F. Juu ya Jinsi ya Kutekeleza Kumtii Mungu
391. Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
392. Kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu? Hata wale walio tu na moyo nusu wa utii hawawezi kutembea hadi mwisho, sembuse hawa wadhalimu wasio na utii hata kidogo kwa mioyo yao. Kazi ya Mungu haipatwi virahisi na mwanadamu. Hata mwanadamu akitumia nguvu yake yote, ataweza kupata kipande tu na kufikia ukamilifu mwishowe. Na vipi basi kuhusu watoto wa malaika mkuu wanaotaka kuharibu kazi ya Mungu? Je, hawana hata matumaini madogo zaidi ya kupatwa na Mungu? Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa. Wakati huo utakapofika, wale “mashujaa wakubwa wasioshindwa” wa awali watakuwa “waoga wanyonge na wasio na maana” wa chini zaidi na wanaoepukwa zaidi. Hii tu ndiyo inaweza kuonyesha kila kipengele cha haki ya Mungu na kufichua tabia Yake ambayo hairuhusu kosa lolote. Hili tu ndilo linaloweza kutuliza chuki iliyo moyoni Mwangu. Je, hamkubali kwamba hili ni la busara sana?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
393. Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Kuna wengine wanaoweza kuwa wakaidi na kusema, “Sitafanya tu Usemavyo.” Basi Nakwambia kwamba sasa umefika mwisho wa njia umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza ku kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ili maisha yako yaweze kukua. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
394. Kujisalimisha kwa kazi ya Mungu lazima kugusike na kuishi kwa kudhihirishwa. Kujisalimisha kwa kiwango cha juu juu hakuwezi kupokea idhini ya Mungu, na kutii tu vipengele vya juujuu vya neno la Mungu bila kutaka mgeuzo wa tabia ya mtu, hakutaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Utiifu kwa Mungu na kujinyenyekeza kwa kazi ya Mungu ni kitu kimoja. Wale wanaomtii Mungu tu lakini hawatii kazi Yake hawawezi kudhaniwa kuwa watiifu, sembuse wale wasiotii kwa kweli na kwa nje hao ni wa kujipendekeza. Wale ambao kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu wote wanaweza kufaidika kutokana na kazi na kupata ufahamu wa tabia na kazi ya Mungu. Wanadamu kama hawa tu ndio kweli wanajinyenyekeza kwa Mungu. Wanadamu kama hawa wanaweza kupata maarifa mapya kutokana na kazi mpya na kuwa na uzoefu wa mabadiliko mapya kutoka hayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wana idhini ya Mungu; mwanadamu wa aina hii tu ndiye amekamilishwa, ndiye amepitia mabadiliko ya tabia yake. Wale wanaopokea idhini ya Mungu ni wale wanaojisalimisha kwa Mungu kwa furaha, na pia kwa neno na kazi Yake. Mwanadamu wa aina hii tu ndiye yuko sahihi; mwanadamu wa aina hii tu ndiye kweli anamtamani Mungu, na anamtafuta Mungu kwa dhati.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
395. Wakati wa Mungu akiwa ndani ya mwili, utii Anaohitaji kwa watu sio ule ambao watu wanafikiri—kutohukumu au kutopinga. Badala yake, Anahitaji kwamba watu wafanye maneno Yake kuwa kanuni yao ya maisha na msingi wa kuendelea kuishi kwao, kwamba wanaweka kikamilifu kiini cha maneno Yake katika matendo, na kwamba wanayaridhisha kabisa mapenzi Yake. Kipengele kimoja cha kuhitaji watu kumtii Mungu mwenye mwili kinahusu kuweka maneno Yake katika matendo, huku kipengele kingine kinarejelea kuwa na uwezo wa kutii ukawaida na utendaji Wake. Haya yote mawili lazima yawe bila shaka. Wale ambao wanaweza kutimiza vipengele hivi viwili ni wale wote ambao wana moyo wa upendo wa kweli kwa Mungu. Wote ni watu ambao wamepatwa na Mungu, na wote wanampenda Mungu kama wanavyopenda maisha yao wenyewe. …
Kikundi cha watu ambao Mungu mwenye mwili Anataka kuwapata leo ni wale wanaokubali mapenzi Yake. Watu wanahitaji tu kutii kazi Yake, sio daima kujishughulisha na mawazo ya Mungu aliye mbinguni, waishi ndani ya hali isiyo dhahiri, au kufanya mambo kuwa magumu kwa Mungu mwenye mwili. Wale ambao wanaweza kumtii ni wale wanaoyasikia kabisa maneno Yake na kutii mipango Yake. Watu hawa hawajali kamwe jinsi Mungu mbinguni alivyo kwa kweli au ni kazi ya aina gani Mungu wa mbinguni Anafanya sasa kwa wanadamu, lakini wao humpa Mungu aliye duniani mioyo yao kabisa na kuweka nafsi zao zote mbele Yake. Kamwe hawazingatii usalama wao wenyewe, wala hawalalamiki kamwe juu ya ukawaida na utendaji wa Mungu katika mwili. Wale wanaomtii Mungu katika mwili wanaweza kukamilishwa na Yeye. Wale wanaomwamini Mungu mbinguni hawatapata kitu. Hii ni kwa sababu si Mungu mbinguni, lakini ni Mungu hapa duniani ndiye Anayetoa ahadi na baraka juu ya watu. Watu hawapaswi daima kumtukuza Mungu aliye mbinguni na kumwona Mungu duniani kama mtu wa wastani. Hii si haki. Mungu mbinguni ni mkuu na wa ajabu na mwenye hekima ya ajabu, lakini hii haipo kabisa. Mungu duniani ni wa wastani sana na asiye na maana; Yeye pia ni wa kawaida sana. Hana mawazo ya ajabu au vitendo vya kimiujiza. Anatenda tu na kuongea kwa njia ya kawaida na ya matendo. Ingawa Hazungumzi kwa njia ya ngurumo au kuita upepo na mvua, Yeye kwa kweli ni mwili wa Mungu aliye mbinguni, na kwa kweli ni Mungu anayeishi kati ya wanadamu. Watu hawapaswi kumtukuza yule wanayeweza kumwelewa na ambaye analingana na mawazo yao wenyewe kama Mungu, au kumwona Yeye ambaye hawawezi kumkubali na kabisa hawawezi kufikiria kama wa chini. Yote haya ni uasi wa watu; yote ni chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa
396. Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. Wale ambao hawana hiari ya kuwa na kiu ya Mungu hawana uwezo wa kuwa na akili ya kumtii Mungu, na wanaweza tu kumpinga Mungu kama matokeo ya kuridhika kwao na jinsi hali ilivyo. Kwamba mtu hawezi kumtii Mungu ni kwa sababu amefungwa na kitu kilichotangulia kabla. Mambo ambayo yalikuja kabla yamewapatia watu kila namna ya dhana na njozi za uongo kuhusu Mungu ambazo zimekuwa ndiyo taswira ya Mungu akilini mwao. Hivyo, kile wanachoamini ni dhana zao wenyewe, na viwango vya mawazo yao wenyewe. Ikiwa utampima Mungu ambaye anafanya kazi halisi leo dhidi ya Mungu wa mawazo yako mwenyewe basi imani yako inatoka kwa Shetani, na ni kulingana na mapendeleo yako mwenyewe—na Mungu hataki imani kama hii. Bila kujali sifa zao ni za juu sana kiasi gani, na bila kujali kujitoa kwao—hata kama wamejitoa jitihada za maisha yao yote katika kazi Yake, na wamejitoa mhanga—Mungu hakubali imani yoyote kama hii. Anawaonyesha tu neema kidogo, na kuwaacha waifurahie kwa muda. Watu kama hawa hawawezi kuuweka ukweli katika vitendo, Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao, na badala yake Mungu atamwondoa kila mmoja wao. Bila kujali ama ni wazee au vijana, wale ambao hawamtii Mungu katika imani yao na wana motisha mbaya, ni wale ambao wanapinga na kuingilia, na watu kama hao bila kuhoji wataondolewa na Mungu. Wale ambao hawana utii kwa Mungu hata kidogo, ambao wanalitambua tu jina la Mungu, na wana ufahamu kiasi juu ya mapenzi na wema wa Mungu lakini hawaenendi sawa na hatua za Roho Mtakatifu na hawatii kazi na maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu—watu kama hao wanaishi katikati ya neema ya Mungu, na hawatachukuliwa na kukamilishwa na Mungu. Mungu huwakamilisha watu kupitia utii wao, kupitia kula kwao, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu, na kupitia mateso na usafishaji maishani mwao. Ni kupitia tu imani kama hii ndipo tabia za watu zinaweza kubadilika, baada ya hapo tu ndipo wanaweza kuwa na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka. Watu ambao hawafanyi kitu zaidi ya kufurahia neema za Mungu hawawezi kukamilishwa, au kubadilishwa, na utii wao, uchaji Mungu, na upendo na ustahimilivu vyote hivyo ni vya juujuu tu. Wale ambao wanafurahia tu neema za Mungu hawawezi kumfahamu Mungu kweli, na hata pale wanapomjua Mungu, maarifa yao ni ya juujuu, na wanasema mambo kama vile Mungu anampenda mwanadamu, au Mungu ni mwenye huruma kwa mwanadamu. Hii haiwakilishi maisha ya mwanadamu, na haionyeshi kwamba kweli watu wanamjua Mungu. Ikiwa, maneno ya Mungu yatakapowasafisha, au majaribu yake yatakapowajia, watu hawataweza kumtii Mungu—ikiwa, badala yake, watakuwa watu wa mashaka na kuanguka chini—basi hawana utii hata kidogo. Ndani yao, kuna kanuni na masharti mengi kuhusu imani kwa Mungu, uzoefu wa zamani ambao ni matokeo ya miaka mingi ya imani, au mafundisho mbalimbali kutoka kwenye Biblia. Je, watu kama hawa wanaweza kumwamini Mungu? Watu hawa wamejawa na mambo ya wanadamu—wanawezaje kumtii Mungu? Wote wanatii kulingana na mapendeleo yao binafsi—je, Mungu anaweza kutamani utii kama huu? Huku sio kumtii Mungu bali ni kufungamanishwa na mafundisho, ni kujiridhisha na kujifariji mwenyewe. Ikiwa unasema kwamba huu ni utii kwa Mungu, je, hivi hutakuwa unamkufuru Yeye?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
397. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atamshughulikia na kumkomesha kila mmoja.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
398. Katika kupima ikiwa watu wanaweza kumtii Mungu au la, jambo muhimu la kuangalia ni ikiwa wanatamani kitu chochote cha kupita kiasi kutoka kwa Mungu, na ikiwa wana nia mbaya au la. Ikiwa watu humdai Mungu kila wakati, inathibitisha kuwa wao sio watiifu Kwake. Chochote kinachotokea kwako, ikiwa huwezi kukipokea kutoka kwa Mungu, huwezi kutafuta ukweli, kila wakati wewe unazungumza kutoka kwa hoja yako ya dhahania na kuhisi kila wakati kuwa wewe tu ndiye uliye sahihi, na hata bado una uwezo wa kumshuku Mungu, basi utakuwa taabani. Watu kama hao ndio wenye kiburi na waasi zaidi kwa Mungu. Watu ambao daima humdai Mungu hawawezi kamwe kumtii kweli. Ukimdai Mungu, hii inathibitisha kwamba unafanya maafikiano na Mungu, kwamba unachagua mawazo yako mwenyewe, na kutenda kulingana na mawazo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivi, unamsaliti Mungu, na huna utiifu. Hakuna maana katika kumdai Mungu; ikiwa unaamini kweli kwamba Yeye ni Mungu, basi hutathubutu kumdai, wala hutastahiki kumdai, yawe madai ya maana au la. Ikiwa una imani ya kweli, na unaamini kuwa Yeye ni Mungu, basi hutakuwa na budi ila kumwabudu na kumtii. Siku hizi, sio tu kuwa watu wana chaguo, lakini hata wanadai kwamba Mungu atende kwa mujibu wa mawazo yao wenyewe, wanachagua mawazo yao wenyewe na wanataka Mungu atende kulingana nayo, na hawahitaji wao wenyewe kutenda kulingana na kusudi la Mungu. Kwa hivyo, hakuna imani ya kweli ndani yao, wala kiini ambacho kimo ndani ya imani hii.
Kimetoholewa kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
399. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima wafuate, kuelewa matokeo ambayo Mungu ananuia kufanikisha katika binadamu na mafanikio Anayonuia kufikia ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo mnapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
400. Wakati Nuhu alipofanya kama vile Mungu alivyomwagiza hakujua nia za Mungu zilikuwa nini. Hakujua ni nini ambacho Mungu Alitaka kukamilisha. Mungu alikuwa amempa tu amri, Akamwagiza afanye kitu, lakini bila ya maelezo mengi, na akaendelea mbele na kukifanya. Hakujaribu kuelewa kwa siri nia za Mungu zilikuwa nini, wala hakumpinga Mungu au kuwa na fikira mbili kuhusu jambo hilo. Alienda tu na kuifanya vilivyo kwa moyo safi na rahisi. Chochote ambacho Mungu alimruhusu kufanya alifanya, na kutii na kusikiliza neno la Mungu vyote vilikuwa ni imani yake ya kufanya mambo. Hivyo ndivyo alivyokuwa mnyofu na mwepesi wa kushughulikia kile ambacho Mungu alimwaminia kufanya. Kiini chake—kiini cha vitendo vyake kilikuwa ni utiifu, sio kutarajia kwa kukisia, sio kupinga, na zaidi; kutofikiria kuhusu maslahi yake binafsi na faida zake na hasara zake. Zaidi ya hayo, wakati Mungu aliposema Angeuangamiza ulimwengu kwa mafuriko, Nuhu hakuuliza ni lini au kuuliza kile kitakachovifanyikia vitu, na bila shaka hakumuuliza Mungu namna hasa alivyopanga kuangamiza ulimwengu. Alifanya tu kama Mungu alivyomwagiza. Njia yoyote ile aliyotaka Mungu, safina hiyo iweze kujengwa na hasa kujengwa na nini, alifanya tu vile ambavyo Mungu alimwomba na pia akaanza kazi mara moja. Alitenda kulingana na maagizo ya Mungu kwa mwelekeo wa kutaka kutosheleza Mungu. Je, alikuwa akifanya hivyo kujisaidia yeye kuepuka janga? La. Je, alimwuliza Mungu ni baada ya muda gani zaidi kabla ulimwengu ungeangamizwa? Hakuuliza. Je, alimwuliza Mungu au alijua ingechukua muda gani kuijenga safina? Hakujua hilo pia. Alitii tu, akasikiliza, na kufanya hivyo inavyohitajika.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I
401. Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki. Fikiria kwamba wewe unaweza kumfanyia Mungu kazi, ilhali wewe humtii Mungu, na huna uwezo wa kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa njia hii, wewe hutakuwa tu umekosa kutimiza wajibu wa kiumbe cha Mungu, lakini pia utalaaniwa na Mungu, kwa kuwa wewe ni mtu ambaye hana ukweli, ambaye hana uwezo wa kumtii Mungu, na ambaye si mtiifu kwa Mungu. Wewe unajali tu kuhusu kumfanyia Mungu kazi, na hujali kuhusu kuweka ukweli katika vitendo, ama kujifahamu. Wewe humfahamu ama kumjua Muumba, na humtii ama kumpenda Muumba. Wewe ni mtu ambaye asilia si mtiifu kwa Mungu, na hivyo watu kama hawa hawapendwi na Muumba.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
402. Kuwa na ushahidi mkuu kwa Mungu hasa kunahusiana na ikiwa una ufahamu wa Mungu wa vitendo au la, na ikiwa unaweza au huwezi kutii mbele ya mtu huyu ambaye ni wa kawaida na kutii mpaka hata kifo. Ikiwa unamshuhudia Mungu kwa kweli kupitia utii huu, hiyo inamaanisha kuwa umepatwa na Mungu. Kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo, na kuwa bila malalamiko mbele Yake, kutohukumu, kutokashifu, kutokuwa na mawazo, na kutokuwa na makusudi mengine—kwa njia hii Mungu atapata utukufu. Utiifu mbele ya mtu wa kawaida ambaye anadharauliwa na mwanadamu na kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo bila mawazo yoyote—huu ni ushuhuda wa kweli. Uhakika ambao Mungu anataka watu waingie ndani ni kwamba unaweza kutii maneno Yake, unaweza kuweka maneno Yake katika matendo, kuweza kuinama mbele ya Mungu wa vitendo na kujua upotovu wako mwenyewe, kuweza kufungua moyo wako mbele Yake, na mwishowe kupatwa na Yeye kupitia maneno haya Yake. Mungu hupata utukufu wakati maneno haya yanakushinda na kukufanya uwe mtiifu kikamilifu Kwake; kwa njia hii Anamwaibisha Shetani na kukamilisha kazi Yake. Wakati huna mawazo yoyote ya utendaji wa Mungu mwenye mwili, yaani, unaposimama imara katika jaribio hili, basi wewe huwa na ushuhuda mzuri. Ikiwa kuna siku ambayo uko na uelewa mkamilifu juu ya Mungu wa matendo na unaweza kutii mpaka kifo kama Petro, utapatwa na Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Kile ambacho Mungu hufanya ambacho hakilingani na mawazo yako ni jaribio kwako. Ikiwa kingelingana na mawazo yako, hakingekuhitaji kuteseka au kusafishwa. Ni kwa sababu kazi Yake ni ya vitendo sana na kwamba hailingani na mawazo yako ndiyo inakuhitaji kuyaachilia mawazo yako. Hii ndiyo sababu ni jaribio kwako. Ni kwa sababu ya utendaji wa Mungu ndiyo maana watu wote wako katikati ya majaribio; kazi Yake ni ya vitendo, siyo ya kawaida. Kwa kuelewa kikamilifu maneno Yake ya vitendo, matamshi Yake ya vitendo bila mawazo yoyote, na kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli zaidi ndivyo kazi Yake ilivyo ya vitendo zaidi, utapatwa na Yeye. Kundi la watu ambao Mungu atapata ni wale wanaomjua Mungu, yaani, ambao wanajua utendaji Wake, na hata zaidi ni wale wanaoweza kutii kazi ya vitendo ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa
403. Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja