Kwa Nini Mungu Anakuja Katika Mwili Katika Siku za Mwisho, Si Katika Roho?
Tangu Mwenyezi Mungu, Mwokozi, aonyeshe ukweli kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, watu wengi wametafuta na kuichunguza njia ya kweli, na kisha wakakaribisha kurudi kwa Mwokozi. Wameona jinsi maneno ya Mwenyezi Mungu yalivyo na mamlaka na nguvu ya ajabu, kwamba maneno hayo ni ukweli, na kuthibitisha hii ni sauti ya Roho Mtakatifu, kwamba hakuna mtu wa kawaida anayeweza kutamka maneno haya. Kwa kusikia sauti ya Mungu, wamemkubali Mwenyezi Mungu, wameinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Watu wateule wa Mungu hula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu kila siku, ambayo huchangamsha mioyo yao zaidi na zaidi. Hawafurahii tu uwepo wa Mungu, bali pia wanapata nuru ya maneno Yake, wakijifunza ukweli mwingi sana na kuelewa mambo mengi sana. Pia wanajifunza mafumbo mengi sana ya Biblia, ambayo ni furaha kubwa sana. Wamebubujika imani na upendo wao kwa Mungu umeimarishwa. Watu wengi wateule wa Mungu hawana woga wanapokumbwa na ukandamizaji, kukamatwa, na mateso ya Chama cha Kikomunisti cha China. Wanaziacha familia zao na mahusiano ya kidunia, wakiwa na wajibu wa kushiriki injili katika ushuhuda kwa Mungu. Wanateseka kwa sababu ya kukamatwa na kuteswa kikatili na CCP, lakini wanaendelea kumfuata Mungu kwa ujasiri, bila woga na kutoa ushuhuda Kwake. Hawajashindwa, na hakika hawajaangamizwa. Wametoa ushahidi mkubwa sana kwa Mungu. Injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu sasa imeenea katika kila nchi duniani, na Kanisa la Mwenyezi Mungu limeanzishwa katika nchi nyingi kati ya hizo. Watu zaidi na zaidi wameisikia sauti ya Mungu na wanamgeukia Mwenyezi Mungu. Idadi ya wale wanaoichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu mtandaoni inaongezeka. Hili linatimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27). Kama tu yanavyosema maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye ‘Mlima wa Mizeituni’ wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni).
Matamko ya Mwenyezi Mungu, kama nuru kuu, tayari yameenea kutoka Mashariki hadi Magharibi. Watu wateule wa Mungu kutoka kila nchi huhubiri injili, kutoa ushahidi Kwake, na kumsifu Mungu kwa furaha kwa kumshinda Shetani na kupata utukufu wote tayari. Mwokozi Mwenyezi Mungu alionekana na kuanza kufanya kazi kabla ya majanga, na Amelifanya kundi la washindi. Injili Yake ya ufalme imeenea katika kila taifa, na majanga yakafuata ipasavyo. Tunaweza kuona kwamba kazi ya hukumu inayoanza na nyumba ya Mungu tayari ilikuwa na mafanikio makubwa, na baada ya hapo, Mungu amekuwa akitumia majanga ya kila aina kuuhukumu na kuuadibu ulimwengu huu. Maafa haya yanasaidia kupanua injili ya ufalme, kuwaokoa watu zaidi kutoka dhambini na kutoka katika nguvu za Shetani. Kipengele kingine cha jambo hili ni kwamba Mungu hutumia majanga kuadibu na kukomesha enzi hii ya giza na uovu, ili kufuta nguvu zote za uovu zinazompinga Mungu. Haya ndiyo matunda ambayo kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho itazaa. Mwenyezi Mungu, Mwokozi, ameonyesha ukweli mwingi sana, Amefanya kazi kubwa, na Ameutikisa ulimwengu. Lakini wengi katika ulimwengu wa kidini bado wamepotoshwa na joka kuu jekundu, CCP, na bado wamefungwa na nguvu za wapinga Kristo ndani ya dini. Wanashikilia wazo kwamba Bwana anapasa kushuka juu ya wingu katika umbo la roho, kwamba haiwezekani arudi katika mwili kama Mwana wa Adamu. Hiyo ndiyo maana wana hakika kwamba yeyote asiyekuja juu ya wingu ni wa uongo, kwamba ushuhuda wowote kwamba Yeye ni Mwana wa Adamu ni wa uongo, kwamba ni imani tu katika mwanadamu. Mbali na wao kushindwa kutafuta na kuchunguza maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, au kutafuta na kusikiliza sauti ya Mungu, wao pia wanawafuata wapinga Kristo wa kidini, wakihukumu bila kukoma, wakishutumu, na kukufuru kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo maana bado hawajamkaribisha Bwana, bali wameanguka katika maafa, wakilia na kusaga meno yao, na hakuna anayejua kama ataishi au kufa. Wengi wana swali. Bwana Yesu alionekana katika umbo la roho kwa siku arubaini baada ya kufufuka Kwake, kwa hiyo anapasa kurudi katika umbo la roho. Kwa nini Mwenyezi Mungu asingeonekana kama Roho, lakini kama Mwana wa Adamu mwenye mwili? Watu wengi sana huuliza swali hili, na wengi hawatamkubali Mwenyezi Mungu kwa sababu yuko katika mwili, na wala si roho. Jambo la kusikitisha lililoje! Wanakosa nafasi yao ya pekee ya wokovu, jambo ambalo watajutia milele. Linalofuatia, Nitashiriki ushirika kiasi ili kushughulikia swali la kwa nini Mungu anaonekana katika mwili, na wala si roho katika siku za mwisho.
Kwanza, kuhusu jinsi Bwana anavyoonekana na kufanya kazi katika siku za mwisho, tunaweza kuthibitisha kwamba Bwana Yesu anarudi ulimwenguni katika mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho kufanya kazi Yake. Hili linatokana na unabii mwingi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe, si jambo lililoamuliwa na mwanadamu. Bwana hakika kurudi katika roho au katika umbo la mwili kama Mwana wa Adamu ni jambo lililoamuliwa kabla na Mungu zamani, na hakuna chaguo la mwanadamu katika hili. Kama wanadamu, tunachoweza kufanya ni kutii, sio kuwekea vitu mipaka kulingana na dhana na mawazo yetu wenyewe. Kwa kweli, hata kama namna ya kuonekana kwa Mungu iliyoamuliwa kabla hailingani na mawazo ya wanadamu, hiyo ndiyo bora zaidi, na yenye maana zaidi na yenye manufaa kwa wokovu ajili ya wetu. Haiwezi kuwa na makosa. Hatuwezi kuichukulia kulingana na kile tunachoweza kukuwa tukiwaza. Ni lazima tuwe mabikira wenye busara, si wale wapumbavu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kukaribisha kuonekana kwa Bwana. Watu wanaweza kusisitiza kufuata mipaka waliyojiwekea wenyewe, wakikataa kukubali chochote isipokuwa Bwana kushuka juu ya wingu, wakimkataa Mwana wa Adamu mwenye mwili. Matokeo ya mtazamo huu ni yapi? Hakika wataanguka katika misiba na kuadhibiwa, wakikaribisha maangamizo yao wenyewe. Iwapo sisi ni mabikira wenye busara, tunapaswa kufanya kama vile Bwana anavyohitaji, tutafute na kusikiliza sauti ya Mungu ili kumkaribisha Bwana, tukikubali kwa furaha na kumtii Yeye bila kujali umbo Analochukua, si kujaribu kujichagulia. La sivyo, tutakuwa mabikira wapumbavu, tukianguka katika maafa, kulia na kusaga meno. Kwa hiyo ni nini hasa kinachotukia katika siku za mwisho? Je, Mungu anarudi katika umbo la roho, au kama Mwana wa Adamu? Kwanza, hebu tuzungumze kuhusu kama ni rahisi kuingiliana na Roho wa Mungu, au na Mwana wa Adamu. Je, ni rahisi Kwake kunena nasi kwa njia ya Roho, au kupitia mwili? Watu wengi wangejibu kwamba ni rahisi zaidi kwa Mwana wa Adamu, kwa maswali yote mawili. Hiyo ni sahihi. Hiyo ndiyo maana Mungu alikuwa mwili Alipoonekana na kufanya kazi katika Enzi ya Neema. Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Adamu. Aliishi miongoni mwa wanadamu, akila, akinywa, na kuishi pamoja nasi. Watu wengi walimfuata Bwana, wakifanya ushirika naye, wakizungumza, na kuingiliana naye. Ilikuwa ni huru na rahisi kabisa, bila vizuizi au vikwazo. Wote walishuhudia uzuri wa Bwana Yesu. Watu waliweza kujifunza ukweli mwingi baada ya kunyunyiziwa, kuruzukiwa na kutegemezwa. Baada ya Bwana kuonyesha ukweli mwingi, Alisulubishwa msalabani, akawa sadaka ya dhambi ya wanadamu. Mtu yeyote awaye angeweza kusamehewa dhambi zake kwa kumkubali tu Bwana Yesu kama Mwokozi wake, kuungama na kutubu Kwake. Kisha angeweza kufurahia amani na furaha ya kusamehewa dhambi zake, na neema iliyotolewa na Mungu. Baada ya Bwana kusulubiwa, kufufuka, na kisha kupaa mbinguni, watu zaidi na zaidi walianza kushiriki injili Yake, wakimtolea Yesu Kristo ushuhuda kama Mwokozi, kama kuonekana kwa Mungu. Injili ya Bwana Yesu zamani zile ilifika katika kila nchi ulimwenguni. Hilo linathibitisha kwamba Mungu kufanyika mwili kama Mwana wa Adamu ili kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu kuna matokeo bora zaidi. Watu hawawezi kumwona au kumgusa Roho wa Mungu—hawawezi kuingiliana na Yeye kwa namna hiyo. Hatuwezi kuwasiliana na Roho wa Mungu. Roho wa Mungu anapozungumza, kila mtu hutetemeka kwa hofu. Tungewezaje kuwasiliana kwa njia hiyo? Zaidi ya hayo, haingewezekana Roho wa Mungu asulubiwe. Je, kitu ambacho watu hawawezi kukiona au kukigusa kingewezaje kusulubiwa, sivyo? Hili linatuonyesha kwamba ni bora kwa Mungu kufanya kazi kama Mwana wa Adamu. Mungu alitukuzwa Bwana Yesu alipomaliza kazi Yake ya kuwakomboa wanadamu. Hili liko dhahiri kwa kila mtu kuliona. Tunaweza kuwa na uhakika kutokana na ukweli wa kazi ya Bwana Yesu, kwamba katika kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, iwe ni kazi Yake ya ukombozi au kazi ya hukumu ya siku za mwisho, kupata mwili kama Mwana wa Adamu ndiko kunakofaa zaidi. Hilo lina matokeo bora zaidi. Pia, Mungu kupata mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho kunatimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “uji0 wa Mwana wa Adamu,” “atakapokuja mwana wa Adamu,” na “Mwana wa Adamu atakuwa katika siku Yake.” Wale wanaoijua Biblia vizuri wanaweza kuona kwamba maneno ya Bwana yametimia. Basi kwa nini watu wengi hushikilia dhana zinazomzunguka Mwana wa Adamu kuonekana na kufanya kazi? Kwa nini watu wengi bado wanasisitiza kwamba Bwana atashuka juu ya wingu katika umbo la roho? Huu kweli ni upumbavu na ujinga. Mungu anaonekana na kufanya kazi kama Mwana wa Adamu, mnyenyekevu na aliyefichika, si tu kwa sababu njia hii ni yenye ufanisi zaidi, lakini pia ili tuweze kuiona tabia ya Mungu, na jinsi unyenyekevu na kufichika Kwake kulivyo. Mungu anakutana na mwanadamu moja kwa moja kama Mwana wa Adamu, yuko ana kwa ana nasi, akila, akinywa, na kuishi pamoja nasi, akionyesha ukweli ili kutunyunyizia, kutuchunga, na kutuokoa. Huu ni upendo mkuu wa Mungu! Kwa nini watu wasiweze kuona hili? Kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yanavyosema: “Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mtu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mtu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. … Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Ni kwa namna hii tu ndipo Ataweza kuwapa wanadamu njia ya vitendo wanayohitaji kama viumbe. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki ni mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa njia zote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Kazi ambayo ina thamani kubwa kwa mwanadamu aliyepotoka ambayo inatoa maneno sahihi, malengo wazi ya kufuata, na ambayo inaweza kuonekana na kuguswa. Ni kazi yenye kuwezekana tu, na uongozi wa wakati ndio unaofaa kwa ladha ya mwanadamu, na kazi halisi ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika tabia yake iliyopotoka na kusawijika. Hii inaweza kufanywa na Mungu mwenye mwili tu; ni Mungu mwenye mwili peke yake ndiye Anayeweza kumwokoa mwanadamu kutoka katika hali yake ya zamani ya kupotoka” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).
Maneno ya Mwenyezi Mungu yako wazi kabisa. Ni kwa kufanyika mwili kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho pekee ndipo Mungu anaweza kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na kutuongoza hadi kwenye hatima nzuri. Tumemshuhudia Mwenyezi Mungu binafsi miongoni mwetu, akiishi pamoja nasi, daima akipatikana kushiriki ukweli na kutatua matatizo ya vitendo. Anaona upotovu wa binadamu, akiandika maneno Yake na kutupa ukweli. Tunafurahia maneno ya Mungu kwa kweli na roho zetu zinawekwa huru. Mungu anaposhiriki ukweli nasi, tunaweza kumuuliza maswali, na Yeye hujibu kwa subira. Mwenyezi Mungu anaishi miongoni mwa binadamu, akizungumza na kufanya ushirika nasi. Kila neno letu, kila ishara yetu, na hata kila wazo letu ni wazi kabisa kwa Mungu, mbele ya macho Yake. Anaweza kuonyesha ukweli wakati wowote au mahali popote, akidhihirisha tabia zetu za kishetani na dhana na mawazo yetu juu Yake, akirekebisha makosa yaliyo katika imani yetu na mitazamo yetu potovu kuhusu ufuatiliaji. Hivi ndivyo Mungu katika mwili anavyotunyunyizia maji na kutuchunga, akitufundisha na kutusaidia, ana kwa ana. Ni tukio la ajabu, la kuchangamsha moyo kwetu. Mungu ni mwenye kupendeza sana na mwenye kufikiwa. Tunaona vipengele vingi vya kupendeza vya Mungu na kumpenda kwa dhati. Kristo huonyesha ukweli mwingi na anafanya kazi kubwa sana, lakini Yeye ni mnyenyekevu sana na amejificha, kamwe hajionyeshi wala kujipendekeza Mwenyewe kama Mungu. Yeye ni mtu wa kawaida sana na mchangamfu katika mwingiliano Wake nasi, kamwe halazimishi mtu yeyote kumsikiliza. Kristo hana hata chembe ya majivuno au maringo. Maneno ya Kristo ni ya kuaminika, hayana uwongo, unafiki, na hila. Yeye hututendea kama washiriki wa familia, akinena, akizungumza nasi kwa ukunjufu. Ni jambo la kutia moyo sana kwetu. Tunaweza kuona kwamba hakuna upotou katika ubinadamu wa Kristo. Yeye ana ubinadamu wa kawaida—ubinadamu mwema, mtakatifu. Kristo anaweza kuonyesha ukweli mahali popote, wakati wowote, ili kutulea, kutusaidia, na kutuelekeza. Tuna uhakika zaidi kwamba Kristo hana tu ubinadamu wa kawaida, bali pia ana kiini kitakatifu. Yeye kweli ni kuonekana kwa Mungu, Mungu wa vitendo katika mwili. Kwa kumfuata Kristo hadi sasa, tunajua kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Mbali na Kristo, hakuna watu mashuhuri au wakuu wanaoweza kuonyesha ukweli na kuwaokoa wanadamu. Katika umbo la Mungu la mwili, tunaona mengi sana ya kile Mungu anacho na alicho. Tunaona kiini cha uungu cha Kristo, na tunaona kwamba tabia ya Mungu ni takatifu na ya haki. Pia tunaona jinsi Mungu alivyo mnyenyekevu na aliyejificha, na kwamba Yeye ni mkarimu na mwenye kupendeza kabisa. Hili hutuleta karibu na Mungu, kumtii na kumpenda Yeye. Kazi ya Mungu katika mwili kuwaokoa wanadamu ni yenye umuhimu mkubwa sana. Si tu kwamba inamweka Mungu na mwanadamu karibu, lakini pia inaturuhusu kupata maarifa ya vitendo na ufahamu wa Mungu. Ni kupitia kazi ya vitendo ya Mungu ndiyo tunaelewa ukweli hatua kwa hatua na kuingia katika uhalisi, tunajiondolea tabia nyingi potovu kama vile kiburi na udanganyifu. Tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu na kupata neema ya wokovu wa Mungu. Kupitia katika kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, tunahisi kwa ndani sana jinsi kazi ya Mungu katika mwili ilivyo ya kweli! Kama Mungu hangepata mwili, hatungeweza kamwe kupata unyunyizaji na riziki thabiti kutoka kwa Mungu, sembuse kuelewa na kupata ukweli, kutupilia mbali dhambi, na kuokolewa kikamilifu na Mungu. Hilo linaweza tu kufanikishwa Mungu akitekeleza kazi Yake ya hukumu katika mwili.
Kwa hivyo sasa kila mtu anapaswa kuona wazi kwamba Mungu anakuwa mwili katika siku za mwisho, akionyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu kikamilifu kwa ajili ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Ikiwa Mungu angeonekana na kufanya kazi katika roho, sisi, watu wapotovu, hatungekuwa na nafasi ya kuelewa na kupata ukweli, na hatungeweza kamwe kuutupilia mbali upotovu wetu na kuokolewa na Mungu. Hakuna shaka hata kidogo. Hata hivyo, wengi katika ulimwengu wa kidini wanaona kwamba Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana, na kukubali kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yana mamlaka na nguvu, lakini kwa sababu Yeye ni Mwana wa Adamu mwenye mwonekano wa kawaida, wanamhukumu na kumshutumu Mwenyezi Mungu, wakisema Yeye ni mwanadamu, wala si Mungu. Wao hata hupinga kwa kichaa, kulaani, na kukufuru kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Hatuna budi ila kufikiria miaka 2,000 iliyopita, Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi. Kwa kuwa Bwana Yesu alikuwa na mwonekano wa kawaida, Mafarisayo walimchukulia kama mtu wa kawaida tu, wakisema, “Je, si huyu ni Mnazareti?” “Je, huyu si mtoto wa seremala?” Haijalishi ni ukweli kiasi gani Alioonyesha, ni miujiza gani mikuu Aliyofanya, Mafarisayo hawakutafuta na hawakumkubali. Badala yake, walimhukumu na kumshutumu Bwana Yesu, wakisema alikuwa akitoa pepo kwa msaada wa pepo mkuu, na hatimaye wakamsulubisha msalabani, wakaishia kutenda dhambi mbaya sana. Walilaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Mungu sasa ameonekana na kufanya kazi katika mwili kama Mwana wa Adamu mara mbili. Kwa hivyo kwa nini watu hawamtambui, bali wanampinga, kumshutumu, na kumkataa Kristo? Wanakosea wapi? Ni kwa sababu wanatazama nje tu, kwamba Kristo anaonekana kama mtu wa kawaida. Hawachunguzi, na hawatambui ukweli wote ambao Kristo anaonyesha. Hawaoni kiini cha kiuungu cha Kristo, bali wanapigana tu na kumshutumu Kristo kwa sababu ya dhana zao za kibinadamu. Kwa hiyo wanaadhibiwa na kulaaniwa kwa sababu ya jambo hili. Biblia inasema, “Yule amwaminiye Mwana ana uzima wa milele: na yule asiyemwamini Mwana hatauona uzima; ila ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake” (Yohana 3:36). Yeyote anayemshutumu na kumpinga Mwana wa Adamu aonyeshaye ukweli anafanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu, na hawezi kusamehewa katika ulimwengu huu au ujao. Mabikira wenye busara lazima wajifunze kutafuta ukweli na kuisikiza sauti ya Mungu. Kurudi kwa Bwana katika siku za mwisho ni kama Mwana wa Adamu, akizungumza na kufanya kazi. Wale wanaomkubali ni wale wanaopenda ukweli. Wale wote wanaomkataa, kumpinga, na kumshutumu Mwana wa Adamu wanauchukuia ukweli. Mungu humfichua kila mtu jinsi alivyo kupitia mwonekano na kazi ya Mwana wa Adamu. Hii ni hekima ya Mungu, na inafichua uweza Wake.
Kumalizia, hebu tuangalie vifungu kadhaa vya maneno ya Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na pia Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote. Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hamumkubali kwa urahisi?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).
“Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?