. Yeye kwa ukarimu hutoa vyote vinavyoliwa na kunywewa. Maisha, maneno, matendo, mawazo, nia—mwanga Wake mtukufu huwatia nuru wote. Yeye huongoza kila hatua ya njia, na kama moyo wowote ni muasi basi hukumu Yake itatokea mara moja.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 15

171. Mwana wa Adamu Ameshuhudiwa, na Mungu Mwenyewe amefichuliwa waziwazi. Utukufu wa Mungu umekuja, uking’aa vikali kama jua lichomalo! Uso Wake mtukufu unawaka kwa mwanga ung’aao; ni macho ya nani yatathubutu kumtendea kwa upinzani? Upinzani husababisha kifo! Hakuna hata chembe ya rehema kwa kitu chochote unachofikiri katika moyo wako, neno lolote usemalo au chochote ufanyacho. Nyinyi nyote mtakuja kuelewa na kuja kuona ni nini ambacho mmekipata—hakuna chochote ila hukumu Yangu! Naweza kukistahimili wakati nyinyi hamuweki juhudi zenu katika kula na kunywa maneno yangu, lakini hudakiza kiholela na kuharibu ujenzi Wangu? Mimi sitamhurumia mtu wa aina hii! Mengine makubwa zaidi na utaangamizwa katika moto! Mwenyezi Mungu hudhihirika katika mwili wa kiroho, bila hata chembe ya mwili au damu ikiunganisha mwili mzima. Yeye huvuka mipaka ya ulimwengu dunia, kama Ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi katika mbingu ya tatu, Akisimamia mambo yote! Ulimwengu na vitu vyote vimo mikononi Mwangu. Kama Nikisema, itakuwa. Kama Nikiliamua, ndivyo litakavyokuwa. Shetani yu chini ya miguu Yangu, yu katika kuzimu! Sauti Yangu itakapotoka, mbingu na nchi zitapita na kuwa bure! Mambo yote yatafanywa upya na huu ni ukweli wa kweli sana usiobadilika. Nimeushinda ulimwengu, kuwashinda waovu wote. Naketi hapa nikizungumza nanyi; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza na wale wote wanaoishi wanapaswa kukubali.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 15

172. Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, na kila kitu chini ya mbingu hung'aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika ulimwengu na hadi miisho ya dunia vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari, na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli, na wamesisimka kana kwamba wameamka kutoka ndotoni, kana kwamba wao ni chipuko zinazochipuka kutoka mchangani!

Ah! Mungu mmoja wa kweli, Huonekana mbele ya dunia. Je, nani anathubutu kumtendea kwa upinzani? Kila mmoja hutetemeka kwa hofu. Hakuna ambao hawajaridhishwa kabisa, mara kwa mara kuomba msamaha, wote kwa magoti yao mbele Yake, vinywa vyote vikimuabudu! Mabara na bahari, milima, mito, vitu vyote kumsifu bila kikomo! Vuguvugu la upepo mwanana wa masika huja na masika kuleta mvua mzuri wa masika. Kama watu wote, mikondo ya mito hutiririka kwa huzuni na furaha, ikitoa machozi ya kuwiwa na kujilaumu. Mito, maziwa, chafuko na mawimbi, yote yanaimba, yakihimidi jina takatifu la Mungu Wa kweli! Sifa hizi zinavuma kwa wazi sana! Mambo yote ya zamani ambayo kwa wakati mmoja yalikuwa yamepotoshwa na Shetani, kila mmoja atafanyia upya, atabadilika, na kuingia katika hali mpya kabisa …

Hili ni tarumbeta takatifu linasikika! Sikiliza. Sauti hiyo, tamu sana, ni kiti cha enzi kinatoa mlio, kutangaza kwa mataifa yote na watu, wakati umefika, hatima ya mwisho imefika. Mpango Wangu wa usimamizi umemalizika. Ufalme Wangu huonekana hadharani duniani. Falme za duniani zimekuwa ufalme—wa Mungu—Wangu. Matarumbeta Yangu saba yanasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, na ni maajabu gani yatatokea! Watu katika miisho ya dunia watakurupuka pamoja kutoka kila upande kwa nguvu ya lundo na uwezo wa radi, baadhi yao baharini, baadhi yao wakiendesha ndege, baadhi yao watakuja kwa magari ya kila muundo na ukubwa, baadhi yao watakuja mgongoni mwa farasi. Angalia kwa karibu. Sikiliza kwa makini. Hawa wapandao farasi wa kila rangi, pepo kuchochewa, wenye majivuno na waadhimu, kama kuchukua uwanja wa vita, wao hawajali kifo. Katikati ya milio ya farasi na makelele ya watu ya kupiga mayowe wakimwita Mungu wa kweli, wanaume, wanawake na watoto wengi watakanyagwa na kwato zao mara moja. Baadhi yao watakufa, baadhi yao watakuwa wakivuta pumzi yao ya mwisho, baadhi yao watapondwa, pasipo na mtu wa kuwatunza, wakipiga kelele kwa kupagawa, wakilia kwa uchungu. Wana wa uasi! Je, hizi si hatima zenu za mwisho?

Hufurahia kuona watu Wangu, ambao husikia sauti Yangu, na kukusanyika kutoka kila taifa na nchi. Watu wote, uhifadhi Mungu wa kweli daima katika midomo yao, kusifu na kuruka kwa furaha bila kukoma! Wao huushuhudia kwa ulimwengu, na sauti ya ushuhuda wao kwa Mungu wa kweli ni kama sauti ya ngurumo ya maji mengi. Watu wote watasongamana katika ufalme Wangu.

Matarumbeta Yangu saba yatapaza sauti, kuamsha walio lala! Shughulika kwa haraka, muda hujakwisha. Angalia maisha yako! Fungua macho yako na uone ni wakati upi sasa. Ni nini unatafuta? Kuna nini ya kufikiri? Na ni nini kilicho cha kushikilia? Je, inawezekana kuwa bado hujafikiria tofauti katika thamani kati ya kupata maisha Yangu na mambo yote unayopenda na kushikilia? Acha kuwa makaidi na kucheza kila mahali. Usikose nafasi hii. Wakati huu hautakuja tena! Simama mara moja, tenda kufanyisha roho yako mazoezi, kutumia zana mbalimbali kukuwezesha na kuzuia kila njama na hila za Shetani, na umshinde Shetani, ili kwamba uzeofu wako wa maisha uweze kuwa wa kina zaidi na uweze kuishi kwa kudhihirisha tabia Yangu, ili maisha yako yaweze kukomaa na yawe yenye tajriba na ili uweze daima kufuata nyayo Zangu. Ukiwa bila hofu, ukiwa usiye udhaifu, daima ukisonga mbele, hatua kwa hatua, moja kwa moja hadi mwisho wa njia!

Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti tena, itakuwa mwito wa hukumu, hukumu ya wana wa uasi, hukumu ya mataifa yote na watu wote, na kila taifa litajisalimisha mbele ya Mungu. Uso wa utukufu wa Mungu hakika utaonyeshwa mbele ya mataifa yote na watu wote. Kila mtu atakuwa ameridhishwa kabisa, kupiga kelele kwa Mungu wa kweli bila kikomo. Mwenyezi Mungu Atakuwa Mtukufu zaidi, na wanangu watashiriki katika utukufu, kushiriki ufalme nami, kuhukumu mataifa yote na watu wote, kuadhibu maovu, kuokoa na kuwa na huruma juu ya watu ambao ni Wangu, kuleta uthabiti na utulivu kwa ufalme. Kupitia sauti ya matarumbeta saba, kundi kubwa la watu litaokolewa, kurudi mbele Yangu kupiga magoti na kuabudu, kwa sifa daima!

Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti mara nyingine tena, hilo litakuwa tukio la hitimisho la mwisho wa enzi, mlipuko wa sauti wa tarumbeta ya ushindi dhidi ya ibilisi Shetani, saluti katika mwanzo wa maisha ya wazi wa ufalme duniani! Sauti hii ya kifahari sana, sauti hii inayonguruma pande zote za kiti cha enzi, mlipuko wa sauti ya tarumbeta inayotikisa mbingu na dunia, ni ishara ya mpango Wangu wa usimamizi, na hukumu ya Shetani, kuadhibu duniani hii ya zamani kwa kifo kabisa, jahanamu! Huu mlipuko wa sauti ya tarumbeta unaashiria kwamba lango la neema ni linafungika, kwamba uhai wa ufalme utaanza duniani, ambayo ni kamilifu kabisa. Mungu Huokoa wale wanaompenda. Mara tu watakaporudi kwa ufalme Wake, watu duniani watakabili njaa, ndwele ya kufisha, na mabakuli saba ya Mungu, tauni saba zitaanza kutumika kwa mfululizo. Mbingu na dunia zitapita, lakini neno Langu halitapita!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 36

173. Wakati umeme unatoka Mashariki—ambao pia ni wakati hasa Naanza kutamka maneno Yangu—umeme unapotoka, mbingu yote inaangazwa, na mabadiliko yanatokea kwenye nyota zote. Wanadamu wote wanakuwa kana kwamba wamepangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yao yaking’aa, wakikosa uhakika wa kile wanachopsawa kufanya, na sembuse jinsi ya kuficha sifa zao mbaya. Wao pia ni kama wanyama wanaoitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu amabao wanakimbilia usalama katika mapango ya milimani—ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherehekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wanailaani siku waliyozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kuelezeka; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kwenda mara moja yasionekane tena. Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kuonyesha kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa majivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya katika makao ya joka kubwa jekundu pekee, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa ufalme Wangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma kuwepo milele kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi. Joka kubwa jekundu limetumia njia zote za kuweza kufikiriwa ili kuvuruga mpango Wangu, likitumaini kufuta kazi Yangu duniani, lakini Naweza kukata tamaa kwa sababu ya mbinu zake za udanganyifu? Naweza kutishwa hadi kukosa kujiamini na vitisho vyake? Hakujawahi kuwa na kiumbe hata mmoja mbinguni ama duniani ambaye Simshiki katika kiganja cha mkono Wangu; ni kiwango gani zaidi ambacho huu ni ukweli kuhusu joka kuu jekundu, chombo hiki kinachotumika kama foili[b] Kwangu? Je, pia si kitu cha kutawaliwa na mikono Yangu?

Wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu alifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua akaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kuwa na yeyote ambaye ameuona uso Wangu, ambaye ameona umeme katika Mashariki; sembuse yule ambaye amesikia sauti inayotoka kwa kiti Changu cha enzi? Kwa kweli, kutoka siku za zamani, hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye amewasiliana na nafsi Yangu moja kwa moja; leo tu, wakati Nimekuja duniani, ndipo wanadamu wana nafasi ya kuniona. Lakini hata sasa, wanadamu bado hawanifahamu, jinsi wanavyouangalia uso Wangu na kuisikia tu sauti Yangu, lakini bila kuelewa Ninachomaanisha. Wanadamu wote wako hivi. Ukiwa mmoja wa watu Wangu, je huhisi fahari ya kina unapoona uso Wangu? Na, je, huhisi aibu kwa sababu hunifahamu? Natembea kati ya wanadamu, na Naishi kati ya wanadamu, kwa kuwa Nimekuwa mwili na Nimekuja katika ulimwengu wa binadamu. Lengo Langu sio tu kuwawezesha binadamu kuutazamia mwili Wangu; cha muhimu zaidi, ni kuwawezesha binadamu kunifahamu Mimi. Zaidi, kupitia mwili Wangu, Nitamhukumu binadamu kwa dhambi zao; kupitia mwili Wangu, Nitashinda joka kuu jekundu na kuangamiza pango lake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 12

174. Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, kama ifanyavyo dunia. Binadamu wanafunuliwa wakiwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mtu anatengwa kulingana na aina yake, na kutafuta njia bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Hii itanifurahisha sana. Niko huru kutokana na vurugu, na bila kutambulika, kazi Yangu kuu inatimizwa, na vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikiweka vitu vyote vilivyo na maumbo pamoja na mifano zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu—utapata uhuru wako Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele kali na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa majaaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimami dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26

175. Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo Vyangu. Ufalme unashuka katika dunia ya wanadamu, nafsi Yangu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa ajili furaha? Ee Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi unisherehekee! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina Langu takatifu! Viumbe wote hadi miisho ya dunia! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka Kwangu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu Yangu kuu katika anga! Nazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yangu kwa nyimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Nashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena kamwe!

Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta moto, Naleta ghadhabu, Naleta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito inatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mimi. Siku ambayo watu wengi wameingojea hatimaye imefika! Wananiimbia nyimbo nzuri sana!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Wimbo wa Ufalme

176. Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambao pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, inatetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe katika taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kisha kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaanzishwa duniani. Wakati huu, Naanza kutuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hili pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena. …

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

177. Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kumhusu. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya “wingu jeupe” (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

178. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile binadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru, na wasilazimike kuitafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta waione nuru tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha waone kwamba tayari Nimeshuka juu ya wingu jeupe miongoni mwa wanadamu, kuwaacha waone mawingu mengi meupe na vishada vingi vya matunda, na, zaidi ya hayo, Nitawaacha wamwone Yehova Mungu wa Israeli. Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi aliyengojewa kwa hamu, na kuonekana kamili kwa Mimi niliyeteswa na wafalme kotekote katika enzi. Nitafanya kazi katika ulimwengu mzima na Nitatekeleza kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale ambao wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona Nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambayo imengoja Nionekane kwa mara nyingine, na kwa wanadamu wote wanaonitesa, ili wote wajue kwamba Niliuchukua utukufu Wangu zamani na kuuleta Mashariki, Ili usiwe katika Uyahudi tena. Kwani siku za mwisho tayari zimewadia!

Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

179. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

180. Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya. Nyinyi nyote mmewahi kuyafikiria zaidi ya mara moja—ila matokeo ni gani? Mungu hujidhihirisha wapi? Nyayo za Mungu zipo wapi? Mmepata majibu? Majibu ya watu wengi yangekuwa: Mungu hudhihirika miongoni mwa wale wanaomfuata na nyayo Zake zimo miongoni mwetu; ni rahisi hivyo! Mtu yeyote anaweza kutoa jibu kwa kutumia mbinu fulani, lakini je, mnafahamu kuonekana kwa Mungu ni nini, na nyayo za Mungu ni nini? Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika njia ambayo ni ya asili Kwake, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu, au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi. Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu, utawala na kupata nuru kwa mwanadamu. Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua. Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine. Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi kupitiwa mwanadamu. Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali, na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha, ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya. Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

181. Katika wakati uo huo wa kuelewa kuonekana kwa Mungu, mnapaswa kutafuta nyayo za Mungu vipi? Swali hili si gumu kueleza: Palipo na kuonekana kwa Mungu; mtapata nyayo za Mungu. Maelezo kama haya yanaonekana yapo wazi sana, ila si rahisi kutekeleza kwani watu wengi hawafahamu pale Mungu anapojidhihirisha, wala pale ambapo Angependa kujidhihirishia ama iwapo Anapaswa kujidhihirisha. Wengine kwa msukumo huamini kuwa palipo na kazi ya Roho Mtakatifu kuna kuonekana kwa Mungu. Ama sivyo watu huamini kuwa palipo na watu mashuhuri wa kiroho ndipo Mungu huonekana. Vinginevyo, wanaamini kuwa palipo na watu wanaojulikana vyema ndipo Mungu huonekana. Kwa sasa tusishauriane ikiwa imani hizi ni sahihi au la. Kujibu swali kama hilo, kwanza ni lazima tuwe wazi kuhusu lengo: tunazitafuta nyayo za Mungu. Hatutafuti viongozi wa kiroho, wala kutafuta watu mashuhuri; tunafuata nyayo za Mungu. Kwa hivyo, kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

182. Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.

Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[c] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu. Sura ya nje haiamulii dutu; na zaidi, kazi ya Mungu haiwezi kamwei kuambatana na dhana za mwanadamu. Je, si sura ya nje ya Yesu ilikinzana na dhana za mwanadamu? Je sura Yake na mavazi Yake hayakuweza kutoa dalili yoyote ya utambulisho Wake? Je, si sababu ya Mafarisayo wa zamani kabisa kumpinga Yesu hasa ilikuwa ni kwa sababu waliiangalia tu sura Yake ya nje, na hawakuyaweka moyoni maneno Aliyoongea? Ni matumaini Yangu kuwa ndugu wanaotafuta kuonekana kwa Mungu hawatarudia tanzia ya kihistoria. Hampaswi kuwa Mafarisayo wa wakati huu na kumsulubisha Mungu msalabani tena. Mnafaa kufikiria kwa makini jinsi ya kukaribisha kurudi kwa Mungu, na kuwa na mawazo dhahiri ya jinsi ya kuwa mtu anayetii ukweli. Hili ni jukumu la kila mtu anayengoja Yesu arudi na mawingu. Tunafaa kusugua macho yetu ya kiroho, na tusiwe waathiriwa wa maneno yaliyojaa mambo ya kufurahisha masikio. Tunafaa kuwaza juu ya kazi ya Mungu ya matendo, na tunafaa kuangalia upande wa hakika wa Mungu. Msijisahau ama kupotelea ndotoni, mkitazamia daima ile siku ambayo Bwana Yesu atashuka kwa ghafla juu ya mawingu kuwachukua nyinyi ambao hamjawahi kumjua wala kumwona Yeye, na msiojua kutenda mapenzi Yake. Ni vyema kufikiri juu ya mambo ya kiutendaji!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

183. Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

184. Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharama iliyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi ya kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Ukweli kwamba mmefika siku ya leo ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu, kwa sababu ni ukweli, uzima, na njia Aliyoleta ndivyo vilivyowaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya mwanadamu na Mungu, ikafupisha umbali kati yao, na kufungua kiungo kati ya mawazo ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?

Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

185. Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuikamilisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingeisha lini? Mwanadamu angeingia katika pumziko lini? Nami Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

186. Bila kujali kama wewe ni Mmarekani, Mwingereza, au mtu wa taifa jingine, ni lazima utoke nje ya mipaka yako, ni lazima ujipite, na ni sharti uione kazi ya Mungu kama kiumbe wa Mungu. Kwa njia hii, hutaweka vikwazo katika nyayo za Mungu. Kwa sababu, leo, watu hufikiri kuwa haiwezekani Mungu kudhihirika katika nchi au taifa fulani. Umuhimu wa kazi ya Mungu una undani kiasi gani, na kuonekana kwa Mungu kuna maana ilioje! Vinawezaje kupimwa kwa dhana na fikira za mwanadamu? Na ndiyo maana Ninasema kuwa unafaa kujiondoa katika dhana za uraia wako au kabila lako unapokutafuta kuonekana kwa Mungu. Kwa njia hii, hutafungwa na dhana zako mwenyewe; kwa njia hii, utahitimu kukaribisha kuonekana kwa Mungu. Vinginevyo, daima utakuwa gizani na hutapata kibali cha Mungu.

Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba muanze kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Tanbihi:

a. Maandishi ya awali hayana maneno “matokeo ya.”

b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

c. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Iliyotangulia: D. Maneno Kuonyesha Ukweli ni Nini

Inayofuata: IV. Maneno Juu ya Mafumbo ya Kupata Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp