Ni Nani Anayeweza Kuwaokoa Wanadamu na Kubadilisha Majaliwa Yetu?
Majaaliwa yanapotajwa, watu wengi hulinganisha kuwa na pesa na hadhi, na kufaulu, wao hulinganisha haya na majaliwa mazuri, na hufikiri kwamba masikini, wasiojulikana, wanaopatwa na balaa na shida, wanaodharauliwa, wana majaliwa mabaya. Kwa hivyo ili kubadilisha majaaliwa yao, wao hufuatilia maarifa kwa bidii, wakitumaini kwamba hii itawasaidia kupata utajiri na hadhi, na hivyo kubadilisha majaliwa yao. Je, kuwa na pesa, hadhi, na mafanikio maishani kunamaanisha kuwa na majaliwa mazuri? Je, kuteseka kwa ajili ya maafa na misiba kunamaanisha kuwa na majaliwa mabaya kweli? Watu wengi hawana ufahamu mzuri wa jambo hili na bado wanafuatilia sana maarifa ili kubadilisha majaliwa yao. Lakini je, ujuzi unaweza kubadilisha majaliwa ya mtu? Ni nani hasa anayeweza kuwaokoa wanadamu na kuleta mabadiliko katika majaliwa yetu? Hebu tujitose kwenye swali hili leo.
Katika maisha ya kila siku tunaweza kuona kwamba watu wengi wanaopata maarifa wanaweza pia kupata pesa na hadhi. Wao ni wenye ufanisi maishani na wanaweza hata wanaweza kuwa maarufu au wanaosifiwa. Wakiwa wamefanikiwa na maarufu sana, inaonekana kana kwamba wana majaliwa mazuri. Lakini, je, hiyo ni kweli? Je, wana furaha kweli? Wanaweza kuwa na nguvu na ushawishi na kuonekana kuwa mashuhuri, lakini bado wana hisia ya utupu na huzuni, na kupoteza mng’ao wao wa maisha. Wengine hata hutumia dawa za kulevya au kujiua. Na wengine hutumia nguvu na ushawishi wao kufanya chochote wanachotaka, wakifanya uovu na kufanya uhalifu, na wao huishia kufungwa jela, kwa fedheha kabisa. Je, si hawa ni wasomi mara nyingi? Kwa nini wale watu wanaoonekana kuwa wenye akili, wanaoelewa sheria wafanye mambo ya kutisha namna hii? Kwa nini wafanye mambo ya kipuuzi hivyo? Kwa nini mambo yageuke yawe hivyo? Siku hizi kila mtu anataka elimu, kila mtu anafuatilia maarifa, na tabaka tawala katika nchi zote, watu wote ni wasomi. Hao ndio wanaoshikilia madaraka, ndio wenye sifa nzuri duniani kote. Inaeleweka kwamba kwa kuwa na wasomi katika uongozi, ulimwengu unapaswa kuwa wa kistaarabu na upendo zaidi na zaidi. Lakini ni nini hasa kinachoutendekea ulimwengu? Unaanguka katika ghasia na machafuko, huku watu wakidanganya, kupigana, au hata kuuana. Wote wanamkana na kumpinga Mungu, wanachukia ukweli na kuuinua uovu bila tamanio la kutubu, wakichochea ghadhabu ya Mungu na hasira ya mwanadamu. Maafa yanakuja moja baada ya nyingine, na dunia daima iko ukingoni mwa vita vikuu. Ni wazi kwamba kuwa na wasomi madarakani, kuwa na mifumo ya viongozi weledi hakuleti jamii zenye amani na furaha, badala yake kunatuletea maafa na mateso zaidi na zaidi. Magonjwa ya mlipuko yanaongezeka, vita vinatokea bila kukoma, na matetemeko ya ardhi na njaa vinafuata. Watu wamejawa na hofu, kana kwamba mwisho wa dunia umefika. Sababu halisi ya haya ni ipi? Kwa nini watu wanapopata ujuzi, mamlaka, na hadhi, wanafanya mambo mengi ya kutisha? Kwa nini kuwa na wasomi na mifumo ya weledi madarakani kunaleta maafa makubwa kwenye nchi na watu? Hili linastahili kuzingatiwa sana! Je, kupata maarifa kunaweza kufanya mtu awe bora na asiye na dhambi? Je, kupata maarifa kunaweza kuwafanya watu wawe wapole na kuwazuia wasifanye mambo mabaya? Je, maarifa yanaweza kuwaokoa watu kutoka katika dhambi, na kuwaokoa watu kutoka katika nguvu za Shetani? Nina shaka zaidi na zaidi juu ya uwezo wa maarifa kubadilisha majaliwa ya mtu. Kwa nini baada ya kupata maarifa na hadhi, watu wengi wanazidi kuwa na kiburi na wenye kujidai? Kwa nini kadiri wanavyojua zaidi ndivyo wanavyojiona kuwa wa maana zaidi? Wakishaingia madarakani, wanakuwa wenye maadili mabaya na wa kiholela, wakileta uharibifu na kuleta maafa. Inaonekana kana kwamba pamoja na elimu bora na sayansi iliyoendelea zaidi, nchi inapaswa kutawaliwa vyema na watu wanapaswa kuwa wastaarabu, wenye furaha, na wenye afya zaidi. Lakini je, nchi ya aina hiyo ipo kweli? Haijawahi kuwepo. Hilo linawaacha watu wakikuna vichwa! Nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. … Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote).
Maneno ya Mungu ni sahihi sana, na hakina yanafichua ukweli wa jambo hilo. Maarifa huundwaje hasa? Bila shaka, yametoka kwa wale watu maarufu na wakuu ambao husifiwa katika historia yote. Kuna Ukonfyushasi, nadharia ya Darwin ya mageuzi, Manifesto ya Kikomunisti ya Marx na nadharia ya ukomunisti. Ukana Mungu, uyakinifu, na nadharia ya mageuzi yote yanatokana na mawazo na nadharia ambazo watu hawa mashuhuri waliziandika kwenye vitabu, na ndiyo msingi wa sayansi na nadharia katika jamii yetu ya kisasa. Mafundisho na nadharia hizi zote zimekuzwa na tabaka tawala katika enzi zote. Zimeingia katika vitabu vya kiada na katika madarasa, na kuwa kanuni za ubinadamu. Zimeelimisha, kuharibu, na kudhoofisha kizazi baada ya kizazi, na kuwa zana za tabaka tawala za kuwapotosha na kuwaharibu wanadamu. Wanadamu wote wamezidi kuwa wapotovu chini ya elimu na ushawishi wa maarifa na sayansi, na kwa hivyo jamii imekuwa yenye giza na yenye machafuko zaidi, hadi Mungu na mwanadamu wanakasirika. Sasa maafa yanazidi kuwa ya mara kwa mara na misiba haiachi kutokea. Vita vikubwa vinaweza kuzuka wakati wowote. Watu wanaishi katika hofu, kana kwamba wanakabiliwa na mwisho wa dunia. Hii hakika inatufanya tujiulize kama sayansi na maarifa ni ukweli au la. Watu wanazifuatilia na kuzikubali zaidi na zaidi, lakini hawawezi kuepuka dhambi au kupata furaha, badala yake wanazidi kuwa wapotovu na waovu, wakizama katika dhambi na uchungu ambao hawawezi kuepuka. Hebu tuangalie kiini cha kweli cha watu hao maarufu, wakuu wanaoabudiwa na kila mtu. Wote wamekuwa wakana Mungu na wanamageuzi wanaomkana na kumkataa Mungu. Hawaamini kwamba Mungu yuko, au kuamini kwamba Anatawala juu ya kila kitu. Hasa hawawezi kukubali ukweli ambao Mungu anaonyesha. Katika mazungumzo yao yote, hakuna hata neno moja linalofichua giza la jamii; hakuna hata neno moja linalofichua kiini na uhalisi wa mwanadamu kupotoshwa na Shetani; hakuna hata neno moja linalofichua asili na kiini kiovu cha tabaka tawala, au kutoa ushuhuda wa kuwepo kwa Mungu na kazi ya Mungu, au kutoa ushuhuda wa matendo ya Mungu na upendo wa Mungu, au kupatana na ukweli ulio katika maneno ya Mungu. Maneno yao yote ni uzushi na makosa ya kumkana na kumpinga Mungu. Kwa ujumla, mazungumzo yao ni kutetea masilahi ya tabaka tawala, kupoteza, kupotosha, na kufanya madhara kwa wanadamu, na matokeo yake wamewaongoza wanadamu kwenye njia ya giza na mbaya, na wanadamu wamekuwa mfano wa Shetani wanaompinga na kumsaliti Mungu. Ni watu wa aina gani walio katika tabaka tawala? Je, wao ni wema na wenye hekima? La hasha. Bado hakujawa na mtu mmoja mwema na mwenye busara. Kinachojulikana kuwa wema na hekima zao zimeonyeshwa jinsi zilivyo, na uhalifu wao wote waliotenda bila watu kuona sasa umedhihirika. Ni dhahiri kwamba katika historia nzima ya upotovu wa Shetani kwa wanadamu, hakujakuwa na watawala wema au wenye hekima, na wote walio mamlakani wamekuwa mifano ya Shetani na roho waovu. Ni ipi kati ya mawazo na nadharia zao ambazo zimepotosha wanadamu kwa undani zaidi? Ukana Mungu, uyakinifu, mageuzi, na ukomunisti. Zimeeneza uzushi na uwongo mwingi, ikiwemo “Hakuna Mungu kabisa,” “Hakujawahi kuwa na Mwokozi yeyote,” “Majaliwa ya mtu yako mkononi mwake mwenyewe,” na “Maarifa yanaweza kubadilisha majaliwa yako.” Mambo haya hukita mizizi ndani ya mioyo ya watu tangu wakiwa wenye umri mdogo na kukua polepole. Je, matokeo yake ni yapi? Watu huanza kumkana Mungu na kila kitu kinachotoka Kwake, hata kwamba Mungu aliumba mbingu, dunia na vitu vyote, na kwamba Anatawala juu ya vyote. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, lakini wanakana ukweli huu, na wanageuza ukweli, wakisema kwamba wanadamu walitokana na nyani, kana kwamba mwanadamu alikuwa katika jamii moja na wanyama. Nadharia hizi za uongo, za kipuuzi huchukua akili za watu, zikichukua mioyo yao na kuwa sehemu ya asili yao, kwa hivyo wote humkana Mungu na kujitenga na Yeye na ni vigumu zaidi na zaidi kwao kukubali ukweli. Pia wao huwa wenye kiburi zaidi, waovu, na wapotovu kila wakati. Wanapoteza dhamiri na akili zote, wakipoteza kabisa ubinadamu wao na kuishia kuwa wasioweza kupata wokovu tena. Hivi ndivyo wanadamu wamepotoshwa na Shetani hadi kufikia hatua ya kuwa mapepo. Haya ni matokeo ya kutisha ya watu kufuatilia maarifa na kuyatumia kubadilisha majaliwa zao. Ukweli unaonyesha kwamba sayansi na ujuzi sio ukweli na haviwezi kuwa maisha yetu, lakini ni kinyume na ukweli na havipatani na ukweli. Vinachoweza kufanya ni kupotosha, kuumiza, na kuwaharibu binadamu.
Kwa hivyo kwa nini kusema kwamba mambo haya sio ukweli? Ni kwa sababu maarifa hayatoki kwa Mungu, bali yanatokana na upotovu wa Shetani kwa mwanadamu. Yanatoka kwa wale watu wakuu na maarufu ambao wanadamu wapotovu wanaabudu. Kwa hivyo tunaweza kusema kwa uhakika kwamba ujuzi sio ukweli. Kwanza, maarifa hayawezi kuwasaidia watu kujua kiini chao potovu au kuwapa kujitambua. Pili, maarifa hayawezi kutakasa tabia potovu za watu, lakini huwafanya watu wawe wenye kiburi zaidi na zaidi. Tatu, maarifa hayawezi kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini na kuwatakasa. Nne, maarifa hayawezi kuwasaidia watu kujifunza ukweli na kuja kumjua na kumtii Mungu. Tano, maarifa hayawezi kuwasaidia watu kupata furaha ya kweli au kuwaletea nuru, na hasa hayawezi kuwapa hatima nzuri. Na kwa hivyo, maarifa sio ukweli, na hayawezi kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini au kutoka katika nguvu za Shetani. Kwa hiyo tunaweza kuwa na uhakika kwamba maarifa hayawezi kubadilisha majaliwa ya mtu. Yale tu yatokayo kwa Mungu ndiyo ukweli; maneno ya Mungu pekee ndiyo ukweli. Ukweli pekee ndio unaweza kuwa uzima wa watu na unaweza kusafisha upotovu wao, kuwaacha waepuke dhambi na kuwa watakatifu. Ni ukweli pekee unaowaruhusu watu kurejesha dhamiri na mantiki yao na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu. Ukweli pekee ndio unaoweza kuwapa watu mwelekeo na malengo ya kweli maishani, na ukweli pekee ndio unaweza kuwasaidia watu kumjua Mungu, kupata baraka Zake, na kupata hatima nzuri. Hiyo ndiyo maana ni ukweli pekee unaoonyeshwa na Mungu katika mwili unaoweza kuwaokoa wanadamu kutoka katika nguvu za Shetani, kuwaruhusu kumgeukia Mungu kabisa. Ni Mwokozi pekee anayeweza kuwaokoa wanadamu na kuleta mapinduzi katika majaliwa ya wanadamu, akitupa hatima nzuri. Kwa hivyo kwa nini maarifa yasiweze kumwokoa mwanadamu? Ni kwa sababu mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, akiwa na asili za kishetani na kuishi katika tabia za kishetani, akitenda dhambi kila mara na kufanya maovu. Ana uwezo wa kufanya uovu wowote katika hali zinazofaa, na wakati anapopata mamlaka anaonyesha jinsi alivyo hasa na kuwa asiyezuilika. Na maarifa hutoka kwa binadamu mpotovu, kutoka kwa Shetani, kwa hivyo ujuzi sio ukweli. Haijalishi ni mwanadamu mpotovu hujifunza kiasi gani, hawezi kujua kiini na ukweli wa upotovu wake mwenyewe, na kwa kweli hawezi kutubu na kumgeukia Mungu. Hakuna kiasi cha maarifa kinachoweza kutatua asili ya dhambi ya mtu, sembuse kubadilisha tabia yake potovu. Haijalishi binadamu mpotovu anajua kiasi gani, hawezi kuepuka dhambi au nguvu za Shetani, na kufikia utakatifu. Bila kukubali ukweli, hawezi kufikia utii kwa Mungu, na hawezi kamwe kutatua tatizo la asili yake ya dhambi. Kadiri maarifa ya binadamu mpotovu yanavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi kwake kukubali ukweli na ndivyo anavyokuwa na uwezekano mkubwa wa kumkana na kumpinga Mungu. Wakati watu wanafuatilia maarifa zaidi, wanakuwa wenye kiburi na wenye kujidai, na wenye kutaka makuu zaidi. Hawawezi kujizuia kuingia kwenye njia ya dhambi. Hiyo ndiyo maana maarifa yanaweza tu kupotosha, kudhuru, na kuwaharibu watu. Watu wengi hawawezi kuona kiini cha kweli cha maarifa au kuona manifaa yake hasa. Hawawezi kuona asili, chanzo cha maarifa, lakini wanaabudu kwa upofu na kuufuatilia badala ya kufuatilia ukweli. Kwa nini watu wote hao maarufu wanafanya maovu mengi, kuleta mateso kwa watu na madhara kwa nchi baada ya kupata madaraka, wakisababisha maafa ya kila aina, wakifanya makosa ya kutisha yasiyoweza kukombolewa? Hayo ni matokeo ya kuabudu na kufuatilia maarifa. Hii inatuonyesha kwamba maarifa hayawezi kubadilisha majaliwa ya mtu, na haijalishi maarifa ya mtu ni ya juu kiasi gani, hawezi kuokolewa na Mungu ikiwa hana imani na kukubali ukweli. Hawezi kubarikiwa na Mungu au kuwa na majaliwa mema bila kujali maarifa yake ni ya juu kiasi gani, lakini ataenda kuzimu atakapokufa. Mungu ni mwenye haki na Anayatawala majaliwa ya wanadamu, kwa hivyo yeyote asiyepata kibali Chake au baraka Zake hawezi kuwa na majaliwa mazuri, lakini amehukumiwa uharibifu, kuangamia na kuzimu.
Sasa wenye hekima wameacha kusifu maarifa bali wanatamani Yule Mtakatifu aje, Mwokozi ashuke na kuwaokoa wanadamu. Hakuna anayetumaini kwamba watu mashuhuri na wakuu watawaokoa wanadamu. Hawawezi hata kujiokoa wenyewe, kwa hivyo wanawezaje kuwaokoa wanadamu wote? Ukweli unatuonyesha kwamba maarifa hayawezi kuhakikisha mtu anakuwa na majaliwa mazuri, na wazo la maendeleo kupitia sayansi na elimu ni upuuzi tu. Ni Mwokozi pekee anayeweza kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini na kutoka kwa majeshi ya Shetani; ni Mwokozi tu anayeonyesha ukweli anayeweza kutuongoza kwenye njia ya nuru; ni kukubali tu ukweli wote ulioonyeshwa na Mwokozi ndiko kunaweza kutuweka huru kutokana na upotovu wa Shetani ili tuweze kuokolewa kikamilifu na Mungu na kupata kibali na baraka Zake. Hii ndiyo njia pekee ya kubadilisha kabisa majaliwa yetu. Ni dhahiri kwamba kubadilisha majaliwa ya mtu hufanyika kwa kukubali kuonekana na kazi ya Mwokozi, kwa kukubali ukweli wote ulioonyeshwa na Mwokozi katika siku za mwisho, na kwa kutakaswa kupitia kukubali hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Kwa maneno rahisi, njia pekee ya kupindua majaliwa ya mtu kweli ni kukubali ukweli. Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote).
Sasa tunaweza kuona dhahiri kwamba wasomi hawawezi hata kujiokoa, kwa hivyo wangewezaje kuwaokoa wanadamu? Ni Mwokozi pekee anayeweza kuwaokoa wanadamu kutoka katika dhambi, na kuwaletea wanadamu nuru, furaha, na majaliwa mazuri. Mwokozi ni nani basi? Hakuna shaka kwamba Yeye ni Mungu mwenye mwili katika umbo la mwanadamu, aliyekuja miongoni mwa wanadamu kwa ajili ya kazi ya wokovu. Yeye ni Mwokozi wetu. Tunaweza kusema kwamba Mwokozi ni mfano halisi wa Mungu, kwamba Yeye ni Mungu aliyevikwa mwili wa mwanadamu. Huko ndiko kupata mwili. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili ndiye Mwokozi aliyeshuka miongoni mwetu. Mungu amepata mwili mara mbili ili kuwaokoa binadamu tangu Alipomuumba mwanadamu. Miaka 2,000 iliyopita, Alifanyika mwili kama Bwana Yesu na akasema katika mahubiri, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Alionyesha ukweli kiasi kikubwa na hatimaye alisulubishwa ili kuwakomboa wanadamu, Akifanya kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Hili lilikuwa onyesho la wazi la upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Watu kutoka ulimwenguni kote walimkubali Bwana Yesu kama Mwokozi wao, wakiungama na kutubu kwa Mungu, na kusamehewa dhambi zao. Walifurahia amani na furaha iliyotolewa na Mungu pamoja na wingi wa neema Yake. Wakati Bwana Yesu alimaliza kazi Yake ya ukombozi, Alitabiri mara nyingi, “Naja upesi” na “ujio wa Mwana wa Adamu”. “Kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu” (Mathayo 24:44). Hiyo ndiyo maana kila mtu ambaye amemkubali Bwana Yesu kama Mwokozi wake anamngojea Aje katika siku za mwisho, anangojea Mwokozi ashuke ili amwokoe na kumpeleka katika ufalme wa mbinguni. Bwana Yesu alitabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12-13). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17). Kwa msingi wa unabii Wake, Mungu atapata mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho na kuonyesha ukweli ili kuwatakasa na kuwaokoa binadamu kikamilifu, kuwapeleka binadamu kwenye hatima nzuri. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho ni Mwokozi anayewaonekania wanadamu. Kwa hivyo tunapaswa kumkaribishaje Mwokozi? Bwana Yesu alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu” (Yohana 10:27). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). Bwana Yesu alitukumbusha mara kwa mara kwamba jambo la msingi katika kumkaribisha Bwana ni kusikiliza sauti ya Mungu, na kuukubali ukweli unaoonyeshwa na Mungu atakaporudi katika siku za mwisho. Majanga tayari tunayashuhudia sasa. Tunaweza kuona kwamba duniani kote, Mwenyezi Mungu pekee ndiye Ameonyesha ukweli wote unaowaokoa wanadamu, na hakuna yeyote kando na Mwenyezi Mungu ambaye ametamka ukweli. Hii inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, kwamba Yeye ni Mwokozi aliyekuja kuwaokoa binadamu katika siku za mwisho. Hii ni habari kubwa njema. Njia pekee tunayoweza kubadilisha majaliwa yetu ni kuukubali wokovu wa Mwokozi, na kukubali ukweli ulioonyeshwa na Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).
Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana, ambao umekusanywa katika vitabu vya maneno ya Mungu kama vile Neno Laonekana katika Mwili, kwa jumla yakiwa mamilioni ya maneno. Huu wote ni ukweli ulioonyeshwa na Mungu kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, na ni mwingi zaidi kuliko ukweli ambao Mungu alionyesha katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Mwenyezi Mungu amefichua mafumbo yote ya mpango Wake wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu, Amefichua mafumbo yote ya Biblia ambayo watu hawajawahi kuelewa, na Amefichua ukweli wa wanadamu kupotoshwa na Shetani na asili yetu ya kishetani, inayompinga Mungu. Hii inatuwezesha kutambua chanzo cha dhambi zetu na ukweli wa upotovu wetu. Watu wote wanasadikishwa kikamilifu wanapokabiliwa na ukweli na wanaanza kujichukia, wanakuwa na majuto, na kutubu kwa kweli. Mungu pia anaonyesha ukweli wote ambao watu wanahitaji kutenda na kuingia katika, ili tuweze kuishi kwa kufuata maneno Yake na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu na mfano wa ukweli. Hiyo ndiyo njia pekee ya kupata ahadi na baraka za Mungu. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mwingi sana, wote ambao ni kwa ajili ya kutakasa upotovu wa binadamu na kutuokoa kutoka kwa nguvu za Shetani ili tuweze kumgeukia Mungu na kumjua Mungu. Ukweli huu ndio kanuni pekee za kweli za maisha na mafundisho ya kupata wokovu, na unatosha kubadilisha kwa kiasi kikubwa majaliwa ya mtu, ukimruhusu kufikia hatima nzuri—ufalme wa Mungu. Maafa makubwa tayari yameanza. Njia pekee ya kufanya tumaini lao zuri litimie ni kukubali kuonekana kwa Mwokozi na kazi Yake. Kukubali ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu ndiyo njia pekee ya kupata kibali cha Mungu, kupata ulinzi na baraka za Mungu katika majanga makubwa, kuyanusurika na kuletwa na Mungu katika ufalme Wake. Ikiwa watu hawatakubali ukweli wote ulioonyeshwa na Mwokozi, lakini tu wasubiri mungu wa uongo aliye mawazoni mwao, au roho mbaya aje awaokoe kutokana na maafa, hiyo ni ndoto ya uongo tu. Wataishia mikono mitupu, bila kupata chochote kutokana na juhudi zao. Miungu ya uwongo na roho waovu hawawezi kuwaokoa watu. Mungu aliye mwili pekee, Mwokozi ndiye anayeweza kuwaokoa binadamu, na hiyo ndiyo njia pekee ya watu kupata majaliwa na hatima nzuri. Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). “Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?