E. Juu ya Jinsi ya Kuwa Mtu Mwaminifu
384. Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. Kile Ninachoongea ni rahisi sana lakini ni kigumu maradufu kwenu. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kupima uungwana wa mtu kwa kipimio chenu wenyewe; kwa hiyo kazi Yangu inakuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawatumeni, mmoja baada ya mwingine, katika janga kupitia ili “mfundishwe” kupitia moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama, “Ujanja ndio moyo wa binadamu!” Hali za akili zenu zitakuwa zipi wakati huu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu
385. Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogondogo, anayependelea na asiye na mantiki, aliyekosa hisia ya haki, mwenye mbinu ovu, mdanganyifu na mjanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya kwamba hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasio na ujuzi huu hawatakaribishwa na watapoteza nafasi yao katika nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu hauko kwa kutoelewa kama huku tu; mbaya hata zaidi ni kukufuru kwenu Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upinzani mkubwa dhidi Yangu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
386. Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iwe kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako. Unapoomba, kama una upendo kwa Mungu katika moyo wako, na kama unatafuta utunzaji wa Mungu, ulinzi, na uchunguzi, kama haya ndio nia yako, maombi yako yatafaulu. Unapoomba katika mikutano, ndivyo unafaa kufungua moyo wako na kuomba Mungu, ambia Mungu kile kilicho moyoni mwako, na bila kuongea uongo, basi maombi yako yatafaulu. …
Kuwa muumini katika Mungu kunamaanisha kuwa kila kitu ufanyacho lazima kiletwe mbele za Mungu na kupitia uchunguzi wa Mungu. Kama kile ufanyacho kinaweza kuletwa mbele za Roho wa Mungu lakini sio mbele ya mwili wa Mungu, hii inadhibitisha kuwa hujajitiisha katika uchunguzi wa Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni nani? Mtu huyu aliyeshuhudiwa na Mungu ni nani? Je, Wote si sawa? Wengi Huwaona kama nafsi mbili tofauti, wakiamini kwamba Roho wa Mungu ni Roho wa Mungu, naye mtu anayeshuhudiwa na Mungu ni binadamu tu. Lakini, je, hujakosea? Je, mtu huyu anafanya kazi kwa niaba ya nani? Wale ambao hawaujui mwili wa Mungu hawana uelewa ya kiroho. Roho wa Mungu na mwili Wake ni mmoja, kwa sababu Roho wa Mungu anatokea kwa mwili. Kama mtu huyu si mwema kwako, Roho wa Mungu Atakuwa mwema? Ni nini kimekuchanganya? Leo, hakuna asiyekubali uchunguzi wa Mungu anaweza kupokea idhini ya Mungu, na yeyote asiyemjua Mungu mwenye mwili hawezi kukamilishwa. Jiangalie nawe ujiulize kama kila kitu unachofanya kinaweza kuletwa mbele ya Mungu. Iwapo huwezi kuleta kila kitu unachofanya mbele za Mungu, hii inaonyesha kuwa wewe ni mtenda maovu. Je, watenda maovu wanaweza kufanywa wakamilifu? Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hata maisha yako ya kawaida ya kiroho—maombi yako, ukaribu wako kwa Mungu, jinsi unavyokula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wako na kina ndugu zako na maisha yako ndani ya kanisa—na huduma yako katika ushirikiano wako vinaweza kuletwa mbele za Mungu ili Yeye avichunguze. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha. Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi na kadri unavyokubaliana na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutajipata katika uasherati, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda. Haijalishi kile unachokifanya, hata katika ushirika na ndugu na dada zako, ukiyaleta matendo yako mbele za Mungu na kutafuta uchunguzi wa Mungu, na kama nia yako ni kumtii Mungu Mwenyewe, unachotenda ni sahihi zaidi. Kama tu wewe ni mtu anayeleta kila kitu anachofanya mbele za Mungu na kukubali uchunguzi wa Mungu ndipo utakapokuwa mtu anayeishi kwa hakika katika uwepo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake
387. Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako ili kila mtu aweze kuuona moyo wako, kuona vyote unavyofikiri, na kuuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujaribu kujificha. Hapo tu ndipo watu watakuamini na kukuchukua kuwa mwaminifu. Hili ndilo tendo la msingi kabisa, na sharti, la kuwa mwaminifu. Unaonyesha taswira ya uongo kwa watu, ili waamini kwamba wewe ni mwadilifu, mkuu, anayejitolea, asiyependelea na asiye na ubinafsi. Huu ni udanganyifu. Usijifanye na usijionyeshe usivyo; badala yake, jiweke wazi na uweke wazi moyo wako ili wengine waone. Iwapo unaweza kuweka wazi moyo wako ili wengine waone, na kuweka wazi yote unayofikiri na kupanga kufanya ndani ya moyo wako—bila kujali iwapo ni nzuri ama mbaya—basi wewe huwi mwaminifu? Iwapo unaweza kujiweka wazi kwa wengine waone, Mungu pia atakuona, na kusema: “Umejiweka wazi kwa wengine wakuone, na hivyo mbele Yangu bila shaka wewe ni mwaminifu pia.” Iwapo unajiweka wazi kwa Mungu wakati wengine hawaoni pekee, na daima unajifanya kuwa mkuu na mwadilifu ama mwenye haki na asiye na ubinafsi mbele yao, basi Mungu atafikiri nini na Mungu atasema nini? Mungu atasema: “Kwa kweli wewe ni mdanganyifu, wewe ni nafiki kabisa na anayejishughulisha na mambo madogo madogo, na wewe si mwaminifu.” Mungu atakuhukumu hivi. Iwapo unataka kuwa mwaminifu, basi bila kujali kile unachofanya mbele ya Mungu ama watu, unapaswa kuweza kuufungua moyo wako na kujiweka wazi.
Kimetoholewa kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
388. Hatima yenu na majaliwa yenu ni muhimu sana kwenu—ni za matatizo makubwa. Mnaamini kuwa msipofanya mambo kwa uangalifu sana, itakuwa sawa na kutokuwa na hatima, na uharibifu wa majaliwa yenu. Lakini mmewahi kufikiri kwamba kama juhudi mtu hutumia ni kwa ajili ya hatima zao tu, hizo ni kazi tu zisizo na matunda? Juhudi za aina hiyo si halisi—ni bandia na danganyifu. Kama ni hivyo, wale ambao wanafanya kazi kwa ajili ya hatima yao watapokea maangamizo yao ya mwisho, kwa sababu kushindwa katika imani ya watu katika Mungu hutendeka kwa sababu ya udanganyifu. Hapo awali Nilisema kuwa Mimi Sipendi kusifiwa mno au kupendekezwa, au kuchukuliwa kwa shauku. Ninapenda watu waaminifu kukubali hali ilivyo kuhusu ukweli na matarajio Yangu. Hata zaidi, Ninapenda wakati watu wanaweza kuonyesha uangalifu mkubwa na kufikiria kwa ajili ya moyo Wangu, na wakati wanaweza hata salimisha kila kitu kwa ajili Yangu. Ni kwa njia hii tu ndipo Moyo wangu unaweza kuliwazwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima
389. Watu wakitafuta kuwa waaminifu tu ndiyo wanaweza kujua jinsi walivyopotoka kwa kina na kujua iwapo wana mfano wowote wa binadamu au la; ni wakati tu wanapokuwa wakitenda uaminifu ndipo wanaweza kugundua ni kiasi gani cha uwongo ndicho wao husema na jinsi udanganyifu na uongo wao ulivyojificha sana. Ni wakati tu wanapopitia kitendo cha kuwa waaminifu ndipo watu wanaweza kuja kujua ukweli wa upotovu wao wenyewe na kutambua kiini asili chao, na ni wakati huo tu ndipo tabia zao potovu zinaweza kutakaswa kila wakati. Tabia zao potovu zikitakaswa mara kwa mara tu ndipo watu wataweza kupata ukweli. Chukua muda wako kupitia maneno haya. Mungu hawakamilishi wale walio wadanganyifu. Ikiwa moyo wako si mwaminifu, ikiwa wewe si mtu mwaminifu, basi Mungu hatakupata kamwe. Wewe, pia, hutapata ukweli kamwe, na hutakuwa na uwezo wa kumpata Mungu. Kama huwezi kumpata Mungu, na huelewi ukweli, basi inamaanisha kwamba wewe ni wa uhasama kwa Mungu, hulingani na Mungu, na Yeye si Mungu wako. Na kama Mungu sio Mungu wako, huwezi kupata wokovu. Kama huwezi kupata wokovu, wewe utakuwa adui mkubwa wa Mungu milele, na matokeo yako yameamuliwa. Kwa hivyo, ikiwa watu wanataka kuokolewa, basi lazima waanze kwa kuwa waaminifu. Kuna ishara inayowaonyesha wale ambao mwishowe watapatwa na Mungu. Je, unajua ishara hiyo ni nini? Imeandikwa katika Ufunuo, katika Biblia: “Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo wowote; hawana mawaa.” “Hawa” wanaotajwa ni akina nani? Ni wale ambao wanaokamilishwa na kupatwa na Mungu, na kuokolewa. Je, Mungu anawaelezaje watu hawa? Je, sifa na maonyesho ya matendo yao zipi? (Wao hawana mawaa. Hawasemi uwongo). Nyote mnapaswa kuelewa na kufahamu maana ya kutosema uongo: Inamaanisha kuwa mwaminifu. Maana ya kuwa bila mawaa ni nini? Je, Mungu anamfafanuaje mtu asiye na mawaa? Wale wasio na mawaa wanaweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; wao ndio wanaweza kukaa katika njia ya Mungu. Watu kama hao ni wakamilifu machoni pa Mungu; hawana mawaa.
Kimetoholewa kutoka katika “Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
390. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa, jinsi ilivyoandikwa katika rekodi ya majaliwa yako. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu