527 Maana ya Kweli ya Maneno ya Mungu Haijawahi Kueleweka

1 Binadamu hawajui jinsi ya kufurahia baraka Nilizowaamulia kabla katika mikono Yangu, kwa sababu wao hawajui ni nini hasa maana ya baraka au mateso. Kwa sababu hii, wanadamu wako mbali na kweli katika jitihada zao za kunitafuta. Kama hakungekuwa na kesho, ni yupi kati yenu mliosimama mbele Yangu atakuwa safi kama theluji na asiye na lawama kama jiwe la thamani? Hakika upendo wako Kwangu si kitu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa mlo wenye ladha, au suti yenye ufahari, au ofisi ya juu na mishahara mikubwa? Au inaweza kubadilishwa na upendo ambao wengine wako nao kwako? Hakika, kupitia majaribu hakutawafukuza wanadamu waache upendo wao Kwangu? Hakika, mateso na dhiki hayatasababisha mwanadamu alalamike dhidi ya kile Nimepanga?

2 Hakuna mwanadamu aliyewahi kweli kufahamu upanga ulio katika kinywa Changu: Yeye anajua maana yake ya juu bila kufahamu undani wake. Kama wanadamu wangeweza kweli kuona ukali wa upanga Wangu, wangekimbia kwa hofu hadi ndani ya mashimo kama panya. Kwa sababu ya kutokuwa kwao na hisia, wanadamu hawaelewi kitu chochote cha maana halisi ya maneno Yangu, na hivyo wao hawana kidokezo kuhusu jinsi maneno Yangu ni yenye kuogofya, au kiasi gani asili yao imefichuliwa, na ni kiasi gani cha upotovu wao umepokea hukumu, ndani ya maneno hayo. Kwa sababu hii, kulingana na mawazo yao yasiyo kamili kuhusu maneno Yangu, watu wengi wamechukua msimamo vuguvugu na usio wa kuwajibika.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 15” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 526 Pamoja Na Ukweli Kuna Nguvu

Inayofuata: 528 Watu Hawatendi Kabisa Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp