D. Juu ya Jinsi ya Kupitia Hukumu na Kuadhibiwa, na Majaribu na Usafishwaji

366. Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kutompitisha mwanadamu katika hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki: basi usimamizi wa Mungu ungetamatishwa lini? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

367. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa hasi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: “Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili!” Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha ukaja wakati wa kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

368. Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni utakuwa kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Bila kujali jinsi ambavyo Mungu huwaokoa watu, yote hufanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye huwaokoa kwa kuwafanya watafute uzima. Wasipotafuta uzima basi hawatakuwa na njia yoyote ya kukubali wokovu wa Mungu. Wokovu ni kazi ya Mungu Mwenyewe na kutafuta uzima ni kitu ambacho mwanadamu anapaswa kumiliki ili kupokea wokovu. Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili kwamba waweze kumpa Mungu mioyo yao. Hivyo ni kusema, Yeye kumgusa mwanadamu ni kumwokoa. Aina hii ya wokovu inafanywa kwa kufanya makubaliano. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu atatiimbele ya jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, iwe hukumu ya haki au usafishaji na adhabu visivyo na huruma, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kila anaainishwa kulingana na aina yake, ama makundi ya wanadamu yanafichuliwa, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

369. Anapokabiliwa na hali ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu, Mungu amefanya kazi mpya, Akimruhusu mwanadamu kuwa na ufahamu Wake na utiifu Kwake, na upendo pia na ushahidi. Hivyo, mwanadamu lazima apitie usafishaji wa Mungu kwake, na pia hukumu, ushughulikiaji na upogoaji Wake kwake, ambazo pasi nazo mwanadamu hangewahi kumjua Mungu, na hangewahi kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli na kuwa na ushuhuda Kwake. Usafishaji wa Mungu kwa mwanadamu sio tu kwa ajili ya athari inayoegemea upande mmoja, bali kwa ajili ya athari inayogusia pande nyingi. Ni kwa jinsi hii tu ndiyo Mungu hufanya kazi ya usafishaji kwa wale ambao wako tayari kutafuta ukweli, ili upendo na uamuzi wao ufanywe timilifu na Mungu. Kwa wale walio tayari kuutafuta ukweli na wanaomtamani Mungu, hakuna kilicho cha maana zaidi, au cha usaidizi zaidi, kuliko usafishaji kama huu. Tabia ya Mungu haijulikani wala kueleweka kwa urahisi sana na mwanadamu, kwani Mungu, hatimaye, ni Mungu. Mwishowe, haiwezekani kwa Mungu kuwa na tabia sawa na mwanadamu, na hivyo si rahisi kwa mwanadamu kujua tabia Yake. Ukweli haumilikiwi kwa asili na mwanadamu, na hauleweki kwa urahisi na wale ambao wamepotoshwa na Shetani; mwanadamu hana ukweli na hana azimio la kutia ukweli katika vitendo, na asipoteseka, na asisafishwe au kuhukumiwa, basi uamuzi wake hautawahi kufanywa timilifu. Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli

370. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

371. Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu mtapitia mchakato huu, na mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu. Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea kwa nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli

372. Mnapopitia shida au kikwazo kidogo, ni yenye manufaa kwenu; kama lingekuwa jambo rahisi kwenu basi mngeangamia, na kisha mngelindwaje? Leo, ni kwa sababu mnaadibiwa, kuhukumiwa, na kulaaniwa ndiyo mnapewa ulinzi. Ni kwa sababu mmeteseka sana ndiyo mnalindwa. Kama sivyo, mngekuwa tayari mmepotoka. Huku si kufanya mambo yawe magumu kwenu kwa makusudi—asili ya mwanadamu ni ngumu kubadili, na lazima iwe hivyo ili tabia zao zibadilishwe. Leo, hamna hata dhamiri au akili ambazo Paulo alikuwa nazo, wala hamwezi hata kujitambua kama yeye. Lazima mushurutishwe kila wakati, na kila wakati lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili roho zenu zichangamshwe. Kuadibu na hukumu ndivyo bora kabisa kwa maisha yenu. Na inapolazimu, lazima pia ukweli unaowafikia uadibiwe; ni hapo tu ndipo mtakapotii kikamilifu. Asili zenu ni kana kwamba bila kuadibu na kulaani, hamngetaka kuinamisha vichwa vyenu, hamngetaka kutii. Bila ukweli ulio mbele yenu, hakungekuwa na matokeo. Ninyi ni duni sana na msio na thamani katika tabia! Bila kuadibu na hukumu, itakuwa vigumu kwenu kushindwa, na itakuwa vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kushindwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngefahamu urefu wa mbingu na kina cha dunia, sembuse kujua mnakoelekea. Hamjui hata mlikotoka, hivyo mngewezaje kumjua Bwana wa uumbaji? Bila kuadibiwa na kulaaniwa kwa wakati unaofaa leo, siku yenu ya mwisho ingekuwa imeshawadia kitambo. Hiyo ni kando na majaaliwa yenu—je, hayo hayatakuwa katika hatari ya karibu zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati unaofaa, ni nani anayejua jinsi ambavyo mngekuwa wenye kiburi, au jinsi ambavyo mngekuwa wapotovu. Kuadibu huku na hukumu hii vimewafikisha leo, na vimehifadhi kuwepo kwenu. Kama bado “mngeelimishwa” kwa kutumia njia zile zile kama za “baba” yenu, ni nani ajuaye mngeingia katika ulimwengu upi! Hamna uwezo wa kujidhibiti na kutafakari kujihusu wenyewe hata kidogo. Kwa watu kama ninyi, mkifuata na kutii tu bila kusababisha ukatizaji au usumbufu wowote, malengo Yangu yatatimia. Je, hamfai kufanya vema zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Je, mna chaguo gani jingine?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (6)

373. Kwa kila hatua ya kazi ya Mungu, kunayo njia ambayo watu wanapaswa washirikiane. Mungu Anawasafisha watu ili wawe na imani katikati ya usafishaji. Mungu Anawakamilisha watu ili wawe na imani ya kukamilishwa na Mungu na wako tayari kuukubali usafishaji Wake na kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Roho wa Mungu Anafanya kazi ndani ya watu ili kuwaletea nuru na mwangaza, na kuwafanya washirikiane Naye na kutenda. Mungu Haneni wakati wa usafishaji. Hatoi sauti Yake, lakini bado kuna kazi ambayo watu wanapaswa kuifanya. Unapaswa kushikilia kile ambacho unacho tayari, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kusimama shahidi mbele ya Mungu; hivi utatimiza wajibu wako mwenyewe. Nyinyi wote mnapaswa muone kwa dhahiri kutoka kwa kazi ya Mungu kuwa majaribu Yake ya imani ya watu na upendo inahitaji kuwa waombe zaidi kwa Mungu, na kwamba waonje maneno ya Mungu mbele Zake mara kwa mara. Mungu Akikupa nuru na kukufanya kuelewa mapenzi Yake lakini huyaweki katika matendo hata kidogo, hutapata chochote. Unapoyaweka maneno ya Mungu katika matendo, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba, na unapoyaonja maneno Yake unapaswa utafute kila wakati mbele Zake na uwe umejaa imani Kwake bila kuvunjika moyo ama kuwa baridi. Wale wasioweka maneno ya Mungu katika matendo wamejawa na nguvu katika mikusanyiko, lakini wanaanguka katika giza wanaporudi nyumbani. Kuna wengine ambao hawataki hata kukusanyika pamoja. Kwa hivyo lazima uone kwa wazi ni wajibu gani ambao watu wanapaswa kutimiza. Unaweza kukosa kujua mapenzi ya Mungu ni nini hasa, lakini unaweza kutekeleza wajibu wako, unaweza kuomba inapopaswa, unaweza kuuweka ukweli katika matendo unapopaswa, na unaweza kufanya kile watu wanapaswa kufanya. Unaweza kushikilia maono yako asili. Hivi, utaweza kukubali zaidi hatua ya Mungu inayofuata. Ni shida ukikosa kutafuta wakati ambapo Mungu anafanya kazi katika njia iliyofichika. Anaponena na kuhubiri katika mabaraza, unasikiza kwa shauku, lakini Asiponena unakosa nguvu na kurudi nyuma. Mtu wa aina gani anafanya hivi? Huyu ni mtu ambaye tu anaenda na mkondo. Hana msimamo, hawana ushuhuda, na hawana maono! Watu wengi wako hivyo. Ukiendelea katika njia hiyo, siku moja utakapopitia jaribio kuu, utateremka katika adhabu. Kuwa na msimamo ni muhimu sana katika kukamilishwa kwa watu na Mungu. Kama huna shaka na hatua yoyote ya kazi ya Mungu, unatimiza wajibu ya mwanadamu, unashikilia kwa uaminifu kile Mungu Amekufanya ukiweke katika matendo, hiyo ni, unakumbuka mawaidha ya Mungu, na haijalishi Anachokifanya sasa husahau mawaidha Yake, huna shaka kuhusu kazi Yake, unadumisha msimamo wako, kushikilia ushahidi wako, na una ushindi katika kila hatua ya njia, mwishowe utakamilishwa kuwa mshindi na Mungu. Kama unaweza kusimama imara katika kila hatua ya majaribu ya Mungu, na bado unaweza kusimama imara hadi mwisho kabisa, wewe ni mshindi, na wewe ni mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Kama huwezi kusimama imara katika majaribu yako ya sasa, baadaye itakuwa hata vigumu zaidi. Ukipitia mateso kidogo yasiyo ya muhimu na usiufuate ukweli, hutapata chochote mwishowe. Utakuwa mkono mtupu. Kuna watu wengine ambao wanaacha kufuata wanapoona kuwa Mungu Haneni, na moyo wao unatawanyika. Je, si huyo ni mjinga? Watu wa aina hii hawana ukweli. Mungu Anenapo, wanakimbia huku na kule kila wakati, wakiwa na shughuli nyingi na kuwa na shauku kwa nje, lakini sasa Haneni, hawatafuti tena. Mtu kama huyu hana maisha ya usoni. Katika usafishaji, lazima uingie ndani kutoka kwa mtazamo halisi na usome masomo unayostahili kusoma; unapomwomba Mungu na kusoma neno Lake, unapaswa kulinganisha hali yako mwenyewe nayo, utambue pungufu zako, na ujue kuwa una somo mengi sana unayofaa kusoma. Unapotafuta kwa uaminifu katikati ya usafishaji, ndipo utakapojipata kuwa una pungufu. Unapokuwa unapitia usafishaji kunayo masuala mengi ambayo unapitia; hautayaona kwa wazi, unalalamika, unatambulisha mwili wako wenyewe—ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kugundua kwamba una tabia nyingi sana potovu ndani yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

374. Wakati wanapitia majaribu, ni kawaida kwa watu kuwa dhaifu, au kuwa na uhasi ndani yao, au kukosa uwazi juu ya mapenzi ya Mungu au njia yao ya kutenda. Lakini katika hali yoyote, lazima uwe na imani katika kazi ya Mungu, na usimkane Mungu, kama tu Ayubu. Ingawa Ayubu alikuwa dhaifu na aliilaani siku yake ya kuzaliwa, yeye hakukana kwamba vitu vyote katika maisha ya binadamu vilikuwa vimetolewa na Yehova, na kwamba Yehova pia Ndiye anayeyachukua vyote. Haijalishi jinsi alivyojaribiwa, alidumisha imani hii. Katia kupitia kwako, haijalishi ni usafishaji gani unaopitia katika maneno ya Mungu, kile Mungu anahitaji kutoka kwa wanadamu kwa ufupi ni imani yao na upendo wao Kwake. Anachokamilisha kwa kufanya kazi kwa njia hii ni imani, upendo na matarajio ya watu. Mungu hufanya kazi ya ukamilisho kwa watu, nao hawawezi kuiona, hawawezi kuihisi; katika hali kama hizi imani yako inahitajika. Imani ya watu inahitajika wakati ambao kitu hakiwezi kuonekana kwa macho tu, na imani yako inahitajika wakati huwezi kuziachilia dhana zako mwenyewe. Wakati ambapo huna uwazi kuhusu kazi ya Mungu, kinachohitajika kutoka kwako ni kuwa na imani uchukue msimamo imara na kuwa shahidi. Wakati Ayubu alifikia hatua hii, Mungu alimwonekania na kuzungumza naye. Yaani, ni kutoka ndani ya imani yako tu ndipo utaweza kumwona Mungu, na wakati una imani Mungu atakukamilisha. Bila imani, Hawezi kufanya hivyo. Mungu ataweka juu yako chochote ulicho na matumaini ya kupata. Kama huna imani, basi huwezi kukamilishwa na hutakuwa na uwezo wa kuona matendo ya Mungu, sembuse kudura Yake. Wakati una imani kwamba utaona matendo Yake katika uzoefu wako wa utendaji, basi Mungu atakuonekania, na Atakupa nuru na kuongoza kutoka ndani. Bila hiyo imani, Mungu hataweza kufanya hivyo. Kama umepoteza matumaini katika Mungu, utawezaje kupata uzoefu wa kazi Yake? Kwa hiyo, ni wakati tu una imani na huweki mashaka kumhusu Mungu, ni wakati una imani ya kweli Kwake tu bila kujali Anachokifanya ndipo Atakuangazia na kukupa nuru kupitia katika mapito yako, na ni hapo tu ndipo utaweza kuona matendo Yake. Mambo haya yote yanafanikishwa kupitia kwa imani. Imani huja kupitia tu usafishaji, na wakati hakuna usafishaji, imani haiwezi kukua. Je, neno hili “imani”, linarejelea nini? Imani ni kusadiki kwa kweli na moyo wa dhati ambao wanadamu wanapaswa kumiliki wakati wao hawawezi kuona au kugusa kitu, wakati kazi ya Mungu haiambatani na za binadamu, wakati inazidi uwezo wa binadamu. Hii ndiyo imani Ninayozungumzia. Watu wanahitaji imani katika nyakati za shida na usafishaji, na imani ni kitu kinachofuatwa na usafishaji; usafishaji na imani haviwezi kutenganishwa. Haijalishi jinsi Mungu anavyofanya kazi, na haijalishi mazingira uliyomo, unaweza kufuatilia maisha na kutafuta ukweli, na kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu, na kuwa na ufahamu wa matendo Yake, na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Kufanya hivi ndiko kuwa na imani ya kweli, na kufanya hivyo kunaonyesha kwamba hujapoteza imani katika Mungu. Unaweza tu kuwa na imani ya kweli katika Mungu ikiwa bado unaweza kuendelea kufuatilia ukweli kupitia ukiwa katika usafishaji, ikiwa unaweza kumpenda Mungu kwa kweli na huna na mashaka kumhusu Yeye, ikiwa bila kujali Anachokifanya bado unatenda ukweli kumridhisha Yeye, na ikiwa unaweza kutafuta kwa dhati mapenzi Yake na ujali mapenzi Yake. Zamani, wakati Mungu alisema kwamba ungetawala kama mfalme, ulimpenda, na wakati Alijionyesha hadharani kwako, ulimfuata. Lakini sasa Mungu amejificha, huwezi kumwona, na shida zimekujia—je, hapo unapoteza matumaini kwa Mungu? Hivyo, lazima ufuatilie uzima wakati wote na kutafuta kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hii inaitwa imani ya kweli, na huu ndio aina ya upendo ulio wa kweli na mzuri zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

375. Kusudi la kazi ya usafishaji kimsingi ni ya kukamilisha imani ya watu. Mwishowe, kile kinachofanikishwa ni kwamba unataka kuondoka lakini, wakati huo huo, huwezi; baadhi ya watu bado wanaweza kuwa na imani hata wakati wanaondolewa hata chembe kidogo cha matumaini; na watu hawana tena tumaini kabisa kuhusu matarajio ya siku za zao za usoni. Ni katika wakati huu tu ndipo usafishaji wa Mungu utafikia kikomo. Mwanadamu bado hajafikia hatua ya kuelea kati ya maisha na kifo, na hajaonja mauti, hivyo mchakato wa usafishaji bado haujakamilika. Hata wale ambao walikuwa katika hatua ya watenda huduma hawakuwa wamesafishwa kabisa. Ayubu alipitia usafishaji mkali sana, na hakuwa na kitu cha kutegemea. Watu lazima wapitie usafishaji mpaka ile hatua ambayo hawana matumaini na kitu cha kutegemea—huu tu ndio usafishaji wa kweli. Wakati wa watenda huduma, ikiwa moyo wako daima ulikuwa umetulia mbele ya Mungu, na ikiwa pasipo kujali Alichofanya na pasipo kujali mapenzi Yake kwa ajili yako yalikuwa nini, wewe daima ulitii mipango Yake, basi mwishoni ungeelewa kila kitu ambacho Mungu alikuwa amefanya. Unapitia majaribu ya Ayubu, na wakati uo huo unapitiaa majaribu ya Petro. Wakati Ayubu alijaribiwa, yeye alikuwa shahidi, na mwishowe, Yehova alidhihirishwa kwake. Ni baada tu ya kuwa shahidi ndipo alistahili kuona uso wa Mungu. Kwa nini inasemwa: “Mimi najificha kutoka nchi ya uchafu lakini Najionyesha kwa ufalme mtakatifu”? Hiyo ina maana kwamba wakati tu uko mtakatifu na kuwa shahidi ndipo unaweza kuwa na hadhi ya kuuona uso wa Mungu. Kama huwezi kuwa shahidi kwa ajili Yake, hauna hadhi ya kuuona uso Wake. Ukijiondoa au kufanya malalamiko kwa Mungu ukikabiliwa na usafishaji, hivyo ushindwe kuwa shahidi Wake na uwe kichekesho cha Shetani, basi hutapata sura ya Mungu. Kama wewe ni kama Ayubu, ambaye katikati ya majaribu aliulaani mwili wake na wala hakulalamika dhidi ya Mungu, na aliweza kuuchukia mwili wake bila kulalamika au kutenda dhambi kwa njia ya maneno yake, basi utakuwa shahidi. Unapopitia usafishaji kwa kiasi fulani na bado unaweza kuwa kama Ayubu, mtiifu kabisa mbele ya Mungu na bila mahitaji mengine Kwake au dhana zako mwenyewe, basi Mungu atakuonekania.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

376. Uzoefu wako mwingi wa kushindwa, udhaifu, nyakati zako za uhasi, vyote vinaweza kusemekana kuwa majaribu ya Mungu. Hii ni kwa sababu kila kitu hutoka kwa Mungu, na mambo yote na matukio yako katika mikono Yake. Kama unashindwa au kama wewe ni dhaifu na unajikwaa, yote yako kwa Mungu na vipo katika mfumbato Wake. Kutoka kwa mtazamo wa Mungu, haya ni majaribu yako, na kama huwezi kutambua hivyo, yatageuka majaribu. Kuna aina mbili za hali ambazo watu wanapaswa kutambua: Moja inatoka kwa Roho Mtakatifu, na chanzo cha nyingine huenda ni Shetani. Moja ni hali ambamo Roho Mtakatifu anakuangazia na Anakuruhusu upate kujijua mwenyewe, kuchukia na kuhisi majuto kujihusu mwenyewe na kuweza kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu, kuweka moyo wako katika kumridhisha Yeye. Nyingine ni hali ambamo unajijua mwenyewe, lakini wewe ni hasi na dhaifu. Inaweza kusemwa pia kuwa hii ni hali ya usafishaji wa Mungu, na pia kuwa ni ushawishi wa Shetani. Ukitambua kuwa huu ni wokovu wa Mungu kwako na ukihisi kuwa wewe sasa ni mdeni Wake mkubwa, na kama kuanzia sasa utajaribu kulipa deni Lake na usianguke tena katika upotovu kama huo, kama utaweka juhudi katika kula na kunywa maneno Yake, na kama siku zote unajichukua kama anayekosa, na kuwa na moyo wa hamu, basi haya ni majaribu ya Mungu. Baada ya mateso kumalizika na wewe kwa mara nyingine tena unasonga mbele, Mungu bado atakuongoza, atakuangazia, atakupa nuru, na kukusitawisha. Lakini kama hulitambui na wewe ni hasi, kujiachilia tu kukata tamaa, kama unafikiri hivi, basi kishawishi cha Shetani kimekufikia. Wakati Ayubu alipitia majaribu, Mungu na Shetani walikuwa wanawekeana dau, na Mungu alimruhusu Shetani amtese Ayubu. Hata ingawa ilikuwa ni Mungu aliyekuwa anamjaribu Ayubu, hakika alikuwa ni Shetani ndiye aliyemjia. Kwa Shetani, ilikuwa ni kumjaribu Ayubu, lakini Ayubu alikuwa upande wa Mungu. Kama haingekuwa vile, basi Ayubu angeanguka katika kishawishi. Mara baada ya watu kuanguka katika kishawishi, wao huanguka katika hatari. Kupitia usafishaji inaweza kusemwa kuwa jaribu kutoka kwa Mungu, lakini kama hauko katika hali nzuri inaweza kusemwa kuwa kishawishi kutoka kwa Shetani. Kama hauko na uwazi juu ya maono, Shetani atakushutumu na kukuvuruga katiza mtazamo wa maono. Kabla ya kujua, utaanguka katika majaribu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

377. Katikati ya majaribu, hata kama hajui ni nini Mungu Anataka kufanya na kazi gani Anataka kukamilisha, unafaa kujua kuwa nia za Mungu kwa wanadamu ni nzuri kila wakati. Ukimfuata na moyo wa kweli, Hatawahi kukuacha, na mwishowe kwa kweli Atakukamilisha, na kuwaleta watu katika mwisho unaofaa. Haijalishi ni vipi Mungu Anawajaribu watu kwa sasa, kuna siku moja ambayo Atawatolea watu matokeo yanayofaa na kuwapa adhabu inayofaa kulingana na kile ambacho wamefanya. Mungu Hatawaongoza watu hadi kituo fulani halafu Awatupe tu kando na kuwapuuza. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwaminifu. Katika hatua hii, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya usafishaji. Anamsafisha kila mmoja. Katika hatua za kazi zilizoundwa na majaribu ya kifo na majaribu ya kuadibu, usafishaji katika wakati huo ulikuwa usafishaji kupitia maneno. Ili watu wapate uzoefu wa kazi ya Mungu, lazima kwanza waelewe kazi Yake ya sasa na kuelewa jinsi wanadamu wanafaa kushirikiana. Hili ni jambo ambalo kila mtu anafaa kuelewa. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya, kama ni usafishaji ama kama Haneni, kila hatua ya kazi ya Mungu hailingani na dhana za wanadamu. Yote yanaenda mbali na kupenya katika dhana za watu. Hii ni kazi Yake. Lakini lazima uamini kwamba, kwa kuwa kazi ya Mungu imefika hatua fulani, Hatakubali wanadamu wote waangamie hata iweje. Anawapa ahadi na baraka kwa wanadamu, na wale wote wanaomfuata wataweza kupata baraka Yake, na wale wasiomfuata watatupwa nje na Mungu. Hii inategemea kufuata kwako. Haijalishi chochote, lazima uamini kuwa wakati kazi ya Mungu itakapomalizika, kila mtu atakuwa na mwisho unaofaa. Mungu Amewapa wanadamu matamanio mazuri, lakini wasipofuatilia, hawawezi kuyapata. Unafaa kuweza kuona hii sasa—Mungu kusafisha na kuwaadibu watu ni kazi Yake, lakini kwa watu, lazima wafuate badiliko katika tabia kila wakati.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu

378. Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho. Wale ambao wamekabiliwa na taabu ni wale wasiokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na uelekezi wa Mungu, lakini wale ambao wameshindwa kwa kweli na wanatafuta mapenzi ya Mungu kwa kweli hatimaye watasimama imara; ndio wale ambao wana ubinadamu, na wanaompenda Mungu kwa kweli. Bila kujali Mungu hufanya nini, hawa washindi hawatapungukiwa na maono, na bado watauweka ukweli katika matendo bila kufeli katika ushuhuda wao. Wao ndio watakaosimama mwishowe kutoka kwenye taabu kubwa. Hata ingawa wale wanaovua samaki katika maji yenye mawimbi mengi bado wanaweza kusaidiwa leo, hakuna yeyote atakayeepuka taabu, na hakuna atakayeepuka jaribio la mwisho. Kwa wale wanaoshinda, taabu ya aina hii ni usafisho mkubwa; lakini wale wanaovua katika maji yenye mawimbi, ni kazi ya kuondolewa kamili. Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Watu duni wa aina hii watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na wao hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama kuna faida inayoweza kupatwa, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo haya ambayo yanaweza kuua bila kusita, je, hayatakuwa hatari iliyofichika? Kazi ya kumwokoa mwanadamu haitimizwi kufuatia kazi ya kukamilisha ushindi. Ingawa kazi ya ushindi imefika kikomo, kazi ya kumtakasa mwanadamu haijafika kikomo; kazi hiyo itamalizika tu wakati mwanadamu amesafishwa kikamilifu, wakati wale ambao wamejikabidhi kwa Mungu kikweli wamekamilishwa, na wakati wale wadanganyifu wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao wamesafishwa. Wale ambao hawamridhishi Mungu katika hatua ya mwisho ya kazi Yake wataondolewa kabisa, na wale watakaoondolewa kabisa ni wa yule mwovu. Kwa kuwa hawawezi kumtosheleza Mungu, wao ni waasi dhidi ya Mungu, na hata kama watu hawa wanamfuata Mungu leo, hili si thibitisho kwamba wao ndio watakaosalia mwisho. Kwa maneno mengine “wale ambao humfuata Mungu hadi mwisho watapokea wokovu,” maana ya “kufuata” ni kusimama imara katikati ya taabu. Leo, wengi wanaamini kwamba kumfuata Mungu ni rahisi, lakini wakati kazi ya Mungu inakaribia kuisha, utajua maana halisi ya “kufuata.” Kwa sababu tu kwamba unaweza kumfuata Mungu leo baada ya kushindwa, si thibitisho kwamba umo miongoni mwa wale watakaokamilishwa. Wale wasioweza kustahimili majaribu, wale wasioweza kuwa washindi wakiwa kwenye taabu, hatimaye, watashindwa kusimama imara, na basi kushindwa kumfuata Mungu hadi mwisho kabisa. Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

379. Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Ikiwa inaweza kuionyesha tabia Yako na kuiruhusu tabia Yako ya haki iweze kuonekana na viumbe wote, na kama inaweza kuufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, kwamba naweza kufikia mfano wa yule ambaye ni mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako. Ningependa unihukumu hata zaidi, iwe ni kupitia mazingira ya uhasama au mateso makubwa; haijalishi ni nini Utakayofanya, kwangu ni ya thamani. Upendo Wako ni mkuu, na mimi niko tayari kujiweka katika huruma Yako bila malalamiko hata kidogo.” Huu ni ufahamu wa Petro baada ya yeye kuiona kazi ya Mungu, na pia ni ushahidi wa upendo wake kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

380. Mwanadamu anaishi katika mwili, ambayo ina maana anaishi katika kuzimu ya binadamu, na bila hukumu na adabu ya Mungu, mwanadamu ni mchafu kama Shetani. Mwanadamu atawezaje kuwa mtakatifu? Petro aliamini kwamba adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu! Petro aliomba, “Ee Mungu! Mradi tu Wewe unaniadibu na kunihukumu, nitajua kwamba Wewe hujaniacha. Hata kama Huwezi kunipa furaha au amani, na kufanya niishi katika mateso, na kunirudi mara nyingi, bora tu Hutaniacha moyo wangu utakuwa na amani. Leo hii, adabu Yako na hukumu umekuwa ulinzi wangu bora na baraka yangu kubwa. Neema unayonipa inanilinda. Neema unayoweka juu yangu leo ni kielelezo cha tabia Yako ya haki, na ni adabu na hukumu; zaidi ya hayo, ni majaribu, na, zaidi ya hapo, ni maisha ya mateso.” Petro alikuwa na uwezo wa kuweka kando raha ya mwili na kutafuta mapenzi zaidi na ulinzi zaidi, kwa sababu alikuwa amepata neema nyingi kutoka kwa adabu na hukumu ya Mungu. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

381. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kuwa bora ya yote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba. Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso, na hata nimekuwa karibu na kifo, haya yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu. Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu, basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani. Mwili wa binadamu una faida gani? Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha, ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha, ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami. Kama ingekuwa vile, ni jinsi gani ningeendelea kuishi? Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya miliki ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Ningewezaje kuendelea kuishi? Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia. Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha? Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu, hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho. Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe; ningewezaje kutokupenda Wewe? Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako, ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi, yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha, na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

382. Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: “Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema; ni hukumu Yake na adabu ambazo zimenilinda na kunitakasa. Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu. Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa.” Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Wanapokuwa na uzoefu mpaka mwisho kabisa, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika wataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

383. Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa kanuni za tabia ya mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Iliyotangulia: C. Jinsi ya Kujijua Mwenyewe na Kufikia Toba ya Kweli

Inayofuata: E. Juu ya Jinsi ya Kuwa Mtu Mwaminifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp