429 Jinsi ya Kuutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

1 Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni: Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu. Tafakari na uzingatie maneno ya Mungu na kufikiria kazi ya Mungu kwa moyo wako. Kwanza anza na jambo la sala. Kuwa na nia moja, na uombe wakati usiobadilika. Haijalishi umepungukiwa na muda namna gani, au uwe na shughuli vipi, au chochote kitakachokufanyikia, omba kila siku kama kawaida, na ule na kunywa maneno ya Mungu kama kawaida.

2 Kwa kawaida, lazima moyo wako uweze kusongea karibu na Mungu kwa kawaida, lazima uweze kuzingatia upendo wa Mungu, kutafakari juu ya maneno ya Mungu, na usiweze kuathiriwa na kuingiliwa kwa dunia ya nje. Moyo wako unapokuwa na amani mbele ya Mungu kiasi kwamba unaweza kutafakari, ukiwa, ndani yako mwenyewe, unazingatia upendo wa Mungu, na kusonga karibu na Mungu kwa kweli, bila kujali mazingira uliyomo, na, kwa hakika ukiwa umefika kiwango ambacho unapeana sifa moyoni mwako, na ni bora zaidi hata kuliko kuomba, basi katika hili utakuwa wa kimo fulani. Ni baada tu ya kuwa na uwezo wa kuwa na amani mbele ya Mungu ndipo watu wanaweza kuguswa na Roho Mtakatifu, na kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, ni hapo tu ndipo wanaweza kuwasiliana kwa karibu kwa kweli na Mungu, na kuweza kushika mapenzi ya Mungu na mwongozo wa Roho Mtakatifu—na katika hii, watakuwa wameingia katika njia sahihi katika maisha yao ya kiroho.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 428 Jinsi ya Kutulia Mbele za Mungu

Inayofuata: 430 Desturi wa Kuwa Mtulivu Mbele Ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp