A. Kuhusu Kuwa na Imani katika Mungu
331. Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, sembuse kuweza kutimiza hamu ya Mungu. “Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu. Ilhali watu mara nyingi huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi sana na la kipuuzi tu. Watu wanaomwami Mungu kwa njia hii wamepoteza maana ya kumwamini Mungu, na ingawa wanaweza kuendelea kuamini mpaka mwisho, hawatawahi kupata idhini ya Mungu, kwa sababu wanatembea katika njia mbaya. Leo, kuna wale ambao bado wanaamini Mungu katika nyaraka, katika mafundisho ya dini yaliyo matupu. Hawana habari kuwa imani yao katika Mungu haina dutu, na hawawezi kupata idhini ya Mungu, na bado wanaomba kupata amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu. Tunafaa kuweka kituo na kujiuliza wenyewe: Je, kuamini kwa Mungu linaweza kuwa jambo rahisi ya yote duniani? Je, kuamini kwa Mungu hakumaanishi chochote zaidi ya kupokea neema nyingi kutoka kwa Mungu? Je, watu wanaoamini kwa Mungu na hawamjui, na wanaamini kwa Mungu ila wanamuasi; je watu kama hawa wanaweza kutimiza hamu ya Mungu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
332. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—haya ndiyo mahitaji ya chini kabisa ya imani yako katika Mungu. Imani katika Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha ya mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu; kutoka katika kuishi ndani ya upotovu hadi katika kuishi ndani ya maisha ya maneno ya Mungu; ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii. Ukiwa na maarifa ya Mungu tu ndipo unapoweza kumpenda, na hili ndilo lengo ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
333. Kwa kuwa unamwamini Mungu, basi lazima uyale na kuyanywa maneno Yake, uyapitie maneno Yake, na uishi kwa kuyadhihirisha maneno Yake. Hii tu ndiyo inayoweza kuitwa imani katika Mungu! Ukisema kwa mdomo wako kwamba unamwamini Mungu lakini huwezi kuyaweka maneno Yake yoyote katika vitendo au kutoa ukweli wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni "kutafuta mkate ili kumaliza njaa." Kuzungumza tu kuhusu ushuhuda mdogo, vitu visivyo na maana, na mambo ya juujuu, bila kuwa hata na ukweli mdogo kabisa: hivi havijumuishi imani katika Mungu, na hujafahamu tu njia sahihi ya kuamini katika Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo? Usipokula na kunywa maneno Yake lakini utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Je, hatua ya kwanza ambayo mtu amwaminiye Mungu anapaswa kuchukua ni ipi? Ni kwa njia gani ndiyo Mungu humkamilisha mwanadamu? Je, unaweza kukamilishwa bila kula na kunywa maneno ya Mungu? Je, unaweza kuchukuliwa kama mtu wa ufalme bila ya maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wako? Je, ni nini hasa maana ya imani katika Mungu? Waumini katika Mungu wanapaswa, angalau, kuwa na tabia njema kwa nje; la muhimu zaidi ni kuwa na maneno ya Mungu. Bila kujali chochote, kamwe huwezi kuyaacha maneno Yake. Kumjua Mungu na kutimiza nia Zake vinafanikishwa kupitia katika maneno Yake. Katika siku zijazo, kila taifa, dhehebu, dini, na sehemu zitashindwa kwa njia ya maneno ya Mungu. Mungu atazungumza moja kwa moja, na watu wote watashikilia maneno ya Mungu mikononi mwao, na kwa njia hii, binadamu watakamilishwa. Ndani na nje, maneno ya Mungu yanapenyeza kotekote: Binadamu watazungumza maneno ya Mungu kwa vinywa vyao, watende kulingana na maneno ya Mungu, na kuweka maneno ya Mungu ndani, wakisalia wamelowa na maneno ya Mungu ndani na nje. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza nia za Mungu na wanaweza kumshuhudia, hawa ni watu wanaomiliki maneno ya Mungu kama ukweli wao.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno
334. Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu
335. Unaweza kufikiri kwamba kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kumfanyia mambo ya kila aina; unaweza kufikiri kwamba sababu ya kumwamini Mungu ni ili mwili wako uwe na amani, au ili kwamba kila kitu maishani mwako kiende vizuri, au ili kwamba uweze kuwa na raha na utulivu katika kila kitu. Hata hivyo, hakuna kati ya haya ambayo watu wanapaswa kuhusisha na imani yao katika Mungu. Ukiamini kwa ajili ya sababu hizi, basi mtazamo wako si sahihi na haiwezekani kabisa wewe kukamilishwa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Kuwa na ufahamu huu, unapaswa kuutumia kuondoa moyoni mwako madai, matumaini na fikiza za kibinafsi. Ni kwa kuondoa mambo haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu, na ni kwa kufanua hivi tu ndiyo unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kusudi la kumwamini Mungu ni ili kumridhisha na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na hili pia ndilo lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi kuhusu kuamini katika Mungu na unapaswa kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa lazima uweze kuona matendo Yake ya vitendo, matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kupitia katika uzoefu wao wa vitendo, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Kusudi la haya yote ni ili kuondoa tabia potovu ya kishetani ya watu. Baada ya kuondoa uchafu na udhalimu wote ulio ndani mwako, na baada ya kuondoa nia zako mbaya, na baada ya kukuza imani ya kweli kwa Mungu—ni kwa kuwa na imani ya kweli tu ndiyo unaweza kumpenda Mungu kweli. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha upendo wa kweli kwa Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini kisha hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona kwamba wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, lazima upate utiifu kamili na mzima mbele ya Mungu katika imani yako. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—hizi zote ni tabia za watu walio na mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti kubadilisha tabia zao na hawafuatilii maarifa ya Mungu, lakini badala yake wanatafuta tu masilahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini; hii siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu, watu lazima wamiliki moyo ulio tayari kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Watu wasipokidhi haya masharti mawili, imani yao katika Mungu haihesabiki, na hawataweza kufanikisha mabadiliko katika tabia yao. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
336. Kwa miaka na mikaka Nimeona watu wanaomsadiki Mungu. Kusadiki huku kunachukua mfumo gani? Baadhi ya watu wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu. Watu hawa hawana majibu ya maswali kuhusu uwepo wa Mungu kwa sababu hawawezi kuhisi au kuwa na ufahamu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu, sikuambii hata kuuona waziwazi au kuuelewa. Kwa nadharia yao, watu hawa wanafikiria kwamba Mungu hayupo. Baadhi wanasadiki katika Mungu ni kana kwamba Yeye ni binadamu. Watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hawezi kufanya mambo yale ambayo wao hawawezi kufanya, na kwamba Mungu anafaa kufikiria namna wanavyofikiria. Ufafanuzi wa mtu huyu kuhusu Mungu ni “mtu asiyeonekana na asiyegusika.” Kunalo pia kundi la watu wanaosadiki katika Mungu kana kwamba Yeye ni kikaragosi; watu hawa wanasadiki kwamba Mungu hana hisia. Wanafikiria kwamba Mungu ni sanamu ya matope, na kwamba wanapokabiliwa na jambo, Mungu hana mwelekeo, hana mtazamo, hana mawazo; Anatawaliwa na binadamu. Watu wanasadiki tu wanavyotaka kusadiki. Wakimfanya kuwa mkubwa, Yeye ni mkubwa; wakimfanya kuwa mdogo, Yeye ni mdogo. Wakati wanapotenda dhambi na wanahitaji rehema ya Mungu, wanahitaji uvumilivu wa Mungu, wanahitaji upendo wa Mungu, basi Mungu anafaa kutoa rehema Zake. Watu hao wanafikiria kuhusu Mungu kwenye akili zao binafsi na kumfanya Mungu kutimiza mahitaji yao na kutosheleza matamanio yao yote. Haijalishi ni lini na ni wapi, na haijalishi hata mtu huyu anafanya nini, watakubali mvuto huu katika matendo yao kwa Mungu na kusadiki kwao katika Mungu. Kuna hata wale wanaosadiki katika Mungu kuweza kuwaokoa baada kuikera tabia ya Mungu. Hii ni kwa sababu wanasadiki kuwa upendo wa Mungu hauna mipaka, tabia ya Mungu ni haki, na kwamba bila kujali ni vipi ambavyo watu wanakosea Mungu, Hatakumbuka chochote. Kwa sababu makosa ya binadamu, dhambi za binadamu na kutotii kwa binadamu ni maonyesho ya mara moja ya tabia ya mtu huyo, Mungu atawapatia watu fursa, kuvumilia na kuwa na subira nao. Mungu angali atawapenda kama awali. Kwa hivyo tumaini la wokovu wao lingali kubwa. Kwa hakika, haijalishi ni vipi mtu anavyosadiki Mungu, mradi tu hafuatilii ukweli basi Mungu anashikilia mwelekeo mbaya kwake. Hii ni sababu wakati unamsadiki Mungu, labda unakithamini kile kitabu cha neno la Mungu unakichambua kila siku, unakisoma kila siku, lakini unamweka Mungu halisi pembeni, unamchukulia kama hewa tupu, unamchukulia Yeye kama mtu, na baadhi yenu mnamchukulia kuwa kikaragosi. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu kutokana na vile Ninavyoona, licha ya kama unakabiliwa na suala au kukumbana na hali, yale mambo yanayopatikana katika nadharia yako, yale mambo ambayo yameimarishwa ndani kwa ndani—hakuna kati ya haya ambayo yana uunganisho wa neno la Mungu au yanafuatilia ukweli. Unajua tu kile wewe mwenyewe unatafuta, maoni yako wewe binafsi, na kisha mawazo yako binafsi, mitazamo yako binafsi inalazimishiwa Mungu. Inakuwa mitazamo ya Mungu. Akilini mwako hii inakuja kuwa mitazamo ya Mungu, na unafanya hii mitazamo kuwa viwango ambavyo unavishikilia bila kutetereka. Kwa muda, kuendelea namna hii kunakufanya uwe mbali na mbali kutoka kwa Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha
337. Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atamshughulikia na kumkomesha kila mmoja.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
338. Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu
339. Unamwamini Mungu na unafuata Mungu, na kwa hivyo moyoni mwako ni lazima umpende Mungu. Ni lazima uache tabia yako potovu, lazima utafute kutimiza mapenzi ya Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako kama kiumbe wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini na kumfuata Mungu, unapaswa kutoa kila kitu kwake, na hupaswi kufanya uamuzi au madai ya kibinafsi, na unapaswa kutimiza ukamilishaji wa mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa uliumbwa, unapaswa kumtii Bwana aliyekuumba, kwa kuwa wewe huna mamlaka kiasili juu yako mwenyewe, na huna uwezo wa kudhibiti hatima yako. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye anamwamini Mungu, inapaswa utafute utakatifu na mabadiliko. Kwa kuwa wewe ni kiumbe wa Mungu, unapaswa kushika wajibu wako, na kuhifadhi nafasi yako, na ni lazima usivuke mpaka wa wajibu wako. Hii si kwa ajili ya kukuzuia, ama kukukandamiza kupitia mafundisho, bali ndiyo njia ambayo utaweza kutekelezea wajibu wako, na inaweza kufikiwa—na inapaswa kufikiwa—na wote wanaotenda haki.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
340. Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na kwamba ajitolee mwenyewe, na kutii kwa kweli. Kile kigumu sana kwa mwanadamu ni kupeana mwili wake ili abadilishe na imani ya kweli, ambapo kupitia hii anaweza kupata ukweli mzima, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hili haliwezi kupatikana na wale ambao wanafeli, na halipatikani hata zaidi na wale ambao hawawezi kumpata Yesu. Kwa sababu mwanadamu si hodari kwa kujitolea mwenyewe kwa Mungu kabisa, kwa sababu mwanadamu hayuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa Muumba, kwa sababu mwanadamu ameona ukweli lakini anauepuka na kutembea katika njia yake mwenyewe, kwa sababu mwanadamu daima anatafuta kwa kufuata njia ya wale walioshindwa, kwa sababu mwanadamu daima anaasi Mbingu, hivyo, mwanadamu daima hushindwa, huchukuliwa na hila za Shetani, na anakamatwa kwa hila na wavu wake. Kwa sababu mwanadamu hamjui Kristo, kwa sababu mwanadamu hana ustadi katika kuelewa na kushuhudia ukweli, kwa sababu mwanadamu ni wa kuabudu Paulo sana na mwenye tamaa nyingi ya mbinguni, kwa sababu mwanadamu daima anadai kuwa Kristo awe akimtii yeye na kuagiza kuhusu Mungu, hivyo mashujaa hao wakuu na wale ambao wamepitia mabadiliko mabaya ya dunia bado wamo na ubinaadamu, na bado hufa kwa kuadibu kwa Mungu. Yote Ninayoweza kusema kuhusu watu kama hawa ni kuwa wanakufa kifo cha kutisha, na athari yao—kifo chao—si bila haki. Je, si kushindwa kwao hakuvumiliki hata zaidi kwa sheria ya Mbinguni? Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya. Ilhali Kristo hutoa ukweli tu; Yeye haji kuamua ikiwa mwanadamu atafanikiwa katika harakati yake ya kufuata ukweli. Hivyo, kinachofuata ni kuwa mafanikio au kushindwa kwa kweli yote yanategemea harakati ya mwanadamu. Mafanikio au kushindwa kwa mwanadamu kwa kweli kamwe hakuna uhusiano na Kristo, lakini kwa mbadala kunategemea harakati yake. Hatima ya mwanadamu na mafanikio yake ama kushindwa haiwezi kurundikwa kichwani pa Mungu, ili Mungu mwenyewe afanywe wa kuibeba, kwa sababu sio jambo la Mungu mwenyewe, lakini linahusiana moja kwa moja na wajibu ambao viumbe wa Mungu wanapaswa kutekeleza. Watu wengi wana maarifa madogo ya harakati na hatima za Paulo na Petro, lakini watu hawajui lolote ila matokeo ya Petro na Paulo, na hawajui kuhusu siri ya mafanikio ya Petro, au mapungufu yaliyosababisha kushindwa kwa Paulo. Na kwa hivyo, kama ninyi hamwezi kabisa kuelewa kiini cha harakati zao basi harakati ya wengi wenu bila shaka haitafaulu, na hata kama wachache wenu watafaulu, bado hawatakuwa sawa na Petro. Ikiwa njia unayopitia katika kutafuta ni ya kweli, basi una matumaini ya mafanikio. Kama njia unayopitia katika kufuatilia ukweli ni mbaya, basi wewe milele hutaweza kufanikiwa, na utakuwa na hatima sawa na Paulo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
341. Kama unamwamini Mungu, basi ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na kuhukumiwa, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu lakini usalie usiyeweza kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia—hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji, unaweza kushikilia msimamo wako, bali hili bado halitoshi; ni lazima bado uendelee kusonga mbele. Funzo la kumpenda Mungu halikomi kamwe na halina mwisho. Watu huona kumwamini Mungu kama jambo lililo rahisi mno, lakini mara tu wanapopata uzoefu kiasi wa vitendo, wao kisha hutambua kwamba imani katika Mungu si rahisi kama watu wanavyofikiria. Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka. Kadiri usafishaji wa mtu ulivyo mkubwa, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa mkubwa zaidi na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa zaidi kwake. Kinyume chake, kadiri mtu apokeavyo usafishaji mdogo zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa kwa kiwango kidogo zaidi, na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa kwake kwa kiwango kidogo zaidi. Kadiri usafishaji na uchungu wa mtu kama huyo ulivyo mkubwa na kadiri anavyopitia mateso mengi zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli zaidi, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakavyokuwa ya kina zaidi. Katika matukio unayopitia, utawaona watu wanaoteseka sana wanapokuwa wakisafishwa, wanaoshughulikiwa na kufundishwa nidhamu sana, na utaona kwamba ni watu hao ndio walio na upendo mkubwa kwa Mungu na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wao wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuzungumza kuhusu maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa ulioje! Kama Mungu hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi Yake haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Ilisemwa hapo awali kwamba Mungu angelichagua na kulipata kundi hili na kuwakamilisha katika siku za mwisho; hili lina umuhimu mkubwa sana. Kadiri kazi Anayofanya ndani yenu ilivyo kuu, ndivyo upendo wenu kwa Mungu ulivyo mkubwa na safi. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuelewa kitu kuhusu hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
342. Imani katika Mungu inahitaji utiifu Kwake na uzoefu wa kazi Yake. Mungu Amefanya kazi nyingi sana—inaweza semekana kuwa kwa watu yote ni kukamilishwa, yote ni usafishaji, na hata zaidi, yote ni kuadibu. Hakujakuwa na hatua hata moja ya kazi ya Mungu ambayo imelingana na dhana za binadamu; kile watu wamefurahia ni maneno makali ya Mungu. Mungu Atakapokuja, watu wanapaswa kufurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu. Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi. Kama kufuata kwako ni bora kabisa Mungu Anapokubariki, lakini unarudi nyuma bila baraka Zake, si huu ni utakaso? Kwa sababu una uhakika kuwa njia hii ni ya kweli, lazima uifuate hadi mwisho; lazima udumishe ibada yako kwa Mungu. Kwa sababu umeona kuwa Mungu Mwenyewe amekuja duniani kukukamilisha, lazima umpe moyo wako Kwake kabisa. Haijalishi ni nini Anafanya, hata kama Anaamua tokeo lisilofaa kwako mwishowe, bado unaweza kumfuata. Hii ni kudumisha usafi wako mbele za Mungu. Kupeana mwili wa kiroho mtakatifu na bikira safi kwa Mungu inamaanisha kuweka moyo mwaminifu mbele za Mungu. Kwa wanadamu, uaminifu ni usafi, na kuweza kuwa mwaminifu kwa Mungu ni kudumisha usafi. Hii ndiyo unafaa kuweka katika matendo. Unapopaswa kuomba, omba; unapopaswa kukusanyika pamoja katika ushirika, fanya hivyo; unapopaswa kuimba nyimbo za kidini, imba nyimbo za kidini; na unapopaswa kuunyima mwili, unyime mwili. Unapotekeleza wajibu wako hulimalizi kwa kubahatisha; unapokumbana na majaribu unasimama imara. Hii ni ibada kwa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu
343. Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Wale wote wanaogongwa na maneno Yangu makali na bado wanatulizwa nayo na wanaookolewa—hawajafanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Watu wamepokea vitu vingi sana kupitia imani. Kile ambacho wao hupokea sio baraka kila mara—kuhisi aina ya furaha na shangwe ambayo Daudi alihisi, au kuwa na maji yaliyotolewa na Yehova kama alivyofanya Musa. Kwa mfano, Ayubu alibarikiwa na Yehova kwa sababu ya imani yake, lakini pia alipitia maafa. Kama utapokea baraka au kupatwa na baa, yote ni matukio yaliyobarikiwa. Bila imani, hungeweza kupokea hii kazi ya kushinda, sembuse kuyaona matendo ya Yehova yanayoonyeshwa mbele ya macho yako leo. Hungeweza kuona, sembuse kuweza kupokea. Mabaa haya, maafa haya, na hukumu yote—kama haya hayangekufika, je, ungeweza kuona matendo ya Yehova leo? Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure, kwa sababu humtambui Mungu; haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako bado itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisi. Ni baada tu ya kupokea aina hii ya kazi ya kushinda inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona hatima ya viumbe wa Mungu; ni katika hukumu hii ndio unapata kuona kuwa Muumba anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya kushinda ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika kushinda huku unapata kutambua kwa ukamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika kushinda huku unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huku kushinda ndiko unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya kushinda ndiko unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika kushinda huku ndiko unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya upotovu wa mwanadamu; ni katika kushinda huku ndio unapokea furaha na starehe pamoja na kuadibu, nidhamu, na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa wanadamu ambao Aliwaumba; katika kazi hii ya kushinda, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea…. Je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)