Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maneno Mashuhuri Kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

XI Maneno Bora Zaidi Juu ya Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli

(VI) Maneno Juu ya Jinsi ya Kuelewa Tabia Yako ya ishetani na Asili

70. Mtu yeyote anaweza kutumia maneno na vitendo vyake wenyewe kuwakilisha tabia yake halisi. Sura hii ya kweli bila shaka ni asili yake. Kama wewe ni mtu anayeongea bila kuwa dhahiri, basi una asili mbovu. Kama asili yako ni yenye hila sana, basi namna ambayo unafanya mambo ni janja na laghai sana, nawe unafanya iwe rahisi sana kwa watu kulaghaiwa nawe. Kama asili yako ni mbovu sana, huenda maneno yako ni mazuri kusikiliza, lakini vitendo vyako haviwezi kuficha njia zako mbovu. Kama asili yako ni vivu sana, basi kila kitu unachosema vyote vinalenga kukwepa lawama na wajibu wa uzembe na uvivu wako, na vitendo vyako vitakuwa vya polepole sana na vizembe, na vizuri sana katika kuuficha ukweli. Kama asili yako ni yenye uwezo wa kuhisi maono ya wengine sana, basi maneno yako yatakuwa yenye busara na hatua zako pia zitalingana sana na ukweli. Kama asili yako ni aminifu sana, basi maneno yako lazima yawe ya dhati na namna ambayo unafanya mambo lazima iwe yenye kuhusika na mambo halisi, bila mengi ya kufanya bwana wako asikuamini. Kama asili yako ni yenye tamaa sana au ni yenye tamaa ya fedha, basi moyo wako mara nyingi utajazwa na mambo haya na utafanya baadhi ya mambo yaliyopotoka bila kukusudia, mambo maovu ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kusahau na zaidi ya hayo yatawaudhi.

kutoka katika “Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

71. Kama watu wanafaa kujielewa, ni lazima waelewe hali zao za kweli. Kipengele cha muhimu zaidi katika kuielewa hali ya mtu ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zake na mawazo yake. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa. Ikiwa unaweza kudhibiti fikira zako, unaweza kudhibiti vitu vilivyo nyuma yazo. Watu hawawezi kuzidhibiti fikira na mawazo yao, lakini wanapaswa kujua fikira na mawazo haya hutoka wapi, nia zao ni gani, jinsi fikira hizi na mawazo haya huzalishwa, ni nini kinachozidhibiti na ni nini asili yazo. Baada ya tabia yako kubadilika, fikira na mawazo yako, tamaa ambazo moyo wako unatafuta, na maoni yako juu ya vitu unavyokimbiza—ambavyo vimefanyizwa kutoka kwa sehemu zako ambazo zimebadilishwa—zitakuwa tofauti. Hizo fikira na mawazo zinazotoka kwa sehemu zako ambazo hazijabadilika, vitu ambavyo wewe huvielewi kwa dhahiri, na vitu ambavyo hujabadilisha na uzoefu wa ukweli ni vichafu, vyenye taka na visivyovutia. Watu siku hizi, ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa miaka kadhaa, wana hisia na utambuzi kiasi wa mambo haya. Wale ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa kipindi cha muda mfupi bado hawaelewi mambo haya; bado hayako dhahiri. Bado hawajui udhaifu wao uko wapi au ni sehemu gani ambazo ni rahisi kwao kuanguka. Hamjui kwa sasa nyinyi ni mtu wa aina gani, na ingawa watu wengine wanaweza kuona kwa kiasi fulani nyinyi ni aina gani ya watu, hamuwezi kuhisi hilo. Hamuwezi kwa dhahiri kutofautisha fikira zenu za kawaida au nia, na hamna ufahamu dhahiri kuhusu asili ya mambo haya ni ipi. Jinsi unavyokielewa kipengele kwa kina, ndivyo utakavyozidi kubadilika katika kipengele hicho; hivyo, mambo unayoyafanya yatakuwa kwa mujibu wa ukweli, utakuwa na uwezo wa kuyatimiza mahitaji ya Mungu, na utakuwa karibu na mapenzi ya Mungu. Ni kwa kutafuta kwa njia hii tu ndipo utaweza kupata matokeo.

kutoka katika “Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

72. Mnaelewa vipi asili ya mwanadamu? Kuifahamu asili yako kunamaanisha kuchambua kina cha nafsi yako kwa kweli; kunahusu kile kilicho katika maisha yako. Ni mantiki ya Shetani na mitazamo mingi ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo daima; yaani, ni maisha ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo. Ni kwa kufichua tu sehemu za kina kabisa za nafsi yako ndio unaweza kuifahamu asili yako. Vitu hivi vinaweza kufichuliwa namna gani? Kwa njia ya vitendo tu, watu wengi hawawezi kufunua au kuvichambua; zaidi ya hayo, inaweza kuchukua miaka mitatu au mitano kabla uweze kupata hata ugunduzi na ufahamu mdogo wayo. Sasa, ili kujua asili yako, lazima utimize vitu vichache. Kwanza, lazima uwe na uelewa dhahiri wa kile upendacho. Hili halihusu vitu unavyopenda kula au kuvaa; bali, linamaanisha aina ya vitu unavyofurahia, vitu unavyohusudu, vitu unavyoabudu, vitu unavyotafuta, na vitu unavyozingatia moyoni mwako. Je, mnalielewa hili? Je, wajua aina gani za vitu zinahusishwa katika vitu unavyopenda? Ni vitu ambavyo wewe huzingatia, vitu unavyoviabudu, aina ya watu unaofurahia kuwasiliana nao, aina ya vitu unavyopenda kufanya, na aina ya watu unaopenda mno ndani ya moyo wako. Kwa mfano, watu wengi huwapenda watu mashuhuri, watu ambao ni wa madaha katika usemi wao na tabia zao, au kama wale ambao huzungumza kwa lugha ya ushawishi yenye sifa mno au wale ambao hujifanya. Lililotajwa hapa mbeleni linahusu watu ambao wanapenda kushirikiana nao. Kuhusu vitu ambavyo watu hufurahia, hivi vinajumlisha kuwa radhi kufanya vitu fulani ambavyo ni rahisi kufanya, kufurahia kufanya vitu ambavyo watu wengine hufikiri ni vizuri na ambavyo vitasababisha watu kuimba sifa na kupeana taadhima. Katika asili za watu, kuna sifa ya jumla kuhusu vitu ambavyo wao hupenda. Yaani, wanapenda vitu na watu ambao watu wengine wanahusudu kwa sababu ya mwonekano wa nje, wanapenda vitu na watu wanaoonekana wazuri na wa anasa, na wanapenda vitu na watu ambao huwafanya watu wengine kuwaabudu kwa sababu ya sura zao za nje. Vitu ambavyo watu hupenda ni vizuri, vya kung’aa, vya kupendeza, na vya fahari. Watu wote huabudu vitu hivi. Inaweza kuonekana kwamba watu hawana ukweli wowote, wala hawana mfano wa wanadamu wa kweli. Hakuna kiwango hata kidogo cha umuhimu katika kuabudu vitu hivi, ilhali watu bado huvipenda. … kila unachopenda, kile unachozingatia, kile unachoabudu, kile unachohusudu, na kile unachofikiria ndani ya moyo wako kila siku vyote ni viwakilishi vya asili yako. Inatosha kuthibitisha kwamba asili yako inapenda udhalimu, na katika hali mbaya, asili yako ni mbovu na isiyotibika. Unapaswa kuichambua asili yako kwa njia hii; yaani, chunguza kile unachopenda na kile unachoacha katika maisha yako. Labda wewe ni mzuri kwa mtu fulani kwa muda, lakini hili halithibitishi kwamba unampenda. Kile unachopenda sana kweli ndicho hasa kilicho katika asili yako; hata kama mifupa yako ingekuwa imevunjwa, bado ungekifurahia na hungeweza kukiacha. Hili si rahisi kubadilisha.

kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

73. Je, kujua asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, asili ya mtu inapaswa kutazamwa vipi kupitia vitu ambavyo mtu amefichua? Kwanza kabisa, unaweza kuona asili ya mtu kupitia mapendeleo yake. Jinsi gani? Mathalani, baadhi ya watu hususan hupenda kudansi, wengine hususan huwapenda waimbaji ama magwiji wa kuigiza filamu, na watu wengine hususan hupenda sana watu fulani mashuhuri. Kwa kutazama mapendeleo haya, ni nini asili ya watu hawa? Nitatoa mfano mwingine ambao ni rahisi: Wengine huenda wanampenda mwimbaji fulani mno, hata kwa kiasi kwamba wameshika kila mwondoko wa mwimbaji huyu, kila tabasamu, na kila neno lake. Wanatawaliwa na tama ya mwimbaji, na wanapiga picha kila kitu anachovaa mwimbaji huyu na kuiiga. Je, kiwango hiki cha kupenda mno kinaonyesha nini kuhusu asili ya mtu? Kinaonyesha kuwa moyo wa mtu kama huyu una vitu hivyo tu, wala hauna Mungu. Vitu vyote ambavyo mtu huyu huwaza, hupenda, na kutafuta vinafichuliwa kabisa na Shetani; vinamiliki moyo wa mtu huyu, ambao unajishughulisha sana na vitu hivyo. Je, unaona tatizo ni lipi? Ikiwa kitu kinapendwa kupita kiasi, basi kitu hicho kinaweza kuwa maisha ya mtu na kumiliki moyo wake, kudhihirisha wazi kuwa mtu huyo ni mwabudu sanamu asiyemtaka Mungu na badala yake anampenda ibilisi. Kwa hivyo tunaweza kufikia uamuzi kuwa asili ya mtu kama huyu ni ile inayopenda na kuabudu ibilisi, haipendi ukweli, na haimtaki Mungu. Je, hii ni njia sahihi kabisa ya kutazama asili ya mtu? Ni sahihi kabisa. Hivi ndivyo asili ya mtu inavyochanguliwa. Kwa mfano, watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, ni aina gani ya asili ambayo watu wenye tabia hizi humiliki? Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili zao.

kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

74. Inapofikia kujua asili ya wanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yao ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Wale wote walio wa ibilisi wote huishi kwa ajili yao wenyewe. Mitazamo yao ya maisha na kanunizinatoka kwa misemo ya Shetani, kama vile, “Kila mtu kivyake, na ibilisi achukue ya nyuma kabisa.” Maneno yaliyonenwa na hao ibilisi wafalme, wakuu, na wanafalsafa wa dunia yamekuwa maisha yao. Hasa, maneno mengi ya Konfyushasi, ambaye anatangazwa na watu wa Kichina kuwa “mtu mwenye hekima” yamekuwa maisha ya watuyamekuwa maisha ya watu. Pia kuna methali maarufu ya Ubudha na Utao, na misemo maarufu zaidi ya inayosemwa mara kwa mara ya watu mbalimbali mashuhuri; haya yote ni muhtasari wa falsafa ya Shetani na asili ya Shetani. Pia ni vielezo vizuri sana na maelezo ya asili ya Shetani. Sumu hizi ambazo zimetiliwa mioyoni mwa wanadamu zote hutoka kwa Shetani; hakuna hata chembe yao inayotoka kwa Mungu. Uongo na upuuzi kama huu pia ni upinzani wa moja kwa moja kwa neno la Mungu hasa. Ni wazi kabisa kuwa uhalisi wa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu, na vitu vyote hivyo hasi ambavyo huwatia sumu wanadamu hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa” ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya maisha ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. Ebu fikiri kumwuliza mtu ambaye amekuwa mtendaji katika jamii kwa miongo swali lifuatalo, “Umeishi duniani kwa muda mrefu sana na kutimiza mengi sana; je, unafuata misemo ipi maarufu?” “Muhimu sana ni ‘Wale ambao hutoa zawadi kwa wale wenye madaraka rasmi hawagongwi nao, na wale wasiojipendekeza hamna wanachofanikisha.’” Je, hufikiri kuwa hotuba kama hii ni uwakilishi wa asili yake? Asili yake si kuepuka mbinu zozote za kupata hadhi, kuwa na madaraka rasmi ndiko kunakompa uzima. Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika jinsi wanavyoshughulikia mambo, na katika mienendo yao na maafikiano na wengine—karibu wawe bila hata chembe ya ukweli—kwa mfano, falsafa zao za maisha, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, kinachobubujika kwa mifupa na damu ya watu ni vitu vya Shetani vyote. Wale maafisa wote, wale walio mamlakani, na wale wanaofaulu wana njia yao na siri ya kufaulu, hivyo si siri hiyo ni uwakilishi mzuri zaidi wa asili yake? Unaweza kuona kuwa asili ya watu hawa ni yenye hila sana–ni wenye madaraka rasmi ya juu na wameyafanya mambo makuu duniani. Hii inaonyesha kwamba asili yao ni yenye kudhuru kwa siri na ya sumu. Wanadamu wamapotoshwa kwa kina na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya binadamu ni potovu, ovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa ujumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na kumpinga. Asili ya mwanadamu inaweza kujulikana na kila mtu ikichanguliwa hivi.

kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

75. Kama ujuzi wa watu juu yao wenyewe ni wa juujuu sana, watapata kuwa haiwezekani kutatua matatizo, na tabia zao za maisha hazitabadilika kabisa. Ni muhimu kujijua mwenyewe kwa kiwango cha kina kabisa—ambayo inamaanisha kuijua asili yako mwenyewe—na kujua ni vipengele vipi vimejumuishwa katika asili hiyo, jinsi vinavyokuja kuwa na ni wapi vinatoka. Aidha, unaweza kuchukia mambo haya kweli? Je, umeona nafsi yako mwenyewe mbaya na asili yako mbovu? Ikiwa kwa hakika unaweza kuuona ukweli kujihusu mwenyewe, basi utaanza kujichukia mwenyewe kabisa. Wakati unapojichukia mwenyewe kabisa na kisha unatenda neno la Mungu, utakuwa na uwezo wa kunyima mwili na kuwa na nguvu ya kutekeleza ukweli bila shida. Kwa nini watu wengi hufuata tamaa zao za kimwili? Ni kwa sababu wanajiona kuwa wazuri kabisa; wanajihisi kuwa waadilifu na waliothibitishwa, kwamba hawana makosa, na hata kwamba wako sahihi kabisa. Kwa hiyo wao wanaweza kutenda kwa dhana kuwa haki iko upande wao. Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo—jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha—basi yeye si mwenye majivuno sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama hapo awali. Mtu kama huyo huhisi, “Lazima niwe mwenye ari na mpole, na nitende baadhi ya maneno ya Mungu. Kama sivyo, basi siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.” Kwa hakika mtu hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Wakati huu, inakuwa rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye ataonekana kwa kiwango fulani kuwa kama mwanadamu anavyopaswa kuwa. Ni pale tu ambapo watu kwa hakika hujichukia kabisa ndipo wanaweza kunyima mwili. Kama hawajichukii, hawataweza kunyima mwili. Mtu kujichukia kweli kunajumuisha mambo machache: Kwanza, kujua asili yake mwenyewe; na pili, kujiona kama yeye ni mwenye shida na wa kudharaulika, kujiona kuwa mdogo kupindukia na asiye na maana, na kuona nafsi yake kuwa yenye kudharaulika na chafu. Mtu anapoona kikamilifu kile alicho kwa hakika, na matokeo haya yakafikiwa, basi yeye kweli hupata ufahamu juu yake mwenyewe, na inaweza kusemwa kwamba amekuja kujijua mwenyewe kikamilifu. Ni hapo tu ndipo anaweza kwa hakika kujichukia mwenyewe, kufikia hata kujilaani mwenyewe, na ahisi kwa kweli kwamba amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hafanani tena na mwanadamu. Kisha, siku moja, wakati tishio la kifo linapoonekana, mtu kama huyu atafikiri, “Hii ni adhabu ya haki ya Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye haki; Kwa hakika mimi lazima nife!” Wakati huu, yeye hatalalamika, wala kumlaumu Mungu, akihisi tu kwamba yeye ni wa kudharaulika, mchafu sana na mpotovu, kwamba anapaswa kuangamizwa na Mungu na roho kama yake haifai kuishi duniani. Wakati huu, mtu huyu hatampinga Mungu, sembuse kumsaliti Mungu au kulalamika dhidi ya Mungu. Iwapo mtu hajijui mwenyewe, na bado hujiona kuwa mzuri sana, basi wakati kifo kinapokuja kubisha, mtu huyu atafikiria, “Nimetenda vyema sana katika imani yangu. Jinsi nimetafuta kwa nguvu! Nimejitolea mengi sana, nimeumia sana, ilhali hatimaye, Mungu sasa ananiuliza nife. Sijui haki ya Mungu iko wapi. Kwa nini Ananitaka nife? Ikiwa hata mtu kama mimi anafaa kufa, basi ni nani atakayeokolewa? Je! Si jamii ya wanadamu itafikia mwisho?” Kwanza kabisa, mtu huyu ana dhana juu ya Mungu. Pili, mtu huyu analalamika, na hatii hata kidogo. Hii ni kama tu Paulo: Wakati alipokaribia kufa, hakujijua mwenyewe, Na kufikia wakati adhabu ya Mungu ilipokaribia, hakukuwa na muda wa kutubu.

kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

76. Ili kuwaruhusu watu wajijue, Mungu ametumia mbinu nyingi tofauti. Yeye huwaruhusu watu kupata maarifa fulani juu yao wenyewe polepole kupitia uzoefu. Iwe ni majaribu, hukumu au kuadibu, Mungu huwaruhusu watu kupata uzoefu bila kukoma katika maneno Yake na katika ukweli halisi. Watu hupitia hukumu, kuadibu na kufundishwa nidhamu na maneno ya Mungu, na wao pia hupitia nuru na mwangaza wa maneno ya Mungu. Wakati huo huo, Yeye huwaruhusu watu kutambua upotovu, uasi na asili yao. Kwa hivyo lengo la msingi la yote haya ni lipi? Lengo hili la msingi ni kumruhusu kila mtu anayepitia kazi ya Mungu kujua watu ni nini. Je, “watu ni nini” inajumuisha nini? Inajumuisha kuwaruhusu watu kutambua utambulisho, nafasi, wajibu, na jukumu lao. Ni kukujulisha watu ni nani na wewe mwenyewe ni nani. Hili ni lengo la mwisho la Mungu kuwaruhusu watu wajijue.

kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

77. Kila kitu ambacho kiko ndani ya mioyo yetu kinampinga Mungu. Hii ni pamoja na vitu tunavyofikiria kuwa ni vizuri, na hata vile tunavyoamini tayari kuwa ni chanya. Tumeorodhesha vitu hivi kama ukweli, kama sehemu ya ubinadamu wa kawaida, na kama vitu chanya; hata hivyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, ni vitu Anavyovichukia. Je, ghuba kati ya kile tunachofikiri na ukweli ambao Mungu huzungumza ni kubwa vipi? Ni ya kupita kiasi. Kwa hivyo, lazima tujijue. Kuanzia mawazo yetu, mitazamo, na vitendo hadi elimu ya kitamaduni ambayo tumepokea, kila kitu kinafaa kuchunguzwa kwa undani na kuchambuliwa kwa kina. Baadhi ya vitu hivi vinatokana na mazingira ya kijamii, vingine hutoka kwa familia, vingine hutoka kwa masomo ya shule, na vingine hutoka kwenye vitabu. Vingine pia hutoka kwa fikira na mawazo yetu. Vitu kama hivi ni vya kutisha zaidi, kwani hufunga na kudhibiti maneno na matendo yetu, hutawala akili zetu, na kuelekeza nia, dhamira na malengo yetu katika kile tunachofanya. Tusipochimbua vitu hivi, hatutawahi kuyakubali maneno ya Mungu ndani yetu kwa ukamilifu, na hatutawahi kukubali matakwa ya Mungu bila kusita na kuyaweka katika matendo. Almradi unahodhi mawazo na mitazamo yako mwenyewe, na misimamo kuhusu mambo ambayo unaamini kuwa sahihi, kamwe hutakubali maneno ya Mungu kabisa au kwa ukamilifu, wala hutayatenda yakiwa katika hali yao ya asili; bila shaka utayaweka tu kwenye vitendo baada ya kuyatafakari kwanza akilini mwako. Hii itakuwa jinsi ambavyo utafanya mambo, na pia itakuwa njia ambayo utawasaidia wengine kuchanganya vipengele vichache vya binadamu na vipengele vichache kutoka Mungu. Utaendelea kuamini kwamba matendo kama hayo yanamaanisha kwamba unaweka ukweli katika vitendo, kwamba umepata ufahamu wa ukweli na kwamba una kila kitu. Je, si hali ya wanadamu ni ya kusikitisha? Si inatisha?

kutoka katika “Ni kwa Kujua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

78. Ili ujijue, ni lazima ujue kiini chako potovu, udhaifu wako mkuu, tabia yako, na asili yako. Lazima pia ujue, maelezo yote kabisa, mambo hayo ambayo hufichuliwa katika maisha yako ya kila siku—nia zako, mitazamo yako, na msimamo wako kuhusu kila kitu—iwe uko nyumbani au nje, unapokuwa kwenye mikusanyiko, unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu, au katika kila suala unalokumbana nalo. Kupitia vitu hivi lazima uje kujijua. Ili kujijua kwa kina, lazima ujumuishe maneno ya Mungu; unaweza tu kupata matokeo kwa kujijua kulingana na maneno Yake.

kutoka katika “Umuhimu na Njia ya Kufuatilia Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

79. La muhimu katika kufikia badiliko katika tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima lifanyike kulingana na ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake mbaya, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake. Baada ya haya kujulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kujichukia na kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi utakuwa umeianza njia ya Petro.

kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

80. Unawezaje kujua kiini cha mtu ni kipi? Huwezi kujua asili na kiini cha mtu ni kipi asipofanya chochote au anapofanya jambo dogo. Vitu hivi huonyeshwa katika kile anachodhihirisha mara kwa mara, katika nia za matendo yake, katika dhamira ya kile anachofanya, katika matamanio aliyo nayo, na katika njia anayoitembea. Muhimu hata zaidi, vitu hivi huonyeshwa katika jinsi anavyojibu anapokutana na mazingira yaliyopangwa na Mungu, anapokutana na kitu alichofanyiwa yeye mwenyewe na Mungu, anapojaribiwa na kusafishwa, au kushughulikiwa na kupogolewa, la sivyo wakati ambapo Mungu Mwenyewe anamwangazia na kumwongoza. Je, yote haya yanahusisha nini? Yanahusisha vitendo vya mtu, jinsi anayoishi, na kanuni ambazo yeye hutumia hutenda. Pia yanahusisha mwelekeo na malengo ya ufuatiliaji wake, na mbinu anazozitumia kufuatalia. Kwa maneno mengine njia anayochukua mtu huyu, jinsi anavyoishi, kile anachoishi kwa kufuata, na kile kilicho msingi wa kuwepo kwake.

kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Asili na Kiini cha Paulo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

81. Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au unastahili kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hebu tumchukue Paulo kama mfano. Paulo alikuwa mwenye maarifa mno, na alivumilia mengi katika kazi yake ya kuhubiri. Watu wengi walimpenda mno. Kama matokeo, baada ya kumaliza kazi nyingi, alidhani kungekuwa na taji lililowekwa kando kwa ajili yake. Hili lilimfanya atembee zaidi na zaidi kwenye njia isiyo sahihi, hadi mwishowe akaadhibiwa na Mungu. Ikiwa, wakati huo, angetafakari juu yake mwenyewe na kujichambua, basi asingefikiria hivyo. Kwa maneno mengine, Paulo hakuwa amelenga kutafuta ukweli katika maneno ya Bwana Yesu; alikuwa tu ameamini mawazo na fikira zake mwenyewe. Alikuwa amedhani kwamba almradi afanye mambo machache mazuri na kuonyesha tabia nzuri, angesifiwa na kutuzwa na Mungu. Mwishowe, mawazo na fikira zake zilipofusha roho yake na kufunika hali yake ya kweli. Hata hivyo, watu hawakujua hili, na bila Mungu kuliweka wazi, waliendelea kumweka Paulo kama kiwango cha kufikia, mfano wa kuishi kulingana naye, na wakamwona kama ambaye walitamani kuwa kama. Paulo aligeuka lengo la ufuatiliaji wao na kitu cha kuigwa nao. Hadithi hii kumhusu Paulo inatumika kama onyo kwa kila mtu amwaminiye Mungu, ambalo ni kwamba wakati wowote tunapohisi kuwa tumefanya vizuri zaidi, au kuamini kwamba tuna vipawa zaidi katika mambo fulani, au kufikiria kwamba hatuhitaji kubadilika au kushughulikiwa katika jambo fulani, tunapaswa kujitahidi kutafakari na kujijua wenyewe zaidi katika suala hilo; jambo hili ni muhimu. Hii ni kwa sababu bila shaka hujafichua, kutilia maanani au kuchanganua vipengele kujihusu ambavyo mnanafikiri mmefanya vyema, ili kuona kama kweli vina chochote kinachompinga Mungu au la.

kutoka katika “Ni kwa Kujua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

82. Daima kuna tofauti kubwa kati ya jinsi watu wanavyoelewa asili zao wenyewe na jinsi ambavyo Mungu amefichua asili ya binadamu. Hili si kosa katika lile ambalo Mungu hulifuanua, bali badala yake ni ukosefu wa wanadamu wa ufahamu wa kina wa asili yao. Watu hawana ufahamu wa kimsingi au wa kutosha wa wao wenyewe; badala yake, wao wanalenga na kutenga nguvu zao kwa matendo na maonyesho ya nje. Hata kama mtu fulani angelisema jambo mara chache kuhusu kujifahamu, halingekuwa la kina sana. Hakuna mtu aliyewahi kufikiria kwamba yeye ni aina hii ya mtu au ana asili ya aina hii kutokana na kulitenda jambo kama hili au kulifunua jambo. Mungu ameifunua asili na kiini cha mwanadamu, lakini wanadamu wanafahamu kwamba njia yao ya kuyatenda mambo na njia yao ya kusema ni yenye mawaa na yenye kasoro; kwa hiyo, ni kazi yenye kutumia juhudi nyingi kwa watu kutia ukweli katika vitendo. Watu wanafikiria kwamba makosa yao ni udhihirisho wa muda tu ambao unafunuliwa bila kujali, badala ya kuwa ufunuo wa asili yao. Watu ambao hujiona kwa namna hii hii hawawezi kuweka ukweli katika vitendo, kwa sababu hawawezi kukubali ukweli kama ukweli na hawatamani ukweli; kwa hiyo, wakati wanatia ukweli wao katika vitendo wanaifuata tu sheria kwa uzembe. Watu hawaoni asili yao wenyewe kama iliyo potovu sana, na wanaamini kwamba wao si wabaya sana kiasi kwamba wanapaswa kuangamizwa au kuadhibiwa. Wao hufikiri kuwa si jambo kubwa kudanganya mara kwa mara, na hujiona kuwa bora zaidi kuliko jinsi walivyokuwa zamani; kwa kweli, lakini kufuatana na viwango, kuna tofauti kubwa sana katika hili, kwa sababu watu wana maendo fulani tu ambayo kwa nje hayakiuki ukweli, wakati kwa kweli hawatii ukweli katika vitendo.

kutoka katika “Kuifahamu Asili na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

83. Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini hisia zako ni kali sana? Kwa nini unapenda vitu hivyo ambavyo si ya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa mambo haya ni upii? Yanatoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kukubali mambo haya? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba yana sumu ya Shetani. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini wanatenda hivyo, watajibu, “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida: Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanatenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Watu wote hudhani kwamba ni “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine,” hivyo ndivyo tu ilivyo, kwa hivyo kila mtu anafaa kujiishia mwenyewe tu—“kujitafutia nafasi kwa ajili ya starehe za viumbe.” “Kila mtu ajali maslahi yake kwanza, bila kuwafikiria wengine”—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili yake. Kauli hii ni hasa sumu ya Shetani, na inapowekwa moyoni na watu inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na hii kwa maelfu ya miaka. Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anatamani kumpita Mungu, kujiondoa Kwake na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba; kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi watu hujaribu kuificha, katika kila kitu wafanyacho na kila kitu wasemacho, hawawezi kuificha asili yao. Kuna wengine ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini punde tu wengine wanapoingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe, wengine hufikia hitimisho hili: Mtu huyo kamwe hasemi neno lolote la ukweli na ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili ya mtu wa aina hiyo; ni ushahidi na kielezo cha asili yake; falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Asili ya kishetani ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa. Wakati mwingine wewe mwenyewe huna hata habari ya hilo na hulielewi, ilhali kila muda wa maisha yako unategemea hilo. Isitoshe, unafikiri kuwa falsafa hii ni sahihi sana, yenye mantiki na isiyo na kosa. Falsafa ya Shetani imekuwa ukweli wa watu, na wanaishi kulingana na falsafa ya Shetani kabisa, bila kumpinga hata kidogo. Kwa hivyo, kila mara wanaonyesha asili yao ya kishetani. mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na katika vipengele vyote, wanaishi daima kulingana na falsafa ya ya kishetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu.

kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:(V) Maneno Juu ya Kuelewa Kazi ya Roho Mtakatifu na Kutambua Kazi ya Pepo Wabaya

Inayofuata:(VII) Maneno Juu ya Jinsi ya Kuwa Mtu Mwaminifu

Maudhui Yanayohusiana

 • Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

  Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jamb…

 • Kazi na Kuingia (4)

  Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira…

 • Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

  Wale miongoni mwa ndugu ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani, na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolew…

 • Maana ya Kuwa Mtu Halisi

  Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu hue…