Huwezi Kumtambua Mtu kwa Kuonekana Kwake

13/01/2018

Yang Rui Mji wa Yuci, Mkoa wa Shanxi

Moyoni mwangu, niliamini kuwa babangu alikuwa mtu mzuri. Lakini siku moja, nilisikia kwa ghafla kuwa baba yangu alifukuzwa kutoka kanisani. Nilishangaa kabisa wakati huo na sikuweza kuelewa. Katika moyo wangu, baba yangu alikuwa ndiye mtu mkuu mno duniani. Ingawa ana hasira mbaya, alitutunza sana sisi ndugu wa kike na kamwe hakutupiga au kutukemea. Licha ya harakati za familia yetu, hangeturuhusu tuone hasira bila kujali ni shida kiasi gani angepaswa kustahimili. Baada familia yetu yote kuikubali kazi ya Mungu, baba yangu alikuwa aidha amilifu katika kutekeleza wajibu wake, na mara nyingi alitutia moyo kutimiza wajibu wetu vizuri. Ingawa baba yangu alikuwa mkali kidogo wakati mwingine, mara tu palipokuwa na wajibu wa kutimiza, bila kujali upepo na mvua au kiwango cha ugumu, angetafuta njia ya kulikamilisha hilo. Mtu mwema kama huyo angewezaje kufukuzwa? Ikiwa hawezi kupokea wokovu, basi ni nani anayeweza? Hali hiyo iliujaza moyo wangu hasira na mgongano, kwa sababu nilihisi kanisa halikumtendea baba yangu haki. Ingawa sikulisema, niliona vigumu kuutuliza moyo wangu na niliumia vibaya katika mateso.

Siku chache zilizopita, niliona yafuatayo miongoni mwa maneno ya Mungu: “Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu). Baada ya kutafakari juu ya maneno ya Mungu, hatua kwa hatua nilielewa: Kuona kama mtu ni mwenye haki au mwovu, angalia siyo kama tabia yake ya nje ni nzuri au mbaya au jinsi uhusiano wao na watu wengine ulivyo. Badala yake, angalia uhusiano wake na Mungu, na kama ana utii wa kweli kwa Mungu na kumcha, na kama anapatana na Mungu. Mtu anaweza kuwa na uhusiano mzuri na wengine na kuwatendea kwa upendo, lakini kama hawezi kulingana na Mungu, kama hafuatilii ukweli katika imani yake, kama anatia wajibu wake najisi kwa nia zake mwenyewe, na kama anamhukumu na kumpinga Mungu wakati kazi Yake hailingani na dhana zake, basi mtu huyo ni mnafiki. Yeye ni mtu mjanja, mwenye uovu aliye kigeugeu. Nikiwa na ufahamu huu, nilianza kukumbuka maneno Fulani ambayo babangu alikuwa amesema: Katika dhehebu lake la zamani, baba yangu alikuwa kiongozi. Baada ya kuikubali hatua hii ya kazi ya Mungu, ndugu wa kiume na wa kike wa kanisa hawakumchagua kuwa kiongozi kwa sababu asili yake ilikuwa ya kiburi mno. Wakati ule alipoonekana akitii juu juu na kufanya chochote alichoambiwa, nia yake ya siri ilikuwa kuwa na uwezo wa kukalia “enzi” ya kiongozi mara nyingine. Baadaye, wakati nia yake haikufanikishwa, alibainisha tabia yake halisi, daima akionyesha majivuno zaidi katika kanisa, kamwe kutomsikiliza mtu yeyote, na daima akiwalazimisha watu kumsikiliza bila kujali chochote. Kama aliona mfanyakazi ambaye hakumpenda, angempima, amdunishe, na kumdhoofisha. Pia angeanzisha chuki kati ya ndugu, akikatiza na kuharibu vikali maisha ya kanisa. Mara nyingi, viongozi na wafanyakazi walishiriki ukweli naye, walimpogoa na kumshughulikia na kumpa maonyo—lakini alibaki asiyetambua kabisa, sembuse kuonyesha majuto yoyote. Je, si hii ni tabia ya waovu? Kama tu Mungu alivyosema: “Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Kwa mujibu wa maneno ya Mungu, tabia ya baba yangu haikuwa kutii mpango wa Mungu na utaratibu, pamoja na kusababisha vurugu kwa kanisa. Alitenda aina zote za uovu kwa ajili ya kushindania nguvu na hadhi. Kiini kama hicho ndicho ambacho humpinga Mungu na ni cha mtu mwovu. Lakini nilitumia mwenendo wake kwa nje, kama vile kunitunza na kunijali, kuweza kutimiza wajibu wake, kuamua kuwa yeye ni mtu mwema, kufikiri kwamba kanisa halikustahili kumfukuza. Hata hivyo, matendo yake mema ya nje hayana usawa na kumtii Mungu, na pia hayawezi kuitwa yenye haki. Ni wale tu wanaoutii mpango wa Mungu kwa kweli na kukubali kwa hiari kukubali kuadibiwa na hukumu ya Mungu, na kutafuta mabadiliko ya kitabia, wanaoweza kupokea wokovu. Baba yangu alijilaumu mwenyewe tu kwa kuanguka katika hali ambayo yupo leo. Ilikuwa kwa sababu ya asili yake mbaya kabisa na hakuwa na mtu mwingine wa kulaumu. Aidha, hili lilikuwa dhihirisho la tabia ya Mungu ya haki.

Ee Mungu! Asante kwa kutumia mazingira haya na kunipa kipengele hiki cha ukweli ili kupindua kabisa maoni yangu mabaya, na kwa ajili ya kufanya nione utakatifu Wako na kwamba tabia Yako ya haki na ya uadhama ni lazima isikosewe na mtu yeyote. Hili limenifanya nielewe kwamba siwezi kutofautisha au kung'amua mambo bila ukweli. Kuanzia sasa na kwendelea, bila kujali ni nini kinachonitokea, sitampima mtu tena kulingana na sura yake ya nje. Ni sharti nichukue mtazamo wa ukweli na kukubali kila kitu Unachokifanya. Hata kama siwezi kung'amua Unayoyafanya, nitaamini kuwa yote Unayoyafanya ni sawa. Sitachambua na kuchunguza tena kutoka kwa mtazamo wa mtu. Nitasimama upande wa ukweli, mara kwa mara nikijitahadharisha kuwa shahidi kwa ajili Yako.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ukweli Umenionyesha Njia

Na Shizai, Japani Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp