Bwana Yesu Alimaanisha Nini Hasa Aliposema “Imekwisha” Msalabani?

23/04/2023

Waumini katika Bwana wanafikiri kwamba wakati Bwana Yesu aliposema “Imekwisha” msalabani, Alikuwa akisema kwamba kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika. Kwa hivyo kila mtu anahisi hakika kwamba Bwana atakaporudi, hatakuwa na kazi nyingine ya wokovu ya kufanya, lakini Atawainua tu waumini wote juu mbinguni ili kukutana na Bwana, atupeleke mbinguni, na hakutakuwa lingine. Hili ni jambo ambalo waumini katika Bwana wanaamini kabisa. Hiyo ndiyo maana watu wengi hutazama angani kila mara, wakingoja kwa uzembe Bwana awachukue moja kwa moja hadi katika ufalme Wake. Lakini sasa majanga makubwa yamefika na wengi hawajaona kuja kwa Bwana, kwa hiyo imani yao inafifia na wanahisi kuvunjika moyo. Wengine hata wana shaka: Je, ahadi ya Bwana ilikuwa ya kweli? Je, Anakuja, au la? Kwa hakika, Bwana Yesu alirudi kwa siri kama Mwana wa Adamu muda mrefu uliopita, akionyesha ukweli mwingi na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Lakini watu wengi hawajaribu kusikiliza sauti ya Mungu au kutafuta kusikia maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na muda wote wamekuwa wakichukulia kwamba Bwana anapaswa kuja juu ya wingu ili kuwachukua mbinguni, hivyo wanaikosa nafasi ya kumkaribisha Bwana. Hayo yatakuwa majuto ya maisha yote. Hili linaweza kuhusishwa kwa karibu sana na jinsi watu wanavyofasiri maneno ya Bwana Yesu msalabani: “Imekwisha.”

Hebu tuanze na hili. Kwa nini waumini wengi hufikiri kwamba Bwana Yesu akisema “Imekwisha” alimaanisha kwamba kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika? Je, kuna msingi wowote wa kibiblia wa jambo hili? Je, hili linathibitishwa na Roho Mtakatifu? Je, Bwana aliwahi kusema kwamba Hatafanya kazi yoyote zaidi ya kuwaokoa binadamu? Je, Roho Mtakatifu ameshuhudia kwamba maneno haya yalirejelea Mungu kukamilisha kazi Yake ya wokovu? Tunaweza kusema kwa uhakika: Hapana. Hivyo basi, kwa nini kila mtu anafafanua maneno haya kutoka kwa Bwana Yesu kuwa yanamaanisha kwamba kazi ya wokovu ya Mungu ilikamilika kabisa wakati huo? Huo ni upuuzi kiasi, sivyo? Kuelewa maneno ya Mungu si kazi rahisi. Inasema katika 2 Petro 1:20, “Mkilijua hili kwanza, ya kuwa hakuna utabiri wa maandiko ambao unafasiriwa na mtu yeyote binafsi.” Matokeo ya kufasiri Maandiko peke yako ni makubwa sana. Fikiria Mafarisayo—wao walifasiri unabii kuhusu Masihi wao wenyewe, na kwa sababu hiyo, Masihi alikuja, na waliona kwamba Bwana Yesu hakulingana na tafsiri zao. Kwa hivyo waliishutumu kazi Yake na hata kumfanya asulubishwe. Walikabiliwa na matokeo mabaya sana. Hii ilipelekea wao kuhukumiwa moja kwa moja na Bwana Yesu. Walilaaniwa!

Kwa hiyo Bwana Yesu aliposema “Imekwisha” pale msalabani, Alikuwa anazungumzia nini? Kuelewa hili kunahitaji kutafakari kwa uangalifu unabii wa kibiblia kuhusu kurudi kwa Bwana katika siku za mwisho, hasa mambo ambayo Bwana Yesu alisema mwenyewe kwamba Angefanya, na mifano Yake kuhusu ufalme wa mbinguni. Mambo haya yanahusishwa moja kwa moja na kazi Yake katika siku za mwisho. Tunahitaji kuwa na ufahamu wa kimsingi wa unabii huu na mifano hiyo ili tuelewe kwa usahihi kile ambacho Bwana Yesu alikuwa anazungumzia hasa Aliposema haya msalabani. Hata kama hatuelewi kikamilifu, huo si wito wa kuchukulia kwamba Alimaanisha kwamba kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika kabisa. Hii ni imani ya kiholela, ya upuuzi. Kwa hakika, tukizingatia kwa uzito unabii na mifano ya Bwana Yesu ya ufalme wa mbinguni, tunaweza kupata ufahamu wa kimsingi wa ufalme na kazi ya Bwana atakaporudi. Kisha hatutafasiri visivyo kauli Yake, “Imekwisha.” Bwana Yesu alitabiri: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana. … Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:22, 27). Na katika 1 Petro inasema: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Katika Ufunuo, tunaona: “Tazama, Simba wa kabila ya Yuda, Shina lake Daudi, ameweza kukifungua hicho kitabu, na kuzitoa muhiri saba zilizoko(Ufunuo 5:5). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo 2:7). Bwana Yesu pia alitumia mifano mingi kuelezea ufalme wa mbinguni, kama vile “Tena ufalme wa mbinguni ni kama wavu, uliotupwa baharini, na ukakusanya kila aina: Ambao, ulipojaa, waliuvuta ufukoni, na wakaketi chini, na kukusanya walio wazuri ndani ya vyombo, lakini wakawatupa walio wabaya. Basi ndivyo itakuwa mwishoni wa ulimwengu; malaika watajitokeza, na kutenga waovu kutoka miongoni mwa wenye haki. Na atawarusha ndani ya tanuu la moto: kutakuwa na kuomboleza na kusaga meno(Mathayo 13:47-50). Tunaweza kuona kutoka katika unabii huu na mifano hii kwamba Bwana Yesu alisema Angefanya kazi kubwa sana Atakaporudi. Lakini sehemu yake muhimu zaidi ni kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Hili litawaongoza watu kuingia katika ukweli wote na kisha kuwapanga wote kulingana na aina zao. Wale wanaoweza kukamilishwa watakamilishwa, na wale ambao lazima waondolewe wataondolewa. Hili litatimiza kabisa kila kitu ambacho Bwana Yesu alisema kuhusu ufalme. Tafakari kuhusu ngano na magugu, wavu wa kuvua samaki, wanawali wenye hekima na wapumbavu, kondoo na mbuzi, na watumishi wema na waovu. Kazi ya hukumu inayoanza na nyumba ya Mungu itatenganisha ngano na magugu, watumishi wema na waovu, wale wanaopenda ukweli na wale wanaotamani tu faraja. Wanawali wenye hekima watahudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo na kukamilishwa na Mungu. Na wanawali wapumbavu, je? Wataanguka katika maafa, wakilia na kusaga meno yao, kwa sababu hawakuisikiliza sauti ya Mungu. Hii ni kazi ya hukumu ya kuwapanga wote kulingana na aina zao, ikiwatuza wema na kuwaadhibu waovu, na hili litatimiza kikamilifu unabii huu katika Ufunuo: “Yule aliye dhalimu, basi aendelee kuwa dhalimu; na yeye aliye mtakatifu, na awe mtakatifu bado; na yeye aliye mwenye haki, awe mwenye haki bado: na yeye aliye mtakatifu, awe mtakatifu bado(Ufunuo 22:11). “Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa(Ufunuo 22:12). Tunapoelewa kwa kweli unabii wa Bwana Yesu, tunaweza kuona kwamba kuja kwa Bwana katika siku za mwisho ni hasa kwa ajili ya kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu, kumpanga kila mtu kulingana na aina yake na kuamua matokeo yake. Kwa hivyo tunaweza kudai kweli kwamba Bwana Yesu aliposema “Imekwisha” msalabani, Alikuwa akisema kwamba kazi ya Mungu ya kuwaokoa binadamu ilikuwa imekamilika? Je, tutaendelea kutazama angani kwa ujinga, tukimngojea Bwana Yesu ashuke juu ya wingu na kutuchukua juu angani ili tukutane na Yeye? Je, bado tutashutumu kwa urahisi ukweli wote wa Mungu unaoonyeshwa Anapofanya kazi katika siku za mwisho? Je, tutakataa kwa uhodari kwamba Bwana amerudi katika mwili kama Mwana wa Adamu kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho? Maafa makubwa tayari yamefika, na watu wengi wa kidini bado wamepotea katika ndoto yao ya kurudi kwa Bwana, wakifikiri kwamba Yeye hatawahi kuwatupa nje. Ni wakati wa kuamka. Wasipoamka, mara maafa yanapokwisha na Mwenyezi Mungu anaonekana waziwazi kwa watu wote, Mungu atakuwa ameifanya mbingu na dunia upya, na watu hao wote katika ulimwengu wa kidini watakuwa wakiomboleza na kusaga meno yao. Hilo litatimiza unabii huu katika Ufunuo: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7).

Wengi watauliza Bwana Yesu alimaanisha nini hasa aliposema “Imekwisha” pale msalabani. Kwa kweli ni rahisi sana. Maneno ya Bwana Yesu kila mara yalikuwa ya kimatendo sana, kwa hivyo Aliposema haya, kwa hakika Alikuwa anarejelea kazi Yake ya ukombozi. Lakini watu wanasisitiza kuyaelewa maneno haya ya vitendo kutoka kwa Bwana kuwa yanayohusu kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu, lakini hili ni jambo la kiholela kabisa, kwa sababu Mungu alikuwa ameikamilisha Yake ya kuwaokoa binadamu kwa kiasi tu. Bado kulikuwa na hatua muhimu zaidi—kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini usisitize kwamba “Imekwisha” ilimaanisha kwamba kazi yote ya Mungu ya wokovu ilikuwa imekamilika? Je, huo si upuuzi na upumbavu wa namna fulani? Kwa nini Bwana Yesu alisulubishwa? Alifanikisha kupitia hili hasa? Matokeo yalikuwa nini? Waumini wote wanajua hili, kwa sababu hili limeandikwa kwa uwazi sana katika Biblia. Bwana Yesu alikuja kuwakomboa binadamu. Kwa kusulubishwa, Bwana Yesu alitumika kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu, akichukua dhambi za kila mtu ili watu wasilazimike tena kuhukumiwa na kuuawa chini ya sheria. Hivyo watu wangeweza kusamehewa dhambi zao mradi tu wamwamini Bwana, na kuomba na kuungama Kwake, na wafurahie neema ya ajabu kutoka kwa Mungu. Huo ni wokovu kwa neema, na ndio ambao kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ilifanikisha. Ingawa dhambi zetu zilisamehewa kupitia imani yetu, hakuna anayeweza kukataa kwamba bado hatuwezi kujizuia kutenda dhambi kila wakati. Tunaishi katika mzunguko wa kutenda dhambi, kuungama, na kutenda dhambi tena. Hatujaepuka dhambi hata kidogo. Hili linamaanisha nini? Linamaanisha kwamba bado tuna asili ya dhambi, na tuna tabia za kishetani, kwa hiyo hatuwezi kurekebisha tatizo la kuendelea kutenda dhambi baada ya dhambi zetu kusamehewa. Hili linawaacha waumini wote wakiwa wamechanganyikiwa—ni jambo la kuumiza sana. Maneno ya Mungu yanasema, “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, kwa hiyo mtu yeyote ambaye ni mchafu hawezi kumwona. Hivyo inawezekanaje watu ambao daima wanatenda dhambi na kumpinga Mungu wastahili kuingia katika ufalme wa Mungu? Kwa kuwa watu hawajaepuka kabisa dhambi na kutakaswa, je, kazi ya Mungu ya kuwaokoa binadamu kweli inaweza kuwa imeisha? Wokovu wa Mungu utakuwa wokovu kamili—Hawezi kamwe kuiachia kazi Yake katikati. Hiyo ndiyo maana Bwana Yesu alitabiri kurudi Kwake mara nyingi. Amerejea katika siku za mwisho, muda mrefu uliopita, kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli ili kufanya kazi ya hukumu juu ya msingi wa kazi ya Bwana ya ukombozi. Hii ni ili kuwatakasa wanadamu kutoka katika tabia zetu potovu ili tuweze kufunguliwa kutoka katika minyororo ya dhambi. Ni kwa ajili ya kutuokoa kikamilifu kutoka kwa nguvu za Shetani na hatimaye kutuleta katika ufalme wa Mungu. Kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu itakamilika wakati tu kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho itakapokamilika.

Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Sababu ya kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu katika kiini ni ili kuwatakasa binadamu kwa ajili ya pumziko la mwisho; bila utakaso wa aina hii, hakuna binadamu yeyote angeainishwa katika makundi tofauti kulingana na aina yakeama kuingia katika pumziko. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. … Kusudi lote la kazi kuu ya Mungu ya kuadhibu maovu na kuthawabisha mema ni kuwatakasa kabisa wanadamu wote ili Aweze kuleta ubinadamu mtakatifu katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Maneno ya Mwenyezi Mungu ni dhahiri kabisa. Katika Enzi ya Neema, kazi Bwana Yesu ya ukombozi ilikuwa tu kusamehe dhambi za mwanadamu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ndiyo inayomtakasa na kumwokoa binadamu kikamilifu. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanahukumu na kufunua asili ya uasi ya mwanadamu, ya kumpinga Mungu, na yakituruhusu kujua tabia yetu potovu ya kishetani. Inatuonyesha kwamba tumejaa tabia za kishetani, kama vile kiburi, hila, na uovu bila mfano hata kidogo wa binadamu. Hii ndiyo njia pekee ya watu kuona ukweli wa jinsi walivyopotoshwa sana na Shetani, hivyo wanajichukia kwa kweli na kuwa na majuto ya kweli, kisha watubu kwa Mungu. Kisha wanaona jinsi ukweli ulivyo wa thamani na kuanza kuzingatia kuweka maneno ya Mungu katika vitendo na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Hii inawaruhusu waondoe tabia yao potovu hatua kwa hatua na kuanza kubadilika katika tabia ya maisha yao, na hatimaye kuweza kumtii na kumcha Mungu kwa kweli, na kuishi kwa kutegemea maneno Yake. Hivi ndivyo watu wanaweza kutupilia mbali kabisa nguvu za Shetani na kuokolewa kikamilifu na Mungu, kisha wanaweza kulindwa na Mungu na kunusurika majanga makubwa katika siku za mwisho, na kuingia katika hatima nzuri ambayo Mungu amemtayarishia binadamu. Hili linatimiza unabii katika Ufunuo 21:3–6. “Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kuu ikisema, Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita. Naye anayeketi katika kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya vitu vyote kuwa vipya. Na akaniambia, Andika: kwani maneno haya ni ya kweli na ya uaminifu. Na akaniambia, Imekwisha. Mimi ndiye Alfa na Omega, mwanzo na pia mwisho. Nitampa yeye aliye na kiu ya chechichemi ya maji ya uhai bila malipo.” Hapa, Mungu anasema “Imekwisha.” Hii ni tofauti kabisa na kile ambacho Bwana Yesu alisema msalabani: “Imekwisha.” Hii ni miktadha tofauti, maandhari tofauti. Bwana Yesu aliposema “Imekwisha” pale msalabani, Alikuwa akizungumza kuhusu kukamilisha kazi Yake ya ukombozi. Maneno “Imekwisha” katika Kitabu cha Ufunuo ni Mungu akizungumza kuhusu kukamilisha kazi Yake kikamilifu ili kuwaokoa binadamu, wakati tabenakulo ya Mungu iko na wanadamu, Ataishi miongoni mwao, na watakuwa watu wa ufalme Wake, ambapo hapatakuwa na machozi, kifo, au taabu tena. Hii ndiyo alama pekee ya Mungu kukamilisha kazi Yake ya wokovu.

Katika hatua hii, inapaswa kuwa dhahiri kwa kila mtu kwamba kudai kwamba maneno ya Bwana Yesu msalabani yalimaanisha kwamba kazi ya Mungu ya wokovu ilikuwa imeisha ni kinyume kabisa na uhalisi wa kazi ya Mungu na ni fikira ya binadamu tu. Ni tafsiri potovu ya maneno ya Bwana ambayo ni ya udanganyifu na ya kupotosha, na ni vigumu kujua ni watu wangapi ambao wamepotoshwa. Wale wanaong'ang'ania jambo hili bila kufikiri, wakingojea tu Bwana atokee ghafla juu ya wingu ili waweze kuinuliwa kuingia katika ufalme, wakati huo wote wakikataa kuchunguza ukweli mwingi ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu, watakosa kabisa nafasi yao ya kukutana na Bwana. Na bila shaka, hawatawahi kuepuka dhambi na kuokolewa kikamilifu. Kisha imani ya maisha yote itakuwa bure, na wataishia kuanguka katika majanga na kuondolewa na Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Hamjambo ndugu. Tumebahatika sana kukusanyika pamoja—mshukuruni Bwana! Sisi sote ni watu tunaopenda kusikiliza maneno ya Mungu na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp