308 Iko Wapi Imani Yako ya Kweli?

1 Baada ya watu wa Ninawi kusikia maneno ya hasira ya Yehova, mara moja walitubu kwa magunia na majivu. Ilikuwa kwa sababu waliyaamini maneno Yake kwamba walijawa na woga na hofu na wakatubu kwa magunia na majivu. Na ingawa watu wa leo pia wanaamini maneno Yangu na hata zaidi kuamini kuwa Yehova amekuja tena kati yenu leo, mtazamo wenu sio chochote ila usioheshimu vitu vitakatifu, kana kwamba mnamwangalia tu Yesu aliyezaliwa Yudea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita na sasa Ameshuka katikati yenu.

2 Ninaelewa kabisa udanganyifu ulio ndani ya mioyo yenu; wengi wenu hunifuata kutokana na udadisi na mmekuja kunitafuta kutokana na utupu. Wakati matakwa yenu ya tatu yanavunjwavunjwa—kwa ajili ya maisha ya amani na yenye furaha—udadisi wenu pia unatapanywa. Udanganyifu ulio ndani ya mioyo ya kila mmoja wenu wote hufunuliwa kupitia maneno na matendo yenu. Kusema kweli, nyinyi mnataka tu kujua kunihusu, hamwogopi; hamjali matamshi yenu, na mnazuia tabia zenu hata mara chache zaidi. Basi imani yenu iko vipi kwa kweli? Je, ni ya kweli?

3 Mnatumia tu maneno Yangu kuondoa wasiwasi wenu na kupunguza uchoshi wenu, ili kujaza nafasi zilizobaki tupu katika maisha yako. Ni nani miongoni mwenu ambaye ameyatia katika vitendo? Nani ana imani ya kweli? Mnaendelea kupiga kelele kwamba Mungu ni Mungu ambaye huona ndani kabisa ya mioyo ya watu, lakini ni vipi Mungu mnayepiga kelele kuhusu mioyoni mwenu analingana na Mimi? Kwa kuwa mnapiga kelele kwa njia hii, basi kwa nini mnatenda kwa njia ile? Inawezea kuwa kwamba huu ndio upendo mnaotaka kunilipizia nao? Hakuna kiasi kidogo cha upendo kwenye midomo yenu, lakini ziko wapi dhabihu zenu, na matendo yenu mema? Isingalikua maneno yenu kuyafikia masikio Yangu, Ningaliwezaje kuwachukia sana?

Umetoholewa kutoka katika “Maneno kwa Vijana na kwa Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 307 Hii Ndiyo Imani Yako?

Inayofuata: 309 Una Imani na Upendo wa Kweli kwa Kristo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp