293 Walio Gizani Wanapaswa Kuinuka

I

Kwa maelfu ya miaka,

hii imekuwa nchi ya taka,

chafu sana, taabu imesheheni,

na pepo wakitangatanga kwa kila pembe.

Pepo huhadaa, hudanganya,

hufanya mashtaka yasiyo na msingi,

ni wakatilii, waovu,

wakiukanyaga mji huu wa mahame,

wakiuacha kama umechafuliwa na maiti.

Sasa ndio wakati: Watu kwa muda mrefu

wamekusanya nguvu zao zote,

wakatoa juhudi zao zote,

kuukwanyua uso wa kutisha wa pepo huyu.

Hili litawawezesha wale waliopofushwa

waliovumilia kila aina ya mateso, shida,

kuinuka kutoka kwa maumivu yao

na kumkwepa huyu ibilisi muovu mkongwe.

II

Uvundo wa uozo unaenea kote.

Nchi hii imelindwa sana.

Nani anayeweza kuona ulimwengu mbele ya mbingu?

Watu wa mahame haya wangewezaje kumwona Mungu?

Wamewahi kufurahia mapenzi ya Mungu, uzuri?

Wao hufurahia masuala ya ulimwengu?

Ni nani kati yao anayejua mapenzi ya Mungu yenye shauku?

Sasa ndio wakati: Watu kwa muda mrefu

wamekusanya nguvu zao zote,

wakatoa juhudi zao zote,

kuukwanyua uso wa kutisha wa pepo huyu.

Hili litawawezesha wale waliopofushwa

waliovumilia kila aina ya mateso, shida,

kuinuka kutoka kwa maumivu yao

na kumkwepa huyu ibilisi muovu mkongwe.

III

Mbona kuweka kazi ya Mungu mbele ya kizuizi kisichopenyeka?

Mbona kutumia hila mbalimbali za kuwadanganya watu wa Mungu?

Uhuru wa kweli uko wapi, haki za kisheria na maslahi?

Haki iko wapi?

Faraja na wema mwingi viko wapi?

Mbona kutumia mipango ya ujanja kuwahadaa watu wa Mungu?

Mbona kutumia nguvu kama hiyo kuukandamiza ujio wa Mungu?

Sasa ndio wakati: Watu kwa muda mrefu

wamekusanya nguvu zao zote,

wakatoa juhudi zao zote,

kuukwanyua uso wa kutisha wa pepo huyu.

Hili litawawezesha wale waliopofushwa

waliovumilia kila aina ya mateso, shida,

kuinuka kutoka kwa maumivu yao

na kumkwepa huyu ibilisi muovu mkongwe.

IV

Mbona kumfuatafuata Mungu mpaka Hana pa kupumzisha kichwa Chake?

Kufanya hivi kungekosaje kuchochea ghadhabu?

Maelfu ya miaka ya chuki yamejaa ndani ya moyo,

milenia nyingi za uhalifu zimeandikwa juu ya moyo.

Haya yote yangekosaje kuchochea chuki?

Lipizia Mungu kisasi, maliza adui Wake kabisa.

Sasa ndio wakati: Watu kwa muda mrefu

wamekusanya nguvu zao zote,

wakatoa juhudi zao zote,

kuukwanyua uso wa kutisha wa pepo huyu.

Hili litawawezesha wale waliopofushwa

waliovumilia kila aina ya mateso, shida,

kuinuka kutoka kwa maumivu yao

na kumkwepa huyu ibilisi muovu mkongwe.

Umetoholewa kutoka kwa "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 292 Nani Awezaye Kutunza Mapenzi ya Mungu?

Inayofuata: 294 Mapenzi ya Mungu kwa Wanadamu Hayatabadilika Kamwe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki