D. Maneno Kuonyesha Ukweli ni Nini

152. Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

153. Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

154. Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

155. Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

156. Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya. Ilhali Kristo hutoa ukweli tu; Yeye haji kuamua ikiwa mwanadamu atafanikiwa katika harakati yake ya kufuata ukweli. Hivyo, kinachofuata ni kuwa mafanikio au kushindwa kwa kweli yote yanategemea harakati ya mwanadamu. Mafanikio au kushindwa kwa mwanadamu kwa kweli kamwe hakuna uhusiano na Kristo, lakini kwa mbadala kunategemea harakati yake. Hatima ya mwanadamu na mafanikio yake ama kushindwa haiwezi kurundikwa kichwani pa Mungu, ili Mungu mwenyewe afanywe wa kuibeba, kwa sababu sio jambo la Mungu mwenyewe, lakini linahusiana moja kwa moja na wajibu ambao viumbe wa Mungu wanapaswa kutekeleza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

157. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho kuonyesha waziwazi kile Mungu alisema; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu hapendi, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, watu ambao Anawachukia na watu ambao Anawafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

158. Haijalishi kama maneno yanayonenwa na Mungu ni makavu au makubwa katika mwonekano wa nje, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji

159. Neno la Mungu haliwezi kuzungumzwa kama neno la mwanadamu, sembuse neno la mwanadamu kuzungumzwa kama neno la Mungu. Mwanadamu anayetumiwa na Mungu siye Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili siye mwanadamu anayetumiwa na Mungu; katika hili, kunayo tofauti kubwa sana. Pengine, baada ya kusoma maneno haya, hukubali kuwa ni maneno ya Mungu, na kuyakubali tu kama maneno ya mwanadamu ambaye amepewa nuru. Ikiwa hivyo, basi umepofushwa na ujinga. Maneno ya Mungu yatawezaje kuwa sawa na maneno ya mwanadamu ambaye amepewa nuru? Maneno ya Mungu mwenye mwili yanaanzisha enzi mpya, yanaongoza wanadamu wote, yanafichua mafumbo, na kumwonyesha mwanadamu mwelekeo mbele katika enzi mpya. Nuru anayoipata mwanadamu ni utendaji au elimu rahisi. Haiwezi kuelekeza binadamu wote kuingia enzi mpya au kufichua fumbo la Mungu Mwenyewe. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu. Iwapo mwanadamu anachukulia maneno yanayonenwa na Mungu kama kupewa nuru tu na Roho Mtakatifu, na kuchukua maneno yaliyonenwa na mitume na manabii kama maneno yaliyonenwa na Mungu Mwenyewe, basi mwanadamu anakosea.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

160. Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli; ni kiwango tu ambacho kinaweza kufikiwa na mtu. Ni uzoefu unaofaa tu na ufahamu unaofaa ambao mtu anapaswa kuwa nao, ambao ni uzoefu na ufahamu wake halisi wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa ukweli huu kabisa, na wakiweka pamoja uzoefu na ufahamu wao wote, hilo bado halilingani na ukweli huo mmoja. Kama ilivyosemwa zamani, “Nilifupisha hili kwa ajili ya dunia ya binadamu kwa kanuni: Miongoni mwa wanadamu hakuna yule anayenipenda Mimi.” Hii ni kauli ya ukweli, ni asili ya kweli ya maisha, ni kitu chenye cha maana sana, ni udhihirisho wa Mungu binafsi. Unaweza kuipitia. Ukiipitia kwa miaka mitatu utakuwa na uelewa usio na kina, ukiipitia kwa miaka minane utapata uelewa zaidi, lakini uelewa wako hautaweza kuwa mbadala wa kauli ya ukweli. Mtu mwingine akipata uzoefu wake kwa miaka miwili atakuwa na uelewa mdogo; akiupitia kwa miaka kumi atakuwa na uelewa wa juu, na akipata uzoefu kwa maisha yake yote atapata uelewa mkubwa zaidi, lakini mkiuweka uelewa wenu pamoja, haijalisha uelewa wa kiwango kipi, uzoefu wa kiwango kipi, ufahamu kiasi gani, mwanga wa kiasi kipi, ama mifano mingapi ambayo ninyi wawili mnayo, hayo yote hayawezi kuwa mbadala wa kauli hiyo. Ninamaanisha nini na hili? Namaanisha kwamba maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na nia za Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote; hata kama watu wangekuwa na uzoefu wa maisha kadhaa ama wa milenia kadhaa, bado hawangeweza kuupitia ukweli kabisa. Kama umeelewa tu maneno ya juu juu kisha useme kuwa una ukweli, je si hilo halina msingi?

Kimetoholewa kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

161. Wakati watu wanaelewa ukweli, na kuishi na ukweli kama maisha, hili linaashiria maisha gani? Ni maisha ambayo watu wanaishi wakilitegemea neno la Mungu. Watu wanapokuwa na uzima huo ndani yao, basi maisha yao yanaishiwa kulingana na ukweli, maisha yao yanaishiwa katika eneo la ukweli, maisha yao yamejawa na uelewa wa ukweli, na uzoefu wa ukweli, kuwa kwa msingi huu na kutoenda nje ya mawanda hayo—hayo ndiyo maisha yanayorejelewa. Watu wanautegemea ukweli kama maisha yao, na kuishi maisha yao kulingana na ukweli. Si kwamba wakati watu wanautegemea ukweli kama maisha yao basi wana maisha ya ukweli; si kusema pia kuwa kama una ukweli kama maisha unakuwa ukweli, na maisha yako ndani yanakuwa maisha ya ukweli. Mwishowe maisha yako bado ni maisha ya mwanadamu. Unaweza kuishi ukiyategemea maneno ya Mungu, uwe na uelewa fulani wa ukweli, na kuelewa kwa kiwango cha juu, na uelewa huu hauwezi kuchukuliwa kutoka kwako; unapata uzoefu na kuelewa kikamilifu, unahisi kuwa vitu hivi ni vizuri, ni vya thamani sana, na unakuja kuvikubali kama msingi wa maisha yako, na unaishi ukitegemea vitu hivi, basi hakuna anayeweza kubadilisha hayo, haya ni maisha yako. Maisha yako yana vitu hivi tu, yana uelewa pekee, uzoefu, na ufahamu wa ukweli; haijalishi utakachofanya utakuwa unaishi kwa kutegemea vitu hivi, na haijalishi utakachofanya hutaenda zaidi ya mawanda haya, hutaenda zaidi ya mipaka hii; hayo yatakuwa maisha yako, na kusudi la mwisho la kazi ya Mungu ni kwamba watu watakuwa na maisha ya aina hii. Kama Mungu Mwenyewe binafsi Alikamilisha kikundi cha Miungu wakubwa na Miungu wadogo, je huo haungekuwa machafuko? Hata hivyo, hilo ni jambo lisilowezekana, ni jambo la upumbavu, ni dhana ya upumbavu kutoka kwa binadamu, na sio jambo linalowezekana. Mungu Anaweza tu kuwaumba watu, Mungu hawezi kumuumba Mungu; Mungu Anaweza tu kupata mwili kama mfano wa mwili, lakini haimaanishi kuwa Alimuumba Mungu. Mungu hakujiumba Mwenyewe, Yeye ana dutu Yake binafsi, ambayo haitabadilika kamwe. Hakujiumba Mwenyewe, Anaweza tu kuumba watu na kuumba vitu vingine. … Kama una uzoefu fulani na maneno ya Mungu, na unaishi kwa kutegemea uelewa wako wa ukweli, basi neno la Mungu linakuwa maisha yako. Huwezi kusema kuwa ukweli ni maisha yako, kuwa unachoeleza ni ukweli; kama unafikiria hivyo, basi umekosea. Kama una uzoefu fulani na kipengele cha ukweli, je, hili linaweza kuuwakilisha ukweli? Haliwezi kuwakilisha ukweli kabisa. Kwa hivyo unaweza kunena ukweli kabisa? Je, unaweza kueleza ukweli kikamilifu? Huwezi kwa kweli. Unaweza kugundua tabia ya Mungu kutoka kwa ukweli? Unaweza kugundua kiini cha Mungu? Huwezi. Uzoefu wa kila mtu wa ukweli ni kipengele chake kimoja tu na mtazamo mmoja; kwa kupata uzoefu wake katika mawanda yako finyu, huwezi kugusia ukweli wote. Je, watu wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maana asili ya ukweli? Uzoefu wako mdogo unajumuisha kiwango kipi? Chembe ya changarawe ufuoni, tone la maji baharini. Kwa hiyo, bila kujali jinsi ufahamu na hisi zako kutoka kwa uzoefu wako ni ya thamani, hata kama ni za thamani sana—haziwezi kuhesabika kama ukweli. Chanzo cha ukweli na maana ya ukweli ni pana sana. Hakuna kinachoweza kuupinga.

Kimetoholewa kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

162. Mungu Mwenyewe ni ukweli, Mwenyewe anao ukweli, na Yeye ndiye chanzo cha ukweli. Kila kitu chanya na kila ukweli unatoka Kwake. Anaweza kutoa hukumu juu ya wema na ubaya wa mambo yote na matukio yote; Anaweza kutoa hukumu juu ya mambo ambayo yametukia, mambo ambayo yanatukia sasa, na mambo ya baadaye ambayo bado hayajajulikana kwa mwanadamu. Yeye ndiye hakimu wa pekee Anayeweza kutoa hukumu juu ya wema na ubaya wa mambo yote, na hii inamaanisha kuwa wema na ubaya wa mambo yote unaweza kuhukumiwa na Yeye tu. Anajua sheria za mambo yote. Huu ndio mfano halisi wa ukweli, jambo ambalo linamaanisha kwamba Yeye Mwenyewe anacho kiini cha ukweli. Ikiwa mwanadamu angeuelewa ukweli na kupata ukamilifu, basi angekuwa na uhusiano wowote na mfano halisi wa ukweli? Mwanadamu anapokamilishwa, yeye huwa na ufahamu sahihi wa yote ambayo Mungu hufanya sasa na mambo Anayohitaji, naye huwa na njia sahihi ya kutenda; mwanadamu pia huyaelewa mapenzi ya Mungu na hujua tofauti kati ya mema na mabaya. Lakini kuna mambo kadhaa ambayo mwanadamu hawezi kuyafikia, mambo ambayo anaweza kuyajua tu baada ya Mungu kumwambia kuyahusu—je, mwanadamu anaweza kujua mambo ambayo bado hayajajulikana, mambo ambayo bado Mungu hajamwambia? (Hawezi.) Mwanadamu hawezi kufanya utabiri. Aidha, hata kama mwanadamu angeupata ukweli kutoka kwa Mungu, na awe na uhalisi wa ukweli, na ajue kiini cha ukweli mwingi, na awe na uwezo wa kutofautisha mema na mabaya, basi angekuwa na uwezo wa kudhibiti na kutawala vitu vyote? (La.) Hiyo ndiyo tofauti. Viumbe walioumbwa wanaweza tu kuupata ukweli kutoka kwa chanzo cha ukweli. Je, wanaweza kuupata ukweli kutoka kwa mwanadamu? Mwanadamu anaweza kuwapa ukweli? Mwanadamu anaweza kumtunza mwanadamu? Hawezi, na hiyo ndiyo tofauti. Unaweza kupokea tu, siyo kutoa–je, unaweza kuitwa mfano halisi wa ukweli? Kiini cha mfano halisi wa ukweli ni kipi hasa? Ni chanzo kinachoutoa ukweli, chanzo cha utawala na mamlaka juu ya vitu vyote, na pia ni viwango na sheria ambazo kwazo vitu vyote na matukio yote yanahukumiwa. Huu ndio mfano halisi wa ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Kwa Viongozi na Wafanyakazi, Kuchagua Njia Ni Muhimu Sana X” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

164. Katika kuonyesha Kwake ukweli, Mungu huonyesha tabia na kiini Chake; havionyeshwi kulingana na mihutasari ya wanadamu ya mambo mbalimbali chanya na njia za kuzungumza ambazo wanadamu wanatambua. Maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu; maneno ya Mungu ni ukweli. Hayo ndiyo msingi na sheria ambayo kwayo wanadamu wanapaswa kuishi, na hizo zinazodaiwa kuwa kanuni zinazotokana na binadamu zimelaaniwa na Mungu. Hazikubaliwi na Yeye, sembuse kuwa asili au msingi wa matamshi Yake. Mungu huonyesha tabia Yake na kiini Chake kupitia maneno Yake. Maneno yote yaliyotolewa na maonyesho ya Mungu ni ukweli, kwa maana Yeye anacho kiini cha Mungu, na Yeye ndiye uhalisi wa mambo yote chanya. Ukweli kwamba maneno ya Mungu ni ukweli haubadiliki kamwe, bila kujali jinsi wanadamu hawa wapotovu wanavyoyachukulia au kuyafafanua, wala jinsi wanavyoyaona au kuyaelewa. Haijalishi ni maneno mangapi ya Mungu ambayo yamezungumzwa, na bila kujali jinsi binadamu hawa wapotovu na wenye dhambi wanavyoyashutumu kwa kiasi kipi, hata kiasi kwamba hawayasambazi, na hata kufikia kiwango ambacho yanadharauliwa na wanadamu wapotovu—hata katika hali hizi, bado kuna ukweli ambao hauwezi kubadilishwa: Hizi zinazodaiwa kuwa mila na desturi ambazo wanadamu huthamini haziwezi kuwa vitu chanya na haziwezi kuwa ukweli, hata sababu zilizopo hapo juu zikizingatiwa. Hili haliwezi kubadilika. Tamaduni za jadi za wanadamu na njia za kuishi hazitakuwa ukweli kwa sababu ya mabadiliko au kupita kwa wakati, na wala maneno ya Mungu hayatakuwa maneno ya mwanadamu kwa sababu ya shutuma na kusahau kwa wanadamu. Kiini hiki hakitabadilika kamwe; ukweli ni ukweli kila wakati. Kuna ukweli ndani ya hili: Hiyo misemo yote inayofupishwa na wanadamu inatoka kwa Shetani—ni fikira na mawazo ya wanadamu, hata inatokana na hamaki ya binadamu, na haihusiani hata kidogo na mambo chanya. Maneno ya Mungu, kwa upande mwingine, ni maonyesho ya kiini na hadhi ya Mungu. Yeye huyaonyesha maneno haya kwa sababu gani? Kwa nini Ninasema maneno hayo ni ukweli? Sababu ni kwamba Mungu anatawala juu ya sheria, kanuni, vyanzo, viini, uhalisi na siri zote za vitu vyote, na vimefumbatwa mkononi Mwake, na ni Mungu pekee Anayejua kanuni, uhalisi, ukweli, na siri zote za vitu vyote; Anajua asili ya vitu hivyo na vyanzo vyao ni nini hasa. Kwa hivyo, ni ufafanuzi wa vitu vyote uliotajwa katika maneno ya Mungu pekee ndio sahihi kabisa, na mahitaji kwa wanadamu yaliyo ndani ya maneno ya Mungu ndicho kiwango pekee kwa wanadamu—kigezo pekee ambacho mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Ukweli ni Nini” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: C. Maneno Juu ya Kufichua Mawazo, Uzushi na Uongo wa Kidini wa Wanadamu Wapotovu

Inayofuata: III. Maneno Juu ya Kushuhudia Kuonekana Kwa na Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp