356 Nani Awezaye Kuuelewa Moyo wa Mungu?

1 Ndiyo maana duniani, Mungu Anakuwa kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu wala Hazingatii hayo moyoni Mwake hata kidogo, bali Anaendelea kufanya kazi Anayotaka kufanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu aliyetambua upendo wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alionao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba?

2 Roho wa Mungu Baba Aliyeko mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofia moyo Wake kuumia. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, utaona wawili Hawa wanatazamana wakati wote kutoka kwa mbali, sambamba na Roho. Ee binadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu?

3 Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini tena Watengane, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba Anampenda Mwana Wake kama vile Mwana Anavyompenda Baba Yake. Kwa nini sasa asubiri kwa muda mrefu huku Akiwa na shauku hiyo? Ingawa Hawajatengana kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Hii yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani?

4 Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Mungu Anapokuja duniani, Anakabiliana na mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu kama mwanadamu. Mungu Mwenyewe hana hatia, sasa kwa nini Mungu Ateseke kwa maumivu kama mwanadamu? Nani awezaye kuujua moyo wa Mungu? Mungu Anampatia mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 355 Mmempa Mungu Nini Kama Malipo?

Inayofuata: 357 Hakuna Aelewaye Mapenzi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp