234 Bila Kufuatilia Ukweli, Kutofaulu Hakuwezi Kuepukika

1 Ingawa nilihudhuria mikutano na kusoma maneno ya Mungu, sikuzingatia kutenda ukweli. Wakati ambapo ningeweza kutekeleza wajibu fulani, nilidhani kuwa nilimiliki uhalisi wa ukweli. Nilimwomba Mungu lakini sikuwa na ushirika halisi na Mungu. Kwa kufikia matokeo kadhaa katika wajibu wangu, nilidhani kuwa nilikuwa nimepata sifa kiasi njema. Huku nikiridhishwa sana na mimi mwenyewe, nilidhani Mungu angenipa tuzo bila shaka. Kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, nilizinduka mara moja. Nilimwamini Mungu kwa miaka mingi bila kumjua, na bado nilifanya mapatano na Mungu. Ni sasa tu ndipo ninaona kwamba kumwamini Mungu bila kufuatilia ukweli ndio ushinde mkuu zaidi.

2 Mungu huonyesha ukweli kwa ajili kabisa ya kusafisha na kumwokoa mwanadamu kabisa, lakini sikuelewa nia Yake nzuri hata kidogo. Nilitumia fursa hiyo kufanya wajibu wangu ili kufuatilia hadhi na sifa. Katika kazi au mahubiri, nilijisifu kwa upumbavu na kujionyesha mara nyingi sana. Na niliona uwezo wangu wa kuhubiri nadharia ya kiroho kama kuwa na uhalisi wa ukweli. Nilitegemea tu bidii yangu kufanya kazi lakini sikutenda ukweli, nikifanya mambo kwa njia yangu. Nilikuwa mnafiki kama Mafarisayo, lakini nilifikiri kuwa nilikuwa mtu wa dini. Bila hukumu ya Mungu sijui ningezama hadi katika kiwango kipi.

3 Baada ya hukumu na majaribio ya Mungu ya kurudiarudia hatimaye ninaelewa kuwa kufanya kazi kwa bidii bila kufuatilia ukweli, yote ni kazi bure. Ninapochunguza matendo na tabia yangu mwenyewe, nagundua kuwa sina utiifu wa kweli kwa Mungu. Nikiwa na upotovu na udanganyifu katika usemi na vitendo, mimi si mtu mwaminifu. Bila kujali nina mwenendo mzuri kiasi gani, si sawa na mabadiliko ya kitabia. Ufalme wa Mungu ni mtakatifu—ungewezaje kuwaruhusu watu wapotovu waingie? Unafiki hauwezi kuficha ukweli wa kumpinga Mungu. Bila uhalisi wa ukweli, mtu hawezi kamwe kupata sifa za Mungu. Ni wale tu walio mashahidi katikati ya dhiki kuu ndio watakaofaulu katika kumwamini kwao Mungu.

Iliyotangulia: 233 Niko Tayari Kutii Kazi ya Mungu

Inayofuata: 235 Nimeona Jinsi Ukweli Ulivyo wa Thamani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki