(X) Maneno Juu ya Kumcha Mungu na Kuepuka Uovu

(X) Maneno Juu ya Kumcha Mungu na Kuepuka Uovu

116. Kwanza kabisa tunajua kwamba tabia ya Mungu ni adhama, ni hasira. Yeye si kondoo ili achinjwe na yeyote; na hata zaidi Yeye si kikaragosi ili adhibitiwe na watu vyovyote vile wanavyotaka. Yeye pia si hewa tupu ili kuamrishwa huku na kule na watu. Kama kweli unasadiki kwamba Mungu yupo, unafaa kuwa na moyo unaomcha Mungu, na unafaa kujua kwamba kiini halisi cha Mungu hakifai kughadhabishwa. Ghadhabu hii inaweza kusababishwa na neno; pengine fikira; pengine aina fulani ya tabia bovu; pengine tabia ya upole tabia inayoweza kuruhusiwa kwenye macho na maadili ya binadamu; au pengine inasababishwa na falsafa, nadharia. Hata hivyo, punde unapomghadhabisha Mungu, fursa yako inapotea na siku zako za mwisho zinakuwa zimewasili. Hili ni jambo baya! Kama huelewi kwamba Mungu hawezi kukosewa, basi pengine humchi Mungu, na pengine unamkosea Yeye kila wakati. Kama hujui namna ya kumcha Mungu, basi huwezi kumcha Mungu, na hujui namna ya kujiweka kwenye njia ya kutembelea kwa njia ya Mungu—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Punde unapokuwa na habari, unaweza kuwa na ufahamu kwamba Mungu hawezi kukosewa, kisha utajua ni nini maana ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

117. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi haitawezekana kwako kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, haitawezekana wewe kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake utakuwa tu mzembe asiyejali na kuepuka kusema ukweli wote, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Ingawa kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuzilia mbali amri za utawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni kosa dhidi ya amri ya utawala. Sasa unafaa kutambua kwamba kuelewa tabia ya Mungu huja na kujua dutu Yake, nakwamba pamoja na kuelewa tabia ya Mungu huja kuelewa amri za utawala. Bila shaka, amri nyingi za utawala zinahusisha tabia ya Mungu, lakini tabia Yake haijaonyeshwa ndani yao kikamilifu. Kwa hivyo mnawahitaji kuongeza hatua nyingine katika kukuza ufahamu wenu wa tabia ya Mungu.

kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

118. Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au mijibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

119. Kumcha Mungu kuna maana gani? Na mtu anawezaje kuepuka maovu?

“Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kujisalimisha. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na utakatifu na malipo halisi; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.

Punde wanadamu wanapokuwa na imani ya kweli kwa Mungu, watakuwa wa kweli katika kumfuata Yeye na kumtegemea; kwa imani ya kweli pekee na tegemeo kwa Mungu ndipo binadamu watakuwa na kuelewa kwa kina na ufahamu; pamoja na ufahamu wa kweli wa Mungu inakuja kumjali Kwake kwa kweli; ni kwa kumjali Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na utiifu wa kweli kwa Mungu; na ni kwa utiifu wa Mungu kwa kweli pekee ndipo binadamu watakuwa na uwekaji wakfu wa kweli; na ni kwa uwekaji wakfu wa kweli kwa Mungu pekee ndipo binadamu watakuwa na malipo yasiyo na kiwango na kulalamika; ni kwa imani na msimamo wa kweli, kuelewa na kujali kwa kweli, utiifu wa kweli, utakatifu wa kweli na malipo, ndipo binadamu watakuja kujua kwa kweli tabia na kiini cha Mungu, na kujua utambulisho wa Muumba; Watakapopata kumjua Muumba ndipo binadamu wataamsha ndani yao ibada ya kweli na kujisalimisha; watakapokuwa na ibada ya kweli na kujisalimisha kwa Muumba tu ndipo binadamu wataweza kwa kweli kuweka kando njia zao za uovu, hivyo ni kusema, kuepuka maovu.

Hii inajumlisha hatua yote ya “kumcha Mungu na kuepuka maovu” na pia ni maudhui katika kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa ujumla, na pia njia ambayo ni lazima kupitia ili kufikia kumcha Mungu na kuepuka maovu.

kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

120. Katika kila enzi, Mungu huwapa binadamu baadhi ya maneno Anapofanya kazi ulimwenguni, huku akimwambia mwanadamu kuhusu baadhi ya ukweli. Ukweli huu unahudumu kama njia ambayo binadamu anafaa kuitii, njia ya kutembelewa na binadamu, njia ambayo humwezesha binadamu kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, na njia ambayo watu wanafaa kuweka katika vitendo na kuitii katika maisha yao na kwenye mkondo wa safari zao za maisha. Ni kwa sababu hizi ambapo Mungu anampa binadamu maneno haya. Binadamu anafaa kuyatii maneno haya yanayotoka kwa Mungu, na kuyatii ni kupokea uzima. Kama mtu hataweza kuyatii, na hayatii kwenye matendo, na haishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu katika maisha yake, basi mtu huyo hautilii ukweli katika matendo. Na kama hawatilii ukweli katika matendo, basi hawamchi Mungu na hawaepuki uovu, wala hawawezi kumtosheleza Mungu. Kama mtu hawezi kumtosheleza Mungu, basi hawezi kupokea sifa ya Mungu; mtu wa aina hii hana matokeo.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

121. Ni jambo gani kuu ambalo mtu anapaswa kuelewa anapotafuta kupata kuingia katika maisha? Ni kwamba katika maneno yote yaliyonenwa na Mungu, bila kujali yanarejea kipengele kipi, unapaswa kujua mahitaji na viwango Vyake ni gani kwa watu, na kutoka ndani ya maneno hayo, utafute njia ya kutenda. Unapaswa kuyatumia kuchunguza mwenendo wako na mtazamo wako katika maisha, na pia kuchunguza hali na maonysho yako yote kwa kuyatumia maneno hayo. Muhimu zaidi, unapaswa kuchunguza kwa kutumia viwango hivi ili kuamua jinsi ambavyo unapaswa kufanya mambo, jinsi ambavyo unapaswa kuridhisha mapenzi ya Mungu wakati wa kutekeleza wajibu wako, na jinsi unavyoweza kutenda kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu kikamilifu. Kuwa mtu aliye na uhalisi wa ukweli; usiwe mtu ambaye hujizatiti tu kwa maneno na mafundisho na nadharia za dini. Usibuni mambo ya kiroho; usiwe mtu bandia wa kiroho. Lazima umakinikie kutenda na kutumia maneno ya Mungu kulinganisha na kutafakari kuhusu hali zako mwenyewe, na kisha ubadilishe mtazamo na msimamo ambao wewe hutumia kushughulikia kila aina ya hali. Mwishowe, utaweza kumcha Mungu katika kila hali, na hutatenda tena bila subira au kufuata dhana zako mwenyewe, kufanya vitu kulingana na tamaa zako, au kuishi ndani ya tabia potovu. Badala yake, matendo yako na maneno yako yote yatategemea maneno ya Mungu na kwa mujibu wa ukweli; kwa sababu hiyo, utakuza uchaji Mungu polepole. Moyo wa kumwogopa Mungu hufanyizwa wakati wa kufuatilia ukweli; hautokani kwa kujizuia. Yote ambayo kujizuia husababisha ni aina moja ya tabia, lakini hiyo ni aina ya kizuizi cha nje. Uchaji Mungu wa kweli hutokana na—katika kipindi cha kumwamini Mungu—kuelewa ukweli, kutenda kwa mujibu wa ukweli, kupunguza polepole tabia potovu zaidi na zaidi, na kuboresha hali za mtu polepole ili mtu aweze kuja mbele za Mungu mara kwa mara; hii ndiyo aina ya mchakato inayosababisha uchaji wa kweli. Hilo litakapotokea, utajua maana ya kumcha Mungu na jinsi inavyohisi, na kisha utatambua aina ya mtazamo, aina ya hali, na aina ya tabia ambayo watu wanapaswa kumiliki kabla ya wao kumwogopa Mungu kwa kweli na kuonyesha uchaji wa Mungu.

kutoka katika “Ni Wale tu Wanaotenda Ukweli Ambao Wana Moyo wa Kumcha Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

122. Lazima kila mara uje mbele za Mungu, ule na unywe na kutafakari maneno Yake, na kukubali nidhamu na mwongozo Wake kwako. Lazima uweze kutii mazingira, watu, vitu, na mambo yote ambayo Mungu amekupangia, na inapofikia mambo ambayo huwezi kuyaelewa kabisa, lazima uombe mara kwa mara huku ukitafuta ukweli; unaweza kupata njia ya kusonga mbele kwa kuelewa tu mapenzi ya Mungu. Lazima umche Mungu, na ufanye kwa uangalifu kile unachopaswa kufanya; lazima mara nyingi uwe na amani mbele za Mungu, na usiwe mpotovu. Angalau, kitu kinapofanyika kwako, jibu lako la kwanza linapaswa kuwa kujituliza, na kisha uombe mara moja. Kwa kuomba, kungoja, na kutafuta, utapata ufahamu kuhusu mapenzi ya Mungu. Huu ni mtazamo ambao unaonyesha uchaji kwa Mungu, siyo? Ikiwa, ndani kabisa, wewe humcha Mungu na kumtii Mungu, na unaweza kuwa na utulivu mbele za Mungu na kufahamu mapenzi Yake, basi kwa kushirikiana na kutenda kwa njia hii, unaweza kulindwa. Hutakumbana na jaribu, au kumkosea Mungu, au kufanya vitu ambavyo vinakatiza kazi ya Mungu ya usimamizi, wala hutafika kiwango cha kuchochea chuki ya Mungu. Ukiwa na moyo wa kumwogopa Mungu, utaogopa kumkosea Mungu; mara utakapokabiliwa na jaribu, utaishi mbele Yake, ukitetemeka kwa hofu, na kutumaini kwamba katika vitu vyote utaweza kumtii na kumridhisha. Ni kwa kutenda kwa jinsi hii pekee, kuishi mara kwa mara katika hali kama hii, na kuwa na amani mara kwa mara mbele za Mungu ndiyo utaweza kujitenga na jaribu na uovu bila hata kufikiria.

kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

123. Kutembea katika njia ya Mungu hakuhusu kuangalia sheria juujuu. Badala yake, kunamaanisha kwamba unapokabiliwa na suala, kwanza kabisa, unaliangalia kama ni hali ambayo imepangwa na Mungu, wajibu uliopewa wewe na Yeye, au kitu ambacho Amekuaminia wewe, na kwamba unapokabiliana na suala hili, unapaswa kuliona kama jaribio kutoka kwa Mungu. Wakati unapokabiliwa na suala hili, lazima uwe na kiwango, lazima ufikirie kwamba suala hilo limetoka kwa Mungu. Lazima ufikirie ni vipi ambavyo utashughulikia suala hili kiasi cha kwamba unaweza kutimiza wajibu wako, na kuwa mwaminifu kwa Mungu; namna ya kulifanya bila ya kumghadhabisha Mungu; au kukosea tabia Yake. … Kwa sababu ili kutembea katika njia ya Mungu, hatuwezi kuwachilia chochote kinachotuhusu sisi wenyewe, au kinachofanyika karibu nasi, hata yale mambo madogo madogo. Haijalishi kama tunafikiria tunafaa kumakinika au la, mradi tu suala lolote linatukabili hatufai kuliacha. Lote linafaa kuonekana kama jaribio la Mungu kwetu. Mwelekeo aina hii uko vipi? Kama unao mwelekeo aina hii, basi unathibitisha hoja moja: Moyo wako unamcha Mungu, na moyo wako uko radhi kujiepusha na maovu. Kama unalo tamanio hili la kumtosheleza Mungu, basi kile unachotia katika matendo hakiko mbali na kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

124. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea Yeye na Mungu ni Mungu anayewaua watu—je, watu hawajui hili tayari?

kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

125. Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa wanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu—na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu uhuru wa kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

126. Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, isitoshe yeye mwenyewe binafsi alikuwa hajapitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliyokuwa nao wakati wa majaribio kunashuhudiwa na kila mmoja, na kunapendwa, kunafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wakayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na vilevile, wakaimba nyimbo zao za sifa. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo hii mbalimbali isiyo ya kina, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu, kuliko mtu yeyote mwingine. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakukuwa sanasana yenye ushupavu, wala, zaidi, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole, unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea na haki, na iliyopenda mambo mazuri—hakuna kati ya haya aliyomiliki yalimilikiwa na watu wa kawaida wengi. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwenye bidii katika fikira zake, na hivyo basi wakati wake usio wa kina duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na akauona ukubwa, utakatifu, na uhaki wa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na kuona utukufu na mamlaka ya Mungu mwenye mamlaka zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu kuweza kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu, na mtimilifu, na mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na kujiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuata mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawaje alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawaje alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuna binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawaje miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu ukosefu wa kina hiki cha maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika macho yake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Alikuwa hajamwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa kina duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu hakikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala hakikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye amefichwa miongoni mwa mambo yote, katika maisha yake ya kila siku. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti na maneno ya moyoni, ambayo Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote, alionyesha kupitia kwa kutawala Kwake kwa sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule uelewa na maarifa sawa ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu alikuwa hajajionyesha kwa Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kuweza kujitokeza kwa au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote ni tosha kwa binadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo wa Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu ni tosha kumfanya binadamu huyu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

127. “Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu” na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza ayapitie maneno ya Mungu, aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu Kwake na hukumu; iwapo mtu anataka kupitia maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika hali ya aina yote ya mazingira inayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza amiliki moyo wa kweli na mwaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, uamuzi na ujasiri wa kuepuka uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…Kwa njia hii, kuendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata ya kupevuka zaidi.

kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: (IX) Maneno Juu ya Kutimiza Wajibu Wako Kwa Kutosha

Inayofuata: (XI) Maneno Juu ya Uhusiano wa Mwanadamu na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Kazi na Kuingia (10)

Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki