Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

01/05/2023

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo, waumini wote wamekuwa wakitamani sana Mwokozi wetu ashuke juu ya wingu ili wanyakuliwe hadi Kwake. Waumini wanatumaini kunyakuliwa wakati wowote, lakini wanatazama majanga yakitokea mbele yao na bado hawajamkaribisha Bwana akirudi juu ya wingu. Wengi wanahisi kukata tamaa sana. Wanajiuliza kila mara ikiwa Bwana amerudi kweli na ikiwa kuna waumini ambao wamenyakuliwa kufikia sasa, lakini hakuna mtu ambaye ameona kitu cha aina hiyo. Wanachokiona ni majanga yanaongezeka kukua, magonjwa ya milipuko yanazidi kuwa makubwa, na watu wengi zaidi wanakufa katika maafa, hata baadhi ya wachungaji na wazee. Watu wanahisi hofu au labda hata wameachwa na Bwana, wakihisi kama wanaweza kufa katika majanga wakati wowote. Hawawezi kujua kwa nini Bwana hajarudi na kuwanyakua sasa kwa kuwa maafa yameanza. Inawashangaza kwamba Umeme wa Mashariki limekuwa likitoa ushahidi kwamba Bwana Yesu tayari amerudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, Akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Wengi wanaotamani ukweli husoma maneno ya Mwenyezi Mungu, huitambua sauti ya Mungu, na kumgeukia Mwenyezi Mungu. Wanakula na kunywa maneno ya Mwenyezi Mungu kila siku, wakidumishwa na kuruzukiwa nayo, na kuhudhuria karamu ya arusi ya Mwanakondoo. Ni wale ambao wamemkaribisha Bwana na kunyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kabla ya maafa. Watu wengi wa kidini wamechanganyikiwa, wakifikiri, “Umeme wa Mashariki lazima liwe limekosea kuhusu Bwana kuwa amerudi na kunyakuliwa kwao, kwa sababu Biblia inasema, ‘Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa: na hivyo tutakuwa naye Bwana daima’ (1 Wathesalonike 4:17). Ikiwa Bwana amerudi, kwa nini hatujachukuliwa kwenda juu? Je, Hapaswi kuwachukua watu mbinguni? Waumini wa Umeme wa Mashariki hakika bado wako duniani, kwa hivyo wangewezaje kunyakuliwa?” Haileweki kwao hata kidogo. Basi, kunyakuliwa kunamaanisha nini hasa? Watu wengi hawaelewi maana ya kweli ya unyakuo, lakini wanafikiri ina maana ya kuchukuliwa juu angani, hivyo mtu yeyote ambaye bado duniani hajanyakuliwa. Wamekosea sana.

Kutumaini Bwana arudi na kuwanyakua ni sahihi kabisa, kwani Bwana Yesu aliwaambia waumini wamkaribishe. Lakini Paulo alisema “tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa.” Je, hiyo ni sahihi? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema kwamba atakaporudi, Angechukua waumini kwenda kumlaki angani? Hakufanya hivyo. Je, kuna ushuhuda wa hili kutoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna. Je, Paulo angeweza kuzungumza kwa niaba ya Bwana Yesu kuhusu jambo hili? Je, Bwana alithibitisha jambo hilo? Hapana. Njia ambayo Bwana huwanyakua waumini imepangwa na Mungu. Bwana Yesu alisema, “Lakini kuhusu siku hiyo na saa hiyo hakuna mwanadamu aijuaye, hakuna, hata malaika ambao wako mbinguni, wala Mwana, bali Baba(Marko 13:32). Paulo alikuwa mwanadamu, mtume tu, kwa hivyo angewezaje kujua jinsi Bwana anavyowanyakua waumini? Kile ambacho Paulo alisema kiliegemezwa kabisa juu ya mawazo yake mwenyewe na hakikumwakilisha Bwana. Hakika hatuwezi kuweka msingi wa jinsi tunavyomkaribisha Bwana juu ya hili. Tunahitaji kufuata maneno ya Bwana Yesu kuhusu jinsi Anavyorudi na kuwanyakua waumini katika siku za mwisho, kwa sababu Yeye ni Kristo, Bwana wa ufalme, na maneno Yake pekee ndiyo ukweli na yenye mamlaka. Kumkaribisha Bwana kulingana na maneno Yake hakuwezi kuwa kosa. Hebu tuangalie kile ambacho Bwana Yesu alisema. Bwana Yesu alisema, “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu(Mathayo 24:44). “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo Mlango wa 2 na 3). Tunaweza kuona kwamba katika unabii Wake kuhusu kurudi Kwake, Bwana alitaja daima “Mwana wa Adamu,” “ujio wa Mwana wa Adamu,” “atakapokuja Mwana wa Adamu,” “akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango,” na “Kondoo wangu huisikia sauti yangu.” Maneno haya muhimu yanatuambia kwamba Bwana anarudi katika mwili kama Mwana wa Adamu, akija duniani kuzungumza, kubisha mlango wetu. Wale wanaoisikia sauti ya Bwana na kufungua mlango ni wanawali wenye busara wanaomkaribisha Bwana na kuhudhuria karamu Yake. Wananyakuliwa mbele za Bwana. Bwana Yesu hakuwahi kusema Angewachukua watu ili wakutane naye mbinguni, lakini Aliwaambia watu wasikilize sauti Yake ili waweze kumkaribisha, kuja mbele Zake, na kuhudhuria karamu Yake. Ili kumkaribisha Bwana na kukutana na Yeye, tunapaswa kufuata maneno Yake na kuisikia sauti ya Mungu. Mara tu tunaposikia mtu akiita kwamba Bwana harusi anakuja, ni lazima tutoke ili tumlaki, tusingojee kwa upumbavu kupelekwa angani kulingana na mawazo yetu wenyewe. Tukifanya hivyo, hatutaweza kamwe kuisikia sauti ya Bwana na kumkaribisha. Bwana anarudi kama Mwana wa Adamu na anakuja kati yetu, Akizungumza nasi, kwa hivyo ikiwa tunangojea tu kuchukuliwa angani, tuko kwenye njia tofauti na Bwana. Kwa hivyo, imani ya watu kwamba watanyakuliwa ili wakutane na Bwana angani haileti maana. Inakwenda kinyume kabisa na maneno ya Mungu mwenyewe na ni mawazo ya binadamu tu. Kwa hivyo kunyakuliwa ni nini hasa? Maneno ya Mwenyezi Mungu yanatufafanulia hili. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Kunyakuliwa’ si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanaweza kufikiria; hiyo ni fikira potovu sana. ‘Kunyakuliwa’ kunaashiria kujaaliwa Kwangu halafu kuchagua. Hii inawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale wote wataonyakuliwa ni watu waliopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, au wana, auwale ambao ni watu wa Mungu. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104). “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya). Hii linafanya iwe rahisi kuelewa, sivyo? “Kunyakuliwa” si kile tunachofikiri, si kuchukuliwa kutoka chini hadi mahali pa juu, kutoka duniani hadi mbinguni. Hiki si kitu yakini sana na kisicho cha kawaida. “Unyakuo” hutokea wakati ambapo Mungu anapata mwili kama Mwana wa Adamu duniani ili kuzungumza na kufanya kazi, tunasikia matamshi Yake, kutambua huu kama ukweli na sauti ya Mungu, kisha tunaweza kutii na kukubali kazi ya Mungu. Tunakula na kunywa maneno ya Mungu, sisi binafsi tunanyunyiziwa na kulelewa na Yeye, na tunapokea wokovu wa Mungu. Huku ni kunyakuliwa mbele za Mungu. Wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake ya ukombozi, wale wote waliotambua maneno Yake kama sauti ya Mungu, kisha wakamkubali na kumfuata, kama vile Petro, Yohana, na wanafunzi wengine, wote walinyakuliwa mbele za Mungu. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho na anaonyesha ukweli, Akifanya kazi ya hukumu. Watu kutoka madhehebu yote wanaopenda ukweli na kutamani kuonekana kwa Mungu wanapoona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na sauti ya Mungu, wamekubali kazi Yake ya hukumu. Wanakula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, wananyunyiziwa na kuruzukiwa nayo, na kupata hukumu na utakaso wa Mungu. Wao ni wanawali wenye busara walionyakuliwa mbele za Mungu, na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo, ambayo inatimiza kikamilifu unabii katika Ufunuo: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20).

Sasa nadhani sote tunaelewa maana ya kunyakuliwa. Kufikiria sasa kuhusu wazo la kukutana na Bwana angani, je, si hilo ni jambo lisilo la maana na la upumbavu? Bwana Yesu alitabiri mara nyingi “ujio wa Mwana wa Adamu,” akimwonya mwanadamu mara kwa mara aisikiliza sauti Yake. Kwa hivyo kwa nini watu wanasisitiza kufuata maneno ya mwanadamu ili kumkaribisha Yeye, badala ya maneno Yake Mwenyewe? Kwa nini wanashikilia usemi huo wa kipuuzi, “kunyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili kumlaki Bwana hewani”? Hili ni tatizo la aina gani? Je, haliashirii kuwa na hamu ya kubarikiwa sana? Je, si kwa sababu wanataka kuchukuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa Mungu mbali na majanga, ambako watapata baraka? Hebu tufikirie hili. Je, wale ambao wamesamehewa dhambi, lakini bado wanatenda dhambi daima wanaweza kunyakuliwa na kuingia katika ufalme Bwana atakapokuja? Je, wana haki ya kufurahia baraka Zake? Ni kweli kwamba Bwana alitukomboa kutoka dhambini, lakini hatuwezi kukataa kwamba bado tunatawaliwa na asili yetu ya dhambi, na hatuwezi kujizuia kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Hatujaepuka minyororo ya dhambi na kufikia utakaso. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Kwa hivyo, je, watu waliojaa uchafu na upotovu wanaweza kuingia katika ufalme Wake? Je, hiyo si njozi ya binadamu, matamanio tu? Mwenyezi Mungu anasema, “Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, ambayo ilikuwa tu kuwakomboa watu na kutusamehe dhambi, lakini asili yetu ya dhambi bado ipo. Tunaendelea kumwasi Mungu na hatujaokolewa kikamilifu. Kusamehewa dhambi zetu tu na Bwana Yesu haitoshi. Bado tunapaswa kumkaribisha Bwana na kunyakuliwa mbele Zake, kukubali hukumu Yake katika siku za mwisho, na kisha tunaweza kuwekwa huru kutoka dhambini na kuokolewa kikamilifu, tuwe watu wanaomtii na kumcha Mungu. Kisha tunaweza kuingia katika ufalme Wake. Mwenyezi Mungu anakuja katika siku za mwisho Akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Hii ni kwa ajili kutatua kikamilifu asili ya dhambi na tabia potovu ya mwanadamu, ili tuweze kuwekwa huru kutoka dhambini na nguvu za Shetani, na kuokolewa kikamilifu na Mungu. Mwenyezi Mungu ameonekana na kuonyesha ukweli mwingi sana, Akituambia kila kitu tunachohitaji kama wanadamu wapotovu ili tutakaswe na kuokolewa kikamilifu. Amefichua mafumbo ya mpango wa Mungu wa usimamizi, kama vile lengo la Mungu katika kuwasimamia wanadamu, jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi hatua tatu za kazi ya Mungu zinavyomwokoa mwanadamu kikamilifu, maana ya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, mafumbo ya kupata mwili na majina ya Mungu, kila aina ya matokeo na hatima ya mtu, na uzuri wa ufalme. Maneno haya yanafungua macho sana na yanashawishi kabisa. Mwenyezi Mungu pia anahukumu na kufunua kiini cha dhambi ya mwanadamu na upinzani dhidi ya Mungu, ambayo ni asili na tabia yetu ya kishetani. Pia Anafunua ukweli wa jinsi tulivyopotoshwa sana na Shetani, na Anatuonyesha njia ya kuepuka upotovu na kuokolewa kikamilifu. Watu wateule wa Mungu hula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu kila siku. Tunahukumiwa, kuadibiwa, kushughulikiwa na kupogolewa na maneno Yake, na kupitia kila aina ya majaribio, tunajifunza ukweli mwingi na kuja kujua asili yetu ya kishetani. Tunaona kwamba siku zote sisi huishi ndani ya upotovu, tukimwasi Mungu na kumchukiza, na kwamba tutaondolewa na kuadhibiwa na Mungu ikiwa hatutatubu na kubadilika. Tunapitia tabia ya Mungu yenye haki, isiyokubali kosa na kukuza uchaji Kwake. Upotovu wetu unatakaswa na kubadilishwa hatua kwa hatua, na hatimaye tunaweza kuepuka minyororo ya dhambi na kutoa ushahidi wa ajabu kwa Mungu. Mungu tayari amelikamilisha kundi la washindi kabla ya majanga, na majanga yanakuja. Wale wote wanaomkataa na kumpinga Mwenyezi Mungu, na wale walio wa Shetani wataangamizwa katika majanga. Wale wanaopitia hukumu ya Mungu na kutakaswa watapata ulinzi wa Mungu katika majanga, watachukuliwa katika ufalme Wake, na watakuwa na hatima nzuri. Huku ndiko kunyakuliwa kwa kweli na kuingia katika ufalme wa Mungu. Washindi hawa ambao wameokolewa kikamilifu na kukamilishwa na Mungu ni wale wanaotenda maneno ya Mungu na kufanya mapenzi Yake duniani. Hao ndio watu wa ufalme wa Mungu. Hivi ndivyo ufalme wa Kristo unavyotimizwa duniani, na hili linatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni(Mathayo 6:9-10). “Na mimi Yohana nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukija chini kutoka kwa Mungu mbinguni, uliotayarishwa kama mwanamwali aliyevikwa kwa ajili ya mume wake. Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kuu ikisema, Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita(Ufunuo 21:2-4). “Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele(Ufunuo 11:15). Kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yasemavyo, “Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani. Nguzo ya maisha mema kama haya ni lazima iwe hivyo, hivi kwamba baada ya mwanadamu kutakaswa na kushindwa, anajiwasilisha mbele za Muumba. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu kabla ya wanadamu kuingia katika hatima ya ajabu. Maisha kama haya ni maisha ya baadaye ya mwanadamu duniani, ni maisha yanayopendeza zaidi duniani, aina ya maisha ambayo mwanadamu ametamania, aina ambayo mwanadamu hajawahi kamwe kutimiza katika historia ya ulimwengu. Ni matukio ya mwisho ya miaka 6,000 ya kazi ya usimamizi, na ndicho wanadamu wanatamani sana, na pia ni ahadi ya Mungu kwa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu).

Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).

Katika hatua hii, tuna ufahamu kamili kuhusu maana halisi ya kunyakuliwa. Kunyakuliwa hasa ni kuhusu kuisikia sauti ya Mungu, kufuata nyayo Zake, na kumgeukia Mwenyezi Mungu, kuikubali kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Kwa nini ulimwengu wa kidini haujapitia unyakuo kabla ya majanga? Hasa ni kwa sababu hawatafuti ukweli au kuisikia sauti ya Mungu, lakini wanasisitiza juu ya mawazo yao na mistari halisi ya Biblia. Wanasikiliza tu maneno ya mwanadamu, lakini hawamkaribishi Bwana kulingana na maneno Yake. Ndio maana wameanguka kwenye majanga. Watu wanataka tu kumngoja Bwana aje juu ya wingu, na kutamani kubadilisha umbo mara moja na kupelekwa angani kukutana na Yeye, kwa hivyo wanangoja tu bila kujitayarisha au kutafuta kuisikia sauti ya Mungu. Mioyo yao imekufa ganzi. Je, wanawezaje kumkaribisha Bwana kwa njia hii? Wataanguka katika majanga, wakilia na kusaga meno. Mwenyezi Mungu amekuwa Akifanya kazi Yake ya hukumu kwa miongo mitatu sasa. Alikamilisha kundi la washindi kabla ya majanga, na sasa majanga yanakuja. Wale wanaoisikia sauti ya Mungu na kumkaribisha Bwana katika majanga bado wana nafasi ya kunyakuliwa. Huku ni kunyakuliwa katikati ya majanga, na wana matumaini ya kuwekwa. Wale wanaofuata mawazo yao, wakisisitiza kwamba Bwana anapaswa kuja juu ya wingu, wataanguka katika majanga na hawawezi kuokolewa. Mara tu majanga yatakapoisha, Mungu ataonekana waziwazi kwa mataifa yote na watu wote, akitimiza unabii wa Ufunuo 1:7, “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye.” Kuna vifungu kadhaa vya maneno ya Mwenyezi Mungu ambavyo tunaweza kutamatisha navyo. “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba ‘Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo’ watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp