686 Ni Wale tu Wanaopata Wokovu wa Mungu Ndio Waishio

1 Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai, wala sio wafu, wamfanyie Yeye kazi. “Wafu” ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani.

2 Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 685 Shikilia Imara Kile Mwanadamu Lazima Afanye

Inayofuata: 687 Kushindwa ni Fursa Bora ya Kujijua

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp