414 Sababu za Watu Kushindwa Katika Imani Yao kwa Mungu
1 Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na kwamba ajitolee mwenyewe, na kutii kwa kweli. Kile kigumu sana kwa mwanadamu ni kupeana mwili wake ili abadilishe na imani ya kweli, ambapo kupitia hii anaweza kupata ukweli mzima, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hili haliwezi kupatikana na wale ambao wanafeli, na halipatikani hata zaidi na wale ambao hawawezi kumpata Yesu.
2 Kwa sababu mwanadamu si hodari kwa kujitolea mwenyewe kwa Mungu kabisa, kwa sababu mwanadamu hayuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa Muumba, kwa sababu mwanadamu ameona ukweli lakini anauepuka na kutembea katika njia yake mwenyewe, kwa sababu mwanadamu daima anatafuta kwa kufuata njia ya wale walioshindwa, kwa sababu mwanadamu daima anaasi Mbingu, hivyo, mwanadamu daima hushindwa, huchukuliwa na hila za Shetani, na anakamatwa kwa hila na wavu wake.
3 Kwa sababu mwanadamu hamjui Kristo, kwa sababu mwanadamu hana ustadi katika kuelewa na kushuhudia ukweli, kwa sababu mwanadamu ni wa kuabudu Paulo sana na mwenye tamaa nyingi ya mbinguni, kwa sababu mwanadamu daima anadai kuwa Kristo awe akimtii yeye na kuagiza kuhusu Mungu, hivyo mashujaa hao wakuu na wale ambao wamepitia mabadiliko mabaya ya dunia bado wamo na ubinaadamu, na bado hufa kwa kuadibu kwa Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili