97 Mungu Amekuwa Akifanya Kazi Hadi Sasa, Lakini Kwa Nini Bado Huelewi?

1

Mungu wa kweli hufanya kazi hapa duniani, Anajionyesha katika mwili, kumfanya mwanadamu amjue.

ili Apate kushinda moyo wa mwanadamu, ili Apate upendo wa mwanadamu.

Na bado, hujui chochote kuhusu hiki, unatafuta miujiza kwa ukaidi.

Aa! Unawezaje kukosa kuona mapenzi ya Mungu?

Kuja na upepo na kwenda na mvua, Anamfanyia nani hivyo?

Aa! Mungu amekuwa akifanya kazi hadi sasa, lakini kwa nini bado huelewi?

Mungu amekupa upendo mwingi sana, na bado hujui!

2

Unasema unamwamini Mungu mwenye mwili, lakini bado unamtafuta Mungu asiye dhahiri.

Unafikiria jinsi maneno ya Mungu yanavyotimizwa, unatamani kumtazama Mungu wa juu sana.

Lakini ni wakati tu mnaposafishwa na maneno ya Mungu ndipo unajua Mungu wa vitendo.

Aa! Kutafuta kwako hapo zamani kulikuwa bure.

Mungu huzungumza na kufanya kazi kwa njia nyingi.

Aa! Mungu amekuwa akifanya kazi hadi sasa, lakini kwa nini bado huelewi?

Ikiwa hujui kazi ya Mungu, kuzungumza kuhusu kukamilishwa kuna maana gani?

3

Wewe daima humdai Mungu kwa mawazo yako, bila utiifu au upendo hata kidogo.

Kazi ya Mungu ni ya vitendo sana, inawezaje kufuata mawazo ya binadamu!

Kushikilia maoni yako mwenyewe na kufanya madai yenye kuzidi—huko kamwe hakutasaidia.

Aa! Usisahau upendo wa Mungu kabisa.

Moyo wa Mungu na mapenzi ya Mungu: jaribu kuyaelewa.

Aa! Mungu amekuwa akifanya kazi hadi sasa, lakini kwa nini bado huelewi?

Usiwe mkatili kabisa, unapaswa kuudhukuru moyo wa Mungu.

4

Iwapo utapenda, basi kuwa mwaminifu katika kupenda, haina maana yoyote ukifa moyo katikati.

Kujidanganya kuhusu kile kilicho kweli na uwongo, unalegea huku miaka na miezi inapita.

Mungu ameyazungumza maneno mengi sana, kila moja ili kumkamilisha mwanadamu.

Aa! Kwa nini huuelewi moyo wa Mungu?

Kwa nini hutafuti ukweli lakini unamwasi kila mara?

Aa! Mungu amekuwa akifanya kazi hadi sasa, lakini kwa nini bado huelewi?

Tafuta kubadilisha maisha yako haraka kadiri uwezavyo, na kwa hivyo kuufaraji moyo wa Mungu.

Iliyotangulia: 96 Mungu Amelipa Gharama Kubwa Mno

Inayofuata: 98 Upendo wa Mungu Utukuke Milele na Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp