B. Juu ya Kutekeleza Ukweli, Kuelewa Ukweli na Kuingia katika Uhalisi

344. Sasa ni Enzi ya Ufalme. Ikiwa umeingia katika enzi hii mpya inategemea ikiwa umeingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake yamekuwa uhalisi wa maisha yako. Maneno ya Mungu yanafahamishwa kwa kila mtu ili, mwishowe, watu wote wataishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, na maneno Yake yatampa nuru na kumwangazia kila mtu kutoka ndani. Ikiwa, wakati huu, wewe ni mzembe katika kusoma maneno ya Mungu, na huna shauku ya maneno Yake, basi hili linaonyesha kuwa hali yako ni mbaya. Ikiwa huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako; ikiwa umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Je, unaweza kufanya nini mwanzoni mwa Enzi ya Neno ili upate kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

345. Ukweli ambao mwanadamu anahitaji kuwa nao unapatikana katika neno la Mungu, na ni ukweli wenye manufaa na usaidizi zaidi kwa wanadamu. Ni dawa na ruzuku ambayo miili yenu inahitaji, kitu kinachomsaidia mwanadamu kurejesha tena ubinadamu wake wa kawaida. Ni ukweli ambao mwanadamu anapaswa kujitayarisha nao. Kadiri mnavyotenda neno la Mungu, ndivyo maisha yenu yatakavyositawi haraka zaidi, na ndivyo ukweli utakavyokuwa dhahiri zaidi. Mnapozidi kukua katika kimo, mtaona vitu vya dunia ya kiroho kwa dhahiri zaidi, na ndivyo mtakavyokuwa na nguvu zaidi kumshinda Shetani. Ukweli mwingi ambao hamwelewi utafanywa kuwa dhahiri mtakapotenda neno la Mungu. Watu wengi wanaridhishwa kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na hawalengi kujitayarisha kwa mafundisho badala ya kuzidisha uzoefu wao kwa vitendo, lakini, je, hiyo si njia ya Mafarisayo? Kwa hivyo msemo “Neno la Mungu ni uzima” unawezaje kuwa wa kweli kwao? Maisha ya mtu hayawezi kukua kwa kusoma neno la Mungu tu, bali ni wakati tu neno la Mungu linawekwa katika vitendo. Ikiwa unaamini kwamba kuelewa neno la Mungu ndicho kitu pekee kinachohitajika kuwa na uzima na kimo, basi ufahamu wako umepotoka. Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema kwamba unalielewa. Wengine husema kwamba njia ya pekee ya kutenda ukweli ni kuuelewa kwanza, lakini hii ni sahihi kwa kiwango fulani tu, na hakika si sahihi kikamilifu. Kabla uwe na maarifa ya ukweli fulani, hujapitia ukweli huo. Kuhisi kwamba unaelewa kitu unachosikia katika mahubiri si kuelewa kwa kweli—huku ni kuwa na maneno halisi ya ukweli tu, na si sawa na kuelewa maana ya kweli ndani yake. Kuwa tu na maarifa ya juujuu ya ukweli hakumaanishi kwamba kweli unauelewa ama una maarifa yoyote kuuhusu; maana ya kweli ya ukweli hutokana na kuupitia. Kwa hiyo, ni wakati tu unapopitia ukweli ndiyo unaweza kuuelewa, na ni hapo tu ndiyo unaweza kufahamu sehemu zake zilizofichika. Kukuza uzoefu wako ndiyo njia ya pekee ya kuelewa vidokezo, na kuelewa asili ya ukweli. Kwa hiyo, unaweza kuenda popote ukiwa na ukweli, lakini iwapo hakuna ukweli ndani yako, basi usifikirie kujaribu kuwashawishi hata wanafamilia wako sembuse watu wa kidini. Bila ukweli wewe ni kama vipande vidogo sana vya theluji vinavyopepea. lakini ukiwa na ukweli unaweza kuwa na furaha na uhuru, na hakuna anayeweza kukushambulia. Bila kujali jinsi nadharia fulani ilivyo thabiti, haiwezi kuushinda ukweli. Kukiwa na ukweli, dunia yenyewe haiwezi kuyumba na milima na bahari kusogezwa, wakati ukosefu wa ukweli unaweza kusababisha nyuta zenye nguvu za mji kuangushwa na mabuu. Huu ni ukweli dhahiri.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

346. Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama mtu ana uwezo wa mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kulifunza kundi la wanajeshi wazuri wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi au watu ambao hujigamba tu, bali ni kuwafunza wanadamu ambao wanajivunia tu, lakini wanadamu ambao wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, ambao ni wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, na wanaoishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, na hawarudi kwa ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuone uhalisi ulionenwa na Mungu kama rahisi sana. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupata kazi ya Mungu. Hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba utamiliki uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo—komesha misemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Sio tu kwamba kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi

347. Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri kwa na namna hii: Naweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu anasema ni vizuri na kunipa hongera, hivyo inahesabika kama kuelewa neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza nia ya neno la Mungu na kile ambacho yatafanikisha hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure! Je, neno la Mungu linapasa kutafsiriwa vipi? Je, neno la Mungu linapasa kueleweka vipi? Msingi ni kuelewa neno Lake kutoka ndani ya neno Lake. Kila mara Mungu anenapo hakika Haneni kwa ujumla tu. Ndani ya kila sentensi kuna maudhui yenye maelezo ambayo yana uhakika wa kufichuliwa zaidi katika neno la Mungu, na yanaweza kuonyeshwa kwa njia tofauti. Mwanadamu hawezi kuelewa njia ambazo Mungu huonyesha ukweli. Neno la Mungu lina undani na haliwezi kuingiliwa na njia ya mwanadamu ya kufikiria. Watu wanaweza kugundua maana kamili ya kila kipengele cha ukweli mradi watie bidii, na maelezo yanayosalia yanajazwa kabisa Roho Mtakatifu anapotia ufahamu wako nuru wa hali dhabiti kwa kupitia. Sehemu moja ni kuelewa neno la Mungu kwa kupitia neno Lake, kutafuta maudhui mahsusi ya neno Lake. Sehemu nyingine ni kuelewa athari za neno la Mungu kwa kulipitia na kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kimsingi ni kwa njia hizi mbili ndipo ufahamu wa kweli wa Mungu unatimizwa. Ukieleza hili kwa uhalisi au kutoka kwa fikira au mawazo yako mwenyewe, basi ufahamu wako si wa kweli bila kujali jinsi unavyoweza kueleza kwa umbuji. Inawezekana kwamba wewe hata unaweza hata kutoka maana nje ya muktadha na kueleza neno la Mungu vibaya, na hilo ni la taabu hata zaidi. Hivyo, ukweli kimsingi unapatikana kwa kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu kupitia kujua neno la Mungu. Kuelewa maana halisi ya neno Lake au kuweza kulieleza hakuhesabiki kama kupata ukweli. Kama ungehitaji tu kueleza maandishi ya neno Lake, basi kungekuwa na haja gani ya kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu? Katika hali hiyo ungehitaji kuwa na kiwango fulani cha masomo, na wale ambao hawajasoma wangekuwa kwenye hatari kabisa. Kazi ya Mungu si kitu ambacho kinaweza kufahamika na akili ya mwanadamu. Ufahamu wa kweli wa neno la Mungu unategemea hasa kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; hii ni namna ya kuupata ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

348. Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu. Kwa kweli, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa ninyi kupitia neno Lake na vilevile kupatwa na Yeye, ama kuzungumza dhahiri zaidi, kumwamini Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huu ndio uhalisi wa ninyi kumwamini Mungu. Ikiwa mnamwamini Mungu na mnatumai kupata uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu kilicho ndani yenu, basi ninyi ni wapumbavu. Hii itakuwa sawa na kwenda katika karamu na kuangalia tu chakula na kujua na kuweza kuvikariri vitu vitamu bila kuvionja kwa kweli. Je, mtu kama huyu si mpumbavu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

349. Matakwa ya Mungu kwa watu si ya juu sana. Ikiwa watu wataweka hata jitihada kidogo wataweza kupata “alama ya kupita.” Kwa kweli, kufahamu, kujua, na kuelewa ukweli kunatatiza sana kuliko kuutenda ukweli; kuujua na kuutambua ukweli kunakuja baada ya kuutenda ukweli; hizi ndizo hatua na njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi. Unawezaje kutotii? Je, unaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu kwa kufanya mambo kwa namna yako? Je, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kuzingatia ridhaa yako, au kwa msingi wa kasoro zako kulingana na maneno ya Mungu? Haina maana ikiwa huwezi kuliona hili kwa uwazi. Kwa nini watu wengi zaidi wametumia jitihada nyingi kusoma maneno ya Mungu lakini wana maarifa tu na hawawezi kusema kitu chochote kuhusu njia halisi baada ya hapo? Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Je, huo si mtazamo uliokanganywa? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Je, unafanya maonyesho matupu, bila dutu ya kuyasitiri? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha. Je, hili halileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha. Kwa hivyo, zungumza zaidi juu ya matatizo ambayo yapo kwa kweli. Usiyachukulie matukio ya watu wengine kama mali yako binafsi na kuyaonyesha waziwazi ili wengine wastahi; unapaswa kutafuta suluhisho lako binafsi mwenyewe. Hiki ndicho ambacho kila mtu anapaswa kuweka katika vitendo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Sisitiza Uhalisi Zaidi

350. Je, ufahamu wenu wa ukweli umefungamana na hali yenu ya kibinafsi? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, matukio, na vitu ambavyo umekumbana navyo; ni miongoni mwa ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Iwapo hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo ambayo umekumbana nayo lakini badala yake unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, huu ni mtazamo ambao hauna mwelekeo ambao hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo yametendeka kwako, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yana uhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli maalum katika neno la Mungu ambalo linahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya matendo ambayo ni sahihi kwako katika ukweli huo; kutokana na njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kutumia kanuni au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho kuonyesha waziwazi kile Mungu alisema; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu hapendi, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, watu ambao Anawachukia na watu ambao Anawafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu wao umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kunatokea tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo mwenyewe kwa kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

351. Tangu watu waanze kumwamini Mungu, wamekuwa na nia ambazo si sahihi. Wakati ambapo huweki ukweli katika vitendo, unahisi kuwa motisha zako ni sahihi, lakini jambo likikutokea, utaona kuwa kuna motisha nyingi ndani zisizo sahihi. Hivyo, Mungu akiwafanya watu kuwa wakamilifu, Anawafanya kugundua kuwa kuna dhana nyingi ndani yao ambazo zinawazuia kumfahamu Mungu. Ukitambua kuwa motisha zako zina makosa, kama unaweza kuacha kutenda kulingana na motisha na dhana zako, na unaweza kuwa na ushuhuda wa Mungu na kusimama imara katika msimamo wako kwa kila lifanyikalo kwako, hili linathibitisha kuwa umeuasi mwili wako. Ukiasi dhidi ya mwili wako, bila shaka kutakuwa na vita ndani yako. Shetani atajaribu kufanya watu kuifuata, atajaribu kuwafanya wafuate dhana za kimwili na kutekeleza maslahi ya kimwili—ila maneno ya Mungu yatawapa nuru watu na kuwaangazia kwa ndani, na wakati huu itakuwa juu yako ikiwa utamfuata Mungu au utamfuata Shetani. Mungu anawataka watu kuweka ukweli katika matendo kimsingi kushughulikia mambo yaliyo ndani yao, kushughulikiwa fikira zao, na dhana zao ambazo haziufuati moyo wa Mungu. Roho Mtakatifu huwagusa watu ndani ya mioyo yao, na kuwapa nuru na mwangaza. Kwa hivyo katika tukio lolote katika vita: Kila wakati watu wanapoweka ukweli katika vitendo, au kuweka mapenzi ya Mungu katika vitendo, huwa kuna vita vikali, na japokuwa mambo yanaweza kuonekana shwari katika miili yao, ila ndani ya mioyo yao kutakuwa na vita vya kufa na kupona—na ni baada tu ya hivi vita vikali, baada ya kutafakari kwa kina, ndipo ushindi au kushindwa kunaweza kuamuliwa. Mtu anashindwa kujua ama acheke au alie. Kwa sababu motisha nyingi ndani ya watu zina makosa, ama kwa sababu kazi kubwa ya Mungu inakinzana na dhana zao, watu wakiuweka ukweli katika vitendo vita vikali huzuka kisirisiri. Baada ya kuuweka huu ukweli katika vitendo, kisirisiri watu watakuwa wamemwaga machozi mengi sana ya huzuni kabla ya kuamua kumridhisha Mungu. Ni kwa sababu ya vita hivi watu huvumilia shida na usafishaji; huku ni kuteseka kwa kweli. Vita vikikukabili, kama unaweza kusimama kweli upande wa Mungu, utaweza kumridhisha Mungu. Katika harakati ya kutenda ukweli, hakuepukiki kwamba mtu atateseka kwa ndani; ikiwa, wanapoweka ukweli katika vitendo, kila kitu ndani yao kingekuwa sawa, basi wasingehitaji kufanywa wakamilifu na Mungu, na kusingekuwa na vita, na hawangeteseka. Ni kwa sababu kuna mambo mengi ndani ya watu ndipo hawafai kutumiwa na Mungu, na tabia nyingi za uasi wa mwili, ndipo watu wanapaswa kujifunza funzo la kuasi dhidi ya mwili kwa kina zaidi. Huku ndiko Mungu anaita kuteseka ambako Alimtaka mwanadamu kushiriki Naye. Ukikumbana na shida, fanya hima na umwombe Mungu: Ee Mungu! Ninataka kukuridhisha, ninataka kustahimili mateso ya mwisho ili kuuridhisha moyo Wako, na bila kujali kuwa vikwazo ninavyokumbana navyo ni vikubwa kiasi gani, bado ni sharti nikuridhishe. Hata ikiwa ni kuyatoa maisha yangu yote, bado ni sharti nikuridhishe! Ukiomba na hili azimio utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako. Kila wawekapo ukweli katika vitendo, kila wapitiapo usafishaji, kila wanapojaribiwa, na kila wakati kazi ya Mungu inapowashukia, watu wanapitia mateso makubwa. Haya yote ni mtihani wa watu, na kwa hivyo ndani yao wote mna vita. Hii ndiyo gharama hasa wanayolipa. Kusoma zaidi neno la Mungu na kuzungukazunguka zaidi, kwa namna fulani ni gharama. Ndiyo watu wanapaswa kufanya, ndio wajibu wao, na jukumu ambalo ni sharti walitimize, lakini ni lazima watu waweke kando yale yanayofaa kuwekwa kando. Ikiwa hamwezi, basi haijalishi mateso yako yatakuwa makubwa kiasi gani, na utazunguka kiasi gani, yote yatakuwa bure! Hivi ni kusema, ni mabadiliko ndani yako tu yanaweza kuamua iwapo mateso yako ya nje yana thamani. Tabia yako ya ndani ikibadilika na ikiwa umeweka ukweli katika vitendo, basi mateso yako yote ya nje yatapata kibali cha Mungu; ikiwa hakujakuwa na mabadiliko katika tabia yako ya ndani, basi haijalishi unateseka kiasi gani au unazungukazunguka kiasi gani nje, hakutakuwa na kibali kutoka kwa Mungu—na mateso ambayo hayajaidhinishwa na Mungu ni bure! Hivyo, kama gharama ambayo umelipa imedhinishwa na Mungu inaamuliwa na kama umekuwa na mabadiliko ndani yako au la, na kama unatia ukweli katika vitendo na kuasi dhidi ya motisha na dhana zako mwenyewe ili kupata ridhaa ya mapenzi ya Mungu, ufahamu wa Mungu, na uaminifu kwa Mungu. Haijalishi unazungukazunguka kiasi gani, ikiwa hujawahi kujua kuasi dhidi ya motisha zako, unatafuta tu matendo na hamasa za nje, na usitilie maanani maisha yako, basi taabu zako zitakuwa zimepita bure.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

352. Kwa ufupi, kuichukua njia ya Petro katika imani ya mtu kunamaanisha kuitembea njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kupata kujijua na kubadilisha tabia yako kwa kweli. Ni kwa kuitembea njia ya Petro tu ndipo mtu atakuwa katika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe jinsi hasa ya kuitembea njia ya Petro, na vilevile jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia na vitu vyote vya mwili wake mwenyewe. Yeye lazima ajitolee kwa moyo wote; yaani, lazima ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, alenge kula na kunywa maneno ya Mungu, azingatie kutafuta ukweli na kutafuta madhumuni ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi na muhimu zaidi ya utendaji. Hilo ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu anaweza kufanikisha matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu kimsingi kunajumuisha kutafuta ukweli, kutafuta nia za Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka katika maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini, sembuse kuzingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alitilia maanani kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na vile vile kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Petro pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka katika maneno ya Mungu, na vile vile asili potovu ya mwanadamu na dosari yake halisi hivyo kufikia vipengele vyote vya matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. petro alikuwa na vitendo vingi sahihi vilivyofuata maneno ya Mungu; hili lililingana zaidi na mapenzi ya Mungu, na ni njia bora zaidi ambayo mtu angeshirikiana huku akipitia kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, Petro alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajitahidi kuelewa maana ya maneno hayo. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia namna hii ya utendaji, aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini, asili, na dosari mbalimbali za mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, Petro hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika maneno ya Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, na vilevile uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu hakuzungumza wakati huo sana kama Anavyofanya leo, matokeo katika vipengele hivi, hata havyo yalipatikanana Petro. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio, lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Aidha, alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake. Bila kujali ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu, Petro aliweza kufanya juhudi kubwa katika vipengele hivi na kupata uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa kubwa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, Petro aliweza kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari na kuyathamini mara kwa mara. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu, aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii, Petro aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

353. Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake. Wale ambao Mungu hupenda ni watu ambao ni kamili kabisa, watu ambao wamejitolea kwake na hakuna mwingine. Wale ambao Yeye huwachukia ni watu ambao wako shingo upande kumhusu, na ambao wanaasi dhidi Yake. Anawachukia wale wanaomwamini na daima wanataka kumfurahia, lakini hawawezi kujitumia kabisa kwa ajili Yake. Anawachukia wale wanaosema wanampenda lakini wanaomuasi mioyoni mwao. Anawachukia wale wanaotumia maneno matamu ili wafanye udanganyifu. Wale ambao hawajitolei kwa kweli kwa Mungu au hawana utiifu wa kweli Kwake ni watu wasio waaminifu; wao kwa kawaida ni wenye kiburi sana. Wale ambao hawawezi kuwa watiifu kwa kweli mbele ya Mungu wa kawaida, wa vitendo hata ni wenye kiburi zaidi, na hasa wao ni uzao mtiifu wa malaika mkuu. Wale ambao kwa kweli hujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu huweka nafsi zao zote mbele Yake. Wao hutii kwa kweli matamshi Yake yote, na wana uwezo wa kuweka maneno Yake katika matendo. Wao hufanya maneno ya Mungu kuwa msingi wa kuwepo kwao, na wanaweza kutafuta kwa kweli sehemu za matendo katika neno la Mungu. Huyu ni mtu ambaye kwa kweli anaishi mbele ya Mungu. Ikiwa unachofanya ni cha manufaa kwa maisha yako, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yake, unaweza kukidhi mahitaji yako ya ndani na upungufu ili tabia yako ya maisha inabadilishwa, basi hii itatimiza mapenzi ya Mungu. Ikiwa unatenda kulingana na mahitaji ya Mungu, ikiwa huuridhishi mwili lakini unaridhisha mapenzi Yake, huku ni kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Wakati unazungumza juu ya kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu kwa kweli zaidi, kunamaanisha unaweza kutekeleza wajibu wako na kukidhi mahitaji ya Mungu. Aina hizi tu za vitendo ndizo zinazoweza kuitwa kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Ikiwa una uwezo wa kuingia katika uhalisi huu, basi una ukweli. Huu ndio mwanzo wa kuingia katika uhalisi; lazima kwanza ufanye mazoezi haya na ni baada tu ya hayo ndio utakuwa na uwezo wa kuingia katika hali halisi za kina zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa

354. Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi zaidi, ndivyo wanavyokuwa na dhana chache zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kujiweka huru kutokana na tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu. Watu waliopatikana na Mungu ni wale walio na uhalisi, na wanaojua uhalisi; wale ambao wamepatikana na Mungu wamepata kuyajua matendo halisi ya Mungu kutokana na kupitia katika uhalisi. Kadiri hasa unavyoshirikiana zaidi na Mungu na kuudhibiti mwili wako, ndivyo utakavyopokea zaidi kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyopata uhalisi zaidi, na ndivyo utapatiwa nuru zaidi na Mungu—na hivyo ukubwa wa ufahamu wako wa matendo halisi ya Mungu. Ikiwa unaweza kuishi katika mwangaza wa sasa wa Roho Mtakatifu, njia ya sasa ya kutenda itakuwa wazi kwako, na utaweza kujitenga zaidi na dhana za kidini na vitendo vilivyopita zamani. Leo tunalenga uhalisi: Kadiri watu walivyo na uhalisi zaidi, ndivyo ufahamu wao wa ukweli unavyokuwa wazi, na ufahamu wao wa mapenzi ya Mungu unaongezeka. Uhalisi unaweza kuzishinda nyaraka zote na mafundisho yote ya kidini, unaweza kushinda nadharia na utaalamu wote, na kadiri watu wanavyoangazia uhalisi zaidi, ndivyo wanavyompenda Mungu kwa dhati zaidi na kuyatamani maneno Yake. Ikiwa daima unalenga uhalisi, falsafa yako ya maisha, dhana za kidini, na tabia asilia zitafutwa kutokana na kazi ya Mungu. Wale wasiouandama uhalisi, na hawafahamu uhalisi, wanaelekea kutafuta kile kilicho na nguvu za juu, na watalaghaiwa kwa urahisi. Roho Mtakatifu hana namna ya kufanya kazi ndani ya watu kama hao, na kwa hivyo wanajisikia watupu, na kwamba maisha yao hayana maana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kujua Uhalisi

355. Kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na ukweli; kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na upendo wa Mungu; na kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyobarikiwa na Mungu. Kama utatenda kwa njia hii kila mara, upendo wa Mungu kwako utakuwezesha kuona polepole, jinsi tu ambavyo Petro alivyokuja kumjua Mungu: Petro alisema kuwa si kuwa Mungu ana busara ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo pekee, lakini, aidha, kuwa Ana busara ya kufanya kazi halisi ndani ya watu. Petro alisema kuwa Mungu hastahili tu upendo wa watu kwa sababu ya uumbaji Wake wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, lakini, vilevile, kwa sababu ya uwezo Wake wa kuumba mwanadamu, kumwokoa, kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na kutoa upendo wake kwa mwanadamu. Petro alimwambia Yesu: “Je, Hustahili upendo wa watu zaidi ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo? Kuna mengi ndani Yako ambayo yanapendeka, unatenda na kuendelea katika maisha halisi, Roho Wako ananigusa ndani, unanifundisha nidhamu, unanikemea—haya mambo yanastahili zaidi upendo wa watu.” Kama unataka kuona na kupitia upendo wa Mungu, basi lazima uzuru na kutafuta katika maisha halisi, na uwe tayari kuweka kando mwili wako. Lazima ufanye azimio hili: kuwa mtu mwenye uamuzi, ambaye anaweza kumridhisha Mungu katika mambo yote, bila ya kuzembea, au kutamani kuufurahisha mwili, kutoishi kwa ajili ya mwili lakini kuishi kwa ajili ya Mungu. Kunaweza kuwa na nyakati ambazo hukumridhisha Mungu. Hii ni kwa sababu huelewi mapenzi ya Mungu; wakati ujao, hata kama itahitaji juhudi zaidi, lazima umridhishe Mungu, na lazima usiuridhishe mwili. Unapopitia kwa njia hii, utakuja kumjua Mungu. Utaona kuwa Mungu angeweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, na Amekuwa mwili ili watu wamwone kwa uhakika, na kujihusisha na Yeye, kuwa ana uwezo wa kuishi miongoni mwa wanadamu, kuwa Roho Wake aweza kufanya watu kuwa wakamilifu katika maisha halisi, kuwawezesha kuona upendo na uzoefu wa nidhamu Yake, kurudi Kwake, na baraka Zake. Kama huwa unapitia kwa njia hii, katika maisha halisi hutatenganishwa na Mungu, na kama siku moja uhusiano wako na Mungu utaacha kuwa wa kawaida, utaweza kupatwa na aibu, na kuweza kuhisi huzuni. Unapokuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, hutatamani kamwe kutaka kumuacha, na siku moja Mungu akisema Atakuacha, utaogopa, na kusema kuwa ni heri ufe kuliko kuachwa na Mungu. Punde tu unapokuwa na hisia hizi, utahisi kuwa hakuna uwezo wa kumwacha Mungu, na kwa njia hii utakuwa na msingi, na utafurahia upendo wa Mungu wa kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

356. Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kufuatilia ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

357. Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtu kufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Iliyotangulia: A. Kuhusu Kuwa na Imani katika Mungu

Inayofuata: C. Jinsi ya Kujijua Mwenyewe na Kufikia Toba ya Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp