42 Muda Upotezwao Hautawahi Kuja Tena

1 Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya.

2 Ni wa kusikitisha jinsi gani! Jinsi gani walivyo duni! Jinsi gani walivyopofuka! Jinsi gani wanadamu walivyo wakatili! Kwa kweli mnalipuuza neno Langu—je, Ninazungumza nanyi bure? Bado ninyi ni wazembe sana, kwa nini? Kwa nini hivyo? Je, hamjawahi kufikiria kuhusu hilo kabla? Ninasema mambo haya kwa ajili ya nani? Niamini! Mimi ni Mwokozi wenu! Mimi ni Mwenyezi wako! Kesheni! Kesheni! Muda uliopotea hautakuja tena kamwe, kumbuka hili! Hakuna mahali popote duniani ambapo unaweza kununua dawa ambayo itapoza majuto! Kwa hiyo Nitawaambiaje hili? Je, neno Langu halistahili uzingatifu wenu wa makini na kutafakari kwa kurudia?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 30” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 41 Dunia Inaanguka, Ufalme Unapata Umbo

Inayofuata: 43 Vitu Vyote Viko Mikononi Mwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp