Kwa Nini Mungu Mwenye Mwili wa Siku za Mwisho ni Mwanamke?

13/04/2023

Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu mwenye mwili ameonekana ili kufanya kazi na kuonyesha ukweli kiasi kikubwa. Umewekwa kwenye mtandao na umeutikisa ulimwengu mzima, watu wengi zaidi na zaidi wakichunguza kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi Yake. Ni wazi kwamba Mungu kuja katika mwili na kuonyesha ukweli kunadhihirisha kikamilifu nguvu ya maneno ya Mungu na kudura ya Mungu. Watu wengi wanapokuwa wakichunguza njia ya kweli, wanaona kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni yenye mamlaka, nguvu, kwamba ni ukweli, kwamba yanatoka kwa Mungu, na wanasadikishwa na kuachwa bila shaka yoyote. Hata hivyo, wanaposikia kwamba Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ni mwanamke, wengi hutikisa vichwa vyao na kukataa kumkubali. Wanafikiri kwamba Bwana Yesu alipokuja, Alikuwa mwanamume, Roho Mtakatifu pia alishuhudia kwamba Bwana Yesu alikuwa “Mwana mpendwa” wakati huo, na Biblia pia ina kumbukumbu kama hizo, hivyo Bwana atakaporudi, Atakuwa mwanamume, kwa sura ya Bwana Yesu wa Kiyahudi. Hatakuwa mwanamke kabisa. Bila kujali Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli kiasi gani na kazi Anayofanya ni kubwa kiasi gani, wanakataa kukubali, sembuse kutafuta na kuchunguza. Sababu yao ni, “Kama Mwenyezi Mungu angekuwa mwanamume, ningeamini, lakini kama Yeye ni mwanamke, hata useme nini, sitaamini kamwe, kwa sababu Bwana Yesu alikuwa mwanamume.” Kutokana na hili, wanakosa fursa ya kukaribisha kurudi kwa Bwana na wanatumbukia katika maafa, jambo ambalo linasikitisha sana. Hivyo, je, kauli na maoni ya watu hawa wa kidini ni sahihi? Je, yanakubaliana na unabii wa Biblia? Je, yana msingi katika neno la Mungu? La hasha. Hii ni kwa sababu Bwana Yesu hakubainisha iwapo Atakuwa mwanamume au mwanamke Atakaporudi, na Roho Mtakatifu hakushuhudia iwapo Mwana wa Adamu atakuwa mwanamume au mwanamke Atakaporudi. Biblia pia haitabiri kama Mungu atakuwa mwanamume au mwanamke Atakaporudi katika siku za mwisho. Huu ni uthibitisho tosha kwamba semi na mitazamo ya wanadamu havina msingi wa kibiblia na si lolote ila ni fikira na mawazo ya watu. Watu wengi huuliza, “Kwa nini Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho ni mwanamke badala ya mwanamume?” Hapa, nitashiriki ufahamu wangu wa kibinafsi kuhusu swali hili.

Kuna unabii mwingi katika Biblia kuhusu kuja kwa Mungu katika mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho, lakini haufafanui kama Bwana atakuwa mwanamume au mwanamke Atakaporudi katika siku za mwisho. Unasema tu “ujio wa Mwana wa Adamu,” “atakapokuja Mwana wa Adamu,” na “mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake.” Leo, Mwenyezi Mungu amekuja, Ameonyesha ukweli kiasi kikubwa, na Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, jambo ambalo linatimiza unabii huu. Hata hivyo, watu hushangaa wanapogundua Kristo wa siku za mwisho ni mwanamke. Hii hailingani na fikira zetu hata kidogo. Kwa kuwa ni kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, ni kawaida kabisa kwamba watu wana fikira kuhusiana na hilo. Watu walikuwa na suitafahamu hata zaidi Bwana Yesu alipokuja. Lakini kadiri watu wanavyozidi kuwa na fikira juu ya jambo fulani, ndivyo jambo hilo linavyozidi kuwa fumbo. Mungu asipofichua mafumbo haya, hatutayaelewa kamwe. Kwa hivyo, hebu tuangalie kile ambacho Mwenyezi Mungu anasema. Mwenyezi Mungu anasema, “Ikiwa Angepata mwili tu kama mume, watu wangemfafanua kama mume, kama Mungu wa wanaume, na kamwe hawangemwamini kuwa Mungu wa wanawake. Kisha, wanaume wangeamini kwamba Mungu ni wa jinsia sawa na wanaume, kwamba Mungu ni kichwa cha wanaume na je, wanawake? Hii si haki; je, huu sio utendeaji wa upendeleo? Ikiwa ingekuwa hivi, basi wale wote ambao Mungu aliwaokoa wangekuwa wanaume kama Yeye, na hakungekuwa na wokovu wa wanawake. Wakati ambapo Mungu aliumba wanadamu, Alimuumba Adamu na Akamuumba Hawa. Hakumuumba tu Adamu, lakini Aliwafanya wote mume na mke kwa mfano Wake. Mungu sio tu Mungu wa wanaume—Yeye pia ni Mungu wa wanawake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). “Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). Kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaweza kuona kwamba bila kujali kupata mwili kwa Mungu ni mwanamume au mwanamke, ni muhimu. Kuna ukweli wa kutafutwa ndani yake, na unaweza kuturuhusu kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua tabia ya Mungu. Iwapo Mungu mwenye mwili daima angekuwa mwanamume, matokeo yangekuwa yapi? Watu wangemwekea Mungu mipaka kuwa mwanamume daima na kamwe si mwanamke, na wanawake wangekabiliwa na ubaguzi na wasingeweza kuishi kama wanajamii kikamilifu. Je, hiyo ingekuwa haki kwa wanawake? Mungu ni Mungu mwenye haki, na Mungu aliumba mwanamume na mwanamke, hivyo Mungu akawa mwanamume wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, na katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili kama mwanamke. Hili ni jambo la maana sana na ambalo wanawake wote wanapaswa kushangilia na kufurahia, na wasiwe na fikira zozote tena. Iwapo mwanamke bado anaweza kukataa na kumbagua Mungu wa kike mwenye mwili, basi mwanamke huyo ni wa kusikitisha sana! Kwa kweli, haijalishi iwapo kupata mwili kwa Mungu ni kwa kike au kiume. Cha muhimu ni kwamba Anaweza kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya wokovu. Watu hawapaswi kufikiri kwamba Mungu mwenye mwili anaweza tu kufanya kazi ya Mungu ikiwa Yeye ni mwanamume, na kwamba Hawezi kufanya kazi ya Mungu ikiwa Yeye ni mwanamke. Ni jambo la aibu na la kijinga kufikiri hivi. Leo, sote tumeona kwamba wanawake wanaweza kufanya chochote ambacho wanaume wanaweza kufanya. Kwa mfano: Wanaume wanaweza kuendesha ndege, na wanawake pia. Wanaume wanaweza kuwa wanaanga, wanawake pia wanaweza. Wanaume wanaweza kuwa marais, wanawake pia wanaweza. Wanaume wanaweza kuendesha biashara na kudumisha kazi, wanawake wanaweza pia kuendesha biashara na kudumisha kazi. Ukweli unathibitisha kuwa wanawake hawana uwezo mdogo kuliko wanaume. Basi kwa nini Mungu mwenye mwili anaweza tu kuwa mwanamume, na hawezi kuwa mwanamke? Mtazame Mwenyezi Mungu, ambaye Ameonyesha ukweli kiasi kikubwa sana na kufanya kazi nyingi. Je, kuwa mwanamke kumezuia kazi ya Mungu hata kidogo? Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ni kubwa zaidi kuliko kazi iliyofanywa na Bwana Yesu. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli zaidi na wa kina zaidi kuliko ule ulioonyeshwa na Bwana Yesu. Ukweli huu ni dhahiri kwa wote, hivyo kwa nini watu hawawezi kuutambua? Ni wanawake wangapi wanaokandamizwa, kubaguliwa, na kuteseka ulimwenguni leo? Wanahitaji kuwa na hadhi sawa na wanaume, na zaidi ya hayo, wanahitaji wokovu na uhuru. Nani awezaye kuwaokoa wenzetu wa kike? Leo, Mwenyezi Mungu amekuja, na Ameonyesha ukweli ili kuhukumu ulimwengu huu mwovu na wanadamu waovu, ambao wamepotoka sana. Kuna wanawake wengi ambao wameona kwamba Mwenyezi Mungu mwenye mwili ni mwanamke, Anaweza kuonyesha ukweli, na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na kwa hivyo wamejivunia kuwa wanawake. Wanajiamini, wamepata kuhisi uhuru na ufunguliwaji, na wote wanasherehekea na kumsifu Mwenyezi Mungu. Mungu kuja mwilini kama mwanamke kunaonyesha tabia ya Mungu yenye haki. Ni Mungu pekee anayependa wanadamu kwa kweli, na ni Mungu pekee anayeweza kuwatendea watu kwa haki. Mungu ni mwenye kupendeka sana! Sasa tufikirie jambo lingine. Bwana Yesu wa kiume aliweza kubeba dhambi za watu na kumaliza kazi ya ukombozi kwa kusulubiwa. Iwapo Bwana Yesu angekuja kama mwanamke, Angeweza kumaliza kazi ya ukombozi kwa kusulubiwa? Hapana shaka kwamba Angeweza. Kupata mwili kwa Mungu kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu anavaa mwili wa mwanadamu, na bila kujali iwapo mwili huu ni wa kiume au kike, Yeye ni Mungu Mwenyewe. Anaonyesha ukweli na kufanya kazi, na yote hayo hufanywa na kudhibitiwa na Roho wa Mungu. Kwa hivyo, bila kujali iwapo Mungu mwenye mwili ni mwanamume au mwanamke, Anastahili kuwakilisha utambulisho wa Mungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, na hatimaye, kazi itakamilika na Mungu atapata utukufu. Ni kama Mwenyezi Mungu asemavyo: “Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, basi hatua ya leo ya kazi ingelazimika kukamilishwa badala yake na mwanaume, lakini kazi ingekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua hizi zote ni muhimu kwa kiwango sawa; hakuna hatua yoyote ya kazi inayojirudia au kupingana na nyingine(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). Hii inamaanisha kwamba haijalishi iwapo mwenye mwili ni wa kiume au kike. Mradi Anaweza kuonyesha ukweli na kumaliza kazi ambayo Mungu anataka kukamilisha, pamoja na kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Yeye ndiye Mungu mwenye mwili. Ikiwa watu wanafikiri kwamba Mungu mwenye mwili anaweza tu kuwa mwanamume wala si mwanamke, je, haya si matoeko ya kanuni, mawazo na dhana za watu? Je, wanafikiri kwamba Mungu alimuumba mwanamume na hakumuumba mwanamke? Kwa sababu Mungu mwenye mwili ni mwanamke, bila kujali Anaonyesha ukweli kiasi gani au kazi Anayofanya ni kubwa kiasi gani, watu hawamtambui wala kumkubali. Je, hii si kwa sababu tu watu huwakana na kuwabagua wanawake? Je, hii si moja tu ya tabia potovu za wanadamu? Watu hawana haki ya kuchagua jinsi Mungu anavyoonekana na kufanya kazi. Ilimradi Yeye ni mwili wa Mungu, na mradi Anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya Mungu, bila kujali iwapo mwili ni wa kiume au kike, watu wanapaswa kukubali na kutii. Hii ndiyo njia ya mantiki na ya busara. Mungu ni mwenye nguvu zote na mwenye hekima yote, na mawazo ya Mungu yanayapiku mawazo ya mwanadamu. Wanadamu wanawezaje kutumaini kuelewa kazi ya Mungu? Tangu nyakati za kale hadi sasa, kila hatua ya kazi ya Mungu imezidi na kwenda kinyume na mawazo ya mwanadamu. Bwana Yesu alipoonekana na kufanya kazi, kuonekana Kwake, kuzaliwa Kwake na familia Yake vilipiku sana mawazo ya wanadamu. Hii ndiyo sababu Mafarisayo hawakukiri kuwa Alikuwa Masihi aliyetabiriwa katika Maandiko na hatimaye wakamtundika msalabani, na kufanya dhambi mbaya iliyowafanya waadhibiwe na kulaaniwa na Mungu. Lilikuwa somo lililochochea mtu kufikiri na ambalo lilipiwa kwa damu. Kwa hivyo, kila kitu kinachohusisha kuonekana kwa Mungu na kazi Yake ni tukio na fumbo kuu. Watu wasipotafuta ukweli, wasisitize kushikilia dhana zao, na wahukumu na kuamua kirahisi hivyo, wana uwezekano mkubwa wa kuikosea tabia ya Mungu. Ukikataliwa na kuondolewa na Mungu na upoteze wokovu Wake, utakuwa na majuto makubwa zaidi.

Leo, bado kuna watu wengi mno ambao wanakataa kukubali kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi Yake katika siku za mwisho kwa sababu Yeye ni mwanamke, na hata, licha ya kujua kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, hawamkubali. Tatizo ni lipi hapa? Kwa nini fikira za watu hawa ni thabiti mno? Kwa nini hawathamini ukweli na kuonyeshwa kwa ukweli juu ya mengine yote? Kama watu, kama wanadamu, ambao ni viumbe walioumbwa, tunapaswa kumchukulia Mungu na kazi Yake ipasavyo. Iwapo tunajua waziwazi kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye mwili na tunajua waziwazi maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini bado tunashikilia dhana zetu na kukataa kumkubali kwa sababu Yeye ni mwanamke, hili ni tatizo kubwa sana. Kufanya hivi ni kumkana na kumpinga Mungu. Kukataa kumtambua Mungu mwenye mwili au ukweli Anaoonyesha si tatizo la fikira na mawazo pekee. Jambo hilo linakufanya uwe mpinga Kristo, adui wa Mungu, na mtu anayepaswa kulaaniwa! Kama ilivyosemwa katika Maandiko: “Kwa kuwa walaghai wengi wameingia ulimwenguni, ambao hawakubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili. Huyu ni mlaghai na anayempinga Kristo” (2 Yohana 1:7). “Kila roho isiyokubali kuwa Yesu Kristo amefika katika mwili si ya Mungu: na hii ndiyo ile roho ya anayempinga Kristo, ambayo ninyi mmesikia kuwa itakuja; na hata sasa tayari iko duniani” (1 Yohana 4:3). Kwa hivyo, tunaweza kuwa na hakika kwamba yeyote asiyekubali kurudi kwa Mwana wa Adamu na yeyote asiyetambua Mungu mwenye mwili Aliyerudi ni mpinga Kristo. Je, unafikiri kwamba Mungu atawaokoa wapinga Kristo atakaporudi? La hasha. Kwa hivyo, mwisho wa wapinga Kristo ni upi? Je, wapinga Kristo hufanya kosa lipi? Hawampingi mtu tu, wanampinga Kristo wa siku za mwisho, Mungu Mwenyewe. Kiini cha kumshutumu na kumhukumu Mwenyezi Mungu ni nini? Ni dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Dhambi hii haitasamehewa kamwe, siyo sasa au katika siku zijazo.

Watu wengi leo wanamwamini Mungu lakini hawajui kazi ya Mungu, wala hawajui Mwana wa Adamu ni nini, kupata mwili ni nini, au ni nani aliye Mungu mmoja wa kweli. Kwa namna hii, ni rahisi kumpinga Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, sharti tusitumie mawazo na dhana zetu kuwekea mipaka kazi ya Mungu. Badala yake, tunapaswa kutafuta ukweli na kuondoa dhana zetu. Ni kwa njia hii pekee ndiyo tunaweza kupokea baraka za Mungu. Umuhimu wa kazi wakati wa kupata mwili kwa Mungu mara mbili ni wenye athari nyingi na wa kina. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu amesema: “Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyeongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa na binadamu, na tofauti kwamba mmoja alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?). Tunaona kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba Mungu anapokuja katika mwili kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu, haijalishi ikiwa Mungu ni mwanamume au mwanamke, Anatoka katika familia gani, au Anaonekanaje. Hakuna lililo muhimu kati ya mambo haya. La muhimu zaidi ni kwamba Anaweza kufanya kazi ya Mungu, kutekeleza mapenzi ya Mungu, na kumletea Mungu utukufu. Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alizaliwa horini katika familia ya kawaida sana huko Yudea. Watu walikuwa na mawazo juu ya hili. Wote walimhukumu Bwana Yesu kwa kuwa mwana wa seremala kutoka Nazareti na walikataa kukubali kazi Yake kwa sababu hiyo. Matokeo yake ni kwamba walilaaniwa na Mungu na kupoteza wokovu wao. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu amekuja. Alizaliwa katika familia ya kawaida na ana sura ya Mwasia. Kwa nje, Anaonekana kuwa mtu wa kawaida, lakini Anaonyesha ukweli kiasi kikubwa sana, Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, Anawashinda watu na kutengeneza kundi la washindi. Mwenyezi Mungu Amefanya kazi yenye nguvu sana ambayo imetikisa ulimwengu mzima, na pia Amemaliza historia ya Shetani kuwapotosha wanadamu kwa maelfu ya miaka na kuanzisha enzi mpya. Ni nini kinachowaruhusu watu kuwa na fikira kuhusu kuja kwa Mungu katika mwili kama mwanamke? Watu kama hao ni wenye kiburi sana na wasio na akili. Leo, injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu inahubiriwa ulimwenguni kote. Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa mno, zina nguvu, na hazizuiliki, na neno la Mungu litatimiza kila kitu. Hili linafichua kikamilifu tabia ya Mungu yenye haki, kudura, na hekima. Kama Mwenyezi Mungu anavyosema, “Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Ukweli kwamba mmefika siku ya leo ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu, kwa sababu ni ukweli, uzima, na njia Aliyoleta ndivyo vilivyowaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya mwanadamu na Mungu, ikafupisha umbali kati yao, na kufungua kiungo kati ya mawazo ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu).

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno ‘maneno’ linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno).

Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupata Mwili Ni Nini?

Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp