Dhambi Zetu Zimesamehewa—Je, Bwana Atatuchukua Moja Kwa Moja Hadi Katika Ufalme Wake Atakaporudi?

23/04/2023

Maafa yanaendelea kukua na waumini wote wanasubiri kwa hamu ujio wa Mwokozi, wakitamani kuinuliwa juu angani wakiwa usingizini ili wakutane na Bwana na kuepuka taabu ya majanga ya leo yanayozidi kuongezeka. Kwa nini wanangoja kwa imani sana Bwana Yesu ashuke na kuwanyakua ili wakukutane na Yeye? Wanaamini kwamba kwa vile dhambi zao zimesamehewa kwa njia ya imani yao katika Bwana Yesu, Bwana hawaoni tena kuwa ni wenye dhambi, wao wana kila kitu wanachohitaji, na watachukuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme Bwana atakapokuja. Lakini kinachowachanganya wengi ni kwamba maafa makubwa yamefika, hivyo kwa nini Bwana hajaja bado? Wengi wameanza kujiuliza kama kweli Bwana anakuja au la. Ikiwa haji, je, si hilo linamaanishi kwamba wanaweza kuanguka katika majanga na kufa wakati wowote? Wachungaji wengi sasa wanasema kwamba Bwana atakuja katikati au mwisho wa majanga, bila kujua jinsi nyingine ya kueleza jambo hilo. Lakini je, hiyo ni sahihi? Ulimwengu wa kidini haujamkaribisha Bwana, lakini, je, hilo linamaanisha kuwa Hajaja? Sote tunajua kwamba Bwana aliahidi kwamba Kanisa la Filadelfia lingenyakuliwa kabla ya majanga na Angewalinda kutokana na kuteseka katika majanga. Je, Bwana angevunja ahadi Yake kweli? La hasha. Ni kweli kwamba Bwana hajaja juu ya wingu kuwachukua waumini hadi mbinguni kama watu walivyofikiri, lakini sote tunajua kwamba Umeme wa Mashariki limekuwa likitoa ushahidi mara kwa mara kwamba tayari Amerudi kama Mwenyezi Mungu, akionyesha ukweli mwingi, na kufanya kazi ya hukumu ikianzia katika nyumba ya Mungu. Watu kutoka madhehebu yote wanaopenda ukweli wameisikia sauti ya Mungu katika maneno ya Mwenyezi Mungu na kumgeukia, wanaletwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, wakila na kunywa maneno ya Mungu kila siku, wakihudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Wamepitia hukumu na utakaso wa Mwenyezi Mungu na wana ushuhuda wa nguvu. Wanaishi katika uwepo wa Mungu, wakimsifu kwa furaha. Ikilinganishwa na hali ya hofu isiyoisha ya ulimwengu wa kidini kuhusiana na majanga, hii ni usiku na mchana. Waumini wengi wanawaza, je, Mwenyezi Mungu ambaye Umeme wa Mashariki humshuhudia ndiye Bwana aliyerudi? Je, Bwana kweli anafanya hatua ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Lakini wengi bado wana shaka, kama vile, “Bwana tayari amenisamehe dhambi zangu na Yeye hanioni kama mwenye dhambi. Anapasa kunipeleka mbinguni moja kwa moja atakaporudi. Kwa nini Asininyakue moja kwa moja, lakini Afanye hatua ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho?” Hebu tuichunguze mada hii kidogo leo. Je, kusamehewa dhambi zetu kunamaanisha tunaweza kuingia katika ufalme?

Kwanza, hebu tuone kama kuna msingi wowote wa kibiblia wa wazo kwamba wale ambao wamesamehewa wanaweza kuingia moja kwa moja katika ufalme. Je, kuna maneno kutoka kwa Bwana yanayounga mkono jambo hili? Bwana Yesu alisema lini kwamba wale ambao dhambi zao zimesamehewa wanaweza kwenda moja kwa moja katika ufalme wa mbinguni? Roho Mtakatifu pia hakusema kwamba hilo lingemruhusu mtu aende moja kwa moja hadi katika ufalme. Kwa kuwa hakuna msingi wa kibiblia au maneno kutoka kwa Bwana kama thibitisho, kwa nini watu wana hakika kabisa kwamba watanyakuliwa Bwana atakapokuja? Haileti maana yoyote. Bwana alitoa kauli hii dhahiri kuhusu ni nani anayeweza kuingia katika ufalme wa mbinguni: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Kutoka katika kauli hii, tunaweza kuwa na hakika kwamba kusamehewa peke yake hakutoshi kuingia katika ufalme. Kwa nini hilo halitoshi? Hasa, ni kwamba kusamehewa dhambi haimaanishi kwamba umetakaswa, kwamba unamtii Mungu, au kwamba unatekeleza mapenzi ya Mungu. Sote tumeona wazi kwamba hata waumini ambao dhambi zao zimesamehewa daima hudanganya, kulaghai, ni wakora na wenye ughushi. Wao ni wenye kiburi, na hawamsikilizi mtu yeyote mara tu wanapokuwa na ufahamu mdogo wa Biblia. Wanapigania nguvu na faida na kuishi katika dhambi ambayo hawawezi kujinasua kutoka katika. Hii inaonyesha wazi kwamba licha ya kusamehewa, watu bado ni wachafu na wapotovu, na wao hutenda dhambi kila wakati. Siyo tu kwamba wanashindwa kukubali na kujisalimisha kwa ukweli, lakini wanamhukumu na kumpinga Mungu. Kama tu Mafarisayo, wanamshutumu, kumhukumu, na kumkufuru Bwana, na hata kumsulubisha tena. Hii inathibitisha kwamba dhambi za wanadamu zinaweza kusamehewa, lakini sisi bado ni wachafu na wapotovu, na kiini chetu potovu kinampinga Mungu. Maneno ya Mungu yanasema, “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Kwa hivyo, wale wanaoishi katika dhambi hawastahili kuingia katika ufalme—hili ni bila shaka, na linaamuliwa kabisa na tabia ya Mungu yenye haki na takatifu. Ni mwumini yupi anayeweza kuthubutu kudai kuwa hana dhambi, kwamba hatendi tena dhambi na amefikia utakatifu? Hakuna hata mmoja. Hata wale watu wakuu, mashuhuri wa kiroho ambao wameandika mambo mengi sana ya kiroho hawawezi kuthubutu kusema wametupilia mbali dhambi na kuwa watakatifu. Kwa hakika, waumini wote ni sawa, huishi katika hali ya kutenda dhambi mchana na kuungama usiku, wakihangaika sana katika dhambi. Wote hupitia uchungu wa ajabu wa kutegwa na minyororo ya dhambi. Ukweli huu unaonyesha nini? Unaonyesha kwamba wale ambao dhambi zao zimesamehewa hawajaepuka dhambi na kuwa watakatifu, hivyo tunaweza kusema hakika kwamba hawastahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kama vile Bwana Yesu alivyosema, “Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34-35). Tunaweza kuona kwamba hakuna msingi wa kibiblia wa kuingia katika ufalme kwa sababu dhambi zako zimesamehewa, lakini hii ni dhana ya binadamu tu.

Katika hatua hii, swali la kwanza katika mawazo ya watu wengi ni, kwa kuwa hilo halituingizi katika ufalme wa mbinguni, je, ni kitu gani kitakachotuingiza? Njia ya kwenda katika ufalme ni ipi? Bwana Yesu alisema, “Ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni.” Hili ndilo linalohitajika, bila shaka. Kwa hiyo tunawezaje kufikia kufanya mapenzi ya Mungu na kuingia katika ufalme? Kwa hakika, Bwana Yesu alituelekeza kwenye njia hiyo muda mrefu uliopita. Hebu tuangalie unabii wa Bwana Yesu kwa ufahamu bora. Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli(Yohana 17:17). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). Bwana Yesu alitabiri kurudi Kwake mara nyingi, na mistari hii ni unabii Wake kwa ajili ya kazi ambayo Angefanya atakaporudi, ambayo ni kuonyesha ukweli mwingi kufanya kazi ya hukumu, kuwaongoza watu kuingia katika ukweli wote, kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini na kuwaokoa kutoka kwa nguvu za Shetani, na hatimaye kutupeleka katika ufalme Wake ili tuwe na hatima nzuri. Hiyo ndiyo maana lazima tukubali kabisa kazi ya Bwana ya hukumu Atakaporudi. Hadi tupate ukweli, hatuwezi kutakaswa upotovu kikamilifu na asili yetu ya dhambi haiwezi kutatuliwa. Hiyo ndiyo njia pekee ya kutupilia mbali dhambi na kuwa mtakatifu, na kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Tabia zetu potovu zinapaswa kutakaswa ili kutatua kabisa asili yetu ya dhambi. Tunapaswa kutupilia mbali tabia zetu potovu ili tuwe huru kutoka kwa nguvu za Shetani na kumtii Mungu na kufanya mapenzi Yake. La sivyo, hatutakuwa na haki ya kuingia katika ufalme. Kwa hiyo tunaweza kuwa na uhakika kwamba wale tu watakaswao kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho ndio wanaoweza kuwa wale wanaofanya mapenzi ya Mungu. Hili linathibitisha kwamba kukubali hukumu na utakaso wa Mungu katika siku za mwisho ndiyo njia pekee ya kuingia katika ufalme. Hebu tusome vifungu vichache vya maneno ya Mungu kuhusu jambo hili. “Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Maneno ya Mwenyezi Mungu ni dhahiri kabisa. Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Hii ilikuwa tu kusamehe dhambi za mwanadamu na ilikamilisha tu nusu ya kazi ya wokovu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu pekee katika siku za mwisho inayoweza kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Watu lazima wakubali ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu na hukumu na kuadibu Kwake, kisha upotovu wao unaweza kutakaswa na kubadilishwa na wanaweza kuwa watu wanaomtii Mungu na kufanya mapenzi Yake, na wanastahili kuingia katika ufalme Wake. Kwa maneno mengine, watakuwa na pasipoti ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tunaweza kusema kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu ni hatua muhimu zaidi, yenye maana zaidi ya kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na ni hatua ambayo itaamua kuingia kwa mtu katika ufalme. Kukosa hatua muhimu zaidi, kukosa hukumu na utakasaji wa Mwenyezi Mungu, kunamaanisha kushindwa kabisa katika imani yako. Haijalishi umeamini kwa muda gani, umefanya kazi kwa bidii kiasi gani au umekata tamaa kiasi gani, ukimkataa Mwenyezi Mungu, yote uliyofanya yalikuwa bure, na ni kukata tamaa ukiwa katikati. Hutaingia katika ufalme. Hayo yatakuwa majuto ya maisha!

Kwa hivyo Mungu anafanyaje kazi ili kuwahukumu, kuwatakasa, na kuwaokoa binadamu ili kutuleta katika ufalme Wake? Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). Wote ambao wamepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu wanaelewa kwa kina kwamba bila maneno ya Mungu kufichua upotovu na kiini chetu, hatutawahi kuona jinsi tulivyopotoshwa sana, jinsi upotovu wetu ulivyo mbaya. Bila kuhukumiwa, kuadibiwa, kupogolewa, kushughulikiwa, na kufundishwa nidhamu na Mungu, hatungetupilia mbali tabia zetu potovu na hata tungehangaika kujijua wenyewe. Si ajabu kwamba waumini wengi hawana budi kutenda dhambi kila wakati na kuungama, kisha kuungama na kutenda dhambi tena bila kuona kwamba chanzo cha dhambi zao kipo katika kupotoshwa sana na Shetani. Bado wanaamini kimakosa kwamba wanaweza kwenda mbinguni moja kwa moja kwa sababu wamesamehewa. Huu ni upofu na upumbavu kweli, na kukosa kujitambua kabisa. Toba ya kweli huja tu kupitia hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu, na kumcha Mungu na kuepuka maovu huja tu kupitia kuijua tabia ya Mungu yenye haki. Ni hapo tu ndipo tunaweza kumwabudu na kumtii Mungu, na kuwa watu wanaofanya mapenzi Yake. Unaweza tu kujua hili kwa kweli baada ya kupitia hukumu ya Mungu katika siku za mwisho na kutakaswa.

Sasa nadhani sote tuko wazi kwamba njia ya kuingia katika ufalme ni thabiti sana, ni ya vitendo sana, kwamba sio tu kusamehewa na kungoja Bwana atunyakue, kisha kuchukuliwa moja kwa moja hadi mbinguni. Hilo ni jambo lisiliwezekana—hiyo ni njozi. Ikiwa tunataka kuingia katika ufalme wa mbinguni, lililo muhimu zaidi ni kukubali hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu ili upotovu wetu utakaswe na tuweze kufanya mapenzi ya Mungu. Kisha tutastahili kupokea ahadi na baraka za Mungu, na kuchukuliwa katika ufalme Wake. Tukikataa kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu, hatutawahi kupata ukweli na uzima au kutakaswa upotovu wetu kamwe. Kutamani tu Bwana atuchukue mbinguni kwa njia hii ni jambo lisilo na matumaini kabisa, na watu hao ni wanawali wapumbavu ambao wataanguka katika majanga, wakilia na kusaga meno. Tunaweza kusema kwamba kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ni kuinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi. Bado tunapaswa kukubali ukweli Anaoonyesha na hukumu na kuadibu Kwake, kutupilia mbali upotovu na kutakaswa, ili hatimaye tuweze kulindwa na kuhifadhiwa na Mungu katika majanga, na kuingia katika hatima nzuri Aliyotayarisha. Kumkubali Mwenyezi Mungu kwa mdomo tu bila kukubali ukweli, kutotii hukumu na kuadibu Kwake, siyo imani ya kweli, na si kuwa mtu ambaye anapenda ukweli hakika. Wataishia kufichuliwa na kuondolewa. Hebu tutamatishe kwa kifungu kingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupata Mwili Ni Nini?

Sote tunajua kwamba miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alikuja mwilini katika ulimwengu wa mwanadamu kama Bwana Yesu ili kuwakomboa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp