391 Kipaumbele cha Juu cha Imani Katika Mungu

1 Ikiwa unaweza kuelewa vizuri kila kitu ambacho Mungu hufanya, na unaweza kuyatazama mambo kupitia katika maneno Yake, ukisimama upande Wake, basi maoni yako yatakuwa yamekuwa yasiyo na makosa. Kwa hivyo, kuanzisha uhusiano mzuri na Mungu ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuliona kama kazi muhimu sana na tukio kubwa kabisa katika maisha yake. Kila kitu unachofanya kinapimwa na kama una uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida na nia zako ni zisizo na makosa, basi chukua hatua. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupata hasara kwa masilahi yako ya kibinafsi; huwezi kumruhusu Shetani atawale, huwezi kumruhusu Shetani akununue, na huwezi kumruhusu Shetani akufanye uwe kichekesho.

2 Kuwa na nia kama hiyo ni ishara kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida—si kwa ajili ya mwili, bali ni kwa ajili ya amani ya roho, kwa ajili ya kuipata kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali inayofaa, lazima uimarishe uhusiano mzuri na Mungu na urekebishe maoni ya imani yako katika Mungu. Hii ni ili Mungu aweze kukupata, na ili Aweze kudhihirisha matunda ya maneno Yake ndani yako na kukupa nuru na kukuangazia hata zaidi. Kwa njia hii, utakuwa umeingia katika njia inayofaa. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya leo, ingia katika njia ya sasa ya Roho Mtakatifu ya kufanya kazi, tenda kulingana na matakwa ya Mungu ya leo, usifuate mbinu za zamani za kutenda, usishikilie njia za zamani za kufanya mambo, na uingie katika njia ya leo ya kufanya kazi haraka iwezekanavyo. Hivyo, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utakuwa umeanza kutembea katika njia muwafaka ya imani katika Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 390 Kanuni za Matendo kwa Waumini

Inayofuata: 392 Watu Wanapaswa Kumwamini Mungu kwa Moyo Unaomwogopa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp