Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

13/01/2018

Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena

Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi. Baadaye, kanisa lilinipangia kusimamia kazi ya injili, nilianza kuwa na shaka kumhusu Mungu: Mimi ni mpotovu sana na pia nilikuwa nimeichukiza tabia ya Mungu. Ni kwa nini Mungu angenitumia mimi? Je, Ananidanganya? Je, nitaondolewa baada ya kudanganywa? Aa! Kwa kuwa kanisa lilinipa nafasi nitaitunza, hata kama ni lazima niwe mtenda huduma. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilitimiza wajibu wangu nikiwa na akili kama hiyo, lakini bila kutafuta lengo la juu—kufanywa mkamilifu na Mungu.

Wakati fulani, nilipokuwa nikitenda ibada ya roho, niliona maneno haya ya Mungu: “Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli unakupuuza, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha…. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu). Baada ya kula na kunywa kifungu hiki cha neno la Mungu, niliguswa sana ndani. Niliona kwamba nia ya Mungu ni kuwaruhusu watu wote kutafuta kufanywa wakamilifu na wanaofaa kutumiwa na Mungu. Kisha nilifanya uamuzi: Nitaweka mbali wasiwasi wangu mwenyewe na nisiwe tena hasi na baridi. Nitaamini katika maneno ya Mungu na nifanye bidii ili nikamilishwe na Mungu. Lakini pole pole, kwa sababu bado sikujua kiini cha uaminifu wa Mungu, nilianza kuacha kuamini katika maneno ya Mungu tena, kila mara nikiamini kuwa maneno haya yalilengwa kwa mtu mwingine, na kwa mtu kama mimi yangetoa tu faraja na kutia moyo kwa kiasi kidogo. Nilizidi kukumbuka jinsi wakati mmoja nilivyoikosea tabia ya Mungu, kwamba asili yangu ni potovu sana, kwamba wakati mwingine hata nilifichua tabia yangu potovu huku nikitimiza wajibu wangu, kwamba singeweza kukamilishwa haijalishi jinsi nilivyofuatilia, na kufikiri kwamba ninapaswa kuridhika tu na kuwa mtenda huduma. Kwa namna hiyo tu, bila kujua nilianza kuishi katika ubaridi tena. Mpaka siku moja nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Kiini cha Mungu ni uaminifu; Yeye hufanya Anachosema, na chochote Afanyacho hutimizwa …(“Kipengele cha Pili cha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Wakati huu, ilionekana kana kwamba wazo lilieleweka ndani mwangu kwa ghafla, kana kwamba ukungu uliokuwa umetanda juu ya moyo wangu ulitawanyika mara moja. Miaka mingi ya kutoelewa na wasiwasi kwa ghafla iliisha. Kisha tena nikakumbuka kile kifungu cha neno la Mungu ambalo nilikuwa nikila na kunywa: “Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli unakupuuza, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha.” Wakati huu, nilihisi upitishaji wa haki ya ajabu na upendo usio na mipaka kutoka katikati ya mistari ya maneno ya Mungu, niliona kwamba Mungu ni mwema na mkuu, huku wakati uo huo niliona upweke wangu mwenyewe, akili yangu finyu, na uoza. Mungu ni mwaminifu. Hili ni bila shaka na lisiloweza kushukiwa. Mungu ana kiini cha uaminifu, Yeye ni wa kuaminika, na Anajaribu kumwokoa binadamu kwa kiasi kikuu iwezekanavyo. Mradi tu binadamu anafuatilia ukweli na mabadiliko katika tabia kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu atamfanya mwanadamu kamili, kwa sababu kile asemacho Mungu atafanya, Atakifanya na kile Afanyacho kitafanyika! Badala yake, nilishuku kuwa Mungu alikuwa kama binadamu na Angenitupilia mbali mara tu ningekoma kuwa mwenye maana. Sikulichukulia neno la Mungu kama ukweli hata kidogo, na zaidi ya hayo sikuamini katika Mungu kwa kweli na kwa uzuri. Badala yake, niliishi katika fikira na shaka katika mawazo yangu, nikikosa ujasiri mbele ya ukweli na kwa woga kukubali ushawishi wa giza, nisiweze kutetea haki. Ilikuwa ni hapo ndipo nilifahamu kwa kweli kuwa kufuatilia maarifa ya kiini cha Mungu ni muhimu sana. Kama ningekuwa tayari nimekuwa makini kufuatilia ufahamu wa tabia ya Mungu na kiini Chake kabla, nisingeliishi miaka mingi vile katika wasiwasi, nikichelewesha kuendelea kwa maisha yangu mwenyewe.

Asante, Mwenyezi Mungu! Ni Wewe uliyenitunza na kunipa nuru na kuniongoza kujitoa katika pingu ambazo zilikuwa zimenidhibiti kwa miaka mingi sana, kuniruhusu kutoka katika ukungu. Zamani, sikukujua Wewe na mara nyingi niliishi katika kutoelewa, nisiweze kuamini neno Lako na kulichukulia kama tu la kuliwaza na kuwatia watu moyo. Sikulichukulia neno Lako kama ukweli na uzima, na zaidi sikukuchukulia wewe kama Mungu. Lakini Ulinivumilia, na Ulikuwa mwenye subira kwangu. Ulinipa nuru na kuangaza mwanga Wako kwangu, ili kwamba niwe na ufahamu kidogo wa kiini Chako cha haki na uaminifu. Hii hasa ni mfano kamili wa upendo Wako kwa mwanadamu. Ee Mungu! Kuanzia sasa kuendelea nitaweka juhudi kubwa katika ukweli kuhusu kumjua Mungu, kufuata kile unachotarajia kutoka kwangu, nifuatilie ufahamu wa kiini Chako, na kutafuta mabadiliko katika tabia hivi karibuni ili niweze kukamilishwa na Wewe!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kiburi Huja Kabla ya Kuanguka

Na Xinjie, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo...

Pambano la Kuwa Mtu Mwaminifu

Mwenyezi Mungu anasema, “Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp