113 Nitalithamini Neno La Mungu

1

Unanena ili kuniongoza mimi mbele, maisha yangu sasa yana mwangaza.

Kuadibu Kwako kuliniacha na hofu, lakini sikuelewa mapenzi Yako.

Maneno Yako makali yalifichua asili yangu, lakini nikashuku na nikakuumiza Wewe.

Mimi ni mjinga, kutojua kuwa neno Lako ni uzima.

Ninaweza kuja umbali huu, yote kwa sababu ya ukweli huu. Nitafanya bidii kuliweka neno Lako katika matendo.

Nikiacha neno Lako, tabia yangu haitabadilika kamwe.

Neno Lako la uzima, ukarimu Wako–ni motisha yangu.

Sasa ninaona kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima; Yeye ni wangu wa pekee.

2

Neno Lako linamtakasa mwanadamu na kumpa mwanadamu uzima—ni Wewe tu unayestahili sifa.

Uchungu, ugumu, ukandamizaji na kukamatwa, neno Lako linanisaidia katika haya yote.

Ingawa mwili wangu una maumivu, Unanichunga na kunilinda, na ninaupitia upendo Wako ambao wa ni kweli sana.

Ingawa njia iliyo mbele ni yenye mashimo na ya mateso, daima nitaishi kwa kufuata neno Lako.

Kwa kuelewa ukweli, tabia yangu inaanza kubadilika, yote kwa neema Yako.

Hukumu na majaribu ya neno Lako vinaniwezesha kupata ukweli na uzima.

Hukumu na kuadibu Kwako, majaribio na usafishaji Wako, vinanitakasa na kunibadilisha.

Sasa ninaona kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima; Yeye ni wangu wa pekee.

3

Wewe ndiwe ukweli, njia na uzima; neno Lako linashikilia vitu vyote.

Wewe ni Mwokozi na wanadamu wanahitaji maneno yote Unayoonyesha.

Leo naweza kutupilia mbali upotovu wangu na kuishi katika nuru, yote kwa sababu neno Lako limeniokoa.

Unakuwa mwili ambalo linaonyesha mapenzi Yako ya kina na yenye nguvu, neno Lako ni la thamani sana.

Haijalishi jaribio lilivyo kubwa au jinsi dhiki ilivyo kubwa, nitalikumbuka neno Lako vizuri.

Neno Lako ni ukweli na uzima, linafichua uweza na hekima Yako.

Upendo ndio kiini Chako, tabia Yako yenye haki, nami nitakusifu milele.

Sasa ninaona kuwa Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima; Yeye ni wangu wa pekee.

Iliyotangulia: 112 Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa

Inayofuata: 114 Sala ya Watu wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp