416 Maombi ya Kweli

1 Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema. Hii ndiyo maana ya kuomba kwa kweli.

2 Baada ya kuomba kwa kweli, moyoni mwako utahisi kuwa na amani, na kufurahishwa; nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka, na utahisi kwamba hakuna kitu chochote katika maisha yako yote kinachostahili au ni muhimu zaidi kuliko kumpenda Mungu—na yote haya yatathibitisha kuwa maombi yako yamekuwa yenye ufanisi. Sala sio jambo la kupitia urasmi wa kisheria, au kufuata utaratibu, au kukariri maneno ya Mungu, ambalo ni kusema, sala haimaanishi kuiga maneno kama kasuku na kuwaiga wengine. Katika sala, lazima umpe Mungu moyo wako, ukishiriki maneno yaliyo ndani ya moyo wako na Mungu ili uweze kuguswa na Mungu.

3 Ikiwa maombi yako yatakuwa na matokeo, basi lazima yategemee usomaji wako wa maneno ya Mungu. Ni kwa kuomba tu katikati ya maneno ya Mungu ndipo utaweza kupokea nuru na mwangaza zaidi. Sala ya kweli huonyeshwa kwa kuwa na moyo ambao unatamani sana matakwa yaliyowekwa na Mungu, na kuwa tayari kutimiza matakwa haya; utaweza kuchukia yote ambayo Mungu huchukia, kwa msingi huo utakuwa na maarifa, na utajua na kuelewa wazi kuhusu ukweli ulioelezwa na Mungu. Kuwa na azimio, na imani, na maarifa, na njia ya kufanya mazoezi baada ya kuomba—huku tu ndiko kuomba kwa kweli, na sala kama hii tu ndiyo inaweza kuwa na ufanisi.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 415 Kufanikiwa au Kushindwa Kunategemea na Ufuatiliaji wa Mwanadamu

Inayofuata: 417 Mungu Humpa Mwanadamu Anachohitaji Kupitia Kilio Chake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp