Je, Kuwafuata Viongozi wa Dini Kunamfuata Mungu?

02/05/2023

Miaka 2,000 iliyopita, Mwokozi wetu Bwana Yesu alikuja kufanya kazi ya ukombozi na alishutumiwa vikali na wakuu wa makuhani, waandishi, na Mafarisayo wa imani ya Kiyahudi. Kwa sababu Wayahudi wengi waliwaabudu viongozi wao wa kidini, walikubaliana na wale wapinga Kristo katika kumshutumu na kumkataa Bwana Yesu, hatimaye wakachangia kumsulubisha. Hii ilikuwa dhambi kubwa na iliwaletea laana na adhabu ya Mungu, na kuliangamiza taifa la Israeli kwa miaka 2,000. Bwana Yesu amerudi katika siku za mwisho kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Pia anakabiliwa na shutuma na upinzani mkali wa viongozi wa kidini. Wanayafunga makanisa yao, wakiizuia njia ya waumini wanaoichunguza njia ya kweli, na kuwaacha watu wengi wakiogopa kuichunguza na kuikubali ingawa wameona wazi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, kwamba yana nguvu, mamlaka na kwamba yanatoka kwa Mungu. Matokeo yake, wengi wanapoteza nafasi yao ya kumkaribisha Bwana na wanaanguka katika maafa. Je, wamekosea wapi kuhusiana na kumkaribisha Bwana? Ni kwa sababu wanawasifu viongozi wao wa dini! Wanaamini kwamba viongozi wa kidini waliwekwa na Mungu na hutumiwa na Mungu, kwamba kuwatii ni kumtii Mungu, kwa hivyo wanawafuata na kukubaliana nao kabisa, wayakitii maneno yao kana kwamba yametoka kwa Mungu. Wengi pia hufikiri kwamba Bwana Yesu ana uhakika wa kuwaambia makasisi kwanza Atakaporudi, kwa hiyo kutosikia kutoka kwao kunathibitisha kwamba hajarudi. Kisha hawajaribu hata kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu, lakini wanawafuata viongozi wa kidini katika kumshutumu. Na kwa hivyo wanaanguka katika majanga, wakipoteza nafasi yao ya kunyakuliwa. Hili ni kosa la nani? Hakuna jibu rahisi. Mafarisayo ambao zamani walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu walilaaniwa na Mungu, na wengi katika ulimwengu wa kidini leo hawajajifunza funzo hilo chungu kutoka kwao. Kwa sababu wanawaabudu makasisi wao kwa upofu, wanakubaliana nao katika kumshutumu Bwana Yesu aliyerudi, wakimtundika Mungu msalabani tena. Hakika hili ni jambo baya sana! Hivyo basi, je, viongozi wa kidini kweli wameichukua nafasi ya Mungu? Je, kuwatii ni sawa na kumfuata Mungu? Kupata ufahamu kuhusu hili ni jambo la dharura.

Waumini wengi wanadhani viongozi wa dini, makasisi kama vile Papa, maaskofu, wachungaji na wazee, wameteuliwa na kutumiwa na Bwana Yesu na wana mamlaka ya kuwaongoza waumini, hivyo kuwatii ni kumtii Mungu. Msingi wa imani hii ni nini? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema kwamba viongozi wote wa kidini waliwekwa na Mungu? Hakuwahi kusema hivyo. Je, wana ushuhuda wa Roho Mtakatifu, au uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu? Hapana. Hii ina maana kwamba wazo hili ni wazo la kibinadamu tu. Hebu tutafakari juu yake. Kulingana na wazo hili la kibinadamu kwamba viongozi wa kidini wote wamewekwa na Mungu, basi je, hiyo inaweza kuwa kweli pia kuhusu makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo ambao walimpinga na kumhukumu Bwana Yesu? Je, kuwafuata katika kumsulubisha Bwana Yesu pia kulikuwa kumtii Mungu? Hii hakika ni njia ya kipuuzi ya kuwatendea makasisi! Tunaweza pia kuona kutoka katika Biblia kwamba katika kazi ya Mungu katika kila enzi, Yeye huteua watu wa kusaidia katika kazi Yake. Watu hao wote huitwa kibinafsi na kushuhudiwa na Mungu na maneno ya Mungu huonyesha hili. Huwa hawateuliwi kamwe na wanadamu wengine, na hawafunzwi na wanadamu. Fikiria Enzi ya Sheria, Mungu alipomtumia Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri. Maneno ya Yehova Mungu mwenyewe yalishuhudia hilo. Bwana Mungu alimwambia Musa, “Kwa hivyo basi, tazama, nimefikiwa na kilio chao wana wa Israeli: na mimi pia nimeona ukandamizaji ambao Wamisri wanatumia kuwakandamiza. Kwa hivyo njoo sasa, nami nitakutuma kwake Farao, ili uwalete watu wangu, wana wa Israeli, kutoka Misri(Kutoka 3:9-10). Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alimtumia Petro kuyachunga makanisa, na Alitoa ushahidi kwa Petro, pia. Bwana Yesu alimwambia Petro, “Simoni, mwana wa Yona, Unanipenda Mimi? … Walishe kondoo wangu(Yohana 21:17). “Na pia nakuambia, Kwamba wewe ni Petro, na nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba huu; na milango ya jahanamu haitashinda dhidi ya kanisa hilo. Na nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni: na chochote utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni: na chochote utakachoweka huru duniani kitawekwa huru mbinguni(Mathayo 16:18-19). Mungu binafsi huwateua na kuwa na ushuhuda kwa watu Anaowatumia katika kila enzi, na hili linathibitishwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika Enzi za Sheria na Neema, wakati mwingine wale ambao Mungu aliwatumia waliwekwa na kushuhudiwa na Yeye Mwenyewe. Wakati fulani Alitumia njia zingine. Bila uteuzi Wake wa moja kwa moja, Angefichua hili kupitia kwa manabii, au kulikuwa na uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hili halipingiki. Katika ulimwengu wa kisasa wa kidini, ni nani aliyempa Papa, maaskofu, mapadre, wachungaji na wazee nyadhifa wanazoshikilia? Je, kuna uthibitisho wa maneno ya Mungu au kazi ya Roho Mtakatifu? Je, Roho amewashuhudia? Hapana! Kwa hakika, viongozi hao wote wa kidini ndani ya makanisa wengi wao wamehitimu kutoka katika seminari na shule za theolojia na wana digrii za theolojia. Wakiwa na diploma mkononi, wao hupangiwa makanisa kuwaongoza waumini. Wengine wana vipawa na ufasaha, na hujifunza kazi zao vizuri, hivyo wao huteuliwa au kupendekezwa na uongozi wa juu na kupanda vyeo. Takribani makasisi wote wa ulimwengu wa kidini hupata nyadhifa zao kwa njia hii, lakini wengi wao hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Asilimia ndogo yao wanaweza kuwa na kazi kiasi ya Roho, lakini hawana ushuhuda Wake. Kwa hiyo tunaweza kuwa na uhakika kwamba wao si watu ambao Mungu huwashuhudia au kuwatumia. Wanakuzwa na kuchaguliwa kwa uwazi na watu wengine, kwa hivyo kwa nini wanasisitiza kwamba wameteuliwa na Mungu? Je, huko si kwenda kinyume na ukweli? Je, huko si kusema uwongo na kujitolea ushahidi wao wenyewe? Je, matokeo ya hili ni nini? Je, huko si kuwahadaa na kuwadhuru waumini? Baadhi ya viongozi wa dini hata hunukuu maneno ya Bwana Yesu akimwita Petro wakidai bila aibu kwamba mamlaka ambayo Bwana Yesu alimpa Petro yamekabidhiwa kwa Papa, hivyo Papa ameidhinishwa na Mungu na anaweza kumwakilisha Bwana Yesu, na kwa kuwa makasisi humfuata Papa, pia wao wameidhinishwa na Mungu, hivyo wanaweza kusamehe dhambi. Je, huo si ujinga? Je, Bwana Yesu aliwahi kumwambia Petro apitishe mamlaka aliyopewa kwa vizazi vya makasisi? Bwana Yesu hakuwahi kusema hivyo! Je, Petro aliwahi kueleza mambo kama hayo? La hasha! Hakuna kitu kama hicho kilichoandikwa katika Biblia. Pia ni ukweli kwamba hapakuwa na Papa, hakukuwa na makasisi wakati huo. Kwa hiyo viongozi hao wa kidini wanaotangaza kuwa wameidhinishwa na Mungu na wanaweza kumwakilisha Bwana Yesu wanajifanya kuwa Mungu na kuwapotosha watu, sivyo? Je, wale wanaowatii na kuwasujudia hawaabudu masanamu? Je, hiyo si kufanya kazi kinyume na Mungu? Watu wengi hawaelewi hili, na wanaendelea kuwaabudu viongozi wao bila kufikiri, wakifikiri kuwa wameteuliwa na Mungu. Je, unaweza kuona jinsi huu ni upumbavu na ujinga? Je, hii ina tofauti gani na wasioamini wanaoabudu masanamu? Ikiwa wewe ni mwumini lakini hufuati neno la Mungu, ikiwa unaabudu na kupiga magoti mbele ya wanadamu wengine ili kuungama dhambi zako kana kwamba wao ni Mungu, si unamvunjia heshima na kumkufuru Mungu? Je, wale wanaofanya hivi kwa ujinga wanaweza kuokolewa na Mungu? Huenda wasiweze. Wale wanaofanya hivyo kwa ujinga hawawezi kupata kibali cha Mungu.

Tunahitaji kuelewa vizuri kwamba Mungu kumteua mtu si jambo la kawaida au la kiholela. Lazima kuwe na ushahidi. Kulikuwa na uthibitisho wa Mungu kumteua Musa, na angalau Waisraeli walijua hilo. Uteuzi wa Bwana Yesu wa Petro pia ulikuwa halisi, ambao ulijulikana na mitume. Kwa hivyo, dai kwamba Mungu amemweka mtu mahali linahitaji msingi wa kweli. Hakuna binadamu anayeweza kudai hili kiholela. Tunaweza pia kuona kwamba mtu yeyote ambaye Mungu atamweka atakuwa na uongozi wa Roho Mtakatifu na uthibitisho kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kazi yake inaweza kutekeleza mapenzi ya Mungu na itapata matokeo dhahiri kabisa. Wanaweza kutekeleza agizo la Mungu. Hebu tuone kile ambacho Mungu Mwenyezi Anasema. “Kuhusu kiini cha kazi yake na usuli wa kutumiwa kwake, mwanadamu anayetumiwa na Mungu huinuliwa na Yeye, hutayarishwa na Mungu kwa kazi ya Mungu, na yeye hushirikiana katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Hakuna mtu anayeweza kufanya kazi yake badala yake—huu ni ushirikiano wa mwanadamu ambao ni wa lazima pamoja na kazi takatifu. Kazi inayotekelezwa na wafanyakazi wengine au mitume, wakati ule ule, ni uchukuzi na utekelezaji tu wa hali nyingi za matayarisho ya makanisa wakati wa kila kipindi, ama sivyo kazi ya utoaji wa kawaida wa uzima ili kudumisha uzima wa kanisa. Wafanyakazi hawa na mitume hawateuliwi na Mungu, seuze kuweza kuitwa wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Wao huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa na, baada ya kufunzwa na kukuzwa kwa kipindi cha wakati, wale wanaofaa hubaki, huku wale wasiofaa hurudishwa walikotoka. Kwa vile watu hawa huchaguliwa kutoka miongoni mwa makanisa, wengine huonyesha tabia yao halisi baada ya kuwa viongozi, na wengine hata hufanya mambo mengi mabaya na huishia kufutwa. Mtu anayetumiwa na Mungu, kwa upande mwingine, ni mtu ambaye ametayarishwa na Mungu, na aliye na ubora fulani wa tabia, na ana ubinadamu. Ametayarishwa na kukamilishwa mapema na Roho Mtakatifu, na anaongozwa kabisa na Roho Mtakatifu, na, inapofikia kazi yake hasa, yeye huongozwa na kuamriwa na Roho Mtakatifu—kutokana na hilo hakuna mkengeuko katika njia ya kuwaongoza wateule wa Mungu, kwani Mungu kwa hakika huwajibikia kazi Yake mwenyewe, na Mungu hufanya kazi Yake nyakati zote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Mungu Kumtumia Mwanadamu).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanatuonyesha kwamba Mungu huwatayarisha mapema sana wale Anaowateua na kuwatumia kwa kazi Yake, kwamba hao ndio Mungu huwainua ili wawaongoze watu Wake wateule. Kazi na mahubiri yao yanatokana kabisa na utoaji na mwongozo wa Roho Mtakatifu, na yeyote ambaye hajateuliwa na Mungu binafsi hawezi kamwe kuchukua nafasi yao. Musa katika Enzi ya Sheria na Petro katika Enzi ya Neema walifuata maneno na matakwa ya Mungu kwa uthabiti ili kuwaongoza watu Wake wateule, na Mungu alikuwa pamoja nao daima, akiwaongoza kila wakati. Mungu kamwe hatumii mtu mbaya au mtu anayefanya kazi kinyume na Yeye. Daima anawajibika kwa kazi Yake Mwenyewe. Wale ambao Mungu huwatumia daima hutiwa nuru na Roho Mtakatifu katika kazi na maneno yao na wanaweza kushiriki ufahamu safi wa maneno ya Mungu ili kuwasaidia watu wateule wa Mungu kuelewa matamko Yake, mapenzi Yake, na madai Yake. Wanaweza kutumia ukweli kila mara kuwasaidia watu wateule wa Mungu na mapambano yao ya vitendo na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu na njia sahihi katika imani yao. Wakati watu wateule wa Mungu wanakubali na kuutii uchungaji wa wale wanaotumiwa na Mungu wanaweza kupata riziki ya kweli kwa maisha yao, hatua kwa hatua waweze kupata ufahamu zaidi wa ukweli, kuijua kazi na tabia ya Mungu vyema zaidi, na kupanua imani na upendo wao kwa Mungu. Hiyo ndiyo maana wanaungwa mkono na watu wateule wa Mungu ambao wanajua mioyoni mwao kwamba watu hao wameteuliwa na Mungu na wanaufuata moyo wa Mungu. Tunapokubali na kuutii uongozi wao, huku ni kumfuata na kumtii Mungu na ni sawa na mapenzi ya Mungu. Wale ambao Mungu huwatumia huteuliwa ili wawaongoze watu Wake wateule kupata uzoefu wa kazi ya Mungu na kumfuata Yeye, na kazi na mahubiri yao yanatokana kabisa na uongozi na ufahamu wa Roho Mtakatifu. Kukubali na kuutii uongozi wao ni kumtii Mungu. Kuwapinga ni kumpinga Mungu, na kutasababisha kufunuliwa na kuondolewa na Mungu, au labda hata kulaaniwa na kuadhibiwa. Kama tu wakati ambapo Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri, kundi la Kora na Dathani waliopigana naye waliadhibiwa na Mungu. Huo ni ukweli ulio dhahiri.

Hebu tuwaangalie viongozi wa kidini wa leo, Papa, maaskofu na mapadre katika Ukatoliki, na wachungaji, wazee, na makasisi wengine katika Ukristo. Je, wamewekwa na Mungu? Je, Mungu amenena na kuwaunga mkono? Je, wana uthibitisho kutoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu? Je, wana uthibitisho kutokana na matunda ya kazi zao? Hawana lolote kati ya haya. Hilo linathibitisha kwamba walichaguliwa na wanadamu, hawakuteuliwa na Mungu. Kwa kuwa tumeona kwamba walilelewa ndani ya seminari na kuteuliwa na taasisi rasmi za kidini ambazo tunazijua kuwa angalifu sana. Wengi wao hawaamini katika ukweli au kuwa na imani ya kweli katika Mungu. Wanaamini katika theolojia, katika nafasi zao na cheo, katika riziki wanayopata kutokana na kazi hiyo. Haijalishi jinsi ujuzi wao wa Biblia ulivyo juu au jinsi mahubiri yao ni mazuri, hawana kazi na uongozi wa Roho Mtakatifu, au nuru ya Roho. Hii inatuonyesha kwamba wao ni wachungaji wa uongo, wasioamini na Mungu hawakubali. Kwa hivyo kuabudu na kuwafuata sio ujinga wa ajabu? Juu ya wao kukosa ushuhuda wa maneno ya Mungu na uthibitisho kutoka kwa Roho Mtakatifu, kuna sehemu moja muhimu ya ushahidi ambayo inaweza kutusaidia kuyaona kwa jinsi yalivyo. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana, akifichua wazi hali halisi za watu, ikiwa wanapenda ukweli au la, kama wanakiri ukweli au la, kama wanakubali ukweli au la, na kama wanachukia na kukataa ukweli. Yote yamefichuliwa. Wale wanaokubali kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ndiyo ukweli, kwamba Yeye ni Mungu katika mwili, ni wale wanaopenda ukweli na wana kibali cha Mungu. Hao ndio wanawali wenye busara wanaoisikia sauti ya Mungu na kunyakuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi. Ikiwa mtu anaona kwamba Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi lakini anaendelea kupinga, kushutumu, na kukana kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, hii ina maana kwamba wanaudharau ukweli, na wao ni wapinga Kristo wanaompinga na kumshutumu Mungu. Tayari wameanguka katika majanga na wataishia kuadhibiwa na Mungu. Sio tu viongozi wa Kikatoliki na Wakristo, lakini viongozi na watu kutoka katika madhehebu yote ambao wanafanya kazi dhidi ya Mwenyezi Mungu, bila ubaguzi. Ulimwengu wa kidini uko katika mfumbato wa genge hili la wapinga Kristo. Huu ni ukweli unaojulikana sana ambao hakuna anayeweza kuukataa. Kwa hivyo ikiwa tunajua kwamba maaskofu hawa, makasisi, wachungaji, na wazee ni sehemu ya genge la wapinga Kristo wanaopinga na kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu, je, tunapaswa kulichukuliaje hilo? Tunapaswa kuwakataa na kuwalaani, na tujikomboe kutoka katika shutuma zao kali. Huko ni kuwa wenye hekima. Tukiendelea kuwategemea kwa ajili ya njia ya kweli, tuendelee kuwatarajia watuambie lililo sahihi au lisilo sahihi, huo ni upumbavu wa ajabu, na ni upofu na ujinga! Kipofu anayewaongoza vipofu ataishia kwenye maangamizo. Hii inatimiza mistari ya Biblia: “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa hekima” (Mithali 10:21). “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6).

Ni wazi kabisa kwamba viongozi wa Kikatoliki na Wakristo, pamoja na viongozi kutoka madhehebu mengine yote, wanamshutumu Mwenyezi Mungu waziwazi. Ili kulinda hadhi na riziki yao, wanawaweka waumini kwa uthabiti ndani ya uwezo wao, wakichukua pesa zao, wakiwanyonya waumini kama vimelea, kama vile mapepo wakila maiti zao. Wapinga Kristo hawa hueneza kila aina ya uwongo mbaya ili kudumisha nafasi na riziki zao, wakisema habari zozote za kuja kwa Bwana ni za uwongo, kwamba Bwana Yesu lazima aje juu ya wingu, kwamba kukubali kupata mwili kwa pili kwa Bwana ni kumkubali Kristo wa uwongo. Wanasema uwongo ili kuwapotosha watu, wakifanya kila wawezalo kuwazuia waumini wasiichunguze njia ya kweli. Hata wanajipatanisha na CCP ili kuwakamata na kuwatesa wale wanaoshiriki injili ya ufalme. Je, viongozi hawa wa kidini wana tofauti gani na Mafarisayo waliompinga Bwana Yesu katika siku Zake? Je, si wote ni watu wanaomsulubisha Mungu? Je, si wote ni wachungaji wa uongo na wapinga Kristo wanaowapotosha watu na kuwaharibu? Tafakari maneno ya Bwana Yesu akiwashutumu Mafarisayo: “Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie(Mathayo 23:13). “Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko(Mathayo 23:15). Tunaweza kuona kwamba viongozi wengi wa kidini leo si tofauti na Mafarisayo ambao walimpinga Bwana Yesu kwa kichaa na kuizuia njia ya waumini. Wote wanamchukia Mungu na kumpinga Yeye, na wao ni pepo wapinga Kristo wa siku za mwisho.

Hapa kuna vifungu zaidi vya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, ‘Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.’ Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?(Neno, Vol. 3. Mihadhara ya Kristo wa Siku za Mwisho. Sehemu ya Tatu).

Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye ‘mwili imara,’ wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu).

Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi ‘hazina’ anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni ‘mashujaa wasioshindwa,’ kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao ‘mtakatifu na usiokiukwa’. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa ‘wafalme’ katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu).

Sasa nina uhakika sote tunaelewa vizuri kwamba viongozi wengi wa kidini ni wapinga Kristo wanaochukia ukweli, wanaomchukia Mungu, watumishi waovu na wachungaji wa uwongo wanaopotosha watu. Kuwasikiliza na kunyenyekea kwao sio kumtii Mungu, na sio kumfuata Mungu. Ni kumfuata Shetani na kumpinga Mungu, kuwa mshiriki wa Shetani, mtu ambaye Mungu anamchukia na kumlaani. Kwa hivyo kama waumini, tunapaswa kufahamu kwamba tunapaswa kumtukuza Mungu, kumcha, kunyenyekea kwake na ukweli. Hatuwezi kamwe kuabudu au kufuata wanadamu. Kama Bwana Yesu alivyosema, “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni Yeye peke Yake ndiye utakayemtumikia(Mathayo 4:10). Ikiwa kiongozi wa kidini ni mtu anayependa ukweli, ikiwa maneno yake yanapatana na ya Bwana na yanatuongoza kumcha Mungu na kuepuka maovu, basi kufuata na kuyatii maneno hayo yanayopatana na ukweli ni kumtii Mungu. Ikiwa maneno yake hayapatani na ukweli, ikiwa yanakwenda kinyume na maneno ya Bwana, tunapaswa kuyakataa. Tukiendelea kumfuata, huko ni kumfuata mtu, kumfuata Shetani. Ikiwa kiongozi wa kidini ataukataa na kuudharau ukweli, na kuwazuia wengine wasiichunguze njia ya kweli, yeye ni mpinga Kristo na tunapaswa kusimama upande wa Mungu, tukimfunua na kumkataa, na kuthubutu kusema “Hapana,” kuepuka udhibiti wake, kuitafuta na kuikubali njia ya kweli, na kuenda sambamba na nyayo za Mungu. Hiyo ndiyo imani ya kweli, kumfuata Mungu kikweli, na kunalingana na mapenzi Yake. Kama vile Petro alivyosema alipokamatwa na makuhani wakuu na Mafarisayo: “Tunapaswa kumtii Mungu badala ya wanadamu” (Matendo 5:29).

Hebu tusome kifungu kingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. … ‘Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu’ kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake).

Sasa nina hakika tunaelewa vizuri zaidi kwamba kuwa na imani na kumfuata Mungu ni kuhusu kutii na kukubali ukweli, kuikubali kazi ya sasa ya Mungu na maneno, na kwenda sambamba na nyayo Zake. Haijalishi jinsi kazi ya Mungu iko mbali na fikira za watu au ni watu wangapi wanaipinga na kuishutumu, mradi tu ni ukweli na ni kazi ya Mungu, tunapaswa kuikubali na kuitii. Huko tu ndiko kuwa na imani na kumfuata Mungu. Kama inavyosema katika Ufunuo: “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo(Ufunuo 14:4). Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu yuko hapa akifanya kazi na ameonyesha ukweli mwingi. Anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, Akituokoa na uovu na nguvu za Shetani. Hii ni fursa isiyostahili kutupita na ndiyo njia yetu pekee ya kuokolewa na kuingia katika ufalme wa Mungu. Sasa watu zaidi na zaidi duniani kote wanaotamani kuonekana kwa Mungu wamekuwa wakitafuta kazi ya Mwenyezi Mungu mtandaoni. Wameona kwamba maneno Yake yote ni ukweli, kwamba ni sauti ya Mungu. Wanajinasua kutoka katika minyororo ya viongozi wa kidini, wakitoka katika udhibiti wa makanisa yao na kuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ili kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwana kondoo. Lakini bado kuna wengi katika ulimwengu wa kidini wanaofuata na kuwaabudu makasisi bila kufikiri, ambao wamebanwa na kuchukuliwa na nguvu za wapinga Kristo. Wamedhibitiwa kwa nguvu ndani ya nyika, wakingojea bila mafanikio Bwana aje juu ya wingu, waliokataliwa zamani na kuondolewa na Mungu, wakilia na kusaga meno katika maafa. Huu ndio utimilifu wa maneno ya Bwana Yesu “Na kipofu akimwelekeza kipofu, wote wawili wataanguka ndani ya shimo(Mathayo 15:14). Wanadai kumwamini Mungu, lakini kwa hakika, wanaenda kinyume na Mungu na kuwafuata watu. Mungu anawaona kuwa ni wasioamini. Mungu ni Mungu mtakatifu anayechukia maovu na haki Yake haiwezi kukiukwa. Hangeweza kamwe kuwaokoa wale wanaowaabudu wanadamu, wanaofuata wapinga Kristo katika kumpinga na kumkufuru Mungu. Mungu hawezi kamwe kumwokoa mtu yeyote ambaye hapendi au kuukubali ukweli, lakini anaing'ang'ania Biblia bila kufikiri. Mapenzi ya Mungu ni kuwaweka watu huru kutoka kwa Babeli ya kidini, ili tusizuiliwe tena na vizuizi vya ulimwengu wa kidini vya wapinga Kristo, na tuweze kutoka katika dini kutafuta ukweli na kuitafuta kazi ya Mungu ili tuwe na matumaini ya kukaribisha kuonekana kwa Mungu na kazi Yake.

Hebu tuangalie maneno zaidi ya Mwenyezi Mungu. “Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupata Mwili Ni Nini?

Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp