G. Juu ya Jinsi ya Kutimiza Wajibu wa Mtu vya Kutosha

404. Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

405. Unapaswaje kuchukulia Agizo la Mungu? Hili ni jambo zito sana! Ikiwa huwezi kukamilisha kile ambacho Mungu humwaminia mtu, hufai kuishi katika uwepo wa Mungu na unapaswa kuadhibiwa. Ni amri ya mbingu na kanuni ya dunia ya mwanadamu kumaliza kile ambacho Mungu humwaminia; hili ni jukumu la juu kabisa la mwanadamu, muhimu kama maisha yake. Ikiwa hulichukulii Agizo la Mungu kwa uzito, basi unamsaliti Mungu kwa njia kuu zaidi; hili ni la huzunisha zaidi kuliko Yuda na linastahili kulaaniwa. Hivyo, Mungu anamwagiza mwanadamu: Huku ni kutukuzwa kukuu na mapendeleo maalum kutoka kwa Mungu, jambo la utukufu kuu zaidi. Kila kitu kingine kinaweza kuachwa—hata ikiwa itamlazimu mtu kutoa maisha yake bado lazima atimize Agizo la Mungu. Unaona, kuna hata ukweli zaidi wa kutafutwa hapa.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

406. Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

408. Kwa sababu wakati mtu anapokubali kile Mungu amemwaminia, Mungu anacho kiwango cha kuhukumu kama vitendo vya mtu huyu ni vizuri au vibaya na kama mtu huyu amemtii, na kama mtu huyu ametosheleza mapenzi ya Mungu na kama kile anachofanya kimeruhusiwa. Kile anachojali Mungu ni kuhusu moyo wa mtu huyu, si vitendo vyake vya juujuu. Si jambo kwamba Mungu anafaa kubariki mtu mradi tu afanye hivyo, licha ya namna anavyofanya hivyo. Huku ni kutoelewa kwa watu kumhusu Mungu. Mungu huangalia tu mwisho wa matokeo ya mambo, lakini Anatilia mkazo zaidi kuhusu namna moyo wa mtu ulivyo na namna mwelekeo wa mtu ulivyo wakati wa maendeleo ya mambo, na Anaangalia kama kunao utiifu, utiliaji maanani, na tamanio ya kumtosheleza Mungu ndani ya moyo wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

409. Haijalishi ni wajibu upi unaotimiza, lazima utafute kushika mapenzi ya Mungu na kuelewa mahitaji Yake ni yapi kuhusiana na wajibu wako; ni hapo tu ndipo utaweza kushughulikia mambo kwa njia ya maadili. Katika kutekeleza wajibu wajo, huwezi kabisa kufuata upendeleo wako binafsi, kwa kufanya chochote ambacho ungependa kufanya, chochote ambacho unngefurahia na kuridhika unapokifanya au chochote ambacho kingekufanya uonekane kuwa mzuri. Ukimlazimishia kwa nguvu upendeleo wako kwa Mungu au kuutenda kama kwamba ni ukweli, ukiyafuata kana kwamba ni kanuni za ukweli, basi huko si kutekeleza wajibu wako, na kutekeleza wajibu wako kwa njia hakutakumbukwa na Mungu. Watu wengine hawaelewi ukweli, na hawajui kutekeleza wajibu wao vyema kunamaanisha nini. Wao huhisi kwamba kwa kuwa wamejitolea na kutia juhudi, wameukana mwili wao na kuteseka, basi kutimiza kwao wajibu wao kunapaswa kufikia kiwango kinachohitajika—lakini kwa nini, basi, kila mara Mungu haridhiki? Je, watu hawa wamekosea wapi? Kosa lao lilikuwa kutotafuta matakwa ya Mungu, na badala yake kutenda kulingana na fikira zao; walichukulia matakwa, upendeleo, na madhumuni yao wenyewe kama ukweli, na walivichukulia vitu hivyo kana kwamba vilikuwa vile ambavyo Mungu alipenda, kana kwamba vilitosheleza viwango na mahitaji Yake. Waliyaona yale waliyoyaamini kuwa sahihi, mema, na mazuri kuwa ukweli; haya ni makosa. Kusema ukweli, hata ingawa wakati mwingine watu wanaweza kufikiri kuwa jambo fulani ni sahihi na kwamba linaambatana na ukweli, hilo halimaanishi kwamba lazima liwe linaambatana na mapenzi ya Mungu. Kadiri watu wanavyofikiri kwamba jambo fulani ni sahihi, ndivyo wanavyopaswa kuwa waangalifu zaidi na ndivyo wanavyopaswa kutafuta ukweli zaidi ili kuona iwapo kile wanachofikiria kinaridhisha matakwa ya Mungu. Ikiwa kinapingana na matakwa Yake na kinapingana na maneno Yake, basi umekosea kufikiria kwamba ni sahihi, ni wazo la binadamu tu, na si lazima kwamba kitaambatana na ukweli bila kujali jinsi unavyokifikiria kuwa sahihi. Uamuzi wako wa kilicho sahihi na chenye makosa unapaswa kutegemezwa kwa maneno ya Mungu pekee, na bila kujali jinsi unavyofikiria kwamba kitu fulani ni sahihi, ni lazima ukitupilie mbali isipokuwa iwapo kina msingi katika maneno ya Mungu. Wajibu ni nini? Ni agizo lililoaminiwa kwa watu na Mungu. Hivyo unapaswaje kutimiza wajibu wako? Kwa kutenda kwa mujibu wa matakwa na viwango vya Mungu, na kutegemeza tabia yako kwa kanuni za ukweli badala ya matamanio ya dhahania ya binadamu. Kwa njia hii, wewe kutimiza wajibu wako kutakuwa kumefikia kiwango kinachohitajika.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutafuta Kanuni za Ukweli Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kutekeleza Wajibu Wake Vizuri” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

410. Kwa watu wengine, bila kujali suala wanalokumbana nalo wanapokuwa wakitimiza wajibu wao, hawatafuti ukweli na daima wanatenda kulingana na dhana, mawazo, fikira na tamaa zao wenyewe. Wao daima huridhisha tamaa zao za binafsi na tabia zao potovu huwa zinaongoza vitendo vyao kila mara. Ingawa wanaweza kukamilisha wajibu waliopewa, hawapati ukweli wowote. Kwa hiyo mtu huyu anategemea nini katika utimizaji wa wajibu wake? Hategemei ukweli na hamtegemei Mungu. Kiasi cha ukweli anachoelewa hakijachukua nafasi kuu moyoni mwake. Anategemea vipaji na uwezo wake, ujuzi ambao amepata na talanta zake, na pia utashi wao wenyewe au nia nzuri ya kuwezesha kazi hiyo kufanyika. Asili ni tofauti, siyo? Ingawa wakati mwingine unaweza kutegemea asili, mawazo, fikira, ujuzi na kujifunza kwako katika kutimiza wajibu wako, hakuna masuala ya kanuni hujitokeza katika mambo unayofanya. Kwa juu inaonekana kana kwamba hujachukua njia mbaya, lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kupuuzwa: Wakati wa mchakato wa kufanya wajibu wako, ikiwa mawazo, fikira na tamaa zako za kibinafsi hazibadiliki kamwe na hazibadilishwi kamwe na ukweli, ikiwa vitendo na matendo yako hayalingani kamwe na kanuni za kweli, basi matokeo ya mwisho yatakuwa nini? Utakuwa mtendaji huduma, na hili ndilo tu lililoandikwa katika Biblia: “Wengi watasema Kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina Lako? Na kutoa mapepo kupitia jina Lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina Lako? Na hapo ndipo Nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Je, kwa nini Mungu huwaita watu hawa ambao huchangia juhudi zao na ambao hutoa huduma “ninyi ambao hutenda udhalimu”? Kuna hoja moja ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo, na hiyo ni kwamba, haijalishi watu hawa wanafanya wajibu upi au ni kazi ipi wanayoifanya, motisha, chanzo, nia na mawazo ya watu hawa yanatokana kabisa na tamaa zao za ubinafsi, yametegemezwa kabisa kwa mawazo yao wenyewe na juu ya masilahi yao ya kibinafsi, na yamelenga kabisa maanani na mipango kama vile kujiheshimu, hadhi na majivuno, na matarajio ya siku za usoni. Hawana ukweli mioyoni mwao, na hawatendi kulingana na kanuni za ukweli. Kwa hivyo, cha muhimu wewe kufuatilia sasa ni nini? (Kutafuta ukweli, na kutenda wajibu wetu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu.) Unapaswa kufanya nini hasa, wakati ambapo unatekeleza wajibu wako kulingana na mahitaji ya Mungu? Kuhusiana na nia na mawazo uliyo nayo unapokuwa ukifanya kitu, lazima ujue jinsi ya kutambua kama yanakubaliana na ukweli au la, na kama hayo ni kwa ajili ya matamanio yako ya kibinafsi au kwa ajili ya masilahi ya familia ya Mungu. Ikiwa yanakubaliana na ukweli, basi unaweza kufuata mwelekeo wa mawazo yako kufanya wajibu wako. Ikiwa hayakubaliani na ukweli, basi lazima ugeuke upesi na uachane na njia hiyo. Njia hiyo si sahihi, na huwezi kutenda kwa namna hiyo; ukitenda kwa namna hiyo, basi utakuwa mtu anayeshiriki katika udhalimu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kupitia Maneno ya Mungu katika Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

411. Unapokuwa ukitimiza wajibu wako, unapaswa kujichunguza kila wakati ili uone iwapo unafanya mambo kulingana na kanuni, iwapo utendaji wa wajibu wako unafikia kiwango kinachotakiwa, iwapo unaufanya tu kwa uzembe au la, iwapo umejaribu kukwepa majukumu yako na iwapo kuna matatizo yoyote katika mtazamo wako na jinsi unavyofikiri. Mara baada ya kutafakari juu yako mwenyewe na kuelewa kabisa mambo haya, utatimiza wajibu wako kwa urahisi zaidi. Bila kujali unakabiliwa na nini unapokuwa ukifanya wajibu wako—uhasi na udhaifu, au kuwa katika hali mbaya baada ya kushughuliwa—unapaswa kuuchukulia vizuri, na lazima pia utafute ukweli na uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa kufanya mambo haya, utakuwa na njia ya kutenda. Iwapo ungependa kutimiza wajibu wako vizuri, basi sharti usiathiriwe na hali yako ya moyo. Bila kujali unahisi kwamba wewe ni hasi au dhaifu jinsi gani, unapaswa kutenda ukweli katika kila kitu unachofanya, kwa ukamilifu kabisa na kwa kufuata kanuni. Ukifanya hivi, mbali na watu wengine kukupenda, Mungu pia atakupenda. Hasa, utakuwa mtu mwaminifu na anayewajibika; utakuwa mtu mzuri kwa kweli ambaye hutimiza wajibu wake kufikia kiwango kinachotakiwa na anayeishi kwa kudhihirisha kikamilifu mfano wa mtu halisi. Watu kama hao hutakaswa na hufanikisha mabadiliko ya kweli wanapotimiza wajibu wao, na wanaweza kusemekana kuwa waaminifu machoni pa Mungu. Watu waaminifu pekee ndio wanaoweza kuvumilia kutenda ukweli na kufanikiwa katika kutenda kwa maadili, na wanaweza kutekeleza wajibu wao kufikia kiwango kinachotakiwa. Watu ambao hutenda kwa kufuata kanuni hutimiza wajibu wao kwa uangalifu wanapokuwa katika hali nzuri; wao hawatendi kwa njia isiyo ya dhati, sio wenye kiburi na hawajionyeshi ili kuwafanya wengine wawaheshimu sana. Hata hivyo, wanapokuwa katika hali mbaya, wao hukamilisha kazi zao za kila siku kwa njia ile ile ya bidii na kwa uwajibikaji, na hata wakikumbana na kitu ambacho ni cha kudhuru utimizaji wa wajibu wao, au ambacho kinawatia msongo kidogo au kusababisha usumbufu wakati wanafanya wajibu wao, bado wao bado huwa na uwezo wa kuituliza mioyo yao mbele za Mungu na kuomba, wakisema, “Haijalishi shida ninayokumbana nayo ni kubwa kiasi gani—hata mbingu ziporomoke na kuanguka—mradi Mungu aniruhusu niendelee kuishi, ninakusudia kufanya kila niwezalo kutimiza wajibu wangu. Kila siku ninayoruhusiwa kuishi ni siku ambayo nitafanya kazi kwa bidii kutekeleza wajibu wangu ili nistahili wajibu huu niliopewa na Mungu, na vile vile pumzi hii ambayo Ameiweka mwilini mwangu. Haijalishi nitakuwa katika ugumu kiasi gani, nitauweka wote kando, kwa kuwa kutimiza wajibu wangu ndilo jambo muhimu zaidi!” Wale ambao hawaathiriwi na mtu, tukio, kitu au mazingira yoyote, ambao hawadhibitiwi na hali ya moyo au hali yoyote ya nje, na ambao hutanguliza wajibu na maagizo ambayo Mungu amewaaminia—wao ndio watu walio waaminifu kwa Mungu na wanaomtii kweli. Watu kama hawa wamefikia uingiaji katika uzima na wameingia katika uhalisi wa ukweli. Hii ni mojawapo ya maonyesho ya vitendo zaidi na ya kweli ya kuishi kwa kudhihirisha ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Uingiaji Katika Uzima Lazima Uanze na Uzoefu wa Kutenda Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

412. Haijalishi kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako, unahitaji tu kujitolea kikamilifu. Natarajia utaweza kuonyesha uaminifu wako kwa Mungu mbele Yake mwishowe, na maadamu unaweza kuiona tabasamu ya Mungu ya kupendeza Akiwa katika kiti Chake cha enzi, hata kama ni wakati wako kufa, lazima uweze kucheka na kutabasamu macho yako yanapofumba. Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu. Kiumbe anaweza kumfanyia Mungu nini? Kwa hiyo unapaswa kujitolea kwa rehema ya Mungu mapema iwezekanavyo. Maadamu Mungu anafurahia na Anapendezwa, basi mwache Afanye chochote Atakacho. Wanadamu wana haki gani ya kulalamika?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 41

413. Leo hii mnachohitajika kufikia si madai ya ziada, ila ni wajibu wa mwanadamu, na kile kinachofaa kufanywa na kila mtu. Kama hamuwezi hata kufanya wajibu wenu, au kuufanya vizuri, hamuoni mnajiletea masaibu nyinyi wenyewe? Hamwuoni mnajitakia kifo? Mtatarajiaje maisha ya baadaye na matarajio? Kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu, na ushirika wa mwanadamu ni kwa minajili ya usimamizi wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya yale yote Anayopaswa kufanya, mwanadamu anapaswa kufanya vitendo bila kukoma, na kushirikiana na Mungu. Mwanadamu hapaswi kulegeza kamba katika kazi ya Mungu, lazima aonyeshe uaminifu na asijitie katika mawazo mengi au kukaa akisubiri kifo bila kufanya kitu. Mungu Mwenyewe anaweza kujitolea kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asiweze kuwa mwaminifu kwa Mungu? Mawazo na moyo wa Mungu vipo kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asijitolee katika ushirika? Mungu huwafanyia wanadamu kazi, basi ni kwa nini mwanadamu asifanye wajibu wake kwa minajili ya usimamizi wa Mungu? Kazi ya Mungu imefika umbali huu, bado mnaona ila hutendi, mnasikia ila hamsogei. Je, si watu kama hawa wanafaa kuangamizwa kabisa? Tayari Mungu amejitolea kikamilifu kwa ajili ya mwanadamu, basi ni kwa nini siku hizi mwanadamu hafanyi wajibu wake kwa dhati? Kwa Mungu, kazi Yake ni ya kipaumbele Kwake, na kazi ya usimamizi Wake ni ya umuhimu wa hali ya juu. Kwa mwanadamu, kuweka maneno ya Mungu katika vitendo na kutimiza mahitaji ya Mungu ndiyo kipaumbele kwake. Ni lazima nyote myafahamu haya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

414. Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe aliyeumbwa au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wanawiwa mengi na Yeye, lakini wanageuka na kumkong'ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha na Yeye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Kama mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo tu ndipo atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa kweli, na ni mwanadamu kama huyu tu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Na wengi wenu je? Mnamtendeaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje wajibu wenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, hamjapokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyahukumu na kuyalinganisha haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno Yangu na kazi Yangu, kundi lenu litakuwa la kuadhibiwa. Kamwe hamtapata neema, na hamtakuwa na baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Iliyotangulia: F. Juu ya Jinsi ya Kutekeleza Kumtii Mungu

Inayofuata: H. Juu ya Kumcha Mungu na Kuepuka Uovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp