198 Elewa Ukweli na Uwe Huru

1

Katika miaka mingi ya kumwamini Bwana, nilizungumza tu maneno na mafundisho, nikashikilia sheria, na kufanya utaratibu wa kidini.

Kila ombi langu lilikuwa majivuno tupu, sikuwahi kumwambia Mungu maneno ya moyoni mwangu.

Wala sikutafuta ukweli niliposoma maneno ya Mungu; sikuweza kutafakari mapenzi ya Mungu.

Nilidhani kwamba kukariri vifungu maarufu na misemo ya Biblia kulimaanisha kuwa nilikuwa na uhalisi wa ukweli.

Nililenga tu kujizuia kudanganya, na hivyo nilijiona mwaminifu.

Nilijitahidi kwa bidii na kwa furaha kwa miaka ili niingie katika ufalme wa mbinguni na kutunukiwa.

Bahati iliyoje kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yaliniita; niliisikia sauti ya Mungu na nikamrudia Mungu.

Nimeelewa ukweli mwingi kutoka kwa maneno ya Mungu, nimeona kuonekana na kazi ya Mungu.

2

Hukumu ya maneno ya Mungu iliniamsha ghafla; kufuatilia ukweli kunaupendeza moyo wa Mungu kabisa.

Nikimwamini Mungu lakini nisipitie kuadibu na hukumu ya Mungu, tabia yangu potovu haiwezi kubadilika.

Kama simjui Mungu, na simwogopi Mungu, basi tabia yangu nzuri ni ulaghai tu.

Tabia ya Mungu yenye haki haiwezi kukosewa na mwanadamu, tamaa ya mwanadamu mdanganyafu ya kuingia katika ufalme ni ndoto tu.

Nimeamua kutenda na kupitia maneno ya Mungu, kuupata ukweli na kuondoa upotovu wangu.

Katika vitu vyote, natafuta ukweli na kutenda ukweli; moyoni mwangu, nahisi niliyepumzika na mwenye amani.

Natekeleza wajibu wangu kwa uaminifu, na kumtumikia Mungu kwa furaha; siombi baraka, bali kwamba nimpende Mungu tu.

Kwa kuwa sasa naelewa ukweli, sishikilii tena sheria; nikiishi mbele za Mungu, nimewekwa huru.

Iliyotangulia: 197 Fuata Mfano wa Petro na Utafute Kumpenda Mungu

Inayofuata: 199 Ninapoamka Katika Ukungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp