526 Pamoja Na Ukweli Kuna Nguvu

1 Lazima muelewe ni nini maana ya kujitumia kwenu kwa ajili ya Mungu na kwa nini mnataka kufanya haya. Ikiwa ni ili kufuatilia ukweli, kufuatilia uzima, na kufanya machache ili kutimiza jukumu lenu na kulipiza upendo wa Mungu, basi hiyo ni ya haki kabisa, kitu kizuri, na ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya ulimwengu. Katika hali hii, hamtawahi kuwa na majuto, na hamtakuwa hasi. Watu wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na nguvu. Wanapokuwa na ukweli, miili yao inajawa na nguvu isiyoisha. Wanapokuwa na ukweli, wanakuwa na radhi. Bila ukweli, wao ni kama makapi laini ya tofu. Na ukweli, wao ni dhabiti na wenye kutiwa moyo, na hawahisi kuwa mateso yao ni mateso bila kujali jinsi wanavyovumilia.

2 Ikiwa watu wana ufahamu wa kweli wa tabia ya Mungu, na wanaweza kutoa sifa ya kweli kwa utakatifu Wake na haki Yake, basi wanajua Mungu kwa kweli na kumiliki ukweli; ni hapo tu ndipo wanaishi nuruni. Ni wakati tu ambapo maoni ya watu kuhusu dunia na maisha yanabadilika ndipo wanabadilika kimsingi. Mtu anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli, mtu anapomtii Mungu kabisa na kuishi kulingana na neno la Mungu, mtu anapohisi kuwa na amani na kuchangamshwa ndani ya roho yake, moyo wa mtu unapokuwa huru bila giza, na mtu anapoishi kwa huru kabisa na bila kuzuiwa kwa uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli. Aidha, ukweli wote unaomiliki unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe. Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 525 Tafuta Kuwa Yule Anayemwabudu Mungu kwa Kweli

Inayofuata: 527 Maana ya Kweli ya Maneno ya Mungu Haijawahi Kueleweka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp