228 Wote Watumiao Biblia Kumshutumu Mungu ni Mafarisayo

1 Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu.

2 Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 227 Biblia Nzima Imetolewa kwa Msukumo wa Mungu?

Inayofuata: 229 Biblia Imekuwa Pingamizi kwa Mwanadamu Kukubali Kazi Mpya ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp