383 Nani Awezaye Kuepuka Kuja kwa Nuru ya Mungu?

1 Mwanadamu akiwa kwenye usingizi mzito, ni kwa mapigo ya radi Yangu tu ndipo wanaweza kuzinduka kutoka ndotoni mwao. Na wafunguapo macho yao, wengi huumizwa machoni na mwanga huu baridi, hadi kwa kiwango kwamba wanapoteza mwelekeo, na kushindwa kutambua watokako na waelekeako. Watu wengi hupigwa na mwale huu kama wa mshale na kama matokeo huanguka kwenye rundo chini ya dhoruba, na miili yao kusombwa na mafuriko, bila kuacha nyuma dalili yoyote. Katika mwangaza, manusura hatimaye huweza kuuona uso Wangu kwa uwazi zaidi, na hapo ndipo hugundua kitu kuhusu umbo Langu la nje, kwa kiasi kwamba wao hawawezi kuthubutu kuniangalia usoni ana kwa ana, wakihofu pakubwa kuwa Nitailetea tena miili yao kuadibu Kwangu na laana.

2 Watu wengi sana hulia kwa sauti na kwa uchungu mwingi; wengi sana hukata tamaa; wengi sana husababisha mito na damu yao; wengi huwa miili inayoelea huku na kule bila mwelekeo; watu wengi sana, wanapopata sehemu yao katika mwangaza, huhisi uchungu wa mioyo yao ghafla na kulia machozi kwa ajili ya miaka yao ya kukosa furaha. Watu wengi sana, kwa msukumo wa mwangaza huu wa kuogofya hukiri uchafu wao na kuamua kujibadilisha; wengi kwa kuwa wamepofushwa wamepoteza hamu ya kuishi na hatimaye hawawezi kamwe kuuona huu mwangaza na kwa hivyo kukwama, wakisubiri mwisho wao. Na ni watu wengi sana huanza safari ya maisha yao na, chini ya uongozi wa mwanga huu, kwa bashasha wakitumainia kesho. … Leo hii ni nani miongoni mwa binadamu hayumo katika hali sawa na hii? Ni nani hayumo katika mwangaza Wangu? Hata kama wewe ni mwenye nguvu, au hata kama wewe ni mnyonge, unawezaje kuepuka ujio wa mwanga Wangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 13” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 382 Mwisho Wako Utakuwa Upi?

Inayofuata: 384 Maana ya Kweli ya Imani kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp