Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia Yenye Maadili

13/01/2018

Qin Shuting Jijini Linyi, Mkoani Shandong

Kwa muda fulani, ingawa sikuwa nimeacha kula na kunywa manen ya Mungu, sikuhisi mwanga kamwe. Nilikuwa nimeomba kwa Mungu kwa ajili ya hili lakini, baadaye, bado sikuwa nimepata nuru. Hivyo niliwaza, “Kuna wakati wa Mungu kumpa kila mwanadamu nuru, kwa hivyo hakuna maana ya kuiharakisha.” Baadaye, nilishika amri na kula na kunywa maneno ya Mungu bila wasiwasi, nikingoja kwa “subira” kutoa nuru kwa Mungu.

Mpaka siku moja, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu). Katika kutafakari maneno haya ya Mungu, nilielewa: Mungu ni Mungu wa haki. Kamwe yeye Hayuko holela katika kumkidhi mwanadamu, na Hamtolei mwanadamu bila masharti. Ili watu wapate nuru na mwangaza wa Mungu, lazima watulize mioyo yao mbele ya Mungu na wawe na moyo ambao unayatamani sana na kutafuta maneno ya Mungu. Lazima wabebe mzigo kwa ajili ya maisha yao wenyewe na kutafuta mapungufu yao wenyewe ndani ya maneno ya Mungu. Wakibeba mzigo wao, lazima kwa makusudi wale na kunywa maneno ya Mungu kujali mapenzi Yake na kwenda kwa kina zaidi katika ukweli. Ni kwa kulipa gharama kama hiyo kwa vitendo tu kufanya kazi na Mungu ndiyo mtu anaweza kupata nuru ya Mungu. Kwa kufikiria ya zamani, sikuwa nabeba mzigo wowote wala kuwa na moyo wowote wa kutamani sana hata kidogo kula na kunywa maneno ya Mungu. Kila mara nilipochukua kitabu cha neno la Mungu, ningepitia kwa haraka na kuona kwamba nilikuwa nimesoma kifungu hiki na kusoma kifungu kile, nikifikiri kuwa nilikuwa na wazo la juu juu kuhusu kila kifungu. Kisha ningepata chochote cha zamani, nikisome kwa haraka, na kisha ningekuwa nimemaliza. Nilipokula na kunywa maneno ya Mungu, ilikuwa inatosha tu kwangu kuelewa maana halisi ya maneno hayo, nikilenga tu kushika masharti machache na matendo. Bila shaka sikuona ukweli mwingi ambao nilipaswa kuingia ndani yake, wala sikuwa nauridhisha moyo wa Mungu. Sikuwa nabeba mzigo kwa ajili ya maisha yangu hata kidogo, wala sikuwa na wasiwasi kuhusu kutojiandaa na ukweli wa kutosha; nilikuwa nachukulia kula na kunywa kwangu maneno ya Mungu kwa kutojali tu. Na mwelekeo wa kifidhuli kwa maneno ya Mungu hivyo, ningewezaje kupata nuru na mwangaza Wake? Kwa kweli sikuwa nafanya kazi na Mungu, na nilikuwa natumia “Kuna wakati wa Mungu kumpa nuru kila mwanadamu” kama kisingizio kungoja kwa upofu kutoa nuru kwa Mungu. Kwa kweli nilikuwa mpumbavu sana! Ni sasa tu ndipo natambua kwamba, ingawa kuna wakati wa Mungu kumpa nuru kila mwanadamu, hili ni kweli, kuna kanuni katika kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu. Mwanadamu mwenyewe lazima awe na moyo wa tamaa kubwa, ya kutafuta ili kuweza kufanya kazi na Mungu kwa vitendo na kwa utendaji. Ni hapo tu ndipo Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi kwa mwanadamu na kutia nuru na kuangazia kuelewa kwa mwanadamu kwa mapenzi ya Mungu, kumfanya kuelewa ukweli katika maneno Yake.

Ee Mungu! Ninatoa shukrani kwa sababu ya kutoa nuru Kwako kwa muda ufaao ambako kuliniruhusu kuona mkengeuko katika uzoefu wangu mwenyewe. Sasa ninatamani kurudi katika kufanya kazi kwa moyo mwema na kiutendaji pamoja na Wewe, kuweka moyo unaotafuta na kutamani sana, kubeba mzigo wangu wa kula na kunywa maneno Yako, kufuatilia kupata nuru zaidi kunakopatikana kupitia katika maneno Yako, kujifanya kupenyeza zaidi katika ukweli, na kwa maisha yangu kua hata zaidi.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp