Je, Kazi ya Mungu ya Hukumu ya Siku za Mwisho Inawatakasa na Kuwaokoa Vipi Wanadamu?
Watu wametambua kwamba maafa makubwa yanatukabili na wale wanaomtarajia Bwana aje juu ya wingu wamekuwa wakingoja kwa shauku. Baada ya kusubiri kwa miaka mingi, bado hawajamwona Akija. Badala yake, wanaona Umeme wa Mashariki likitoa ushuhuda kwa kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Haya ni maudhi makubwa kwao. Wamekuwa wakitumaini kunyakuliwa moja kwa moja mahali ambapo watakutana na Bwana, bila kutarajia kuwa Atafanya kazi ya hukumu Atakaporudi. Hawataki kukubali hayo. Watu wengi wanafuata nguvu za wapinga Kristo wa ulimwengu wa kidini, wakihukumu na kushutumu kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Wanafikiri, “Dhambi zetu zimesamehewa na tumehesabiwa kuwa wenye haki na Mungu, kwa hivyo hatuhitaji hukumu ya Mungu. Tunamngoja Bwana atuchukue hadi katika ufalme Wake ambapo tutafurahia baraka Zake.” Wanashikilia mawazo yao, hawataki kutafuta wala kuchunguza njia ya kweli, na ndiyo maana bado hawajamkaribisha Bwana, lakini wametumbukia katika maafa. Hili linatimiza kikamilifu maneno ya Bwana Yesu: “Kwa kuwa kila aliye nacho atapewa, naye atakuwa navyo tele: lakini yeye asiye na kitu atanyang'anywa hata kile alicho nacho. Na mtupeni katika giza la nje mtumwa yule asiyefaidi: kutakuwa na kilio na kusaga meno” (Mathayo 25:29–30). Lakini kuna watu wengi wanaopenda ukweli na waliposoma maneno ya Mwenyezi Mungu, waliona nguvu na mamlaka ya maneno hayo, wakaona kwamba yote ni ukweli. Waliitambua sauti ya Mungu na hawakuzuiliwa tena na mawazo yao, bali waliendelea kuchunguza njia ya kweli. Maswali yao ya kwanza yalikuwa ni kwa nini Mungu bado Anahitaji kufanya kazi ya hukumu wakati dhambi zao zimesamehewa na wamechukuliwa kuwa wenye haki na Mungu, na jinsi Mungu anavyowatakasa na kuwaokoa wanadamu kupitia kazi hiyo katika siku za mwisho. Haya ni maswali mawili muhimu zaidi na ya kustaajabisha ambayo kila mtu anayechunguza njia ya kweli anapaswa kuelewa.
Hebu tuanze na kwa nini Mungu anahitaji kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Jambo hili huwatatanisha watu wengi wa dini. Wanafikiri, “Bwana tayari ametusamehe dhambi zetu, na Mungu hatuoni kama wenye dhambi, hivyo tunaweza kuchukuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme Wake, na hatuhitaji hukumu ya Mungu.” Hili ni kosa kubwa mno. Ni kweli kwamba Bwana amesamehe dhambi za wanadamu, lakini je, msamaha huo unamaanisha kwamba tumetakaswa? Je, hiyo inamaanisha kuwa tumetimiza utiifu wa kweli kwa Mungu? La. Sote tumeona ukweli huu: Licha ya kusamehewa dhambi zetu, waumini wote huishi katika mzunguko wa kutenda dhambi na kuungama, kutenda dhambi mchana, na kisha kuungama usiku, kujaribu na kushindwa kufuata amri za Bwana Yesu, kujaribu na kushindwa kumpenda na kumtii Bwana, kuazimia kutenda mema, lakini hata hivyo kusema uwongo na kutenda dhambi pasipo kutaka, wakishindwa bila kujali jinsi wanavyojitahidi kujizuia. Wengi wanahisi kwamba mwili umepotoka sana, na kuishi katika dhambi kunaumiza sana. Basi kwa nini watu hawawezi kujinasua kutoka kwenye vifungo vya dhambi? Kwa nini hatuwezi kujizuia kutenda dhambi kila mara? Ni kwa sababu ya asili ya dhambi ya mwanadamu na tabia za kishetani. Mambo haya ndiyo chanzo cha dhambi. Bila kushughulikia chanzo cha dhambi, hatuwezi kamwe kuwekwa huru kutoka kwayo, bali tutaendelea kumpinga Mungu, kumhukumu, na kuwa na uadui Naye. Tafakari kuhusu Mafarisayo, ambao walikuwa na imani kwa vizazi vingi na walikuwa wakitoa sadaka kwa ajili ya dhambi kila mara. Kwa nini Yehova Mungu alipopata mwili kama Bwana Yesu na kuonyesha ukweli mwingi sana, hawakumtambua Bwana Yesu kama kuonekana kwa Yehova Mungu, bali walimshutumu na kumhukumu, na hata kumfanya Asulubishwe? Tatizo lilikuwa lipi? Sasa katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu Anakuja na kuonyesha ukweli, kwa hivyo kwa nini watu wengi wa kidini hukataa hata kuuchunguza, bali humlaani na kumkufuru kwa hasira nyingi, wakidhamiria kumsulubisha Mungu msalabani kwa mara nyingine tena? Yote haya yanamaanisha nini? Yanaonyesha wazi kwamba ingawa dhambi za watu zimesamehewa, bado wanatawaliwa na asili yao ya kishetani na wanaweza kumhukumu na kumpinga Mungu wakati wowote. Utenda dhambi wa mwanadamu sio tu suala la matendo ya dhambi, bali ni kubwa sana hivi kwamba wanataka kumsulubisha Kristo ambaye anaonyesha ukweli, wakisimama dhidi ya Mungu, dhidi ya ukweli, kutenda na kufanya kazi dhidi ya Mungu na kuwa maadui Wake. Je, watu wachafu na wapotovu kama hawa wanaompinga Mungu wanawezaje kustahili ufalme Wake? Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, na tabia Yake haiwezi kukosewa. Iwapo wale ambao dhambi zao zimesamehewa hawatasafishwa kupitia kazi ya hukumu, bali wataendelea kutenda dhambi na kumpinga Mungu, hawatastahili kamwe ufalme wa Mungu—hakuna shaka kuhusu hili. Hili linatimiza maneno ya Bwana Yesu: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21). “Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34–35). Pia kuna Waebrania 12:14: “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana.” Ndiyo maana Bwana Yesu alisema mara nyingi wakati wa kazi Yake ya ukombozi kwamba Atakuja tena. Kwa hiyo Yeye yuko hapa kufanya nini? Kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini na kutokana na nguvu za Shetani, ili tuweze kumgeukia Mungu kikamilifu na kuwa watu wanaomtii na kumwabudu Mungu. Kisha Atatupeleka kwenye hatima nzuri. Kama Bwana Yesu alivyotabiri: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12–13). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47–48). Na, “Kwa maana wakati umefika ambapo lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). Tunaweza kuona hapa kwamba Mungu alipanga zamani sana kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na hii hasa ndiyo wanadamu wapotovu wanahitaji ili kuokolewa kikamilifu. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Yeye ndiye Roho wa ukweli aliyekuja miongoni mwa wanadamu, Akiwaongoza watu wa Mungu wateule kuingia katika ukweli wote. Hii inatimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu. Sasa hebu tusome baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ili kubaini zaidi kwa nini Mungu anahitaji kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho.
Mwenyezi Mungu Anasema, “Ingawa Yesu alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Alikamilisha tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa dhabihu ya dhambi ya mwanadamu; Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote potovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa Shetani hakukuhitaji tu Yesu kuwa dhabihu ya dhambi na kubeba dhambi za mwanadamu, lakini pia kulihitaji Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu kabisa tabia yake potovu ya kishetani. Na kwa hivyo, kwa kuwa sasa mwanadamu amesamehewa dhambi zake, Mungu amerudi katika mwili ili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu. Kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wale wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watafurahia ukweli wa juu zaidi na kupokea baraka kubwa zaidi. Kwa kweli wataishi katika nuru, na watapata ukweli, njia, na uzima ” (Neno, Juz. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).
“Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. … Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).
Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu mwenyewe alisulubishwa, Akawa dhabihu ya dhambi ya wanadamu na kuwakomboa binadamu kutoka dhambini. Tangu wakati huo, dhambi za mwanadamu zimesamehewa na Mungu hatuoni kama wenye dhambi, kwa hivyo tunaweza kumwomba Mungu moja kwa moja na kuja mbele Zake. Lakini Mungu kutomwona tena mwanadamu kama mwenye dhambi kuna maana kwamba Amesamehe dhambi zetu, si kwamba hatuna dhambi, kwamba sisi ni watakatifu kabisa. Bado tuna asili ya dhambi na tabia ya kishetani. Tunapaswa kupitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ili upotovu wetu uweze kutakaswa na tuweze kuokolewa kikamilifu. Kazi ya Mungu ya ukombozi katika Enzi ya Neema iliiandalia njia kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Yaani, kazi Yake ya hukumu inafanywa juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu. Kazi ya Mungu ya ukombozi ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake kamili ya wokovu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ambayo inaweza kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na ni hatua muhimu zaidi ya kazi ya Mungu ya wokovu. Sharti twende tupitie hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho, tuwekwe huru kutokana na dhambi na kusafishwa kabisa, na kumtii Mungu kwa kweli na kufanya mapenzi ya Mungu ili tustahili ufalme Wake.
Katika hatua hii nadhani tuna ufahamu bora zaidi wa kwa nini Mungu anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Watu wengine huenda wakashangaa jinsi kazi hii inavyowatakasa na kuwaokoa wanadamu. Hebu tuone kile ambacho Mwenyezi Mungu amesema kuhusu hili. “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).
“Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu).
“Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua ‘siri’ katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa).
Hii inasaidia kutoa mwanga kiasi kuhusu jinsi Mungu anavyofanya kazi Yake ya hukumu, siyo? Katika kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, kimsingi Anaonyesha ukweli ili kuhukumu na kufichua kiini potovu cha mwanadamu, na tabia zetu za kishetani ili tuweze kuona ukweli wa upotovu wetu, kuwa na majuto ya dhati, kujichukia na kujidharau, kuukana mwili na kuweka maneno ya Mungu katika vitendo, na kufikia toba na mabadiliko ya kweli. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanafichua kikamilifu udhihirisho wa tabia potovu za mwanadamu kama vile kiburi, udanganyifu, na uovu, pamoja na nia na ughushi katika imani yetu, na hata mawazo na hisia zetu za ndani kabisa zilizofichika zaidi. Haya yote yamefunuliwa kwa uwazi sana. Tunaposoma maneno ya Mwenyezi Mungu, tunahisi kama Mungu yuko pale pale akituhukumu pasipo kujaribu kuficha. Tunaona nafsi zetu chafu, potovu, mbovu zikifichuliwa kikamilifu na Mungu, na kutuacha tukihisi aibu, tukiwa hatuna pa kujificha, na kutofaa kuishi mbele za Mungu. Anapokuwa akimhukumu mwanadamu kwa maneno Yake, Mungu pia huweka hali halisi ili kutufichua, kisha tunapogolewa, tunashughulikiwa, na kujaribiwa na ukweli, ili tuweze kujitafakari na kujijua. Tunapofichuliwa na ukweli, na kisha kufichuliwa zaidi na kuhukumiwa kupitia maneno ya Mungu, tunaona kwa uwazi zaidi ubaya wa sisi kuishi kwa kutegemea asili yetu ya kishetani. Tunajawa na majuto na kujichukia, na polepole kukuza toba ya kweli. Tabia yetu potovu inasafishwa na kubadilishwa. Kisha, hebu tusikilize baadhi ya maneno ya Mungu yanayofichua tabia potovu ya mwanadamu ili tupate wazo bayana zaidi la jinsi Mungu Anavyofanya kazi Yake ya hukumu.
Mwenyezi Mungu anasema, “Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumsikiza na aidha nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za dawa ovu na uchawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu walitaka kutoka Kwangu, walitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba mwnadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?).
“Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu, na nia hiyo ni kupokea Baraka. Watu kama hao hawawezi kujishughulisha kuzingatia kitu chochote kingine ambacho hakihusiani na nia hii moja kwa moja. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila hasira iliyofichwa na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu).
“Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale ambao hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote kama hawa hujisifu wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa la kuchekesha? Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu).
“ Baada ya miaka elfu kadhaa ya ufisadi, mwanadamu hana ganzi na hana akili timamu; amekuwa pepo anayempinga Mungu, kwa kiwango ambacho uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa maelezo kamili ya tabia yake ya uasi—kwa maana mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amepotoshwa na Shetani kiasi kwamba hajui pa kuelekea. Hata leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Mwanadamu anapomwona Mungu, anamsaliti, na wakati hawezi kumwona Mungu, hivyo pia anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana za Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na kwa hivyo Ninasema kwamba hisi ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya asili, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya asili. Mwanadamu ninayemtazama ni mnyama aliyevalia mavazi ya kibinadamu, ni nyoka mwenye sumu kali, na haijalishi jinsi anavyojaribu kusikitisha kuonekana mbele ya macho Yangu, Sitawahi kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hafahamu tofauti kati ya weusi. na nyeupe, ya tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia za mwanadamu zimefifia sana, ilhali bado anatamani kupata baraka; ubinadamu wake ni wa kudharauliwa lakini bado anatamani kumiliki ukuu wa mfalme. Angeweza kuwa mfalme wa nani, kwa akili kama hiyo? Je, yeye pamoja na ubinadamu kama huyo angewezaje kukaa juu ya kiti cha enzi? Mwanadamu hana aibu kweli! Ni mnyonge mwenye majivuno! Kwa wale ambao mnataka kupata baraka, ninapendekeza kwanza utafute kioo na uangalie tafakari yako mbaya—una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mtu ambaye angeweza kupata baraka? Hakujawa na mabadiliko hata kidogo katika tabia yako na hujaweka ukweli wowote katika vitendo, bado unatamani kesho njema. Unajidanganya! ” (Neno, Juz. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu).
Maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya vitendo sana, na kila neno ni halisi sana, na linafichua ughushi na nia mbaya katika imani yetu na vile vile asili yetu ya kumpinga Mungu. Sikuzote tulifikiri kwamba tunaweza kutoa dhabihu, kuteseka, na kulipa gharama kwa ajili ya Mungu, jambo ambalo lilimaanisha kwamba tulikuwa wacha Mungu na watiifu, na tunaweza kupata kibali cha Mungu. Lakini kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, tunatafakari na kujijua wenyewe, na kuona kwamba dhabihu zetu zote zilitiwa madoa, na ili tu kupata baraka. Mungu anapotubariki na maisha ya amani, sisi humtii na kumfanyia kazi, lakini uchungu na maafa yanapotokea, sisi humwelewa Mungu visivyo na kumlaumu kwa kutotulinda, na huenda hata tukaacha kumfanyia kazi. Basi tunaona kwamba imani na dhabihu zetu zimekuwa za kibiashara kabisa, ili kupata neema na baraka kwa nguvu kutoka kwa Mungu. Huku ni kumdanganya na kumtumia Mungu. Ni jambo la ubinafsi na ujanja sana! Hatuna dhamiri wala mantiki kabisa, na hatustahili hata kuitwa wanadamu. Huku tukiwa wachafu sana na wapotovu, bado tunafikiri kwamba tuna haki ya kubarikiwa na kuingia katika ufalme wa Mungu. Huku ni kukosa aibu na mantiki. Maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo yanatuonyesha tabia Yake ya haki, takatifu ambayo haiwezi kukosewa, na kwamba kile ambacho Mungu anataka kutoka kwetu ni uaminifu na kujitolea kwetu. Kuwa na imani na kufanya wajibu ukiwa na nia na uchafu kama huo ni kumdanganya na kumpinga Mungu, na ni maudhi na chukizo Kwake. Mungu hatambui imani ya aina hii. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu na kushughulikiwa na kujaribiwa mara nyingi, tunaweza hatimaye kuona ukweli wa upotovu wetu, kujichukia kwa dhati na kuhisi majuto, na kusujudu mbele za Mungu katika toba. Tunaweza pia kuona haki ya Mungu na kwamba Yeye kweli huona mioyo na akili zetu, na Anatujua nyuma na mbele. Tunaridhika kabisa na kukuza mioyo ya kumcha Mungu. Mtazamo wetu juu ya imani unabadilika, tunatazama wajibu wetu kwa usafi zaidi, bila matamanio mengi ya kupita kiasi, na tunafurahia kutii mipango ya Mungu na kufanya wajibu wa kiumbe bila kujali kama Mungu anatubariki, ikiwa tunapokea baraka za ufalme. Tunapoona jinsi tulivyo kwa kweli, tunakuwa wasio na kiburi kama hapo awali. Tunakuwa wenye mantiki katika maneno na matendo, tunatafuta na kutii ukweli. Hii ni hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake, ambavyo hutusafisha na kubadilisha upotovu wetu polepole. Wale kati yetu ambao tumekuwa tukipitia kazi ya Mungu kwa kweli tunajua jinsi kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho ilivyo ya vitendo, jinsi inavyomtakasa na kumwokoa mwanadamu kikamilifu. Bila hukumu na upogoaji huu, hatungeweza kamwe kuona upotovu wetu, bali tungekwama katika maisha yetu ya kutenda dhambi na kuungama bila kukoma, tukifikiri kwamba tunaweza kuingia katika ufalme wa Mungu kwa sababu dhambi zetu zilisamehewa, kwamba tulikuwa na kibali cha Mungu. Jambo hilo ni la kipumbavu na linasikitisha sana! Kwa msaada wa hukumu ya Mungu, tunaweza kujijua kabisa, tunajifunza ukweli mwingi na tabia zetu potovu zinasafishwa na kubadilishwa. Hilo linakomboa kabisa. Hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake vinatupa mengi sana. Vitu hivyo ni upendo wa Mungu wa kweli kwetu, wokovu Wake mkuu zaidi. Imekuwa miaka 30 tangu Mwenyezi Mungu alipoanza kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu, na tayari Amekamilisha kundi la washindi kabla ya maafa—malimbuko. Hii inatimiza kikamilifu unabii wa Biblia: “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo” (Ufunuo 14:4). Watu wa Mungu wateule wamepitia hukumu, kuadibu, majaribio, na usafishaji, tabia zao potovu zimetakaswa, na hatimaye wako huru kutoka kwa nguvu za Shetani. Wamepata kumtii na kumwabudu Mungu, na kupokea wokovu mkuu wa Mungu. Uzoefu na ushuhuda wao umegeuzwa kuwa filamu na video ambazo zote ziko mtandaoni, na zinashuhudia kwa wanadamu wote kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, na kutoacha shaka mioyoni mwa watazamaji. Injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu imeenea kote duniani, na watu wa Mungu wateule kila mahali wanaeneza maneno ya Mwenyezi Mungu. Kuenea kuzuri sana na kwa kipekee kwa injili ya ufalme kumewadia. Bila shaka, kazi ya hukumu inayoanza na nyumba ya Mungu tayari ina mafanikio makubwa. Mungu amemshinda Shetani na kupata utukufu wote. Kama vile Mwenyezi Mungu anavyosema, “Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu). “Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Sababu ya kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu katika kiini ni ili kuwatakasa binadamu kwa ajili ya pumziko la mwisho; bila utakaso wa aina hii, hakuna binadamu yeyote angeainishwa katika makundi tofauti kulingana na aina yakeama kuingia katika pumziko. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?